Adbox

Saturday, 5 October 2013

Friday, 4 October 2013

MKUU WA MKOA AKIPEWA ZAWADI

10/04/2013 09:51:00 pm
Mkuu wa Mkoa wa Arusha bw,Magesa Mlongo wa kwanza kutoka kulia akikabidhibiwa zawadi na ofsi za Tato mara baada ya kumaliza maandamano ya amani ya utembezi wa tembo kitaifa, ambapo jijini Ausha maadamano hayo yameanzia katika ofis za Tanapa na kuishia kwaenye viwanja vya AICC njiro.

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU NYEREMBE MUNASA AKITOA USHAURI KWA MADREVA TOYO

10/04/2013 08:49:00 pm
Mkuu wa wilaya ya Arumeru bw,Nyerembe Munasa akitoa ushauri kwa waendesha toyo kuendesha toyo zao kwa umakini pale wanapokuwa barabarani ili kuondokana na ajali zisizo kuwa za lazima hapa nchini.

Munasa alisema hayo katika uwanja wa sheikh amri Abed Arusha  ikiwa  ni week ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa.

Alisema kuwa kuna baadhi ya waendesha toyo ambao wamekuwa wakisababisha ajali kwani wengi wao huendesha toyo wakiwa wamelewa pombe hata madawa ya kulevya jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria.

Alisisitiza kwamba wale wote ambao wataenda kinyume na sheria watakamatwa na kuchukuliwa sheria.

WAENDESHA TOYO WAKIWA KWENYE WEEK YA USALAMA BARABARANI

10/04/2013 08:16:00 pm
Baahi ya waendesha pikipiki alimaarufu kama toyo jijini Arusha wakiwa katika uwanja wa sheikh Amri Abedi huku wakipewa ushauri na Mkuu wa wilaya ya Arumeru bw.Nyerembe Munasa kuhusu kutumia pikipiki zao vizuri ili kuepukana na ajali zisizo kuwa za lazima ambapo ilikuwa ni week ya nenda kwa usalama barabarani.

Thursday, 3 October 2013

PINDA AKISISIZA VIONGOZI KUTOPOKEA RUSHWA

10/03/2013 09:45:00 pm
Waziri mkuu Mizengo Piter Pinda akitoa ufafanuzi kwamba kuna baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakikwamisha suala zima la uwekezaji kutokana na tamaa yao mbaya ya kutaka kitu kidogo yaani Rushwa hivyo wawekezaji kukata tamaa na kushindwa kuwekeza na kwamba atakaye bainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.


Pinda  aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa minne Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Tanga,ambapo lilofanyika Mkoani Tanga katika Hotel maarufu Mkonge ambapo kongamano hilo lilijumuisha viongozi wote wa ngazi ya wilaya,wakuu wa mikoa pamoja na wawekezaji.


Wednesday, 2 October 2013

Monday, 16 September 2013

NESI MSTAAFU AKIMPATIA USHAURI MGONJWA

9/16/2013 10:37:00 pm
Bi Antonia ambaye ni mke wa naibu waziri wa ardhi,nyumba na makazi ambaye pia ni mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye,yeye ni bi Antonia ni Nesi mstaafu katika hosp ya Mkoa jijini Arusha,ambapo baada ya kustaafu ameamua kufungua ofsi yake ya kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwa ni pamoja na kuwapatia ushauri wale wenye unene na kuwapima kwa kutumia mashine maalumu ,na hapa anampatia mmoja wa akina mama katika ofsi yake iliyopo mianzini barabara ya vumbi,ambapo anamueleza ni jinsi gani anaweza kutumia vyakula bora ili asweze kuwana unene wa tumbo usio kuwa wa lazima,

WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBWA KWENYE PICHA YA PAMOJA

9/16/2013 10:05:00 pm
Waziri wa elimu na mafunzo dk,Shukuru Kawambwa (wa nne kutoka kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu kutoka vyuo vikuu nchini walipokutana jijini Arusha kwenye ukumbi wa Naura kwa lengo la kujadili na kubadilishana mawazo juu ya kuendeleza elimu ya juu,na kujadili ni jinsi gani ya kutatua changamoto zinazojitokeza katika sekta ya elimu ya juu nchini.

MAMA OLEMEDEYE AKIWA NA WATOTO YATIMA

9/16/2013 07:16:00 am
Bi Antonia wa kwanza kutoka kulia aliyevalia nguo ya kitenge na mkoba mweupe ambaye ni Mke wa naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi na ni mbunge wa Arumeru Magharibi ,Gudluck Ole Medeye akiwa na watoto yatima wa kituo cha Ndoombo kilichopo wilayani Arumeru huku akiwa ameambatana na wafadhili kutoka New yourkbaada ya kufika kuwatembelea watoto hao na kuwapatia msaada wamahitaji mbalimbali.

WAZIRI WA MAJI PRF,JUMANNE KWENYE PICHA YA PAMOJA

9/16/2013 06:14:00 am
Waziri wa maji Prf,Jumanne Magembe wa pili kutoka kulia,akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi watendaji wa idara ya maji AUWSA,waliosimama nyuma yake,mara baada ya uzinduzi wa bodi mpya jijini Arusha,Na wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa,wa kwanza kutoka kushoto ni mkurugenzi wa AUWSA bi Ruth koya,na wa pili kutoka kushoto ni mbunge mstaafu wa jiji la Arusha mjini Felix Mrema.

Sunday, 15 September 2013

Saturday, 14 September 2013

PROFESA MAHENGA AKISISITIZA JAMBO

9/14/2013 11:31:00 pm
Waziri wa maji prf,Jumanne Magembe akiwasisitiza watumishi wa idara ya maji AUWSA kuhusu  kuwa makini na kutenga eneo yenye vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuwa makini katika kuhakikisha miji hayapotei,wakati wa siku ya kuzindua bodi mpya na kuaga bodi inayomaliza muda wake iliyofanyika jijin Arusha kwenye ofsi za Auwsa

WAZIRI WA MAJI PRF,MAGEMBE AKIELEKEA UKUMBINI

9/14/2013 10:36:00 pm
Waziri wa maji Prf,Jumanne Magembe wa kwanza kutoka kulia akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa maji AUWSA bi, Ruth koya wa kwanza kutoka kushoto wakiwa na wanazungumza jambo fulani huku wakifuatwa nyuma  na wajumbe wa bodi ya maji wakielekea ukumbi wa Auwsa jijini Arusha,  ikiwa ni siku ya kuzindua bodi mpya na kuaga bodi iliyomaliza muda wake .

Wednesday, 11 September 2013

waandishi

9/11/2013 01:29:00 pm
baadhi ya waandishi wa habari mkoani arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiwa wamepumzika wakati wa mechi ya bonanza iliyofanyika katika viwanja vya generally taya iliyopo njiro mkoani arusha.

Saturday, 7 September 2013

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YATOA SEMINA KWA WANAHABARI WA ARUSHA

9/07/2013 06:51:00 pm

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akitoa mada katika Semina ya siku moja, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa ASILI YETU TANZANIA BLOG Bw. Victor Machota akiwa na Gadiola Emanuel mwenyekiti wa Arusha Bloggers Associations na Mkurugenzi wa WAZALENDO 25 BLOG katika Semina ya siku moja iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha. Kwa picha zaidi Bofya hapa>>>

Thursday, 5 September 2013

Wednesday, 4 September 2013

Naibu waziri wa maji dk.Mahenge aongea na wananchi

9/04/2013 11:48:00 pm
 Naibu waziri wa maji Dk.Bilinith Mahenge akihutubia wananchi wa wilaya ya monduli alipokuwa kwenye ziara yake ya maji Mkoani Arusha huku akiwaelezea kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji .

Naibu waziri wa maji DK.Bilinithi Mahenge wa tatu kutoka kushoto aliyevaa koti jeus akitoa maelezo kwa wakandarasi wa kisima katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha mara baada ya kutembelea miradi ya maji wilayani humo.
9/04/2013 11:00:00 pm
bustani ya mboga za majani aina ya kabichi inayomilikiwa na mmoja wa wakulima katika kata ya Themi Njiro ambaye hakupenda kuonekana kwenye picha,ambapo hupata mahitaji yake kupitia mboga hizo.

Kumbu Kumbu ya Kumuenzi Marehemu Daudi Mwangosi

9/04/2013 05:28:00 pm

 Wanahabari  wa  vyombo  mbali mbali na  wadau  wa habari  mkoa  wa  Iringa  wakiwa katika  maandamano ya amani ya  kumuenzi  aliyekuwa mwenyekiti  wa klabu ya  waandishi  wa  habari  mkoa  wa Iringa (IPC) .Picha Zote na Francis Godwin
 Maandamano  ya  wanahabari na  wadau  wa  habari yakipita  eneo la soko kuu la manispaa ya  Iringa.
  Katibu  wa IPC  Francis  Godwin  akiongoza  maandamano ya  wanahabari na  wadau huku akiwa  juu ya gari na picha ya marehemu Daudi Mwangosi.
Adbox