Adbox
Showing posts with label habari kijamii. Show all posts
Showing posts with label habari kijamii. Show all posts

Friday, 29 August 2014

MMILIKI WA HOTEL YA SNOCREST ATAKIWA KULIPA ZAIDI YA BILIONI 3

8/29/2014 01:33:00 am

PICHA YA MUONEKANO WA HOTEL YA SNOW CREST

Mahakama kuu nchini kitengo cha biashara kanda ya Arusha imemuamuru mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa ndani ya hoteli hiyo.


Mbali na agizo hilo mahakama hiyo pia imeagiza washtakiwa wanne kati ya watano katika kesi hiyo  walipe  kiasi cha riba cha asilimia 4 ya fedha hizo  tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo na kiasi kingine cha asilimia 7 tangu kufungwa kwa shauri hilo hadi siku ya malipo.


Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Robert Makaramba mbele ya mahakama hiyo mara baada ya kueleza kuridhika na ushahidi uliowailishwa na upande wa mlalamikaji kupitia kwa wakili wake Melkizedek Lutema.


Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa nambari 9 ya mwaka 2012 Ndika alieleza kutapeliwa jumla ya $ 1.7 milioni  sawa na sh,3 bilioni baada ya kupatiwa hati mbili za eneo la hoteli hiyo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba eneo la hoteli hiyo lina hati tatu.


Katika hati ya madai mlalamikaji anadai kuwa hati moja kati ya tatu ilikuwa na mkopo wenye riba wa kiasi cha sh,1.5 bilioni kupitia benki mojawapo hapa nchini na baada ya kugundulika hilo ilikwamisha biashara ya mauziano ya hoteli hiyo.


Kwa mujibu wa nakala ya hukumu iliyosainiwa na Jaji Makaramba washtakiwa watano katika kesi hiyo mshtakiwa wa kwanza ,Wilfred Tarimo,Derick Tarimo,Doreen Tarimo ambaye ni mke wa mshtakiwa wa kwanza Irene Tarimo pamoja na kampuni ya Snowcrest And Wildlife Safaris Ltd  wameamriwa kumlipa Ndika fedha hizo pamoja na kiasi cha riba hadi tarehe ya kukazia hukumu.


Mbali na agizo hilo washtakiwa wote katika kesi hiyo pia waliamriwa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo  tangu ilipoanza kuunguruma huku wakipewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30  tangu hukumu hiyo ilipotolewa.


Akihojiwa jijini Arusha wakili wa upande wa mlalamikaji,Lutema alisema kuwa wao wameridhika na hukumu hiyo na kwa sasa wanajiandaa kuwasilisha gharama za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza kuunguruma mnamo Januari 5 mwaka 2012.

Friday, 25 July 2014

WAZEE WA MILA WAKISHIKILIA MAJANI YA BARAKA

7/25/2014 09:26:00 pm
Meneja wa Shirika la Esirwa Richard Ndoros akiwaonyesha wananchi wake Barua ya usajili wa Shirika hilo kwa ajili ya kuanza kazi ya kuleta maendeleo katika kijiji cha Esirwa Wilayani Ngorongoro
Ni Baadhi ya akina mama jamii ya wamasai katika kijiji cha Esirwa wakitumbuiza nyimbo zao wakati wa sherehe za kumkaribisha kijana wao Richard Ndorosi kuanzisha  Shirika la Esirwa kijijini hapo kwa ajili ya kuleta maendeleo.

VIJANA WA KIMASAI WAKIIMBA NA KUCHEZA

7/25/2014 09:05:00 pm
Hawa ni Baadhi ya Vijana wa Kimaasai katika Kijiji cha Eswira Kata ya Gelai kilichpo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiimba na kucheza wakati wa sherehe za kumkaribisha mmoja wa wanakijiji Richard Ndorosi kwa kuweza kuanzisha Shirika la Esirwa kwa ajili ya kunusuru kijiji hicho kutokana na changamoto za Kimaendeleo zinazowakabili kijijini hapo ambapo imepelekea wakazi jamii ya wamasai kuteseka kwa muda mrefu bila kupatiwa msaada.

Sunday, 10 November 2013

WANANCHI WA KIJIJI CHA SAMARIA WAKISALIMIANA NA MBUNGE WAO NAKUTOA SHUKRANI

11/10/2013 04:30:00 pm
Wananchi wakijiji cha Samaria walayani Arumeru Mashariki wakisalimiana na Mh,mbunge wao Joshua nasari mara baada ya kumaliza kuchangisha Harambee kwa Ajili ya uchimbaji wa visima vya maiji.

Wananchi hao walisema wanamshuru sana Mbuge huyo kwa ujio wake pamoja na kuchangia ujenzi wa visima vya maji kwamba ni dhiki kubwa wamekumbana nayo katika kukosa maji.

Walisema kuwa na zaii ya miaka 100 hawajawahi kupata maji katika kijiji chao hivyo hutumia umbali wa masaa nane kwenda na kurudi jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa sana katika maisha yao.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho bi Ndeshukurwa Andrea Mbise akielezea kwa masikitiko makubwa sana alisema kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji limepelekea wengi wao kuishi bila kuoga ama kuoga mara moja kwa wiki kwani maji yamekuwa ni ya shida hivyo kutengewa kwa ajili ya mapishi tu ya nyumbani.

Pia alisema kwamba tatizo hilo limepelekea kufeli mitihani kwa watoto wao mashuleni kwani ile mida ya asubuhi hulazimika kwenda kuchota maji badala ya kwenda shuleni,na ule muda wanaotoka wanakuwa wamechokakitendo cha kuwafanya washindwe kusoma,ambapo huku wazazi wao wakiwa mashambani na sokoni kwa ajili ya kuwatafutia kitoweo.

Alimalizia kwa kusema kwamba wanamshuru sana Mh,Mbunge Nasari kwa kuja kijijini kwao kwa ajili ya Harambee ya kuchangia uchimbaji wa visima na kwamba kupitia hatua hiyo wataondokana na Hadha hiyo ambayo ni kero kubwa kwao.

Katika harambee hiyo ela iliyopatikana ni kiasi cha shilingi zaidi ya milion kumi na mbili 12.

Thursday, 24 October 2013

MENEJA WA KIMAHAMA AKIELEZEA UMUHIM WA KUSOMA VITABU.

10/24/2013 08:36:00 am
Bw,Emmanuel Absolum ambaye ni meneja wa duka la vitabu la Kimahama akieleza umuhimu wa wananchi kujisomea vitabu.

Amesema kuwa kupitia vitabu unapata elimu juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi kwa mambo ambayo mwananchi hayajui.

Akielezea lengo la kufungua duka hilo amesema kuwa ni kuwasaidia wakazi wa jiji la Arusha kupata elimu kupitia vitabu sambamba na kujijengea mazoea ya kusoma ujuzi na ufanisi katika kutambua mambo mbalimbali.

MENEJA WA KIMAHAMA AKIWA KWENYE DUKA LA VITABU

10/24/2013 08:21:00 am
Meneja wa kimahama Emmanuel Absalom akiwa amesimama kwenye duka la vitabu lililo zinduliwa upya na Mkuu wa chuo Habari maalum bw,Jackson Kaluzi, baada ya kuboreshwa na kuwekwa vitabu mbalimbali vya kuvutia ambapo vitabu hivyo ni kama Biblia,vitabu vya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na vingine vingi vya kuelimisha jamii.

Monday, 7 October 2013

WALIMU WA FURAHA FOUNDATION NA WAZIRI WA MALI ASILI

10/07/2013 07:38:00 pm
Walimu wawili wa Shule ya Furaha foundation waliosimama pembeni kushoto wakiwa kwenye picha na Waziri wa mali asili na utalii Hamis Kagasheki ambaye amesimama kulia akiwa ameshikilia zawadi aliyopewa na walimu hao kwa uwakilishi wa shule ya Furaha foundation,mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo ilikuwa siku ya kuazimisha wanyama Duniani.

Saturday, 5 October 2013

MKURUGENZI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA UTAFITI WA TEMBO AKISISITIZA JAMBO

10/05/2013 01:45:00 pm
Dr Alfred Kikoti ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa Tembo(world Elephant Centre)akiwaelezea wananchi wa jiji la Arusha kuwa pale watakapowabaini majangiri wanao waua Tembo wawekwe kwenye website,mitandao ikiwa njia mojawapo ya kuwafichua majangiri hao.

Dk Alfred aliyasema hayo kwenye uwanja wa Aicc mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo kauli mbiu yao ilikuwa ni ''kila baada ya dk kumi na tano tembo anauwawa ''na kwamba kama hali itaendelea hivo baada ya miaka kumi na mbili Tanzania hatutakuwa na Tembo.

Alisema Tembo ni sawa na binadamu,meno ya tembo,pembe za ndovu wasivitumie kama biashara ni kwa ajili ya tembo,hivyo kujitahidi kukataa biashara haramu ya pembe za ndovu na kila Mtanzania kusema ''hapana''

                                                          

Friday, 4 October 2013

Adbox