Adbox

Thursday, 24 October 2013

MENEJA WA KIMAHAMA AKIELEZEA UMUHIM WA KUSOMA VITABU.

10/24/2013 08:36:00 am
Bw,Emmanuel Absolum ambaye ni meneja wa duka la vitabu la Kimahama akieleza umuhimu wa wananchi kujisomea vitabu.

Amesema kuwa kupitia vitabu unapata elimu juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi kwa mambo ambayo mwananchi hayajui.

Akielezea lengo la kufungua duka hilo amesema kuwa ni kuwasaidia wakazi wa jiji la Arusha kupata elimu kupitia vitabu sambamba na kujijengea mazoea ya kusoma ujuzi na ufanisi katika kutambua mambo mbalimbali.

MENEJA WA KIMAHAMA AKIWA KWENYE DUKA LA VITABU

10/24/2013 08:21:00 am
Meneja wa kimahama Emmanuel Absalom akiwa amesimama kwenye duka la vitabu lililo zinduliwa upya na Mkuu wa chuo Habari maalum bw,Jackson Kaluzi, baada ya kuboreshwa na kuwekwa vitabu mbalimbali vya kuvutia ambapo vitabu hivyo ni kama Biblia,vitabu vya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na vingine vingi vya kuelimisha jamii.

Tuesday, 8 October 2013

AINA YA SAMAKI WA BAHARINI

10/08/2013 10:00:00 pm
Hawa ni samaki wekundu kwa jina maarufu(changu mwekundu) smaki hawa wanavutia sana kwa muonekano wao,samaki hawa  wanaopatikana katika bahari ya hindi,ambapo samaki hawa hawawezi kupatikana sehemu nyingine kama kwenye maziwa fofauti na kupatikana kwenye maji ya chumvi ya baharini.

Kama wanavyoonekana hapo juu hawa samaki hawjakaushwa wala kukaangwa hapa ni wametolewa baharini kuvuliwa katika sehemu ya uvuvi  bahari ya Hindi  Mkoani Tanga katika eneo lililopo mkabala kabisa na Radio ya Huruma fm iliyopo ufukweni mwa Bahari.

J

VIONGOZI WA TYCC WAKISOMA RISALA

10/08/2013 09:35:00 pm
Mwanafunzi ambaye ni Mmoja wa viongozi wa Tyccc kanda ya Tanga kwa jina la Douglos Gasper aliyevalia miwani(wa kwanza kutoka kushoto)ambaye pia ni mhazini wa kikundi hicho,akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kidato cha nne yaliyofanyika katika ukumbi wa Magreth Hall uliopo jijini Tanga.

Kiongozi huyo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi pamoja na kadamnasi iliyokuwepo kwenye mahafali hayo ambapo alielezea changamoto wanazokumbana nazo katika kuendesha kikundi chao wakiwa shuleni.

Gasper alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakizuiliwa na uongozi wa shule katika suala zima la kuendesha vipindi vyao dini ikiwemo kuimba kwaya wawapo mashuleni  huku walimu hao wakitumia vipindi hivyo kufundisha masomo mengine jambo ambalo limepelekea wanafunzi wengi kutokuwa na hofu ya Mungu hata kutofahamu kabisa neno la Mungu.

Pia alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili katika utendaji kazi wao ni ufinyu wa kipato kwani hawana biashara yoyote hivyo kulazimika kutoa ela zao mifukoni pale kunapokuwa kumehitajika utatuzi wa jambo fulani na kwamba hali hiyo imepelekea shughuli zao kutokwenda kwa ufanisi.

Waliiomba serikali na uongozi wa dini ya kikristo kuwapa msaada pale watakapokuwa wanahitji msaada ikiwa ni pamoja na kuwawekea walimu wa dini kwenye shule zao ili kuweza kuepukana na tatizo lililokihtiri la kufeli masomo ya dini ya kikristo tofauti na dini nyingine.

Monday, 7 October 2013

WALIMU WA FURAHA FOUNDATION NA WAZIRI WA MALI ASILI

10/07/2013 07:38:00 pm
Walimu wawili wa Shule ya Furaha foundation waliosimama pembeni kushoto wakiwa kwenye picha na Waziri wa mali asili na utalii Hamis Kagasheki ambaye amesimama kulia akiwa ameshikilia zawadi aliyopewa na walimu hao kwa uwakilishi wa shule ya Furaha foundation,mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo ilikuwa siku ya kuazimisha wanyama Duniani.

Saturday, 5 October 2013

WANAFUNZI WA TYCC KANDA YA TANGA WAKIPEWA USHAURI NA MGENI WAO RASMI BW,AMOS MOMBO

10/05/2013 10:19:00 pm
Wanafunzi wa dini ya katoliki(TYCC) kutoka shule mbalimbali za kanda ya Tanga wakiwa wanamsikiliza katibu mstaafu wa kwaya ya st,Antony Tanga kwa jina la Amos Mombo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kuhitimu kidato cha nne,ambapo mahafali hayo yalifanyika katika ukumbi wa Magreth hall(ridoch)uliopo jijini Tanga. 

Aidha bw,Amos aliwashauri kuwa ufuatia kuchafuka kwa dunia vijana wamekuwa wakijiingiza katika tabia mbaya na kusahau amri za Mungu hivyo wajitahidi kuepukana nazo kwa kuwekw sala mbele za Mungu.

Pia alisema kuwa wanapaswa kushikamana kwa mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kuepukana na makundi yasiyo kuwa na tija kwa jamii kwani kuna baadhi ya makundi sio mazuri ambayo ujihusisha na masuala ya madawa ya kulevya na kutomjua Mungu. 

WANAFUNZI WA SHULE YA FURAHA FOUNDATION WAKITUMBUIZA WIMBO MBELE YA WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII

10/05/2013 02:24:00 pm
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya furaha foundation wakitumbuiza nyimbo zao na kucheza kwa mbwembwe mbele ya huku  mgeni Rasmi Waziriwa Mali asili na Utalii Hamis Kagasheki wakati alipokuwa kwenye viwanja vya Aicc Mkoani Arusha mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo yaliyoanzia katika Ofsi za Tanapa.

Ambapo wimbo wao ulihusu kumshukuru waziri Kagasheki kwa kazi yake nzuri anayoifanya,kwa kushirikiana na mashirika ya hifadhi ya Wanyama.

MKURUGENZI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA UTAFITI WA TEMBO AKISISITIZA JAMBO

10/05/2013 01:45:00 pm
Dr Alfred Kikoti ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa Tembo(world Elephant Centre)akiwaelezea wananchi wa jiji la Arusha kuwa pale watakapowabaini majangiri wanao waua Tembo wawekwe kwenye website,mitandao ikiwa njia mojawapo ya kuwafichua majangiri hao.

Dk Alfred aliyasema hayo kwenye uwanja wa Aicc mara baada ya kumaliza matembezi ya Tembo ambapo kauli mbiu yao ilikuwa ni ''kila baada ya dk kumi na tano tembo anauwawa ''na kwamba kama hali itaendelea hivo baada ya miaka kumi na mbili Tanzania hatutakuwa na Tembo.

Alisema Tembo ni sawa na binadamu,meno ya tembo,pembe za ndovu wasivitumie kama biashara ni kwa ajili ya tembo,hivyo kujitahidi kukataa biashara haramu ya pembe za ndovu na kila Mtanzania kusema ''hapana''

                                                          

Friday, 4 October 2013

MKUU WA MKOA AKIPEWA ZAWADI

10/04/2013 09:51:00 pm
Mkuu wa Mkoa wa Arusha bw,Magesa Mlongo wa kwanza kutoka kulia akikabidhibiwa zawadi na ofsi za Tato mara baada ya kumaliza maandamano ya amani ya utembezi wa tembo kitaifa, ambapo jijini Ausha maadamano hayo yameanzia katika ofis za Tanapa na kuishia kwaenye viwanja vya AICC njiro.

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU NYEREMBE MUNASA AKITOA USHAURI KWA MADREVA TOYO

10/04/2013 08:49:00 pm
Mkuu wa wilaya ya Arumeru bw,Nyerembe Munasa akitoa ushauri kwa waendesha toyo kuendesha toyo zao kwa umakini pale wanapokuwa barabarani ili kuondokana na ajali zisizo kuwa za lazima hapa nchini.

Munasa alisema hayo katika uwanja wa sheikh amri Abed Arusha  ikiwa  ni week ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa.

Alisema kuwa kuna baadhi ya waendesha toyo ambao wamekuwa wakisababisha ajali kwani wengi wao huendesha toyo wakiwa wamelewa pombe hata madawa ya kulevya jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria.

Alisisitiza kwamba wale wote ambao wataenda kinyume na sheria watakamatwa na kuchukuliwa sheria.

WAENDESHA TOYO WAKIWA KWENYE WEEK YA USALAMA BARABARANI

10/04/2013 08:16:00 pm
Baahi ya waendesha pikipiki alimaarufu kama toyo jijini Arusha wakiwa katika uwanja wa sheikh Amri Abedi huku wakipewa ushauri na Mkuu wa wilaya ya Arumeru bw.Nyerembe Munasa kuhusu kutumia pikipiki zao vizuri ili kuepukana na ajali zisizo kuwa za lazima ambapo ilikuwa ni week ya nenda kwa usalama barabarani.

Thursday, 3 October 2013

PINDA AKISISIZA VIONGOZI KUTOPOKEA RUSHWA

10/03/2013 09:45:00 pm
Waziri mkuu Mizengo Piter Pinda akitoa ufafanuzi kwamba kuna baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakikwamisha suala zima la uwekezaji kutokana na tamaa yao mbaya ya kutaka kitu kidogo yaani Rushwa hivyo wawekezaji kukata tamaa na kushindwa kuwekeza na kwamba atakaye bainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.


Pinda  aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa minne Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Tanga,ambapo lilofanyika Mkoani Tanga katika Hotel maarufu Mkonge ambapo kongamano hilo lilijumuisha viongozi wote wa ngazi ya wilaya,wakuu wa mikoa pamoja na wawekezaji.


Wednesday, 2 October 2013

Adbox