Friday, 4 October 2013

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU NYEREMBE MUNASA AKITOA USHAURI KWA MADREVA TOYO

Mkuu wa wilaya ya Arumeru bw,Nyerembe Munasa akitoa ushauri kwa waendesha toyo kuendesha toyo zao kwa umakini pale wanapokuwa barabarani ili kuondokana na ajali zisizo kuwa za lazima hapa nchini.

Munasa alisema hayo katika uwanja wa sheikh amri Abed Arusha  ikiwa  ni week ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa.

Alisema kuwa kuna baadhi ya waendesha toyo ambao wamekuwa wakisababisha ajali kwani wengi wao huendesha toyo wakiwa wamelewa pombe hata madawa ya kulevya jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria.

Alisisitiza kwamba wale wote ambao wataenda kinyume na sheria watakamatwa na kuchukuliwa sheria.
Categories:

0 comments: