Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Samaria wilayani Arumeru Mashariki Mkoani Arusha wakiwa wanachangia fedha wakimkabidhi mbuge wao Nasari waliyoiandaa kwa ajili yauchimbaji wa visima vya maji tatizo ambalo limewakabili na kuwa kilio kikubwa katika maisha yao ya kila siku.
Baadhi ya akina mama wa kijiji cha Samaria kilichopo wilayani Arumeru mashariki wakiwa kwenye mkutano wa Harambee ya kuchangia uchimbaji wa visima vay maji mara baada ya Mbunge wao Joshua Nasari kufika kijijini hapo.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari (katikati)akiwa na wenyejiti wa kijiji cha Samaria mara baada ya kufika kijijini hapo kwa ajili ya harambee ya kuchangia uchimbaji wa visima vya maji tatizo lililokithiri kwa muda wa zaidi ya miaka 100.
Bw,Emmanuel Absolum ambaye ni meneja wa duka la vitabu la Kimahama akieleza umuhimu wa wananchi kujisomea vitabu.
Amesema kuwa kupitia vitabu unapata elimu juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi kwa mambo ambayo mwananchi hayajui.
Akielezea lengo la kufungua duka hilo amesema kuwa ni kuwasaidia wakazi wa jiji la Arusha kupata elimu kupitia vitabu sambamba na kujijengea mazoea ya kusoma ujuzi na ufanisi katika kutambua mambo mbalimbali.
Meneja wa kimahama Emmanuel Absalom akiwa amesimama kwenye duka la vitabu lililo zinduliwa upya na Mkuu wa chuo Habari maalum bw,Jackson Kaluzi, baada ya kuboreshwa na kuwekwa vitabu mbalimbali vya kuvutia ambapo vitabu hivyo ni kama Biblia,vitabu vya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na vingine vingi vya kuelimisha jamii.
Meneja wa Kimahama Bookshop bw,Emmanuel Absalom akiwa anaonesha baadhi ya vitabu vipya vilivyozinduliwa kwenye duka hilo lililopo jijini Arusha Mkabala na Hotel ya Golden Rose.
Hawa ni samaki wekundu kwa jina maarufu(changu mwekundu) smaki hawa wanavutia sana kwa muonekano wao,samaki hawa wanaopatikana katika bahari ya hindi,ambapo samaki hawa hawawezi kupatikana sehemu nyingine kama kwenye maziwa fofauti na kupatikana kwenye maji ya chumvi ya baharini. Kama wanavyoonekana hapo juu hawa samaki hawjakaushwa wala kukaangwa hapa ni wametolewa baharini kuvuliwa katika sehemu ya uvuvi bahari ya Hindi Mkoani Tanga katika eneo lililopo mkabala kabisa na Radio ya Huruma fm iliyopo ufukweni mwa Bahari.
Mwanafunzi ambaye ni Mmoja wa viongozi wa Tyccc kanda ya Tanga kwa jina la Douglos Gasper aliyevalia miwani(wa kwanza kutoka kushoto)ambaye pia ni mhazini wa kikundi hicho,akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kidato cha nne yaliyofanyika katika ukumbi wa Magreth Hall uliopo jijini Tanga. Kiongozi huyo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi pamoja na kadamnasi iliyokuwepo kwenye mahafali hayo ambapo alielezea changamoto wanazokumbana nazo katika kuendesha kikundi chao wakiwa shuleni.
Gasper alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakizuiliwa na uongozi wa shule katika suala zima la kuendesha vipindi vyao dini ikiwemo kuimba kwaya wawapo mashuleni huku walimu hao wakitumia vipindi hivyo kufundisha masomo mengine jambo ambalo limepelekea wanafunzi wengi kutokuwa na hofu ya Mungu hata kutofahamu kabisa neno la Mungu.
