Thursday, 3 October 2013

PINDA AKISISIZA VIONGOZI KUTOPOKEA RUSHWA

Waziri mkuu Mizengo Piter Pinda akitoa ufafanuzi kwamba kuna baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakikwamisha suala zima la uwekezaji kutokana na tamaa yao mbaya ya kutaka kitu kidogo yaani Rushwa hivyo wawekezaji kukata tamaa na kushindwa kuwekeza na kwamba atakaye bainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.


Pinda  aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa minne Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Tanga,ambapo lilofanyika Mkoani Tanga katika Hotel maarufu Mkonge ambapo kongamano hilo lilijumuisha viongozi wote wa ngazi ya wilaya,wakuu wa mikoa pamoja na wawekezaji.


Categories:

0 comments: