PICHA YA MUONEKANO WA HOTEL YA SNOW CREST
Mahakama kuu nchini kitengo cha
biashara kanda ya Arusha imemuamuru mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa
hoteli ya Snowcrest ya jijini Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake
kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya
Grand Alliance Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa
ndani ya hoteli hiyo.
Mbali na agizo hilo mahakama hiyo pia
imeagiza washtakiwa wanne kati ya watano katika kesi hiyo walipe
kiasi cha riba cha asilimia 4 ya fedha hizo tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo na kiasi
kingine cha asilimia 7 tangu kufungwa kwa shauri hilo hadi siku ya malipo.
Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa mwishoni
mwa wiki iliyopita na Jaji Robert Makaramba mbele ya mahakama hiyo mara baada
ya kueleza kuridhika na ushahidi uliowailishwa na upande wa mlalamikaji kupitia
kwa wakili wake Melkizedek Lutema.
Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa
nambari 9 ya mwaka 2012 Ndika alieleza kutapeliwa jumla ya $ 1.7 milioni sawa na sh,3 bilioni baada ya kupatiwa hati
mbili za eneo la hoteli hiyo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba eneo la
hoteli hiyo lina hati tatu.
Katika hati ya madai mlalamikaji
anadai kuwa hati moja kati ya tatu ilikuwa na mkopo wenye riba wa kiasi cha
sh,1.5 bilioni kupitia benki mojawapo hapa nchini na baada ya kugundulika hilo
ilikwamisha biashara ya mauziano ya hoteli hiyo.
Kwa
mujibu wa nakala ya hukumu
iliyosainiwa na Jaji Makaramba washtakiwa watano katika kesi hiyo
mshtakiwa wa
kwanza ,Wilfred Tarimo,Derick Tarimo,Doreen Tarimo ambaye ni mke wa
mshtakiwa
wa kwanza Irene Tarimo pamoja na kampuni ya Snowcrest And Wildlife
Safaris Ltd wameamriwa kumlipa Ndika fedha hizo pamoja na kiasi
cha riba hadi tarehe ya kukazia hukumu.
Mbali na agizo hilo washtakiwa wote katika
kesi hiyo pia waliamriwa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza kuunguruma huku wakipewa
nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30
tangu hukumu hiyo ilipotolewa.
Akihojiwa jijini Arusha wakili wa
upande wa mlalamikaji,Lutema alisema kuwa wao wameridhika na hukumu hiyo na kwa
sasa wanajiandaa kuwasilisha gharama za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza
kuunguruma mnamo Januari 5 mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment