Adbox
Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Friday, 22 August 2025

TBN Yajumuika na Viongozi wa Habari Kuelekea Uchaguzi 2025

8/22/2025 12:12:00 pm


IMG-20250821-WA0061
Dar es Salaam, Agosti 21, 2025: 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi, ametaja majukumu makuu matano ambayo sekta ya habari nchini inapaswa kuyatekeleza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akisisitiza umuhimu wa taaluma, weledi na maadili katika kuripoti.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Profesa Kabudi alisema vyombo vya habari ni mhimili muhimu katika kukuza demokrasia na kulinda amani wakati wa uchaguzi.

“Vyombo vya habari vinapaswa kuhakikisha wananchi wanajua haki na wajibu wao, kutoa elimu juu ya sera za wagombea, kufuatilia ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, kuhamasisha ushiriki wa makundi maalum kama vijana na wanawake, na kupambana na taarifa potofu badala ya kuzisambaza,” alisema Profesa Kabudi.

IMG-20250821-WA0057
IMG-20250821-WA0059

Aidha, alisisitiza kuwa utekelezaji wa majukumu hayo lazima uongozwe na misingi ya taaluma na maadili ya uandishi wa habari ili kulinda heshima ya tasnia na kuepusha vurugu au uvunjifu wa amani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Wakili Patrick Kipangula, alikumbusha waandishi wa habari kuhakikisha wanakuwa na ithibati kabla ya kufanya kazi za kihabari, hususan katika kuripoti uchaguzi.
IMG-20250821-WA0028
IMG-20250821-WA0031
IMG-20250821-WA0030

“Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari kinasema bayana kuwa mtu yoyote anayetaka kufanya kazi ya uandishi ni lazima awe amepewa ithibati na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari. Hivyo ni kosa la jinai kwa mwandishi wa habari kufanya kazi bila ithibati,” alisema Kipangula.

Aliongeza kuwa uhalali wa waandishi wa habari katika kipindi hiki ni jambo lisiloweza kupuuzia, kwani tasnia hiyo inahusisha majukumu makubwa yanayoathiri utulivu wa taifa.
IMG-20250821-WA0046(1)
Mkutano huo uliwahusisha wadau mbalimbali wa sekta ya habari na utangazaji, ambao walijadili nafasi ya vyombo vya habari katika kulinda maadili ya kitaifa na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
IMG-20250821-WA0058
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Mwaluko Kabudi (wa nne kutoka kushoto waliokaa), akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wadau wa sekta ya habari na utangazaji baada ya kufungua Mkutano wa Wadau wa Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Patrick Kipangula, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Mbuya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Gerson Msigwa, pamoja na Kamishna na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam. 

Waliosimama nyuma ni viongozi wa Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) akiwemo Muhidin Issa Michuzi (Mdhamini), Mwenyekiti wa TBN Beda Msimbe, Mjumbe Joachim Mushi na Mweka Hazina ambaye pia ni Mtaalamu wa Habari, Cathbert Kajuna.

Tuesday, 29 July 2025

WATOTO WATANO WAMEFARIKI DUNIA KWA MOTO TABORA

7/29/2025 07:56:00 pm

 







NA LUCAS RAPHAEL,TABORA 


Watoto watano wamefarikia dunia wengine 17 wamenusurika kifo baada ya kuwaka kwa bweni la wasichana  kwa kushika  moto katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Igambilo kilichapo kata ya Misha  manispaa Tabora Mkonia hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurungezi wa kituo hicho na mwasisi wake Halima Laswai alisema kwamba kituo tukio lilitokea mida ya saa 5 usiku baada ya kudai kutokea shot ya umeme.  

Alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa hiyo alipinga simu kituo cha kizima moto na kutoa ushiriiano kwa ajili ya kuzima moto huo.

Alisema kwamba wakazi wa kijiji hicho cha misha walifanya kazi kubwa kwa ajili ya kuzima moto na kuokoa vitu mbalimbali vilivyokuwepo eneo hilo.