Pia alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili katika utendaji kazi wao ni ufinyu wa kipato kwani hawana biashara yoyote hivyo kulazimika kutoa ela zao mifukoni pale kunapokuwa kumehitajika utatuzi wa jambo fulani na kwamba hali hiyo imepelekea shughuli zao kutokwenda kwa ufanisi. Waliiomba serikali na uongozi wa dini ya kikristo kuwapa msaada pale watakapokuwa wanahitji msaada ikiwa ni pamoja na kuwawekea walimu wa dini kwenye shule zao ili kuweza kuepukana na tatizo lililokihtiri la kufeli masomo ya dini ya kikristo tofauti na dini nyingine.
Meneja wa mjasirimali kwanza enterprises bw,Saravai r.Izini aliyevalia koti jeusi ameinama huku wakiwaelekeza baadhi ya watu waliokuja kujifunza ujasiriamali jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji ambapo semina hiyo il;ifanyika katika ukumbi wa Golden Rose jijini Arusha.
Waziri wa mali asili Hamisi Kagasheki akiwakabidhi cheti wawakilishi wa shule ya msingi st,Magreth walioshiriki kwenye siku hiyo ya matembezi ya tembo jijini Arusha ikiwa ni siku ya kuazimisha wanyama Duniani.
Mkuu wa Mkoa Magesa Mlongo pembeni kabisa kulia ambaye amevalia jaketi lenye rangi ya njano,kijani na nyeusi yuko nyuma kidogo na Askari akishiriki na wananchi katika matembezi ya Tembo ambapo ilikuwa siku ya wanyama Duniani
Waziri wa mali asili na utalii Hamis Kagasheki aliyevalia kofia nyeupe akipokea zawadi yake aliyopewa na uongozi wa shirika la Tato na shule ya furaha foundation wakati alipokuwa kwenye matembezi ya Tembo jijini Arusha ikiwa ni siku ya maadhimisho ya wanyama duniani.
Baadhi ya Wananchi Mkoani Arusha wakiwa kwenye maandamano ya amani ya kutembeza Tembo ambapo ni siku ya kuazimisha wanyama Duniani. Matembezi hayo yalihudhuriwa na mamia ya watu jijini hapa ambapo maandamano hayo yalianzia katika ofisi za Tanapa majengo na kuishia katika viwanja vya Aicc
Walimu wawili wa Shule ya Furaha foundation waliosimama pembeni kushoto wakiwa kwenye picha na Waziri wa mali asili na utalii Hamis Kagasheki ambaye amesimama kulia akiwa ameshikilia zawadi aliyopewa na walimu hao kwa uwakilishi wa shule ya Furaha foundation,mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo ilikuwa siku ya kuazimisha wanyama Duniani.
Wanafunzi wa dini ya katoliki(TYCC) kutoka shule mbalimbali za kanda ya Tanga wakiwa wanamsikiliza katibu mstaafu wa kwaya ya st,Antony Tanga kwa jina la Amos Mombo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kuhitimu kidato cha nne,ambapo mahafali hayo yalifanyika katika ukumbi wa Magreth hall(ridoch)uliopo jijini Tanga. Aidha bw,Amos aliwashauri kuwa ufuatia kuchafuka kwa dunia vijana wamekuwa wakijiingiza katika tabia mbaya na kusahau amri za Mungu hivyo wajitahidi kuepukana nazo kwa kuwekw sala mbele za Mungu.
Pia alisema kuwa wanapaswa kushikamana kwa mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kuepukana na makundi yasiyo kuwa na tija kwa jamii kwani kuna baadhi ya makundi sio mazuri ambayo ujihusisha na masuala ya madawa ya kulevya na kutomjua Mungu.
Kikundi cha wanafunzi wa TYCC kanda ya Tanga wakicheza wimbo wao wa dini kwenye ukumbi wa magret holl ikiwa ni siku sherehe yao ya kuhitimu kidato cha nne.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya furaha foundation wakitumbuiza nyimbo zao na kucheza kwa mbwembwe mbele ya huku mgeni Rasmi Waziriwa Mali asili na Utalii Hamis Kagasheki wakati alipokuwa kwenye viwanja vya Aicc Mkoani Arusha mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo yaliyoanzia katika Ofsi za Tanapa. Ambapo wimbo wao ulihusu kumshukuru waziri Kagasheki kwa kazi yake nzuri anayoifanya,kwa kushirikiana na mashirika ya hifadhi ya Wanyama.
Dr Alfred Kikoti ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa Tembo(world Elephant Centre)akiwaelezea wananchi wa jiji la Arusha kuwa pale watakapowabaini majangiri wanao waua Tembo wawekwe kwenye website,mitandao ikiwa njia mojawapo ya kuwafichua majangiri hao.
Dk Alfred aliyasema hayo kwenye uwanja wa Aicc mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo kauli mbiu yao ilikuwa ni ''kila baada ya dk kumi na tano tembo anauwawa ''na kwamba kama hali itaendelea hivo baada ya miaka kumi na mbili Tanzania hatutakuwa na Tembo. Alisema Tembo ni sawa na binadamu,meno ya tembo,pembe za ndovu wasivitumie kama biashara ni kwa ajili ya tembo,hivyo kujitahidi kukataa biashara haramu ya pembe za ndovu na kila Mtanzania kusema ''hapana''
Waziri wa mali asili na utalii pia ni mbunge wa Bukoba mjini Hamis Kagashiki(wa tatu kutoka kulia )aliyevalia kofia akipokea zawadi maalumu iliyoandaliwa na shirika la TATO,ikiwa ni siku ya maandamano ya kutembeza Tembo iliyofanyika jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha bw,Magesa Mlongo wa kwanza kutoka kulia akikabidhibiwa zawadi na ofsi za Tato mara baada ya kumaliza maandamano ya amani ya utembezi wa tembo kitaifa, ambapo jijini Ausha maadamano hayo yameanzia katika ofis za Tanapa na kuishia kwaenye viwanja vya AICC njiro.
Viongozi hawa wakiendelea kutembelea mazao mbalimbali wa kwanza kutoka kulia ni waziri wa ndani wa uwekezaji na uwezeshaji ofisi ya waziri mkuu Bi,Mary Nagu,katikati ni waziri mkuu Mizengo Pinda na wa kwanza kutoka kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiangilia baadhi ya bidhaa mara baada ya kutembelea vibanda kwenye maonesho ya wawekezaji ikiwa ni moja ya kuonesha fursa walizonazo hivyo wawekezaji kujitokeza ili kuwekeza katika bidhaa zao ,ambapo kongamano hilo lilifanyika jijini Tanga katika hotel maarufu ya Mkonge.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Arusha wakiongoza maandamano ya week ya nenda kwa usalama barabarani huku wakiimba nyimbo zao kwa madaha.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru bw,Nyerembe Munasa akitoa ushauri kwa waendesha toyo kuendesha toyo zao kwa umakini pale wanapokuwa barabarani ili kuondokana na ajali zisizo kuwa za lazima hapa nchini.
Munasa alisema hayo katika uwanja wa sheikh amri Abed Arusha ikiwa ni week ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa. Alisema kuwa kuna baadhi ya waendesha toyo ambao wamekuwa wakisababisha ajali kwani wengi wao huendesha toyo wakiwa wamelewa pombe hata madawa ya kulevya jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria. Alisisitiza kwamba wale wote ambao wataenda kinyume na sheria watakamatwa na kuchukuliwa sheria.
Baahi ya waendesha pikipiki alimaarufu kama toyo jijini Arusha wakiwa katika uwanja wa sheikh Amri Abedi huku wakipewa ushauri na Mkuu wa wilaya ya Arumeru bw.Nyerembe Munasa kuhusu kutumia pikipiki zao vizuri ili kuepukana na ajali zisizo kuwa za lazima ambapo ilikuwa ni week ya nenda kwa usalama barabarani.
Baadhi ya akina baba wa dini ya kiislamu wakiwa kwenye uwanja wa mpira sheik amri abedi wakati wakimsikliza Sheikh IssaJohn Luvunda kutoka jijini wakati akiombea amani nchi ya Tanzania kufuatia umwagaji damu kukithiri hapa nchini.
Waziri mkuu Mizengo Piter Pinda akitoa ufafanuzi kwamba kuna baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakikwamisha suala zima la uwekezaji kutokana na tamaa yao mbaya ya kutaka kitu kidogo yaani Rushwa hivyo wawekezaji kukata tamaa na kushindwa kuwekeza na kwamba atakaye bainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pinda aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa minne Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Tanga,ambapo lilofanyika Mkoani Tanga katika Hotel maarufu Mkonge ambapo kongamano hilo lilijumuisha viongozi wote wa ngazi ya wilaya,wakuu wa mikoa pamoja na wawekezaji.
Padre Francis Shayo I.C ambaye ni murugenzi wa miito wa shirika la mapendo (Rosminians) Lushoto Tanga akitoa ufafanuzi juu ya vijana wale wenye miito kujitokeza katika kusomea upadre na usister alipokuwa katika kanisa katoloki la Huruma lililopo jijini Tanga.
Bi Antonia ambaye ni mke wa naibu waziri wa ardhi,nyumba na makazi ambaye pia ni mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye,yeye ni bi Antonia ni Nesi mstaafu katika hosp ya Mkoa jijini Arusha,ambapo baada ya kustaafu ameamua kufungua ofsi yake ya kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwa ni pamoja na kuwapatia ushauri wale wenye unene na kuwapima kwa kutumia mashine maalumu ,na hapa anampatia mmoja wa akina mama katika ofsi yake iliyopo mianzini barabara ya vumbi,ambapo anamueleza ni jinsi gani anaweza kutumia vyakula bora ili asweze kuwana unene wa tumbo usio kuwa wa lazima,
Waziri wa elimu na mafunzo dk,Shukuru Kawambwa (wa nne kutoka kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu kutoka vyuo vikuu nchini walipokutana jijini Arusha kwenye ukumbi wa Naura kwa lengo la kujadili na kubadilishana mawazo juu ya kuendeleza elimu ya juu,na kujadili ni jinsi gani ya kutatua changamoto zinazojitokeza katika sekta ya elimu ya juu nchini.
Makamu wa Rais wa Tanzania dk,Ghalibu Bilali akiweka udongo kwenye shimo la mti uliopandwa kwa ishara ya kumbukumbu,wakti alipokuwa katika ofsi za jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.
Watoto yatima katika kituo cha Ndoombo wakiwa wanakula chakula kilicholetwa na wafadhili kwa kusimamiwa na Bi Fiona Pamoja na mke wa Naibu waziri bi Antonia,huku watoto wakifurahiwa siku hiyo
Mke wa Naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi na ni mbunge wa Arumeru M agharibi Goodluck Ole Medeye akiwa kwenye kituo cha akina mama kuwatembelea kinachojishuhulisha na ujasiliamari kilichop Sekei kinaitwa Ndimokiroti.wa kwanza kutoka kulia na mmoja wa wafadhili kwa jina la Fiona
Bi Antonia wa kwanza kutoka kulia aliyevalia nguo ya kitenge na mkoba mweupe ambaye ni Mke wa naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi na ni mbunge wa Arumeru Magharibi ,Gudluck Ole Medeye akiwa na watoto yatima wa kituo cha Ndoombo kilichopo wilayani Arumeru huku akiwa ameambatana na wafadhili kutoka New yourkbaada ya kufika kuwatembelea watoto hao na kuwapatia msaada wamahitaji mbalimbali.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha bi Spora Liana akipongezwa na Waziri wa maji prf,Jumanne Magembe mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya vitendea kazi kwa kumkaribisha katika bodi mpya ya maji ya AUWSA jijini Arusha.
