Adbox

Monday, 16 September 2013

NESI MSTAAFU AKIMPATIA USHAURI MGONJWA

9/16/2013 10:37:00 pm
Bi Antonia ambaye ni mke wa naibu waziri wa ardhi,nyumba na makazi ambaye pia ni mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye,yeye ni bi Antonia ni Nesi mstaafu katika hosp ya Mkoa jijini Arusha,ambapo baada ya kustaafu ameamua kufungua ofsi yake ya kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwa ni pamoja na kuwapatia ushauri wale wenye unene na kuwapima kwa kutumia mashine maalumu ,na hapa anampatia mmoja wa akina mama katika ofsi yake iliyopo mianzini barabara ya vumbi,ambapo anamueleza ni jinsi gani anaweza kutumia vyakula bora ili asweze kuwana unene wa tumbo usio kuwa wa lazima,

WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBWA KWENYE PICHA YA PAMOJA

9/16/2013 10:05:00 pm
Waziri wa elimu na mafunzo dk,Shukuru Kawambwa (wa nne kutoka kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu kutoka vyuo vikuu nchini walipokutana jijini Arusha kwenye ukumbi wa Naura kwa lengo la kujadili na kubadilishana mawazo juu ya kuendeleza elimu ya juu,na kujadili ni jinsi gani ya kutatua changamoto zinazojitokeza katika sekta ya elimu ya juu nchini.

MAMA OLEMEDEYE AKIWA NA WATOTO YATIMA

9/16/2013 07:16:00 am
Bi Antonia wa kwanza kutoka kulia aliyevalia nguo ya kitenge na mkoba mweupe ambaye ni Mke wa naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi na ni mbunge wa Arumeru Magharibi ,Gudluck Ole Medeye akiwa na watoto yatima wa kituo cha Ndoombo kilichopo wilayani Arumeru huku akiwa ameambatana na wafadhili kutoka New yourkbaada ya kufika kuwatembelea watoto hao na kuwapatia msaada wamahitaji mbalimbali.

WAZIRI WA MAJI PRF,JUMANNE KWENYE PICHA YA PAMOJA

9/16/2013 06:14:00 am
Waziri wa maji Prf,Jumanne Magembe wa pili kutoka kulia,akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi watendaji wa idara ya maji AUWSA,waliosimama nyuma yake,mara baada ya uzinduzi wa bodi mpya jijini Arusha,Na wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa,wa kwanza kutoka kushoto ni mkurugenzi wa AUWSA bi Ruth koya,na wa pili kutoka kushoto ni mbunge mstaafu wa jiji la Arusha mjini Felix Mrema.

Sunday, 15 September 2013

Saturday, 14 September 2013

PROFESA MAHENGA AKISISITIZA JAMBO

9/14/2013 11:31:00 pm
Waziri wa maji prf,Jumanne Magembe akiwasisitiza watumishi wa idara ya maji AUWSA kuhusu  kuwa makini na kutenga eneo yenye vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuwa makini katika kuhakikisha miji hayapotei,wakati wa siku ya kuzindua bodi mpya na kuaga bodi inayomaliza muda wake iliyofanyika jijin Arusha kwenye ofsi za Auwsa

WAZIRI WA MAJI PRF,MAGEMBE AKIELEKEA UKUMBINI

9/14/2013 10:36:00 pm
Waziri wa maji Prf,Jumanne Magembe wa kwanza kutoka kulia akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa maji AUWSA bi, Ruth koya wa kwanza kutoka kushoto wakiwa na wanazungumza jambo fulani huku wakifuatwa nyuma  na wajumbe wa bodi ya maji wakielekea ukumbi wa Auwsa jijini Arusha,  ikiwa ni siku ya kuzindua bodi mpya na kuaga bodi iliyomaliza muda wake .

Wednesday, 11 September 2013

waandishi

9/11/2013 01:29:00 pm
baadhi ya waandishi wa habari mkoani arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiwa wamepumzika wakati wa mechi ya bonanza iliyofanyika katika viwanja vya generally taya iliyopo njiro mkoani arusha.

Saturday, 7 September 2013

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YATOA SEMINA KWA WANAHABARI WA ARUSHA

9/07/2013 06:51:00 pm

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akitoa mada katika Semina ya siku moja, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa ASILI YETU TANZANIA BLOG Bw. Victor Machota akiwa na Gadiola Emanuel mwenyekiti wa Arusha Bloggers Associations na Mkurugenzi wa WAZALENDO 25 BLOG katika Semina ya siku moja iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha. Kwa picha zaidi Bofya hapa>>>

Thursday, 5 September 2013

Wednesday, 4 September 2013

Naibu waziri wa maji dk.Mahenge aongea na wananchi

9/04/2013 11:48:00 pm
 Naibu waziri wa maji Dk.Bilinith Mahenge akihutubia wananchi wa wilaya ya monduli alipokuwa kwenye ziara yake ya maji Mkoani Arusha huku akiwaelezea kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji .

Naibu waziri wa maji DK.Bilinithi Mahenge wa tatu kutoka kushoto aliyevaa koti jeus akitoa maelezo kwa wakandarasi wa kisima katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha mara baada ya kutembelea miradi ya maji wilayani humo.
9/04/2013 11:00:00 pm
bustani ya mboga za majani aina ya kabichi inayomilikiwa na mmoja wa wakulima katika kata ya Themi Njiro ambaye hakupenda kuonekana kwenye picha,ambapo hupata mahitaji yake kupitia mboga hizo.

Kumbu Kumbu ya Kumuenzi Marehemu Daudi Mwangosi

9/04/2013 05:28:00 pm

 Wanahabari  wa  vyombo  mbali mbali na  wadau  wa habari  mkoa  wa  Iringa  wakiwa katika  maandamano ya amani ya  kumuenzi  aliyekuwa mwenyekiti  wa klabu ya  waandishi  wa  habari  mkoa  wa Iringa (IPC) .Picha Zote na Francis Godwin
 Maandamano  ya  wanahabari na  wadau  wa  habari yakipita  eneo la soko kuu la manispaa ya  Iringa.
  Katibu  wa IPC  Francis  Godwin  akiongoza  maandamano ya  wanahabari na  wadau huku akiwa  juu ya gari na picha ya marehemu Daudi Mwangosi.

Saturday, 22 June 2013

Monday, 22 April 2013

MHE. GODBLESS LEMA, MHE. CHRISTOPHER OLE SENDEKA NA MBUNGE WA MONDULI MHE. EDWARD LOWASSA NA WAZIRI WA HABARI ,MICHEZO NA UTAMADUNI DR. FENELLA MUKANGARA KATIKA MAADHIMISHO YA KUMUENZI HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE MONDULI ,ARUSHA.

4/22/2013 06:34:00 pm



 "Dickson Marwa"kutoka katika Club ya "Holili"  ndiye mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 10 za kumuenzi hayati "Edward Moringe Sokoine" zilizofanyika Monduli Arusha.
Mzee wa Kimasai akimalizia mbio ,huku akishuhudiwa na Mratibu na Mwanaharakati wa Mashindano hayo Bw. Wilhelm Gidabuday ( mwenye Jezi ya Bluu) na mzee Kamili kushoto kwakwe katika mbio hizo za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.

 Mshindi wa pili "Leonard John" (mwenye nyeusi kushoto) kutoka katika Club ya (Winning Spirit) akiwa na mshindi wa tatu "Msenduki Mohamed" kutoka katika Club ya (Hakika) wakiandikishwa mara baada ya kumaliza mbio za kilometa 10, katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.

 Mshindi wa kilometa 10 kwa wanawake - Catherine Lange akiwa akihojiwa na waandishi wa habari ,katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
 Mshindi wa kilometa 10 kwa wanawake - Catherine Lange akihojiwa na TBC1 katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
 Mshindi wa kilometa 10 kwa wanawake - Catherine Lange akipokea tuzo na waziri wa Habari ,michezo na Utamaduni Dr. Fenella Mukangara katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.

Mshindi wa pili katika kilometa 10 kwa wanawake kwa wanariadha wa Kimataifa, akiandikishwa mara baada ya kumaliza mbio, katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.

 Mshindi wa kwanza kwa Wanafunzi wa wilaya ya Monduli kwa wasichana kilometa 2 (kulia) Irene Simon akiwa na mshindi wa pili (kushoto) Hapiness Charles katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
 Mshindi wa kwanza kwa Wanafunzi wa Wilaya ya Monduli Wanaume (kulia) ni Nganeni Shilalo akiwa na mshindi wa pili Lewanga Melita na watatu  Lonyoike Tulito katika mbio za  kilomita 2 ,katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.

Mshindi wa tatu (kushoto) Ngeani Ng'arde, kwa Wanafunzi wa wilaya ya Monduli wasichana katika mbio za kilometa 2 akiwa na mshindi wa pili ,katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
Mbunge wa Simanjiro Mhe. Christopher Ole Sendeka akishiriki mbio za 'Moringe Sokoine Mini Marathon 'katika mbio hizo za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
  Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema mwenye ngwanda na namba kifuani katika mstari wa kuandikishwa baada ya kumaliza mbio za kilometa 2 za 'Moringe Sokoine Mini Marathon 2013' katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.Mbele yake ni Seria Tumainiel (Wiki Likis) Mmiliki wa blog ya Arusha 255 nae alishiriki mbio hizo.
Waziri wa Habari ,Michezo na Utamaduni Dr. Fenella Mukangara akiwahutubia mamia ya watu waliohudhuria siku ya kumbu kumbu ya kutimiza miaka 29 ya hayati waziri mkuu "Edward Moringe Sokoine" huko Monduli, mkoani Arusha.

Waziri Mukangara aliwaomba wananchi kuikumbuka siku aliyofariki Edward Sokoine 12/4/1984 pamoja na mema aliyowatendea wananchi wake.


Kutoka kushoto:ni Waziri wa Habari ,Michezo na Utamaduni Dr. Fenella Mukangara ,Mhe. Edward Lowassa, Mhe. Namelok Sokoine(viti maalum na mtoto wa hayati Edward Sokoine) na Mhe. Christopher Ole Sendeka katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
Viongozi na wanafamilia wakishuhudia matukio ya michezo yaliyokuwa yakiendelea, katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
Kutoka kushoto:Mh. Godless Lema , Waziri wa Habari ,Michezo na Utamaduni Dr. Fenella Mukangara ,Mhe. Edward Lowassa, Mhe. Namelok Sokoine(viti maalum na mtoto wa hayati Edward Sokoine) na Mhe. Christopher Ole Sendeka katika mbio za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha.
Mzee wa kimaasai akimalizia mbio ,huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa riadha Mkoa wa Arusha Bw. Joseph Jorwa katika mbio hizo za kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine Monduli ,Arusha. Kwa hisani ya Wazalendo 25 Blog
Adbox