Adbox

Saturday, 22 November 2025

IGP Wambura awataka Watanzania kutokubali kugawanyika kwa sababu yoyote ile, iwe ya kidini, kisiasa au rasilimali

11/22/2025 01:39:00 pm
Ataka Upendo na mshikamano vidumu kama Desturi ya Watanzania

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amewataka Watanzania kutokubali kugawanyika kwa sababu yoyote ile, iwe ya kidini, kisiasa au rasilimali na badala yake waendeleze upendo na amani ya taifa.

IGP Wambura aliyasema hayo Novemba 21, 2025 wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Askari Polisi Kozi Namba 1/2024/2025 katika Shule ya Polisi Tanzania - Moshi, Kilimanjaro.

IGP Wambura amesema amani ya nchi ni jambo la muhimu hivyo kila mmoja anawajibu wa kuendeleza amani na usalama wa nchi ambayo imedumu kwa muda mrefu tangu tumepata uhuru.

Pia, amewataka watanzania kuendeleza ushirikiano, umoja na mshikamano na Jeshi la Polisi kwa maslahi ya taifa letu.

Aidha, IGP Wambura amewataka askari wahitimu kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza kwa kuhakikisha kuwa wanaimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu.

Vilevile, amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuendelea kutoa ajira ndani ya Jeshi la Polisi pamoja na kuboresha vitendea kazi, makazi, ofisi na kuboresha maslahi ya askari Polisi.

Jumla ya Askari 4826 wamehitimu mafunzo hayo ya awali yaliyodumu kwa muda wa miezi kumi na mbili ambapo wahitimu hao wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika nchini.

4,826 WAHITIMU MAFUNZO YA POLISI MOSHI, IGP AKIONYA KUHUSU UGAIDI NA DAWA ZA KULEVYA

11/22/2025 10:26:00 am

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP Camillus Wambura amesema miongoni mwa changamoto watakazokutana nazo wahitimu wapya wa mafunzo ya awali ya Polisi ni pamoja na matishio ya ugaidi wa dunia, uwepo wa dawa za kulevya, usafirishaji haramu wa binadamu na uhamiaji haramu.

IGP Wambura amebainisha hayo  Moshi Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya Polisi kwa Kozi namba moja ya mwaka 2024/25, akisema kazi za Polisi zinahitaji ushirikiano wa dhati na wa karibu ili kuweza kuzuia na kupambana na changamoto hizo.

IGP Wambura pia akisisitiza kuhusu umuhimu wa usalama kama nyenzo ya maendeleo na ustawi wa Binadamu, ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kudhibiti uhalifu na wahalifu kote nchini Tanzania.

" Tusikubali pia kugawanyika kutokana na sababu yeyote ile iwe ya kisiasa, kidini au rasilimali. Tuendelee kutunza tunu yetu ya usalama na amani ya nchi yetu iliyodumu takribani kwa miongo mingi sasa. Tushirikiane popote kuhakikisha tunakuwa salama." Amesisitiza IGP Wambura.

Awali wakati wa maelezo yake, Mkuu wa Chuo hicho Ramadhan Mungi  amesema askari wapya 4, 826 wakiwemo wanaume 3, 436 na wanawake 1, 390 wamehitimu mafunzo hayo, huku wanafunzi 217 wakiondolewa chuoni hapo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa nidhamu na uwezo mdogo katika kujifunza.

Friday, 21 November 2025

ZAIDI YA WAGENI 500 WAHUDHURIA KONGAMANO LA DINI ARUSHA, WASIFU AMANI NA UTULIVU

11/21/2025 08:50:00 pm

 Wakaribisha wengine nchini wakiwataka kuachana na upotoshaji wa Mtandaoni* 

Zaidi ya Wageni 500 kutoka kwenye Mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na nje ya Afrika wamekutana kwa siku mbili Mkoani Arusha kwenye Kongamano la kujadili kuhusu mchango wa dini katika uchumi na maendeleo, wengi wakifurahia amani na utulivu walioushuhudia nchini tangu kuwasili kwao siku tano zilizopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, miongoni mwa washiriki hao kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchini Senegal, wameeleza kuwa Kongamano hilo lilitaka kuahirishwa kutokana na kile walichokuwa wakikiona kwenye Mitandao ya Kijamii.

"Wakati tunakuja Tanzania tulisikia vitu vingi, tukaangalia kwenye runinga na tukaona habari za uwepo wa machafuko, tukawa na wasiwasi wa Kongamano letu kiasi cha kuanza kufikiria kuahirisha lakini tunamshukuru Mungu tumefika na tumekuta amani ya kutosha na Mungu ni mwema sana kwasababu amewezesha amani Tanzania, tunamshukuru sana Mungu." Amesema Joela Athumani, Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Bi. Joela amewataka watanzania kuishikilia kwa nguvu baraka ya amani waliyobarikiwa na Mwenyenzi Mungu, akiwataka wale wote waliokuwa wamepanga kuja nchini kutokuwa na wasiwasi wowote wa kiusalama kwani hali ni shwari na shughuli zinaendelea kama kawaida.

Kwa upande wake Bw. Ogi Kabongo, Mkazi wa Kinshasa nchini DRC,  ameeleza athari za ukosefu wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akiwataka Watanzania kudumisha amani ya Tanzania kwa gharama yoyote ile kwani ukosefu wa amani unadhorotesha na kuua kabisa ustawi na maendeleo ya wananchi.

Aidha Bw. Fransis Owusu, Raia wa Senegal na Rais wa Full Gospel Business Men's Fellowship International ameitaka Jamii kuendelea kuiombea amani ya Tanzania, akisema amani hiyo mara zote imekuwa msingi muhimu wa maendeleo na kiwezeshi kikubwa cha mafanikio katika shughuli za kiuchumi

UVUNJIFU WA AMANI USIWEPO TENA TANZANIA- MATUKU

11/21/2025 01:28:00 pm

Bi. Zawadi Matuku, Mfanyabiashara wa Chanika kwa Ngwale Mkoani Dar Es Salaam ameishukuru serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama kwa udhibiti wa amani na utulivu nchini, akisema kilichotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 hakuwahi kukizoea kwani Tanzania inasifika kwa amani na utulivu kote duniani.


Matuku ameyasema hayo wakati akieleza uzoefu wake dhidi ya uvunjifu wa amani uliojitokeza, akisema kwamba aliamini siku hiyo ya upigaji kurwa ungekuwa wa amani na wafanyabiashara wangeendelea na shughuli zao kama kawaida baada ya kupiga kura.

Ameomba suala hilo kutokujirudia tena, akiwahamasisha Vijaba kujiepusha na mikumbo na kuwataka kutumia muda wao mwingi katika kujiendeleza kiuchumi na kusimamia ustawi wa maisha yao badala ya kutumika na makundi yasiyoitakia mema Tanzania.

Vijana wazidi kupaza sauti kukemea maovu na wanaotishia amani ya Nchi.

11/21/2025 01:19:00 pm

Vijana wamehamasishwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea maovu na kulinda amani na utulivu uliopo nchini pamoja na kujiepusha na makundi yenye kutenda Vitendo visivyokubalika kisheria na vyenye kuhatarisha amani ya Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa kufuatia matukio ya uvunjifu wa amani yaliyojitokeza kwenye Miji mbalimbali ya Tanzania wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, suala ambalo limemlazimu Rais Samia Suluhu Hassan kuunda Tume maalum kufuatilia chanzo cha vurugu kutokana na kuwa tukio lililowagharimu wengi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bw. Hamis Jumanne, Mkazi wa Kichangani, Temeke amewaomba Vijana kuyakataa makundi yanayotishia amani ya Tanzania, akiwataka kutumia muda wao mwingi kujiendeleza kiuchumi badala ya kutumika kuharibu amani.

Jumanne amesisitiza kutafuta namna nzuri ya kushughulikia matatizo na mapungufu yaliyopo kwa namna ifaayo na isiyoharibu tunu za Taifa, akihimiza mazungumzo zaidi kati ya wananchi na Viongozi katika kutatua kero zilizopo.

TIRA YAITAKA JAMII KUONDOA DHANA POTOFU KWAMBA BIMA NI YA MATAJIRI"

11/21/2025 11:12:00 am
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA)imetoa rai kwa vyombo vya habari nchini kuunga mkono jitihada za TIRA katika kutoa elimu ya bima kwa umma ili kuondoa dhana ya upotoshaji kuhusu ukubwa wa gharama za bima,ucheleweshaji wa malipo pamoja na dhana ya kuwa bima ni kwajili ya matajiri tu kitu ambacho siyo kweli.

Wito huo umetolewa jijini hapa jana na Kamishna wa Bima Dkt.Baghayo Saqware wakati akifungua mafunzo ya Wahariri wa Habari Tanzania kuhusu masuala ya Bima na Umuhimu wa Taarifa ya Soko la Bima.

Dkt.Baghayo alisema Elimu ni ufunguo wa kuongeza uelewa na matumizi ya bima nchini hivyo alitoa wito kwa wahariri 
Kuongeza weledi katika uandishi wa masuala ya bima.

"TIRA ipo tayari kushirikiana nanyi katika kutoa mafunzo na taarifa muhimu,Toeni kipaumbele kwa habari za bima. Haya ni masuala yanayogusa maisha ya wananchi wote kutoka mfanyabiashara mdogo hadi mwekezaji mkubwa.

"Fichueni Wadanganyifu katika bima kwa kufuatilia kwa karibu kesi mbalimbali zinazoendelea kwenye Mahakama zetu. Endeleeni kutumia Taarifa ya Soko la Bima kama nyenzo ya uchambuzi wa habari na  taarifa hizi ni msingi mkubwa wa uandishi wenye tija,"alisema Dkt.Baghayo.

Aidha alisitiza kuwa ushirikiano kati ya TIRA na vyombo vya habari ni muhimu sana katika kuifanya sekta ya bima kuwa chachu ya maendeleo ya taifa.

Hivyo alisema Kupitia majadiliano kama hayo,wanaweza kujenga taifa lenye uelewa mpana wa bima, kuongeza matumizi ya huduma hizi, na hatimaye kuimarisha ustawi wa wananchi.

Kwa upande wake Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania kutoka Ofisi ya Usuluhishi wa Migogoro Tanzania(TIO),Margaret Mngumi alisema kuwa TIO imekuwa kiungo muhimu kati ya wananchi, kampuni za bima na Serikali, na imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utatuzi wa migogoro ya bima hapa nchini.

Huku akitaja lengo kuu la uwepo wao katika mafunzo hayo kuwa ni kuweka msingi imara wa ushirikiano kati ya TIO na vyombo vya habari ili kwa pamoja kuijenga Tanzania yenye uelewa mpana zaidi kuhusu haki, wajibu na taratibu za kudai fidia za bima.

"Vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika,Kufikisha elimu sahihi kwa wananchi kuhusu hatua za kudai fidia,Kusaidia kupunguza malalamiko yasiyo na msingi kwa kutoa taarifa sahihi, Kuelimisha umma dhidi ya udanganyifu wa madai ya bima (insurance fraud) na Kuimarisha uwajibikaji wa kampuni za bima kupitia uandishi wa uwazi na wa haki,

"TIO inatambua nguvu mlizo nazo, na tungependa leo tuanzishe ukurasa mpya wa ushirikiano, ili kuboresha zaidi mazingira ya utatuzi wa migogoro ya bima kwa maslahi ya Watanzania,"alisema Mngumi. 

Pamoja na hayo Mngumi alisema kuwa 
Kwa niaba ya Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima,wako tayari kufanya kazi bega kwa bega na waandishi, wahariri na vyombo vya habari vyote katika kusambaza elimu, kutoa taarifa za kitaalamu na kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoathiri sekta ya bima.

Mwisho.

TUYAKATAE MAKUNDI YASIYOFAA, YATATUGHARIMU

11/21/2025 08:04:00 am

Wito umetolewa kwa Vijana kujiepusha na makundi yasiyofaa pamoja na kutofuata kila wanachoambiwa kwenye Mitandao ya Kijamii nchini katika kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kuwepo.

Wito huo umetolewa na Mzee Ally Bomba Omar, Mkazi wa Tandika Mabatini Mkoani Dar Es Salaam, akieleza kuwa tangu kuzaliwa kwake Mwaka 1949 hakuwa kushuhudia vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

"Tangu kipindi cha Mwalimu Nyerere tulikuwa tunaishi kwa amani, matatizo haya yaliyotokea hapa yamenishangaza na watu hawa sijui wametokea wapi. Sisi tusiokuwa nacho na tuliozoea kununua unga nusu kilo nusu kilo tuliteseka sana na bahati mbaya hata ukiwa na visenti unanunua wapi vitu? Maduka yote yalikuwa yamefungwa." Amesema Mzee Bomba.

Mzee huyo amefahamisha kuwa ana amini kwamba kila mmoja ana akili timamu, akisema makundi mabaya yatawapoteza, akisema maandamano yasiyo rasmi yanaleta matatizo mengi ikiwemo vifo, majeraha na uharibifu wa mali na maisha.

Thursday, 20 November 2025

_Ajira za Migodini Zafikia 19,874, Watanzania Wafanya Kazi kwa Asilimia 97.5_

11/20/2025 08:20:00 pm
TUME YASISITIZA ELIMU YA LOCAL CONTENT NA UTEKELEZAJI WA CSR
DODOMA 

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, ametoa wito kwa Waratibu wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content) na CSR katika mikoa kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wananchi ili kuhakikisha Watanzania wananufaika ipasavyo na rasilimali za madini.

Akizungumza leo Novemba 20, 2025 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa waratibu hao, Mhandisi Lwamo amesema ni muhimu kusimamia kwa umakini Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini pamoja na Wajibu wa Wamiliki wa Leseni kwa Jamii (CSR) ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa madini na sekta nyingine zinazohusiana.

“Elimu kwa wananchi ni nguzo muhimu ya kuwawezesha kuchangamkia fursa za ajira na biashara migodini, hususan baada ya Tume kutangaza orodha ya bidhaa na huduma zinazopaswa kutolewa na kampuni zinazomilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100,” amesema Mhandisi Lwamo.

Aidha, amewataka waratibu kuwa kiungo madhubuti kati ya Makao Makuu ya Tume ya Madini na Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa katika kuhakikisha usimamizi wa Local Content na CSR unatekelezwa ipasavyo.

Mhandisi Lwamo ameongeza kuwa sekta ya madini inaendelea kukua kwa kasi, huku mchango wake katika Pato la Taifa ukifikia asilimia 10 kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Annasia Kwayu, amesema Tume itaendelea kusimamia kikamilifu ushirikishwaji wa Watanzania katika maeneo yote ya sekta hiyo, ikiwemo ajira na manunuzi ya migodi. 

Amebainisha kuwa hadi sasa sekta imezalisha jumla ya ajira 19,874, ambapo asilimia 97.5 ni Watanzania na asilimia 2.5 pekee ni wageni.

Kuhusu manunuzi, Kwayu amesema kuwa mwaka 2024 migodi ilinunua bidhaa na huduma zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 2.03, huku kampuni za Kitanzania zikichangia Dola za Marekani Bilioni 1.79, sawa na asilimia 88 ya manunuzi yote kiashiria cha mafanikio katika utekelezaji wa Local Content.

TUMEPATA JUKWAA LA KUSHUGHULIKIA MASUALA YETU- FAUSTINE

11/20/2025 08:10:00 pm


Tunashukuru sana kwa hii Wizara ya Vijana iliyoundwa tunaona hata sisi sasa tutafikiwa kwasababu kuna wakati mawazo yetu tulikosa hata pa kuyapeleka kwahiyo kwa ujio wa Wizara hii ya Maendeleo ya Vijana naamini tutaitumia kuwasilisha mawazo na maoni yetu."- Denis Faustine, Mkazi wa Ilala Mkoani Dar Es Salaam akizungumza leo Alhamisi Novemba 20, 2025.

VIJANA WAPONGEZA HOTUBA YA RAIS SAMIA BUNGENI, WAAHIDI USHIRIKIANO KWA NANAUKA

11/20/2025 01:45:00 pm

Said Mkono, Mkazi wa Dar Es Salaam nchini Tanzania, ameeleza kufurahishwa na dhamira njema ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kushughulikia changamoto za Vijana kwa kuunda Wizara ya Maendeleo ya Vijana nchini, akisema wizara hiyo itaenda kuondoa kero na malalamiko waliyokuwa nayo Vijana.

Wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la Tanzania, Rais Samia alieleza dhamira yake ya kuunda Wizara mpya ya Maendeleo ya Vijana na siku chache baadae alipotangaza baraza la Mawaziri kati ya Wizara 27 alizozitangaza Viongozi wake, alimtaja Mhe. Joel Nanauka kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Maendeleo ya Vijana ambaye atasimamia Wizara hiyo chini ya wasaidizi kadhaa kutoka Ofisi ya Rais.

Akiisifu hotuba ya Rais Samia Bungeni na kuonesha matumaini makubwa ikiwa aliyoyasema yatatekelezwa, Mkono amemshukuru Rais Samia kwa kuunda Wizara hiyo, akiomba Viongozi watakaosimamia Wizara hiyo chini ya Waziri Nanauka kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha matokeo chanya yanapatikana kwa Vijana.

Kauli ya Rais Samia na hali ya mtanziko iliyokuwepo kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani yaliyoibua vurugu siku ya uchaguzi Oktoba 29 na siku zilizofuata, kundi la vijana likitajwa kuongoza, zilifanya wengi kusubiri kwa hamu kuundwa kwa wizara hiyo lakini pia kujua atakayeiongoza pamoja na majukumu yaliyoko mbele yake.

Mtaalamu wa saikolojia na mwezeshaji, Charles Nduku amenukuliwa akizungumza na Vyombo vya habari akisema eneo kubwa ambalo Waziri Nanauka anapaswa kulishughulikia ni pamoja na kubadili mtazamo wa vijana juu ya wanavyotazama fursa na kuwaonyesha vitu vya kufanya, kwani Tanzania ni tajiri, lakini vijana wanakosa maarifa.

PALIPO NA UTULIVU NA AMANI PANA MAENDELEO- HOKORORO

11/20/2025 10:11:00 am

Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani wamehimizwa kutunza amani katika maeneo yao ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii hivyo kuwezesha ustawi na maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkaguzi wa Polisi, Elieza Hokororo kutoka Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Pwani alipokua akizungumza na maafisa usafirishaji kwa njia ya Pikipiki maarufu kama Bodaboda, bajaji na wafanyabiashara wa kituo cha Mabasi Kibaha kuhusu ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Mkaguzi Hokororo amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa inapokosekana amani, wao kama maafisa usafirishaji hawawezi kutoka kufanya kazi za kupakia abiria au mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hawawezi kupata chakula wala matibabu na huduma nyingine muhimu za kijamii.

Naye Msemaji wa wafanyabiashara wa kituo cha mabasi Kibaha, Bwana Rashid Madaraka amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa namna wanavyoshirikiana nao kama wafanyabiashara kwa kutoa elimu mara kwa mara kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kutunza amani na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Mkaguzi Hokororo aliambatana na Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kibaha, Wakaguzi wa kata za Maili moja, Tangini, Kongowe, Tumbi na Boko Mnemela ili kuyafikia makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo maafisa usafirishaji na wafanyabiashara na kuwaelimisha umuhimu wa amani kwa maendeleo ya jamii.

Wednesday, 19 November 2025

CCM YAAPA KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WAZEMBE, YAANZA VIPIMO VIPYA VYA UWAJIBIKAJI

11/19/2025 09:33:00 pm

Na Sebastian Mavyeo, Dodoma.📍

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wazembe, wala rushwa na wale wote watakaoshindwa kuwajibika ipasavyo kwa wananchi, kikisisitiza kuwa nidhamu na utendaji wenye matokeo ndiyo msingi wa uongozi katika serikali na chama.

Akizungumza jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi, alisema chama kimejipanga kuanzisha vipimo maalum vya kutathmini utendaji wa viongozi katika ngazi zote ili kuhakikisha maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan, yanatekelezwa kwa ufanisi.

Kihongosi alisema Mawaziri na Manaibu Waziri walioteuliwa na Rais wanapaswa kwenda sambamba na kasi ya utendaji wa kiongozi wa nchi, akibainisha kuwa uteuzi wao ni heshima lakini pia una jukumu kubwa la kutekeleza kazi kwa matokeo yanayoonekana kwa wananchi.

“Rais hana mzaha katika masuala ya utumishi wa umma. Viongozi wote lazima wafanye kazi kwa kasi, uadilifu na matokeo. Yeyote atakayekwenda kinyume na maelekezo ya Rais, hatua kali zitachukuliwa,” alisema.

Aidha, Kihongosi alisisitiza kuwa CCM kipo bega kwa bega na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha amani, utulivu na maendeleo vinaimarika nchini.

Katika hatua nyingine, aliwapongeza viongozi walioapishwa akiwemo Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, Dk. Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, akiwataka kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kwa kuzingatia masilahi ya wananchi.

Akizungumzia hatua ya Rais Samia kuomba vijana waliokamatwa kutokana na vurugu za Oktoba 29 waachiwe, Kihongosi alisema kitendo hicho kinaonesha uongozi wa busara, huruma na utulivu. 

Pia alisifu uundwaji wa timu maalum ya kuchunguza vurugu hizo pamoja na ahadi ya Rais ya kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 100.

Kihongosi aliongeza kuwa ndani ya siku 11 tangu mabadiliko kufanyika, tayari ajira zimeanza kutolewa, hospitali zimekatazwa kutoza malipo yasiyo rasmi ikiwemo ada za kuweka maiti, na huduma za umma zimeelekezwa kutolewa kwa haki bila usumbufu kwa wananchi.

MC PILIPILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA, POLISI DODOMA WACHUNGUZA CHANZO

11/19/2025 06:19:00 pm

Na Sebastian Mavyeo, Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kifo cha msanii maarufu wa vichekesho Emmanuel Mathias Matebe, maarufu kama MC Pilipili, kilichotokea Novemba 16, 2025 katika Kituo cha Afya Ilazo, jijini Dodoma, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Novemba 19, 2025, Kamishna Msaidizi wa Polisi William Mwamafupa alisema kuwa MC Pilipili alifikishwa kituoni hapo akiwa katika hali mbaya na alifariki dunia majira ya saa 9:00 alasiri.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, kabla ya kifo chake, majira ya saa 8:00 mchana, msaidizi wake Hassan Ismail alipigiwa simu na mtu asiyefahamika na kuitwa mahali fulani kwa mazungumzo. 

Baada ya muda, walitokea watu watatu ambao hawakufahamika wakimtumia MC Pilipili wakiwa ndani ya gari dogo jeupe na kumkabidhi kwa msaidizi wake kisha kuondoka kwa haraka.

Wataalamu wa afya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamebaini kuwa marehemu alionyesha dalili za kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili, hali iliyosababisha majeraha makubwa na hatimaye kifo.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi wa kina unaendelea ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Kifo cha MC Pilipili kimetikisa tasnia ya sanaa na burudani nchini, ambapo wasanii na wafuasi wake wameendelea kumiminika mitandaoni kutoa salamu za rambirambi na kushangazwa na mazingira ya kifo chake.

VIJANA TUSISHAWISHIKE KUVUNJA AMANI- MNENGA

11/19/2025 04:48:00 pm

Mjasiriamali wa kuosha Magari Jijini Dar Es Salaam Bw. Salum Salum Mnenga ametoa rai kwa Vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kuitetea amani ya Tanzania, akisema kukosekana kwa amani kuna gharama kubwa zaidi na wengi ya waathirika wamekuwa wananchi wa kipato cha chini.

Mnenga ametoa kauli hiyo kufuatia vurugu, uharibifu na wizi uliotokea katika maeneo mbalimbali ya Tanzania siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 29, 2025, akisema vurugu hizo ziliwaathiri zaidi katika uchumi kutokana na kushindwa kuendelea na shughuli zao kwa takribani siku tano mpaka ilipotoka kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba Watanzania waendelee na shughuli zao za kiuchumi na kijamii kama ilivyokuwa hapo awali.

Bw. Mnenga pia amewasihi Vijana kutoshawishika kufanya maandamano ama kujihusisha na matukio ya uvunjifu wa amani, akisisitiza umuhimu wa kuwa na sababu za msingi na kuzingatia sheria na taratibu za nchi kabla ya kufanya jambo lolote lile.

WALIOFANYA VURUGU ZA OKTOBA 29, WENGI WALIFUATA MIKUMBO- ABDALLAH

11/19/2025 04:37:00 pm

Vijana wametakiwa kujiepusha na mikumbo na kufuata yale yanayosemwa katika Mitandao ya Kijamii yakiwa yanahatarisha amani, usalama na Umoja wa Watanzania kwani mambo hayo yana athari hasi zaidi kuliko matarajio chanya waliyonayo Vijana.

Wito huo umetolewa na Hamad Abdallah, Mkazi wa Chanika Jijini Dar Es Salaam kufuatia vurugu na matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea siku ya ya uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisema jambo lile lilikuwa gumu na lisililokubalika.

Amewasihi Vijana kuachana na mikumbo hiyo, akisema ana uhakika kuwa wengi wa Vijana walioshiriki katika matukio yale ya uhalifu hawakuwa wakijua chanzo na asili ya matukio yale kutokana na wengi wao kuwa wamerubuniwa kupitia kwenye Mitandao ya Kijamii.

Monday, 17 November 2025

Mkazi wa Sangara bado yuko gizani "sikuwahi kuzoea kile ambacho Kilitokea Oktoba 29

11/17/2025 07:49:00 pm

Bi. Aisha Athuman Yunga Mkazi wa Mtaa wa Sangara, Chanika Mkoani Dar Es Salaam amesema hakuwahi kuzoea kile ambacho Kilitokea Oktoba 29, 2025, akimuomba Mwenyenzi Mungu kusaidia katika kuilinda na kuistawisha amani ya Tanzania.

Bi. Aisha pia ametoa wito kwa wananchi kuilinda amani na kutoshawishiwa kufanya tena vurugu na ghasia kama zilizotokea Jumatano ya Oktoba 29, 2025, akisema kutetereka kwa amani ya Tanzania ni kuharibika kwa maisha ya watanzania, hivyo ni muhimu kuilinda kwa maslahi ya Tanzania na ustawi wao binafsi.

"Tulishazoea kuwa uchaguzi ukifanyika, ukimalizika tunaendelea na shughuli zetu lakini siku ile ilikuwa siku ya tofauti kabisa na matokeo yake tukawekwa ndani suala ambalo hatuliwezi kutokana na mtindo wetu wa maisha, mimi niombe tu kila mtu aendelee kuhamasisha amani nchini." Amesema Bi. Yunga.

Bi Yunga pia amewashukuru Viongozi wa dini kwa kuendelea kuiombea Tanzania izidi kuwa na amani, akiwakumbusha wananchi kuwa amani ndiyo kila kitu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, akiwataka wananchi kuwakataa kwa nguvu zote wale wote wanaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, akiwataka Vijana kuachana na wanaofuata mikumbo na ushawishishi.

MWANAJESHI WA MAREKANI KUTOKA KENYA ASHIKILIWA KWA KUINGIA NA MABOMU NCHINI

11/17/2025 01:03:00 pm


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya Novemba 16, 2025 majira ya saa sita mchana  katika eneo la Mpaka wa T Janzania na Kenya- Sirari, limethibitisha kumkamata Bw. Charles Onkuri Ongeta (30) Mwenye Uraia Pacha wa Kenya na Marekani akiwa na mabomu manne ya kurushwa kwa mkono aina ya CS- M68 akitokea Kenya kuingia Tanzania.

Kulingana na Taarifa ya Polisi kwa Vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP ) Mark Njera, Ongeta ni Mwanajeshi wa Jeshi la Marekani mwenye cheo cha  Sajenti na alikuwa akiingia nchini kwa kutumia gari yenye usajili wa KDP 502 Y, aina ya Toyota Landcruiser.

Polisi imesema mabomu hayo kulingana na sheria za nchi za umiliki wa silaha ni marufuku kuingia nchini hata kama angekuwa na kibali ambapo ushahidi unaendelea kukusanywa sambamba na kuhojiwa kwa tuhuma hizo ili hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa huyo.

Saturday, 15 November 2025

TAIFA LAPATA TUMAINI JIPYA KUPITIA HOTUBA YA RAIS SAMIA

11/15/2025 06:54:00 pm

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali linalo shughulikia watu wenye ulemavu la Disability of Hope Maiko Salali (FDH)amepongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa  bungeni, akisema imekuwa ni mwanga mpya kwa taifa lililopitia mtihani mzito katika kipindi cha uchaguzi.

Ametoa pole kwa Watanzania wote kwa changamoto na maumivu yaliyotokea katika kipindi hicho, akisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia, taifa litapita salama na kurejea kwenye mshikamano.

Akichambua hotuba ya Rais Samia amesema imejibu matarajio na mahitaji ya Watanzania, hasa yale yanayohusu kuponya majeraha, kurejesha imani, na kufungua ukurasa mpya wa maridhiano ya kitaifa.

Ameeleza kuwa hotuba hiyo ilisubiriwa kwa hamu kubwa na imekuja kujibu maswali yote yaliyokuwa yakizungumzwa na wananchi kwa muda mrefu.

“Rais amefungua mlango wa mazungumzo na hii ina maana kubwa — Tanzania ina kiongozi msikivu, anayejali watu wake na anayetamani kuona nchi inaendelea mbele kwa umoja,” amesema.

Amegusia pia athari zinazowakumba watu wenye ulemavu pindi kunapotokea uvunjifu wa amani amesema,asiyeona hawezi kukimbia hatari,kiziwi anaweza asisikie tahadhari, kwa ujumla, kundi hilo ndilo huwa katika hatari zaidi wakati wa vurugu, "ameeleza

Amesema hatua ya Rais Samia ya kutoa msamaha na kuwaachia huru vijana waliowekwa ndani inaonekana kama tiba ya majeraha , hasa kwa makundi kama watu wenye ulemavu ambao huathirika moja kwa moja wakati amani inapotea.

Kiwanja cha maridhiano, amesema, kinatoa fursa ya taifa kujiponya na kurejesha nguvu ya pamoja. Ameongeza kuwa watu wenye ulemavu wanampongeza Rais kwa uamuzi wake wa busara na kwa kuonyesha uongozi unaotanguliza maelewano kuliko migawanyiko.

Akitoa wito kwa vijana, amekumbusha kuwa walinzi wakuu wa nchi ni vijana wenyewe, hivyo wanapaswa kujilinda kwa kujiepusha na mambo yanayoweza kuivuruga Tanzania au kupandikiza mgawanyiko.

“Tutofautiana kwa mitazamo, ndiyo demokrasia,lakini tusitofautiane mpaka kuliumiza taifa.”amesema

Amewataka viongozi wa kisiasa kuona kipindi hiki si cha kunyoosheana vidole, bali ni muda wa kurejesha utamaduni wetu wa amani, upendo na umoja  misingi ambayo imeijenga Tanzania kwa vizazi vingi.

UPIGAJI KURA NI NJIA YA KHERI NA SALAMA YA KUBADILISHA UONGOZI

11/15/2025 06:53:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewashukuru na kuwapongeza Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki vyema kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania suala ambalo limeonesha wananchi kuthibitisha kuwa ushiriki wa uchaguzi ndiyo njia ya uhakika na salama ya kubadilisha Viongozi wasioridhika nao.

"Njia nyingine zozote hazina kheri wala salama ndani yake." Amesisitiza Dkt. Samia wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ijumaa Novemba 14, 2025 Bungeni Mjini Dodoma.

Dkt. Samia ameipongeza pia Tume huru ya Taifa ya uchaguzi kwa kuendesha vyema uchaguzi Mkuu huu, ukiwa wa kwanza tangu kuundwa upya kwa tume hiyo, akisema kwa mara ya kwanza Wakurugenzi wa Halmashauri hawakusimamia uchaguzi na hakuna Mgombea aliyepita bila ya kupingwa kwenye Majimbo na Kata zilizoshiriki uchaguzi.

"Utaratibu pia uliofanyika wa kuongeza vituo vya kupigia kura ulisaidia sana kuondoa msongamano katika Vituo vya kupigia kura na kwa hakika upigaji wa kura ulirahisishwa sana na haikuchukua muda mwingi kwa wananchi suala ambalo limewafanya baadhi ya waangalizi wa uchaguzi kudhani kwamba wananchi hawakujitokeza kupiga kura." Amesema Rais Samia.

Aidha Dkt. Samia pia ameipongeza Tume hiyo kwa namna mchakato wa Kampeni ulivyoratibiwa Vyema, akisema wagombea wote na Vyama vyao vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi hakuna aliyekosa uwanja wa kufanyia kampeni.

NIMEUNDA TUME KUCHUNGUZA CHANZO, VURUGU ZA OKTOBA 29- RAIS SAMIA

11/15/2025 06:53:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza Wabunge wa Bunge la Tanzania na wageni waalikwa kusimama na kuomba kwa dakika moja kwaajili ya Wananchi waliopoteza maisha kwenye vurugu na ghasia za Jumatano ya Oktoba 29, 2025 katika Miji ya Arusha, Dar Es Salaam, Mbeya, Mwanza na Songwe.

Rais Samia ameongoza jambo hilo leo Ijumaa Novemba 14, 2025 Bungeni Mjini Dodoma wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 13 la Tanzania akitangaza pia kuunda Tume maalumu ya kuchunguza tukio hilo, akitoa pole pia kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao.

"Serikali imechukua hatua ya kuunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea ili tujue kiini cha tatizo, taarifa hiyo itatuongoza kujielekeza kwenye mazungumzo ya kuleta maelewano na amani." Ametangaza Rais Samia.

Akieleza namna ambavyo ameumizwa na tukio hilo, Rais Samia pia amewaombea kheri majeruhi wote huku pia akiwaomba waliopoteza mali zao kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Friday, 14 November 2025

JUMUIYA YA KIKRISTO NCHINI YAUNGA MKONO AHADI YA RAIS SAMIA YA MARIDHIANO YA KITAIFA

11/14/2025 02:21:00 pm

Jumuiya ya Kikristo nchini Tanzania CCT, imesisitiza haja ya kufanyika kwa mazungumzo ya Kitaifa na yatakayojumuisha wadau mbalimbali ili kufanya tathimini ya matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29,2025 na kuweka kwa pamoja mikakati ya umoja, amani, haki na maridhiano nchini.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya CCT Askofu Dkt. Stanley Hotay alipozungumza na waandishi wa habari Mjini Dar Es Salaam, akiungana na  msisitizo wa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuanzisha mchakato wa maridhiano mara baada ya uchaguzi Mkuu.

"CCT inashauri kufanyika kwa mazungumzo ya Kitaifa yatakayojumuisha wadau mbalimbali kwa lengo la kufanyika kwa tathmini ya matukio yaliyotokea na kuweka mikakati ya kuimarisha amani, umoja na maridhiano kama alivyosema Mhe. Rais." Amesema Dkt. Hotay.

Kiongozi huyo wa dini amesema serikali pia inapaswa kutoa msaada ea kibinadamu kwa familia zilizoathirika ikiwa ni pamoja na kuwasaidia majeruhi na kuchukua hatua za kurejesha hali ya utulivu nchini, akisema kanisa hilo linaamini kuwa amani ya kweli hupatikana kwa haki.

RAIS SAMIA AMTAHADHARISHA DKT. MWIGULU DHIDI YA VISHAWISHI VYA MARAFIKI WA MADARAKA

11/14/2025 02:16:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtakia kheri Waziri Mkuu mpya wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akimtaka kuepuka vishawishi vya ndugu, jamaa na marafiki na badala yake ajielekeze zaidi katika kuwatumikia Watanzania.

Rais Samia amebainisha hayo leo Ijumaa Novemba 14, 2025 katika hotuba yake muda mfupi baada ya kumuapisha Dkt. Nchemba Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, akimtaka kusimamia kikamilifu utekelezaji wa yale yaliyoahidiwa kwa watanzania wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu.

"Kwa umri wako mzigo huu ni mkubwa na vishawishi ni vingi kutoka kwa marafiki, ndugu, jamaa na wengine, nafasi yako hii haina rafiki, haina ndugu, haina jamaa- ni nafasi ya kulitumikia Taifa kwahiyo nikutakie kila la kheri katika utumishi wako." Amesema Rais Samia.

Rais Samia amesisitiza kuwa muda ni mchache katika kutekeleza yale waliyoahidi kwa wananchi, akimtaka kusimamia vyema baraza la Mawaziri kwa kutumia vyema uzoefu wake katika Wizara ya fedha na kumsimamia vyema atakayekuwa Waziri wa fedha ili fedha zipatikane katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Dkt. Samia katika hatua nyingine leo mchana anatarajiwa kuzindua Bunge la 13 la Tanzania, akieleza kuwa katika hotuba yake ataeleza mwelekeo wa Serikali yake na vile vitakavyokuwa vipaumbele katika miaka mitano ijayo.

Thursday, 13 November 2025

WABUNGE WAFUNGUKA UTEUZI WA WAZIRI MKUU NCHI IMEPATA WAZIRI MKUU SAHIHI.

11/13/2025 08:00:00 pm

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu, uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni uamuzi sahihi unaoonyesha dhamira ya kuhakikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kwa weledi na ufanisi.

Wakizungumza nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Dkt. Mwigulu kuthibitishwa rasmi na Bunge kwa kura 369 kati ya kura 371, wabunge hao wamesema wana imani kubwa kuwa Waziri Mkuu huyo ataendelea kusimamia ipasavyo maendeleo ya nchi na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu, na Mbunge wa Simanjiro  (CCM) James Ole Millya wamesema wanaaamini  kuwa Dkt. Mwigulu atatoa kipaumbele katika kutatua changamoto za vijana, hususan tatizo la ukosefu wa ajira, ili kuhakikisha kundi hilo muhimu katika maendeleo ya taifa linanufaika na fursa zilizopo.

Wabunge hao wameongeza kuwa uteuzi huo ni uthibitisho wa uongozi makini wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza misingi ya uwajibikaji, utendaji bora na maendeleo endelevu kwa Watanzania wote.

LUKUVI AMMWAGIA SIFA DKT. MWIGULU "RAIS SAMIA HAJAKOSEA KUMTEUA"

11/13/2025 03:48:00 pm


Mbunge wa Jimbo la Isimani Mkoani Iringa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. William Lukuvi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hajakosea kumteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kutokana na weledi, uwezo wa uzoefu wake katika uongozi nchini.

Lukuvi, Miongoni mwa wanasiasa wa muda mrefu kwenye Bunge la Tanzania ameutaja ubobevu wa kitaaluma wa Dkt. Nchemba kama sababu nyingine muhimu wa yeye kuridhia uteuzi wake, akisema kufanya kwake kazi Benki kuu ya Tanzania kabla ya kuingia kwenye siasa kunathibitisha uwezo mkubwa alionao Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Lukuvi amezungumzia pia uzoefu wa Dkt. Nchemba ndani ya Chama Cha Mapinduzi, akisema amekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa miaka mingi, Mjumbe wa kamati kuu na Mjumbe wa sekretarieti ya Chama hicho pamoja na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kati ya mwaka 2012-2015.

Leo Alhamisi Bunge la 13 la Tanzania limemthibitisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu kwa kura 369 kati ya kura 371 zilizopigwa na sasa kulingana na taarifa ya Ikulu Mteule huyo ataapishwa Ijumaa ya Novemba 14, 2025 Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

TUMEPATA WAZIRI MKUU SAHIHI- ANNA MALECELA

11/13/2025 03:23:00 pm

Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mkoani Kilimanjaro Mhe. Anne Kilango Malecela amesema Rais Samia Suluhu Hassan amegusa mioyo ya Watanzania wengi kutokana na kumteua Mbunge wa Iramba Magharibi Mkoani Singida Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
"Sifa kubwa ya Dkt. Mwigulu ni mtu anayefikika na lazima niseme ukweli kuna watu wakiwa mawaziri wanakuwa vigumu kuwafikia lakini kwa Mwigulu tangu akiwa Naibu Waziri, Waziri mpaka Waziri wa fedha ni mtu anayefikika na kila mtu na nyumbani kwake ni nyumbani kwa watu wengi." Amesema Mhe. Anna Malecela.

Amemuelezea pia kama mtu mwenye upendo kwa kila mmoja, akisema Wabunge wa Bunge la 13 pamoja na Wananchi wa Tanzania wamempata Kiongozi sahihi anayeweza kusimama kuwasemea na kuwatetea.

Malecela ametoa kauli hiyo mapema leo Novemba 13, 2025 Bungeni Mjini Dodoma wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipowasilisha Jina la Dkt. Mwigulu Bungeni hapo ili kuweza kuidhinishwa kuwa Waziri Mkuu, akitarajiwa kuapishwa kesho Ijumaa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tayari kuanza majukumu yake mapya kwa miaka mitano ijayo katika serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

WAZIRI MKUU MTEULE AAHIDI KUREJESHA HESHIMA YA UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

11/13/2025 01:46:00 pm

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Alhamisi Novemba 13, 2025 limemthibitisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiahidi kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha kuwa maono na ahadi za Rais Samia Suluhu Hassan zinateketekelezwa ili kuwaletea wananchi ustawi na maendeleo kwa miaka mitano ijayo.

Uteuzi wa Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa miaka mitano ya awali ya serikali ya awamu ya sita, umetangazwa rasmi bungeni mjini Dodoma, akithibitishwa kwa kura 369 za ndio kati ya 371 zilizopigwa na wabunge huku kura mbili zikiharibika.

Mwigulu anajulikana kama mfano wa mafanikio yanayotokana na bidii na kujituma. Alikulia katika mazingira ya kijijini na alitoka katika familia yenye hali ya kawaida, ambapo aliwahi kuchunga ng'ombe nyikani akiwa kijana mdogo. Maisha hayo yalimfundisha nidhamu, uvumilivu na kuthamini kazi halali. Mara kadhaa amekuwa akisimulia hadithi ya maisha yake kama njia ya kuwahamasisha vijana kupambana kupitia elimu na kujituma.

Akieleza kutambua namna ambavyo Dkt. Samia amejitambulisha kama Kiongozi wa matokeo, katika hotuba yake ya shukrani bungeni Dkt. Mwigulu ametoa rai kwa Watanzania kumtanguliza Mungu na kuhakikisha amani inaendelea kuwepo nchini, akitoa onyo kwa watumishi wazembe, wala rushwa na wenye lugha chafu kwa Watanzania.

"Kwa kuzingatia kazi kubwa iliyopo mbele yetu naomba niseme kuwa watumishi wa umma na Watanzania lazima tuwe tayari, lazima tuende na gia ya kupandia mlima, watumishi wa umma wavivu, wazembe, wala rushwa na wenye lugha mbaya kwa Watanzania tuwe tayari na nitakuja na fekeo na rato, lazima maono ya Rais na ahadi zake zitekelezwe." Amesisitiza Mhe. Mwigulu.

Aidha Mwigulu amemshukuru Rais Samia kwa imani yake kwake pamoja na Wabunge wenzake kwa kumuamini na kumkopesha imani, akisema Watanzania wote watasikilizwa kwa nidhamu kila ofisi ya umma na pamoja na kutoa nafasi sawa kwa wabunge wote wa Bunge la 13 hasa kwa wale walio wachache, wanaotokana na vyama vya upinzani.

Dkt. Mwigulu amewahi kushika nafasi mbalimbali serikalini. Alianza kama Naibu Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete. Baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mwaka 2015, kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2016. Mwaka 2021 aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, nafasi aliyoishikilia hadi uteuzi wake kuwa Waziri Mkuu.

Wednesday, 12 November 2025

WANANCHI WAHIMIZA UVUMILIVU, MCHAKATO WA MARIDHIANO YA KITAIFA

11/12/2025 11:30:00 am


Kama ilivyoahidiwa na Rais wa Tanzania kwamba moja ya ahadi zake ni pamoja na kutafuta maridhiano ya Kitaifa na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya ili kulileta Taifa pamoja na kushughulikia changamoto za wadau mbalimbali, wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamewashauri makundi mbalimbali ya kijamii kuacha mihemko na kuisikiliza serikali, huku serikali pia ikitakiwa kuusikiliza upande wa wananchi kujua kile wanachokitaka.

Kauli za wananchi zinakuja siku chache pia mara baada ya Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kusisitiza dhamira hiyo ya Rais Samia kuhusu maridhiano ya Kitaifa ili kusikiliza wananchi na kuendelea kuifanya Tanzania kuwa yenye amani na utulivu.

"Ni dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaanzisha mazungumzo ya maridhiano ili kuhakikisha hata hao wachache wanapata nafasi ya kusikilizwa ili kuwa na taifa lenye amani na umoja na kuendelea kuwa mfano wa utulivu katika Afrika na dunia.”Alisema Dkt. Nchimbi kwenye Mkutano wa Kimataifa uliofanyika siku mbili zilizopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wanaoishi Chanika, Jijini Dar Es salaam wamesisitiza umuhimu wa maridhiano hayo ili kujenga jamii yenye amani na ustawi, wakirejea athari kubwa zilizotokea wakati wa ghasia na vurugu za Oktova 29, 2025.

Wamelaani pia utafutaji wa haki kwa kuhamasisha na kutenda vitendo vyenye kuhatarisha amani ya Tanzania, wito zaidi ukitolewa kwa vijana kuachana na mihemko na ushawishi wa kufanya vurugu na badala yake kupendelea zaidi njia ya mazungumzo na masikilizano katika kushughulikia changamoto zinazowakabili katika maeneo mbalimbali.

Tuesday, 11 November 2025

RC MAKALLA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI ARUSHA, WAFANYA DUA MAALUM KUOMBEA AMANI

11/11/2025 05:43:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla  amekutana na Viongozi wa dini na wa kimila kutoka Mkoa wa Arusha, akitoa Rai kwa Viongozi hao kuendelea kuhubiri amani kwa waumini na wafuasi wao pamoja na kuiombea nchi ya Tanzania.

CPA Makalla kando ya kujadiliana masuala mbalimbali na Viongozi hao wa dini katika ujenzi wa jamii yenye amani, upendo na mshikamano, alishiriki sala na dua  maalumu iliyoongozwa na Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali akiwemo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya maridhiano ya amani Tanzania Dkt. Israel Ole Maasa.

Rc Makalla amesisitiza umuhimu wa Viongozi hao pia kuendelea kuhubiri kuhusu amani na kushirikiana na waumini wao kuliombea Taifa la Tanzania, Viongozi hao wa dini wakiahidi pia kushirikiana na serikali katika kuhakikisha jamii inakuwa na amani na mazingira tulivu.

"Muhimu kuhubiri kuwa hakuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania na ili tusonge mbele katika maendeleo ni muhimu kuendelea kuwa na amani na utulivu kwahiyo kila mmoja wetu arejeshe matumaini na maombi hayo kwamba Watanzania tunahitaji amani hivyo sala na maombi yetu kwa Mwenyenzi Mungu ni amani na sisi serikali tutaendelea kupokea ushauri wenu na kuufanyia kazi." Amesisitiza Mhe. Makalla.

Viongozi hao wa dini katika maombi yao, wameombea amani ya Tanzania na kuwaombea Viongozi wakuu wa Tanzania wakiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wao wa ngazi mbalimbali akiwemo Mhe. Makalla wakimuomba Mwenyenzi Mungu awape baraka, nguvu na utashi zaidi katika kuwatumikia watanzania na kuhakikisha Tanzania inabaki salama.

TUWAKATAE WACHOCHEZI, GHASIA, VURUGU VINATURUDISHA NYUMA KIMAENDELEO

11/11/2025 05:42:00 pm

Mjasiriamali Kijana Bw. Peter Shaaban Gerald, Mkazi wa Kimara Dar Es Salaam amewasihi Vijana wenzake kujiepusha na uratibu na ufanyaji wa matukio ya ghasia na vurugu, yenye kuhatarisha amani ya Tanzania kwani athari za Kijamii na kiuchumi ni nyingi kutokana na mtindo wa maisha na namna ya kujipatia Kipato kwa Watanzania wengi hususan Vijana.

Ameyaeleza hayo wakati akizungumzia uzoefu alioupata kwa takribani siku saba zilizopita, zikitokana na uharibifu na ghasia za Oktoba 29, 2025 kwenye Majiji na Miji ya Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Songwe, akisema uchumi wake umetetereka pakubwa kutokana na kukosa kipato kulingana na kazi yake ya kumtaka kuwa barabarani kila wakati ili kuwafuata na kuwatafuta wateja.

"Sisi tumezoea kutembea barabarani kujitafutia chochote, na unajua maisha ya Vijana ni gheto (Vyumba vya kuishi) sasa si sahihi kuandamana kwasababu sisi Vijana wengi tuliumia, wengine walizipoteza pia familia zao na tumezoea Tanzania ni nchi ya amani hivyo ni muhimu kuilinda amani yetu sisi kama Vijana." Amesisitiza Bw. Peter.

Peter amekumbusha pia wajibu wa Vijana katika kulinda amani ya Tanzania kwa msingi wa kuliandaa Taifa la kesho kutokana na nguvu kazi yao, akiishukuru serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama kwa kurejesha amani katika maeneo yote nchini na hivyo kuruhusu shughuli za kiuchumi na kijamii kuweza kuendelea kama kawaida.
                 https://www.instagram.com/reel/DQ50-bXjEhQ/?igsh=cDg0djlpdXZtZGNn

Monday, 10 November 2025

MOSHI MWEUPE NJIA YA MARIDHIANO, VIONGOZI WA CHADEMA AKIWEMO AMANI GOLUGWA WAACHIWA KWA DHAMANA

11/10/2025 09:18:00 pm


Siku moja baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza  kuondoa mifarakano na kulileta pamoja Taifa, tayari Viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  wameachiwa kwa dhamana.
Viongozi hao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara John Heche, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa, Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama Boniface Jacob (Boni Yai) na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema,  dhamana yao umetolewa leo 10 Novemba 2025

Hii inaweza kuwa hatua nzuri kwenye safari ya Maridhiano kama alivyotangaza  Dkt. Nchimbi, kuondoa mifarakano na kuleta pamoja taifa, kulinda amani na kurudisha umoja baada ya migawanyiko ya Uchaguzi!?

Heche yeye alikuwa anashikiliwa na Polisi tangu Oktoba 22, 2025, alipokamatwa nje ya geti la Mahakama Kuu Dar es Salaam, alipokuwa akienda mahakamani, kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini.

BODABODA WENYE PIKIPIKI ZA MKATABA WALIA NA VURUGU NA GHASIA ZA OKTOBA 29.

11/10/2025 03:15:00 pm

Bwana Issa Salala, Afisa usafirishaji abiria kwa kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda anayefanya shughuli zake Jijini Dar Es Salaam ameeleza namna ambavyo ghasia, vurugu na maandamano ya Oktoba 29, 2025 yalivyomuingiza kwenye madeni makubwa yasiyolipika, kutokana na ghasia zile kuzuka wakati ambao hakuwa na akiba yoyote ndani kwake.

Salala amebainisha hayo wakati akizungumzia athari za ghasia na uharibifu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025 kwenye maeneo mbalimbali ys Mkoa huo, akisema suala hilo lilimfanya yeye kutotoka ndani zaidi ya siku tano, akiendesha pikipiki isiyokuwa yake, suala ambalo lilifanya aliyemkodishia pikipiki kudai malipo yake wakati alipokuwa amesimama kufanya kazi kutokana na vurugu hizo.

Aidha Salala amezungumzia pia mfumuko mkubwa wa bei uliojitokeza kutokana na uhaba wa bidhaa na huduma mbalimbali kwenye eneo lake, akisema Unga uliokuwa ukiuzwa Kilogramu moja shilingi 1,500 waliuziwa shilingi 4,000 huku Mchele wa Shilingi 2,000 kwa Kilo moja wakiuziwa zaidi ya shilingi 5,000.

"Ni muhimu kwasisi Vijana kufikiria mbele kabla hujafanya kitu, vijana walioandamana hawakufikiria matokeo ya baadae. Leo unga wa 1, 500 unaununua 4, 000, Mchele wa 2,000 unaunua 5,000 na kipindi hicho kuna zuio la kutotoka nje kutokana na usalama, sasa hela unatoa wapi? Tumeingia ndani nilikuwa mnene, tumetoka nimepungua kwani mwili umeisha huu sasa hivi." Amesema.

Ni huzuni kila kona vurugu za oktoba 29,2025 zakosesha huduma za kijamii Mwanza

11/10/2025 11:02:00 am
Ghasia, vurugu na uharibifu mkubwa uliofanywa na magenge ya Vijana hapo Oktoba 29, 2025, umewaacha wananchi wa Mkoa wa Mwanza kukosa huduma muhimu za kijamii, huku pia mamia ya wananchi wakikosa ajira na kipato kutokana na matukio ya moto na wizi ulioangamiza maeneo yao ya kazi katika Eneo la Buhongwa Mkoani humo.

Kwa nyakati tofauti, magenge ya Vijana  katika siku ya uchaguzi Mkuu wa Jumatano Oktoba 29, 2025, wakati wengine wakipiga kura kuwachagua Viongozi wao watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo, wao  walivamia, kuiba na kuchoma moto Chuo cha Ufundi stadi VETA cha Buhongwa Mkoani Mwanza pamoja na kuiba na kuteketeza kwa moto Vituo vya uuzaji mafuta vya Olypic Petrol na Lake Oil Energies pamoja na kituo cha uuzaji wa bidhaa mbalimbali cha Empire store Kilichopo Igoma sambamba na magari yaliyokuwa yamepaki kwenye maeneo hayo.

Aidha wahalifu hao pia kando ya kuiba na kuteketeza kwa moto Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Buhongwa Mkoani humo, waliiba mali na samani mbalimbali za Ofisi pamoja na kuteketeza kituo cha Polisi Buhongwa, Kiwanda cha magodoro cha Super Banco na Kiwanda cha Vita Foam mkoani humo, suala ambalo limetajwa kuwaacha mamia ya Vijana na wananchi wa Mkoa huo na Mikoa ya jirani kukosa huduma mbalimbali na zaidi ajira kutokana na uharibifu huo mkubwa.

TUIJENGE NCHI YETU KWA PAMOJA NA KUOMBEA AMANI IDUMU- KIROBA

11/10/2025 11:02:00 am

Adam Kiroba, Mkazi wa Mkera, Chanika, Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam,  amewataka watanzania hususani Vijana kote nchini kudumisha amani, mshikamano na upendo kwenye jamii na kujiepusha na vurugu na uvunjifu wa amani kwani mara zote waathirika wakubwa wa vurugu mara zote wamekuwa akinamama, Watoto, Wazee pamoja na wale wasiokuwa na hatia kutoka kundi la wananchi wenye kipato cha chini.

"Mimi ninachowaomba watanzania ni kuwa nchi yetu inasifika kuwa kisiwa cha amani, tuendelee na sifa hiyo kwasababu machafuko ya juzi athari zake tumeziona na wengine mpaka leo biashara na sehemu za kuishi hawana. Niwasihi watanzania wenzangu tudumishe amani iliyopo na tusiwe sehemu ya kuhamasisha hicho kinachoendelea na tuwe wavumilivu na kuangalia namna ya kuijenga nchi yetu." Amesisitiza Bw. Kiroba.

Bw. Kiroba akizungumza na mwandishi wetu wa habari leo Jumapili Novemba 09, 2025 amewataka pia Vijana kutofuata mikumbo kutoka kwa baadhi ya watu, akiwahamasisha pia wale wote wenye kuamini katika Mungu kupitia dini zao na madhehebu mbalimbali kuendelea kuiombea nchi ya Tanzania ili amani, umoja na mshikamano viendelee kudumu kwa maslahi ya kila Mtanzania.

Amesisitiza pia umuhimu wa kutambua faida za amani kwenye jamii, akisema ghasia na vurugu za Oktoba 29, 2025 kumewagharimu pia watu wasiokuwa na hatia, kusababisha ugumu wa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii pamoja na kupanda kwa gharama za maisha na kuyumba kwa uchumi kwa watu wengi wa kipato cha chini.

Saturday, 8 November 2025

Amani imerejea aeleza namna mfumuko wa bei uliwaathiri asema mafuta ya petroli yaliuzwa kwa shilingi 15,000 kwa Lita moja

11/08/2025 06:11:00 pm
AMANI IMEREJEA, TUNAISHUKURU SERIKALI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

Shaban Moshi Shaban, Afisa usafirishaji kwa kutumia Pikipiki maarufu kama Bodaboda kwenye eneo la Kimara mwisho Mkoani Dar Es Salaam, ameishukuru serikali pamoja Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania, kwa jitihada kubwa zilizochukuliwa ili kuirejesha amani ya Tanzania, akieleza kuwa vurugu za Oktoba 29, 2025 ziliwaweka kwenye wakati mgumu kiuchumi na kijamii.

Bw. Moshi wakati akizungumza na chombo hiki cha habari, amesema ghasia hizo pamoja na zuio la kutoonekana nje kuanzia saa kumi na mbili Jioni lililotolewa na Jeshi la Polisi liliwaletea athari nyingi za kiuchumi kutokana na kukosa abiria na kipato, kwani shughuli za usafirishaji walikuwa wamezoea kuzifanya kwa muda wa saa 24.

"Kitu walichokifanya waliokuwa wakijiita waandamanaji ni kitu ambacho hakifai kwani maandamano haya hayakuwa na ujumbe wowote kwa serikali lakini pia maandamano yale yalikuwa kosa kisheria kwasababu walifanya uhalifu pia katika baadhi ya sehemu kwahiyo niwashauri waache hicho walichokifanya." Amesema Bw. Moshi.

Aidha ameeleza pia namna ambavyo mfumuko wa bei uliwaathiri kwa kiasi kikubwa, akisema mafuta ya petroli yaliuzwa kwa shilingi 15,000 kwa Lita moja hivyo kusababisha adha kubwa kwao ikiwa ni pamoja na kuwapoteza wateja waliolalamikia kupanda kwa bei za usafiri huo wa Pikipiki.

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUFUATA TARATIBU SAHIHI KUDAI HAKI ZAO

11/08/2025 11:12:00 am

Wito umetolewa kwa watanzania wa kutii sheria, kuisikiliza serikali na kutafuta haki kwa namna na taratibu zinazoruhusiwa kisheria badala ya kuratibu na kufanya ghasia, uharibifu na vurugu kama sehemu ya kushinikiza serikali kutekeleza matakwa mbalimbali.

Asraji Likwati, Mwenyekiti wa wasafirishaji abiria kwa njia ya Pikipiki Kimara Mkoani Dar Es Salaam ametoa wito huo leo Novemba 08, 2025 wakati akizungumzia athari za ghasia zilizotokea Jumatano ya Oktoba 28, 2025 siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akiwakosoa baadhi ya vijana ambao walifanya ghasia hizo na kuiba na kuharibu mali na vitega uchumi vya wananchi wa hali ya chini wasiokuwa na nafasi yoyote kisiasa na wasiohusika na kile kilichokuwa kikilalamikiwa na makundi hayo.

"Nitoa wito tu kwamba tuisikilize serikali, haki tuitafute kwa taratibu sahihi kwani ni wengi waliovunjiwa na kuibiwa mfano unaenda kumuibia mangi ambaye hana hata ushawishi na masuala ya kisiasa. Juzi hapa tumelalamika kuhusu mwendokasi serikali ikatusikia na kuleta mabasi mapya, leo wanayachoma moto, kiukweli hii haikubaliki." Amesisitiza Bwana Likwati.

Ameeleza athari nyingine kuwa ni pamoja na kudorora kwa mzunguko wa fedha, kuathirika kwa biashara kati ya Tanzania na nchi jirani zenye kuitegemea bandari ya Dar Es Salaam pamoja na kutikisika kwa sifa ya Tanzania kimataifa ya kuwa Taifa lenye amani, uhuru na mshikamano kwa watu wake.

MALI ZA UMMA NA WATU BINAFSI ZIMECHOMWA, HAYAKUWA MAANDAMANO, ZILIKUWA VURUGU

11/08/2025 09:07:00 am

Samwel Salum Mkazi wa kimara Jijini Dar es Salaam amelaani maandamano ya Oktoba 29 akieleza kuwa lengo lake lilikuwa kuharibu mali, kujeruhi na kusababisha hasara kubwa kwa uchumi wa Tanzania.


Bwana Samwel ameyasema haya alipozungumza na waandishi wa Habari kuhusu manufaa na athari za maandamano hayo ambayo kwake ameyaita vurugu na Wala sio maandamano kwani yalikuwa hayana ujumbe wowote kwa Serikali

Friday, 7 November 2025

WANANCHI WALIA NA UGUMU WA MAISHA ULIOSABABISHWA NA GHASIA ZA OKTOBA 29

11/07/2025 10:15:00 am


Kutatizika kwa shughuli za kiuchumi kwa takribani siku tano mara baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kumeelezwa kusababisha adha kubwa ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam hasa kwa wale ambao wamekuwa tegemeo kwa familia na wazazi wao.

Kauli hiyo imeelezwa na wananchi wa Mkoa huo wakati wakizungumza na waandishi wa habari, siku chache mara baada ya Tangazo la Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutaka shughuli za Kijamii na kiuchumi kuendelea kama kawaida mara baada ya ghasia na vurugu za Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

"Kutokana na vurugu na ghasia za Oktoba 29, sisi wananchi tunaotegemewa na familia na wazazi tumeathirika sana, siku tano kwenye maisha yetu ni nyingi sana na bahati mbaya hali hii ambayo mimi ni mara ya kwanza kuishuhudia haijaangalia kipato cha mtu kwasababu kukosekana kwa amani kulikotokea kumesababisha hata wenye kipato kukosa huduma na bidhaa muhimu." Amesema Bw. Habibu Sadick, Dereva wa Bajaji Jijini Dar Es Salaam.

Kwa upande wake Iddi Mzese, Mkazi wa Changarawe Jijini Dar Es Salaam kando ya kusisitiza namna ambavyo ghasia na vurugu hizo zilivyosababisha ugumu wa maisha, amewataka Vijana kujiepusha na mikumbo yenye kupelekea kujiingiza kwenye ghasia na uvunjifu wa amani, akihimiza ulinzi wa amani na mshikamano uliopo nchini.

Thursday, 6 November 2025

MPAKA WA TANZANIA NA KENYA NI SALAMA- RC MAKALLA*

11/06/2025 08:24:00 pm

 *_Aridhishwa na usalama na ufanyaji biashara eneo la Namanga_* 

 *_Aeleza umuhimu wa Mpaka huo kibiashara na ustawi wa Jamii_* 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ameeleza kuridhishwa na hali ya ulinzi na usalama katika Mpaka wa Namanga unaounganisha Mataifa ya Tanzania na Kenya kupitia Mkoa wa Arusha, akiwashukuru watendaji wa Pande zote mbili wanaofanya kazi kwenye Kituo cha pamoja cha forodha Namanga kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa pande zote.

Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Alhamisi Novemba 06, 2025 Mjini Namanga wakati alipoambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kwaajili ya kukagua hali ya Ulinzi na usalama katika eneo hilo pamoja na kuangazia ufanyaji wa biashara katika eneo hilo mara baada ya maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka shughuli zote za Kijamii na kiuchumi kuendelea katika maeneo mbalimbali nchini mara baada ya uchaguzi Mkuu.

"Nithibitishe kuwa Mpaka wa Tanzania na Kenya ni salama na kituo cha pamoja cha forodha Namanga kipo salama. Kituo hiki ni muhimu kwa nchi zetu zote mbili na kwa wananchi hususani hawa wa Mpakani kwani wao pia ni wanufaika wa moja kwa moja na fursa za kiuchumi na biashara kwahiyo ni muhimu kuendelea kueneza amani, umoja na mshikamano kwenye mpaka huu kwani sote ni wanufaika." Amesema Mhe. Makalla.

CPA Makalla kadhalika amewapongeza  Viongozi na watendaji wa kituo hicho cha forodha ka kuendelea kuimarisha mahusiano na kukuza biashara katika eneo hilo suala ambalo limekifanya Kituo hicho pia kuwa eneo muhimu la mabadilishano ya bidhaa kati ya Tanzania na Kenya, akisema kutetereka kwa Mpaka huo kuna athari kubwa kwa uchumi wa nchi hizo na ustawi wa jamii.

Kwa Upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) kwenye Kituo hicho cha Namanga Bw. Nicholous Mugambi amemuhakikishia CPA Makalla kuwa wataendelea kushirikiana na Mamlaka za Tanzania katika kukuza mahusiano na biashara miongoni mwa nchi hizo mbili, akisisitiza umuhimu wa amani kama msingi wa kufikia mafanikio katika biashara na ustawi wa wananchi wa Tanzania na Kenya.

HAKUNA VITA NZURI, TUILINDE AMANI YA NCHI YETU- MOSHI

11/06/2025 03:40:00 pm

Mfanyabiashara ndogondogo wa Mitaa ya Kongo na Pemba, Kariakoo Jijini Dar Es salaam Bw. Elia Moshi amesisitiza kuwa mara zote haki huwa haidaiwi kwenye machafuko na ghasia, akitoa wito wa Vijana kufikiri juu ya athari za machafuko kabla ya kujiingiza kwenye Hamasa zinazotolewa kwenye Mitandao ya Kijamii na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania.

Bw. Moshi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar Es Salaam, siku tatu mara baada ya hali ya ulinzi na utulivu kurejea katika maeneo mengi nchini mara baada ya ghasia na fujo zilizojiri kwenye Miji mbalimbali nchini wakati wa uchaguzi Mkuu wa Tanzania Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

"Vijana niwaaambie kuwa hakuna Vita nzuri, Vita vina athari kubwa hasa kwetu sisi wa kipato cha chini. Wanaohamasisha Vijana kuingia barabarani wana maisha yao mazuri na hutowaona barabarani ni muhimu kutathmini wale wanaohamasisha ghasia hizo na athari zake kabla ya kuchukua maamuzi." Amesema.

Akizungumzia athari za ghasia hizo, Moshi amesema uchumi ulidorora na kusababisha mfumuko wa bidhaa muhimu za kila siku, akisema kukosa utamaduni wa kuweka akiba kwa Watanzania wengi kumekuwa sababu pia ya wengi kuathirika kutokana na kukosa akiba ya chakula kwenye nyumba zao.

TUTUMIE MITANDAO YA KIJAMII VIZURI NA TULINDE MIUNDOMBINU YETU

11/06/2025 03:40:00 pm

Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wametoa wito wa matumizi sahihi ya Mitandao ya Kijamii na kujiepusha na utoaji wa maoni na uhamasishaji wa uvunjifu wa amani kupitia Mitandao hiyo, wakiiomba serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwasamehe Vijana waliojiingiza katika uvunjifu wa amani kwa kufanya vurugu za Oktoba 29, 2025 katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa nyakati tofauti wakizungumza na Chombo hiki cha habari, Wananchi hao akiwemo Mombeki Gervas na Baraka Nyange, wameeleza pia athari za machafuko na ghasia hizo zilizotokea kwenye Mkoa huo, wakisema mbali ya uharibifu wa miundombinu na mali za umma na za binafsi, wenye familia wamekuwa waathirika zaidi wa ghasia hizo zilizodumu kwa zaidi ya siku mbili.

"Sisi tuna majukumu na zaidi familia zetu. Tofauti na mazoea tuliyokuwa nayo tunapomaliza uchaguzi, Uchaguzi wa mwaka huu umekuja na maandamano na tulikuwa hatuna akiba na maisha ya dar tunayajua huwezi kula bila ya kutoka." Amesisitiza kusema Bw. Mombeki.

Kwa upande wake Bw. Nyange amesema "Hii nchi ni ya kwetu, miundombinu iliyoharibika ni ya Watanzania kwahiyo tunapoharibu miundombinu tunayotumia sisi wenyewe maana yake tunajiumiza wenyewe na tunaumiza uchumi wetu wenyewe." Amesisitiza.

Nyange kando ya kuwataka watanzania hususani Vijana kutumia vyema mitandao ya kijamii nchini kwa maslahi ya Tanzania, amesisitiza pia kulinda na kuitunza miundombinu inayojengwa na serikali nchini, akisema miundombinu hiyo imejengwa kwa faida ya watanzania wenyewe katika kurahisisha shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Wednesday, 5 November 2025

HUDUMA YA MWENDOKASI YASITISHWA KUPISHA TATHMINI YA UHARIBIFU ULIOFANYIKA OKTOBA 29.

11/05/2025 07:46:00 am

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Albert John Chalamila ametangaza kusitisha huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu kama mwendokasi kati ya Gerezani - Kimara na Gerezani - Mbagala Jijini Dar Es Salaam.

Kusitishwa kwa huduma hiyo kulingana na Mhe. Chalamila katika Taarifa yake kwa Vyombo vya habari, kunalenga kutoa nafasi ya kufanyika kwa tathmini ili kujua uharibifu uliofanyika wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025 jijini Dar es Salaam.

Katika maandamano hayo, waandamaji waliharibu miundombinu hususan vituo vya mwendokasi, zaidi katika vituo vilivyopo barabara ya Morogoro kwa kuvunja vituo, mifumo ya ukataji wa tiketi na kuvichoma moto baadhi ya vituo vya kushusha na kupakia abiria.

Chalamila katika taarifa yake amewataka wananchi wote waliokuwa watumiaji wa usafiri huo kutafuta njia mbadala za usafiri katika kipindi hiki wakati ambao unafanyika utaratibu wa kurudisha hali kama ilivyokuwa awali.

“Tunasitisha mara moja usafiri huu ili kufanya tathmini ya kina ya uharibifu uliotokea kwani mifumo ya ukataji tiketi imeharibiwa jambo ambalo linahitaji muda ili kurudisha hali kama ilivyokuwa awali,” amesema Chalamila.

Mkuu huyo wa Mkoa katika hatua nyingine amewaagiza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA kutoa vibali vya muda mfupi kwa mabasi ya kawaida ili yaweze kutoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwenye njia hizo ambazo zilikuwa zikitegemea mabasi ya mwendokasi yaliyosimama kutoa huduma katika barabara tajwa.

WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAHIMIZA AMANI, WAKITAKA WANASIASA KUACHA MALUMBANO

11/05/2025 07:45:00 am

Wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam wameeleza athari kubwa za kiuchumi na Kijamii zilizotokana na ghasia na vurugu za baada ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025, wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake ya kutaka ulinzi na usalama kuimarishwa na shughuli za kijamii na kiuchumi kurejea katika hali yake ya kawaida.

Bw. Eliezer Wilson, Mjumbe wa Taasisi ya Machinga wa Kariakoo (KAWASO) kwa niaba ya wafanyabiashara wadogo wa soko hilo, ametoa kauli hiyo siku moja mara baada ya kuapishwa kwa Rais Samia, ambapo katika hotuba yake ya awali alikemea vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani vilivyotokea Oktoba 29- 31, 2025 kwa baadhi ya watu kuvunja, kuharibu na kutekeleza mali za umma na za binafsi katika mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Mkoani Songwe.

Naye Mfanyabiashara na Kiongozi wa Wafanyabiashara wa soko hilo Bw. Jabir Makunga 
ameeleza athari za ghasia hizo zilizodumu tangu siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 29, 2025 kuwa ni pamoja na Vifo na tabu zilizotokana na kukosekana kwa huduma za matibabu kwenye Vituo vya afya kwenye Mikoa iliyokumbwa na ghasia hizo, huduma za usafiri kudorora, mfadhaiko, hofu na wasiwasi, ukosefu wa mahitaji muhimu ya kila siku pamoja na mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu.

Akieleza kuhusu athari kubwa za Kijamii na kiuchumi zilizojitokeza kutokana na vurugu, ghasia na maandamano ya Oktoba 29, 2025 Mkoani Dar Es Salaam, Mfanyabiashara Fadhil Mwango amewataka Vijana kujiepusha na kufuata mikumbo isiyofaa na yenye kuhamasisha kuhusu Uvunjifu wa amani nchini badala yake wafuate taratibu rasmi zilizopo katika kuwasilisha kero walizonazo.
Adbox