Kikundi cha akina mama jijini Arusha wakitumbuiza nyimbo zao za kumkaribisha waziri wa maji prf,Jumanne huku wakicheza kwa madaha na kwa shangwe na vigelegele mara baada ya kufika jijini Arusha katika idara ya maji (AUWSA) katika uzinduzi wa bodi mpya ya majiji na kuiaga bodi ya zamani.
Waziri wa maji Prf,Jumanne Magembe wa pili kutoka kulia,akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi watendaji wa idara ya maji AUWSA,waliosimama nyuma yake,mara baada ya uzinduzi wa bodi mpya jijini Arusha,Na wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa,wa kwanza kutoka kushoto ni mkurugenzi wa AUWSA bi Ruth koya,na wa pili kutoka kushoto ni mbunge mstaafu wa jiji la Arusha mjini Felix Mrema.
Katibu wa chama cha waandishi wa habari jijini Arusha bw,Sefu wa kwanza kutoka kulia akisalimiana na mbunge mstaafu wa Arusha mjini bw,Felix Mrema,na wa kwanza kutoka kushoto ni katbu tawala wa Mkoa mstaafu wa jiji la Arusha bw,Joshua kileo.
Baadhi ya wafanyakazi wa idara ya maji jiji la Arusha AUWSA wakitoa vipulizio kwenye box huku wakivirusha hewani ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa bodi mpya,mbele yao ni Waziri wa maji prf,Jumanne Magembe akifurahia jinsi vipulizio vinavyruka hewani.
Waziri wa maji prf,Jumanne Magembe akiwasisitiza watumishi wa idara ya maji AUWSA kuhusu kuwa makini na kutenga eneo yenye vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuwa makini katika kuhakikisha miji hayapotei,wakati wa siku ya kuzindua bodi mpya na kuaga bodi inayomaliza muda wake iliyofanyika jijin Arusha kwenye ofsi za Auwsa
Mkurugenzi wa AUWSA bi,Ruth Koya akisoma hotuba mbele ya Waziri wa maji wakati wa kuzindua bodi mpya na kuaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika katika ukumbi wa ofsi za AUWSA jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyakaziwa idara ya maji AUWSA jijini Arusha wakiwa wamekaa na kumsikilza Waziri wa maji Prf,Jumanne Mahenga wakati wa hotuba yake katika siku ya uzinduzi wa bodi mpya,wa pili kutoka kulia ni Mhasibu katika idara hiyo ya maji kwa jina la ADAM
Waziri wa maji Prf,Jumanne Magembe wa kwanza kutoka kulia akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa maji AUWSA bi, Ruth koya wa kwanza kutoka kushoto wakiwa na wanazungumza jambo fulani huku wakifuatwa nyuma na wajumbe wa bodi ya maji wakielekea ukumbi wa Auwsa jijini Arusha, ikiwa ni siku ya kuzindua bodi mpya na kuaga bodi iliyomaliza muda wake .
waziri wa maji Jumanne Magembe mbele kabisa (katikati)ambae yuko karibu na bendera akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika kwenye ofsi za AUWASA jijini Arusha huku akiwa na na wajumbe wa bodi ya maji
Waziri wa maji Jumanne Magembe akielekea ofsini ofsini baada ya kurejea kwenye eneo la ofsi za idara ya maji Auwasa nyuma yake ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa.
waziri wa maji Jumanne Magembe akisalimiana na mwenyekiti wa bodi na ni mbunge mstaafu wa Arusha mjini kwa jina la Felix Mrema,baada ya kuwa amefika katika ofsi za idara ya maji wakati wa siku ya uzinduzi wa bodi mpya na kuaga bodi mpya iliyomaliza muda wake.
-
[image: SPORT AND THE SUSTAINABLE DEVELOPMENT]
*The United Nations* have long recognized, advocated for and supported the
important contributions of spor...
Munere veritus fierent cu sed, congue altera mea te, ex clita eripuit evertitur duo. Legendos tractatos honestatis ad mel. Legendos tractatos honestatis ad mel.
, click here →