Adbox

Tuesday, 15 July 2014

KATIBU MKUU MAPUNDA AFANYA ZIARA MKOA WA ARUSHA

7/15/2014 10:34:00 am
six14Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akiendelea na ujenzi katika uwanja wa michezo wa st.Benjamin uliopo Usa river kwa ufadhili wa edinburgh global partnerships na YES Tanzania katika ziara yake ya kwanza ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Arusha
six16Aliyevalia sweta ni mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akisalimiana na viongozi wa chama Wilayani hapo ambapo mradi huo umetekelezwa kulia ni Katibu mkuu UVCCM Sixtus Mapunda akifurahia jambo
six17Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akipokelewa na viongozi na wa chama hicho mapema kabla ya kutembelea miradi
 six12Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhi cheti mmoja wa wa vijana waliojitolea katika mradi wa ujenzi wa kiwanja cha michezo
six11Hapa viongozi na wadau wakishuhudia jiwe la msingi katika kiwanja hicho cha michezo kilichozinduliwa rasmi na Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda
six10Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhi cheti mshindi wa mbio za pikipiki greengad maarufu kwa jina la Mjusi.
six9Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akizindua shina la Ngarasero
six8Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Arusha Robson Meitinyiku akiongea katika mkutano wa hadhara katika kata ya Leguruki Mkoani Arusha ambapo aliwahimiza vijana wadumishe upendo,Amani katika Nchi yao huku akiwataka kuepuka uvinjifu wa Amani
six6 six5Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhi cheti mmoja wa wadau waliodhamini maradi wa uwanja wa michezo kutoka kamapuni ya YES
sixx18Zaidi ya Wanachama wapya 27 kutoka chama cha demokrasia na maendeleo chadema waliochukua rasmi kadi za CCM wakionyasha kadi zao mara baada ya kukihama chama hicho
six20Umati wa wananchi waliojitokeza kumsikiliza Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda
six21
six 19Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhikadi mwanachama mpya kutoka chadema
six22six20
six4
six3Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhicheti mkurugenzi wa YES Tanzania Samwel Mpenzu
six2
six1Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akiongea baada ya uzinduzi wa uwanja pamoja na mashina katika kata ya Ngarasero Mkoa Arusha katika ziara yake ya kwanza ya kikazi toka ateuliwe (Pamela Mollel jamiiblog)

Monday, 10 February 2014

BANANA INVESTMENT YATOA ZAWADI KWA MAWAKALA WAO.

2/10/2014 01:20:00 pm

Mshindi wa kwanza kitaifa ni Bw. Peter Assenga kutoka Morogoro aliyejishindia zawadi ya Gari,hapa akionyesha ufunguo wake katika sherehe zilizoandaliwa na kampuni ya Banana Investment iliopo jijini Arusha.  Mshindi wa pili ni Dorothea kutoka Rombo, Tarakea , na Mshindi wa tatu alipata friji ambae ni Bw. Ibrahim Kikweche kutoka Dar es Salaam. washindi wengine kutoka Arusha ni Bw. Zefania Kira kutoka Namanga aliyeshishindia Tv, Bw. Victor Massawe kutoka Mbuguni aliyejishindia Flat Screen Tv, Bw. Gabriel Shibu Kutoka Ulonga Shangarai

Mmoja wa wakala akipokea zawadi ya Flat Screen TV' 21'' katika sherehe zilizoandaliwa na kampuni ya Banana Investment iliopo Moshono, jijini Arusha.
Wakala akipokea zawadi yake katika sherehe za kuwakabidhi zawadi zilizoandaliwa na kampuni ya Banana Investment iliopo jijini Arusha. Kwa picha Zaidi Bofya hapa >>>

Wednesday, 29 January 2014

Monday, 13 January 2014

MCHUNGAJI AWAAMURU WAUMINI WAKE WALE MAJANI KAMA NG'OMBE AFRIKA KUSINI

1/13/2014 01:42:00 pm

God forgive for saying this, but how stupid can some people be? And how do you follow and obey another human being so blindly? A pastor in South Africa, Pastor Lesego Daniel is making his members eat grass. Yes, grass!

Pastor Daniel, who is the founder and Head Pastor at Rabboni Centre Ministries, situated at Zone 2 Ga-Rankuwa, north of Pretoria, said he was basically trying to prove that humans can be controlled by the spirit and they can eat anything to feed their bodies. I don't know how he managed to convince his members to go outside the church and start eating grass, but he! Unbelievable!


Huyu dada anakula majani kama mbuzi....
Kila mmoja anakula majani kwa style yake....ee Mungu Tusaidie..
Binadamu anatafuna majani...
  Mchungaji mwenyewe ndo huyo hapo juu anajiita 'Pastor Daniel Lesego'

  Hapa anawaombea akiwakanyaga kama magunia...Source: www.wazalendo25.blogspot.com

Sunday, 10 November 2013

WANANCHI WA KIJIJI CHA SAMARIA WAKISALIMIANA NA MBUNGE WAO NAKUTOA SHUKRANI

11/10/2013 04:30:00 pm
Wananchi wakijiji cha Samaria walayani Arumeru Mashariki wakisalimiana na Mh,mbunge wao Joshua nasari mara baada ya kumaliza kuchangisha Harambee kwa Ajili ya uchimbaji wa visima vya maiji.

Wananchi hao walisema wanamshuru sana Mbuge huyo kwa ujio wake pamoja na kuchangia ujenzi wa visima vya maji kwamba ni dhiki kubwa wamekumbana nayo katika kukosa maji.

Walisema kuwa na zaii ya miaka 100 hawajawahi kupata maji katika kijiji chao hivyo hutumia umbali wa masaa nane kwenda na kurudi jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa sana katika maisha yao.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho bi Ndeshukurwa Andrea Mbise akielezea kwa masikitiko makubwa sana alisema kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji limepelekea wengi wao kuishi bila kuoga ama kuoga mara moja kwa wiki kwani maji yamekuwa ni ya shida hivyo kutengewa kwa ajili ya mapishi tu ya nyumbani.

Pia alisema kwamba tatizo hilo limepelekea kufeli mitihani kwa watoto wao mashuleni kwani ile mida ya asubuhi hulazimika kwenda kuchota maji badala ya kwenda shuleni,na ule muda wanaotoka wanakuwa wamechokakitendo cha kuwafanya washindwe kusoma,ambapo huku wazazi wao wakiwa mashambani na sokoni kwa ajili ya kuwatafutia kitoweo.

Alimalizia kwa kusema kwamba wanamshuru sana Mh,Mbunge Nasari kwa kuja kijijini kwao kwa ajili ya Harambee ya kuchangia uchimbaji wa visima na kwamba kupitia hatua hiyo wataondokana na Hadha hiyo ambayo ni kero kubwa kwao.

Katika harambee hiyo ela iliyopatikana ni kiasi cha shilingi zaidi ya milion kumi na mbili 12.

Thursday, 24 October 2013

MENEJA WA KIMAHAMA AKIELEZEA UMUHIM WA KUSOMA VITABU.

10/24/2013 08:36:00 am
Bw,Emmanuel Absolum ambaye ni meneja wa duka la vitabu la Kimahama akieleza umuhimu wa wananchi kujisomea vitabu.

Amesema kuwa kupitia vitabu unapata elimu juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi kwa mambo ambayo mwananchi hayajui.

Akielezea lengo la kufungua duka hilo amesema kuwa ni kuwasaidia wakazi wa jiji la Arusha kupata elimu kupitia vitabu sambamba na kujijengea mazoea ya kusoma ujuzi na ufanisi katika kutambua mambo mbalimbali.

MENEJA WA KIMAHAMA AKIWA KWENYE DUKA LA VITABU

10/24/2013 08:21:00 am
Meneja wa kimahama Emmanuel Absalom akiwa amesimama kwenye duka la vitabu lililo zinduliwa upya na Mkuu wa chuo Habari maalum bw,Jackson Kaluzi, baada ya kuboreshwa na kuwekwa vitabu mbalimbali vya kuvutia ambapo vitabu hivyo ni kama Biblia,vitabu vya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na vingine vingi vya kuelimisha jamii.

Tuesday, 8 October 2013

AINA YA SAMAKI WA BAHARINI

10/08/2013 10:00:00 pm
Hawa ni samaki wekundu kwa jina maarufu(changu mwekundu) smaki hawa wanavutia sana kwa muonekano wao,samaki hawa  wanaopatikana katika bahari ya hindi,ambapo samaki hawa hawawezi kupatikana sehemu nyingine kama kwenye maziwa fofauti na kupatikana kwenye maji ya chumvi ya baharini.

Kama wanavyoonekana hapo juu hawa samaki hawjakaushwa wala kukaangwa hapa ni wametolewa baharini kuvuliwa katika sehemu ya uvuvi  bahari ya Hindi  Mkoani Tanga katika eneo lililopo mkabala kabisa na Radio ya Huruma fm iliyopo ufukweni mwa Bahari.

J

VIONGOZI WA TYCC WAKISOMA RISALA

10/08/2013 09:35:00 pm
Mwanafunzi ambaye ni Mmoja wa viongozi wa Tyccc kanda ya Tanga kwa jina la Douglos Gasper aliyevalia miwani(wa kwanza kutoka kushoto)ambaye pia ni mhazini wa kikundi hicho,akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kidato cha nne yaliyofanyika katika ukumbi wa Magreth Hall uliopo jijini Tanga.

Kiongozi huyo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi pamoja na kadamnasi iliyokuwepo kwenye mahafali hayo ambapo alielezea changamoto wanazokumbana nazo katika kuendesha kikundi chao wakiwa shuleni.

Gasper alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakizuiliwa na uongozi wa shule katika suala zima la kuendesha vipindi vyao dini ikiwemo kuimba kwaya wawapo mashuleni  huku walimu hao wakitumia vipindi hivyo kufundisha masomo mengine jambo ambalo limepelekea wanafunzi wengi kutokuwa na hofu ya Mungu hata kutofahamu kabisa neno la Mungu.

Pia alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili katika utendaji kazi wao ni ufinyu wa kipato kwani hawana biashara yoyote hivyo kulazimika kutoa ela zao mifukoni pale kunapokuwa kumehitajika utatuzi wa jambo fulani na kwamba hali hiyo imepelekea shughuli zao kutokwenda kwa ufanisi.

Waliiomba serikali na uongozi wa dini ya kikristo kuwapa msaada pale watakapokuwa wanahitji msaada ikiwa ni pamoja na kuwawekea walimu wa dini kwenye shule zao ili kuweza kuepukana na tatizo lililokihtiri la kufeli masomo ya dini ya kikristo tofauti na dini nyingine.

Monday, 7 October 2013

WALIMU WA FURAHA FOUNDATION NA WAZIRI WA MALI ASILI

10/07/2013 07:38:00 pm
Walimu wawili wa Shule ya Furaha foundation waliosimama pembeni kushoto wakiwa kwenye picha na Waziri wa mali asili na utalii Hamis Kagasheki ambaye amesimama kulia akiwa ameshikilia zawadi aliyopewa na walimu hao kwa uwakilishi wa shule ya Furaha foundation,mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo ilikuwa siku ya kuazimisha wanyama Duniani.

Saturday, 5 October 2013

WANAFUNZI WA TYCC KANDA YA TANGA WAKIPEWA USHAURI NA MGENI WAO RASMI BW,AMOS MOMBO

10/05/2013 10:19:00 pm
Wanafunzi wa dini ya katoliki(TYCC) kutoka shule mbalimbali za kanda ya Tanga wakiwa wanamsikiliza katibu mstaafu wa kwaya ya st,Antony Tanga kwa jina la Amos Mombo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kuhitimu kidato cha nne,ambapo mahafali hayo yalifanyika katika ukumbi wa Magreth hall(ridoch)uliopo jijini Tanga. 

Aidha bw,Amos aliwashauri kuwa ufuatia kuchafuka kwa dunia vijana wamekuwa wakijiingiza katika tabia mbaya na kusahau amri za Mungu hivyo wajitahidi kuepukana nazo kwa kuwekw sala mbele za Mungu.

Pia alisema kuwa wanapaswa kushikamana kwa mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kuepukana na makundi yasiyo kuwa na tija kwa jamii kwani kuna baadhi ya makundi sio mazuri ambayo ujihusisha na masuala ya madawa ya kulevya na kutomjua Mungu. 

WANAFUNZI WA SHULE YA FURAHA FOUNDATION WAKITUMBUIZA WIMBO MBELE YA WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII

10/05/2013 02:24:00 pm
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya furaha foundation wakitumbuiza nyimbo zao na kucheza kwa mbwembwe mbele ya huku  mgeni Rasmi Waziriwa Mali asili na Utalii Hamis Kagasheki wakati alipokuwa kwenye viwanja vya Aicc Mkoani Arusha mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo yaliyoanzia katika Ofsi za Tanapa.

Ambapo wimbo wao ulihusu kumshukuru waziri Kagasheki kwa kazi yake nzuri anayoifanya,kwa kushirikiana na mashirika ya hifadhi ya Wanyama.

MKURUGENZI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA UTAFITI WA TEMBO AKISISITIZA JAMBO

10/05/2013 01:45:00 pm
Dr Alfred Kikoti ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa Tembo(world Elephant Centre)akiwaelezea wananchi wa jiji la Arusha kuwa pale watakapowabaini majangiri wanao waua Tembo wawekwe kwenye website,mitandao ikiwa njia mojawapo ya kuwafichua majangiri hao.

Dk Alfred aliyasema hayo kwenye uwanja wa Aicc mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo kauli mbiu yao ilikuwa ni ''kila baada ya dk kumi na tano tembo anauwawa ''na kwamba kama hali itaendelea hivo baada ya miaka kumi na mbili Tanzania hatutakuwa na Tembo.

Alisema Tembo ni sawa na binadamu,meno ya tembo,pembe za ndovu wasivitumie kama biashara ni kwa ajili ya tembo,hivyo kujitahidi kukataa biashara haramu ya pembe za ndovu na kila Mtanzania kusema ''hapana''

                                                          
Adbox