Matukio mbalimbali yakimuonesha Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma Mchungaji Stanley Tabulu akikagua jengo la utawala Shule ya Sekondari Embeko iliyopo Jimbo la Kondoa Dayosisi ya Dodoma.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa Jesho hilo Mchungaji Tabulu ameupongeza uongozi wa Shule chini ya Mkuu wa shule hiyo ,l Christian Siara kwa usimamizi mzuri wa mradi huo kwa weledi Mkubwa.
Aidha amesema kuwa Uongozi wa Dayosisi upo nao bega kwa bega katika kulijenga Taifa ambapo ameahidi kupitia Ofsi ya Dayosisi watahakikisha wanaunga mkono jitihada zao za ujenzi wa jengo hilo.
Nae Mkuu wa shule ya Sekondari Embeko Mwalimu Christian Siara amesema ujenzi huo ambao umefikia hatua ya lenta ni nguvu ya shule bila kutegemea michango kutoka nje ya nchi.
amesema kumalizika kwa jengo hilo itakuwa faraja kwa walimu na wanafunzi kwani ni jengo la kisasa ambalo limekidhi vigezo vyote na litasaidia kufanya kazi katika mazingira rafiki.





No comments:
Post a Comment