Alisema kwamba Chanzo kilikuwa  umeme unawake na kuzima kisha balubo moja kupasuka na kutoa cheche zilizoangukia kwenye moja ya godoro kwenye kitanda na kuzalisha moto uliosambaa .

Halima alisema kwamba vitu mbalimbali vimeteketea na moto vikiwemo vyakula ambavyo vilikuwa upande wa bweni hilo lillilo shika moto.

Alisema vingine ni vifaa vyote vya shule walivyokuwa wanatumia watoto hao kwa ajili ya maosmo vikimo madfutari na sare ,kwani wengi ya watoto wanasoma shule za msingi.

“Watakwenda kuomba uongozi wa shule ya msingi ili watoto hao waweze kutumia nguo za nyumbani kwa ajili ya kuendelea na masomo yao hasa wale walipo kwenye madarasa ya mitihani ambayo ni Darasa la saba na Nne”alisema Halima

Mkurungezi huyo aliaendelea kubainishwa kwamba kutokana na hali hiyo wawalifanikiwa kuokoa maguni mawili ya unga na Mwili ya maharagwe.

Aidha wanaomba wasamalia wema kujitoa kwa ajili ya kuwasidia watoto wao ili waweza kurudia katika hali zao za kawaida kwa ajili ya kupatia vifaa vya shule na chakula

Afisa ustawi wa kituo hicho. Mwajuma Hassani alisema kwamba mida hile ya usiku akiwa amelala upande mwingine wa bweni kwenye kituo hicho alsiia watoto wanapinga kelele za kuomba masaa na kusema moto moto.

Alisema ndipo walipotoka kwenda kwenye bweni lililoshika na moto na kuvunja mlango wa geti na kufanikiwa kuwatoa watoto ila moshi ulikuwa ni mwingi sana .

Alisema walibofika faya walianza zozezi la kuzima moto ila kipindi hicho wenyeji wa eneo hilo walikuwepo kuwasaidia kuzima moto huo  

Alisema kwamba bweni hilo lilikuwa na watoto waliokuwa wanalala ni 23 kati yao walifariki ni 5 na 17 wamenurika na ajili hiyo ya moto.

kamanda wa jeshi la zimamotona  uokoaji mkoani Tabora Mohamed Jihad aliwataja walifarikia kuwani Pili Nasoro (5) Nusra Adam (11)Amina Ismail(7)Tatu Sharif (4) Norata Bakari (5)

Alibainisha kwamba tuki hilo limeleta simazi kubwa katika mkoa wa Tabora licha ya hali hiyo tahadhari zinatakiwa kuchyukuliwa ili kuoka majanga kama hayo.

Alisema kwamba ushari unaotolewa na jeshi hilo lnafuta kuchukuliwa kwa umakini mkubwa ili kuweza kupunguza ajili zinazoweza kusabishwa namoto.

Hata hivyo waliwataka wananchi na Taasisi mbali  mbali kuchukua hatua za tadhari kwa kuangali vifaa kinga kama vinafanya kazi ipasavyo  na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo na nyumba za kuishi

kituo hicho ni kiliazishwa mwaka 1997 kikiwa na watoto 7 tu na sasa kituo hicho kinawatoto wapatao 50 ila waliotoka ni wengi ambao wapo sehemu mbalimbali kwa ajili ya elimu ya juu na kati 

Thursday, 24 July 2025

RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA MASHUJAA KESHO JULAI 25 MWAKA HUU

7/24/2025 04:14:00 pm

Na Doreen Aloyce, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mashujaa yatakayofanyika 25 Julai, 2025 katika Viwanja vya Mnara wa Mashujaa vilivyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Akizungumza leo Julai 24 ,2025 Jijini Dodoma na waandishi wa habari jijini Dodoma kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (Mb), amesema maadhimisho hayo ni alama muhimu ya kuenzi mchango wa Watanzania waliojitolea kwa ajili ya uhuru, amani na maendeleo ya Taifa.



 “Siku ya Mashujaa ni siku ya kitaifa inayotukumbusha uzalendo wa mashujaa wetu  waliolinda mipaka ya Taifa, waliopambana kwa ajili ya uhuru na waliotoa sadaka kubwa kwa ajili ya amani tunayoifurahia leo,” amesema Dkt. Biteko.

Ameeleza Maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika, huku akisisitiza kuwa Julai 24, 2025 saa 6:00 usiku, Mwenge wa Kumbukumbu ya Mashujaa utawashwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule kwa niaba ya Rais, kuashiria kuanza kwa siku ya maombolezo ya mashujaa wa Taifa.



Amesema Maadhimisho ya Julai 25 yataanza saa 3:00 asubuhi kwa gwaride rasmi la heshima linaloongozwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Usiku wa siku hiyo, saa 6:00, Mwenge wa Kumbukumbu utazimwa rasmi kuashiria hitimisho la shughuli za maadhimisho kwa mwaka huu.

Mbali na hayo Dkt. Biteko ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika tukio hilo muhimu kwa historia ya Taifa, akieleza kuwa kila Mtanzania anao wajibu wa kutambua na kuenzi mchango wa mashujaa kwa vitendo vya uzalendo, mshikamano na kuchapa kazi kwa maendeleo ya nchi.



“Tunapoadhimisha siku hii, tunapaswa kujiuliza: Je, sisi kama kizazi cha sasa tunaendeleza misingi waliyoiacha mashujaa wetu? Ushujaa hauishii vitani pekee, bali uko katika kila tendo jema kwa Taifa letu,” amesisitiza.

Amevitaka vyombo vya habari, wanahabari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kushirikiana na Serikali katika kuelimisha umma kuhusu maana, historia na umuhimu wa Siku ya Mashujaa.

“Hii ni siku ya kumkumbuka Mtanzania mwenzetu aliyesimama kwa ajili ya wengine,tuwaambie watoto wetu maana ya ushujaa, thamani ya kujitolea, na umuhimu wa kupenda Taifa lao,” amesema Dkt. Biteko.

Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa hufanyika kila mwaka nchini kote kama njia ya kuenzi maisha, mchango na maono ya waliolinda uhuru wa Taifa, na mwaka huu 2025, Serikali imepanga kuyafanya kwa heshima, uzito na mshikamano wa hali ya juu.

=MWISHO=

Sunday, 24 July 2016

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ALIPOTEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI

7/24/2016 01:19:00 am


 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya kuanza kutumika hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)

Tuesday, 16 February 2016

OFA YA UPENDO KUTOKA HUAWEI MSIMU HUU WA VALENTINE

2/16/2016 06:12:00 pm
Mabalozi wa Huawei wakipozi siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakipata picha ya ukumbusho na balozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa wateja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wateja walioshiriki katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Kushoto) akimkabidhi Mteja mfuko wa zawadi pamoja na kadi katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3   inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki hii, Mlimani City Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa mabalozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam. 

Na Mwandishi wetu, 
Kampuni ya simu ya Huawei, inayoshika nafasi ya tatu kwa utengenezaji na uuzaji wa simu za mkononi ulimwenguni imezindua promosheni ya Valentine ya muda wa wiki 3 inayohusisha vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji zawadi kwa wanunuzi wa simu za Huawei kutoka kwenye maduka yao mbalimbali ya rejareja yaliyosajiliwa.
Promotion hiyo itahusisha simu kuu mbili ambazo ni Huawei P8 na Huawei G8. Zawadi zinazotolewa kwa wateja ni pamoja na “selfie sticks, spika za Bluetooth na T-shirts. Pamoja na zawadi zote hizo ,wateja hao pia wanapewa fursa ya kupata picha nzuri za kumbukumbu ili waweze kuzitumia kwenye mitandao ya kijamii kama instagram na mingine.
Kampeni hii Iliyozinduliwa wikiendi hii mjini Dar es Salaam eneo la  Mlimani City, inawaahidi wateja wa Huawei kuona thamani ya pesa yao kutokana na zawadi watakazopatiwa .
Kwa mujibu wa report ya simu za mkononi ya hivi karibuni nchini Tanzania ilivyochapishwa mwaka jana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya watanzania wanaotumia simu za mkononi, waliojisajili imeongezeka kwa asilimia 16 kwa mwaka 2014 kufikia milioni 31.86 hiyo ni sawa na asilimia 67 kwa watanzania wote wanaotumia simu.
Huawei Tanzania wanaahidi kuendelea kutatua uhitaji wa wateja wao kwa kuwapatia   simu zenye ubora wa hali ya juu na orijino.
Tunatarajia kutoa huduma bora ya mawasiliano na intanet kwa bei nafuu kwa wananchi na pia kuwazawadia wateja wetu wale wazamani na wapya,  vifaa bora na vya kisasa vitakavyoweza kuongeza wigo katika matumizi ya simu zao za smatiphone  na intaneti pia” alisema Bw. Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania katika uzinduzi wa Promotion hiyo.
Akielezea promosheni hiyo, Bw. Peter Zhangjunliang alisema; promosheni hii ya wiki 3 ni ya nchi nzima na ipo wazi kwa watanzania wote watakao nunua simu za G8 na P8 kutoka Huawei.”

