Sunday, 10 November 2013

WANANCHI WA KIJIJI CHA SAMARIA WAKISALIMIANA NA MBUNGE WAO NAKUTOA SHUKRANI

Wananchi wakijiji cha Samaria walayani Arumeru Mashariki wakisalimiana na Mh,mbunge wao Joshua nasari mara baada ya kumaliza kuchangisha Harambee kwa Ajili ya uchimbaji wa visima vya maiji.

Wananchi hao walisema wanamshuru sana Mbuge huyo kwa ujio wake pamoja na kuchangia ujenzi wa visima vya maji kwamba ni dhiki kubwa wamekumbana nayo katika kukosa maji.

Walisema kuwa na zaii ya miaka 100 hawajawahi kupata maji katika kijiji chao hivyo hutumia umbali wa masaa nane kwenda na kurudi jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa sana katika maisha yao.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho bi Ndeshukurwa Andrea Mbise akielezea kwa masikitiko makubwa sana alisema kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji limepelekea wengi wao kuishi bila kuoga ama kuoga mara moja kwa wiki kwani maji yamekuwa ni ya shida hivyo kutengewa kwa ajili ya mapishi tu ya nyumbani.

Pia alisema kwamba tatizo hilo limepelekea kufeli mitihani kwa watoto wao mashuleni kwani ile mida ya asubuhi hulazimika kwenda kuchota maji badala ya kwenda shuleni,na ule muda wanaotoka wanakuwa wamechokakitendo cha kuwafanya washindwe kusoma,ambapo huku wazazi wao wakiwa mashambani na sokoni kwa ajili ya kuwatafutia kitoweo.

Alimalizia kwa kusema kwamba wanamshuru sana Mh,Mbunge Nasari kwa kuja kijijini kwao kwa ajili ya Harambee ya kuchangia uchimbaji wa visima na kwamba kupitia hatua hiyo wataondokana na Hadha hiyo ambayo ni kero kubwa kwao.

Katika harambee hiyo ela iliyopatikana ni kiasi cha shilingi zaidi ya milion kumi na mbili 12.
Categories:

0 comments: