Adbox
Showing posts with label habari dini. Show all posts
Showing posts with label habari dini. Show all posts

Thursday, 24 October 2013

Tuesday, 8 October 2013

VIONGOZI WA TYCC WAKISOMA RISALA

10/08/2013 09:35:00 pm
Mwanafunzi ambaye ni Mmoja wa viongozi wa Tyccc kanda ya Tanga kwa jina la Douglos Gasper aliyevalia miwani(wa kwanza kutoka kushoto)ambaye pia ni mhazini wa kikundi hicho,akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kidato cha nne yaliyofanyika katika ukumbi wa Magreth Hall uliopo jijini Tanga.

Kiongozi huyo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi pamoja na kadamnasi iliyokuwepo kwenye mahafali hayo ambapo alielezea changamoto wanazokumbana nazo katika kuendesha kikundi chao wakiwa shuleni.

Gasper alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakizuiliwa na uongozi wa shule katika suala zima la kuendesha vipindi vyao dini ikiwemo kuimba kwaya wawapo mashuleni  huku walimu hao wakitumia vipindi hivyo kufundisha masomo mengine jambo ambalo limepelekea wanafunzi wengi kutokuwa na hofu ya Mungu hata kutofahamu kabisa neno la Mungu.

Pia alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili katika utendaji kazi wao ni ufinyu wa kipato kwani hawana biashara yoyote hivyo kulazimika kutoa ela zao mifukoni pale kunapokuwa kumehitajika utatuzi wa jambo fulani na kwamba hali hiyo imepelekea shughuli zao kutokwenda kwa ufanisi.

Waliiomba serikali na uongozi wa dini ya kikristo kuwapa msaada pale watakapokuwa wanahitji msaada ikiwa ni pamoja na kuwawekea walimu wa dini kwenye shule zao ili kuweza kuepukana na tatizo lililokihtiri la kufeli masomo ya dini ya kikristo tofauti na dini nyingine.

Saturday, 5 October 2013

WANAFUNZI WA TYCC KANDA YA TANGA WAKIPEWA USHAURI NA MGENI WAO RASMI BW,AMOS MOMBO

10/05/2013 10:19:00 pm
Wanafunzi wa dini ya katoliki(TYCC) kutoka shule mbalimbali za kanda ya Tanga wakiwa wanamsikiliza katibu mstaafu wa kwaya ya st,Antony Tanga kwa jina la Amos Mombo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kuhitimu kidato cha nne,ambapo mahafali hayo yalifanyika katika ukumbi wa Magreth hall(ridoch)uliopo jijini Tanga. 

Aidha bw,Amos aliwashauri kuwa ufuatia kuchafuka kwa dunia vijana wamekuwa wakijiingiza katika tabia mbaya na kusahau amri za Mungu hivyo wajitahidi kuepukana nazo kwa kuwekw sala mbele za Mungu.

Pia alisema kuwa wanapaswa kushikamana kwa mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kuepukana na makundi yasiyo kuwa na tija kwa jamii kwani kuna baadhi ya makundi sio mazuri ambayo ujihusisha na masuala ya madawa ya kulevya na kutomjua Mungu. 

Thursday, 3 October 2013

Adbox