Huawei, rafiki yako kwa simu origino.

Kuhusu Huawei
Kampuni ya Huawei imejizatiti katika kutengeneza bidhaa bora kwa matoleo tofauti ulimwenguni, kutoa huduma rafiki za simu, kwenye intaneti kwa wateja wake. Kampuni ya Huawei inajulikana duniani katika utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti na vifaa vya majumbani.
Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2015, bidhaa vya Kampuni ya Huawei zinapatikana  zaidi ya nchi 150 ulimwenguni kote. Huawei ni kampuni ya 3 katika usambazaji wa simu (2015) ikiwa imesambaza zaidi ya milioni 100 ulimwenguni. Kampuni ya Huawei imeanzisha ushirikiano  na makampuni makubwa duniani kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom. 
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea www.huaweidevice.com

Monday, 25 May 2015

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CHADEMA ,JAFARY MICHAEL AFUNGUA MATAWI MAPYA MOSHI

5/25/2015 03:48:00 pm

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema na meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi katika kata ya Longuo mjini Moshi.
Ofisi mpya ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Longuo B .
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema taifa na meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael akikata utepe kufungua ofisi mpya ya kata ya Longuo B.
Meya Michael akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kufungua ofisi ya kata ya Chadema.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema akitia saini katika kitabu cha wageni wakati wa ufunguzi wa ofisi ya kata ya Longuo B.
Diwani wa kata ya Longuo B,Ray Mboya akitia saini katika kitabu hicho.
Baadhi ya makada wa Chadema manispaa ya Moshi wakishuhudia zoezi hilo.
Ofisi mpya ya Chadema kata ya, Longuo  manispaa ya Moshi ikafunguliwa rasmi.

Na Dixon Busagaga .

Wednesday, 12 November 2014

Mkutano wa TCRA na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wafanyika jijini Dar

11/12/2014 11:11:00 am

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Prof. John Nkoma akitoa hotuba yake wakati wa ufungumzi wa Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.Picha na Othman Michuzi.
Inginia Andrew Kisaka akitoa Mada katika  Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali katika wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini.
Sehemu ya Maafisa wa TCRA wakiwa kwenye Mkutano huo.
Moja ya Mada zinazoendeleo kutolewa katika Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Assah Mwambene akitoa hotuba yake wakati  akifunga Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania uliokuwa na lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,unaoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wanablog waliohudhulia Mkutano huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Mabel Masasi akizungumza katika Mkutano huo.
Baadhi ya Wanalibeneke wakiendelea kuuliza maswali mbali mbali katika mkutano huo.
Mdau Josephat Lukaza na Dada Shamim Mwasha wakiwa mkutanoni hapo.
Prof. John Nkoma akijibu maswali ya wanablog.

Mdau Fred Njeje akidaka taswira.

Mkutano ukiendelea.
Mdau Henry Mdimu akitoa hoja.
Mdau akitafakari kabla ya kuuliza swali.
Wanablog kazini.


Adbox