Adbox

Tuesday, 21 October 2025

WANNE JELA MIAKA SABA KWA JARIBIO LA KUMTEKA MFANYABIASHARA

10/21/2025 06:38:00 pm

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Kinondoni, Dar Es Salaam imewahukumu Vijana wanne wakiwemo Mabondud 3ia wawili kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kumteka Mfanyabiashara Deogratus Tarimo, tukio lililoteka hisia za wengi Mitandaoni, wengi wakiwahusisha watu hao na Maafisa wa Vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Vijana hao waliohukumiwa ni Fredrick Nsato (21) Mkazi wa Kibamba, Isaack Mwaifuani (29) Mkazi wa Kimara, Benki Mwakalebela (40) na Bato Twelve (32) Mkazi wa Kimara Bonyokwa Mkoani Dar Es Salaam.

Kabla ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhani Rugemalira kusoma hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Daisy Makakala amesema pamoja na kuwa hana kumbukumbu za makosa ya nyuma ya watuhumiwa wote wanne lakini anaiomba mahakama itoe adhabu sawa na kifungu cha sheria walichoshtakiwa nacho ili jamii ya Tanzania na dunia nzima ifahamu kuwa wanaotenda vitendo vya utekaji wa Raia wa makundi mbalimbali siyo Maafisa waJeshi la Polisi, bali ni watu wa kawaida ambao wamekuwa wakifanya vitendovya kiuhalifu kwa sababu mbalimbali.
"Naomba mahakama iwape adhabu kali washtakiwa kwa sababu vitendo vya utekaji vimeshamiri sana nyakati hizi, hali inayopelekea Jeshi la Polisi kulaumiwa kwa utekaji huo. Hawa watuhumiwa wangefanikiwa kumkamata Deogratius Tarimo akapotea asionekane Jamii ingeamini kuwa ni Polisi ndiyo wamempoteza hasa na vile wakati wanamkamata walikuwa wakijitambulisha kama Askari Polisi toka Kituo cha Gogoni wakati wakijua ni uongo. Hivyo ili kutoa fundisho kwa hawa watuhumiwa waliokutwa na hatia na jamii yote kwa ujumla mahakama iwape adhabu kali."amesema Wakili Makakala.

Kwa upande wao washtakiwa wao waliomba wapunguziwe adhabu na kudai kuwa wao walikuwa wanasaidia kumteka tu baada ya rafiki yao Frederick kuwaomba wamsaidie kumteka, kwa madai kuwa wanahisi Deo alitembea na mke wa rafiki yake Fredrick.

Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka, Fredrick na wenzake walitenda kosa hilo Novemba 11, 2024 eneo la Kiluvya Madukani Lingwenye, lllilopo Wilaya ya Ubungo ambapo Ilielezwa kuwa siku hiyo ya tukio katika eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja walijaribu kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo kwa nia ya kumuweka kizuizini isivyo halali ambapo Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani mahakamani hapo, Desemba 6, 2024 na kusomewa shtaka hilo.

TUNALAANI WOTE WANAOHAMASISHA MAANDAMANO- MALAIGWANAN K'NJARO

10/21/2025 04:27:00 pm

 _Waahidi kuwachagua walinda amani na mshikamano wa Taifa_ 

Viongozi wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania maarufu kama (Malaigwanan) wametoa tamko lao rasmi kwa nchi nzima, la kuunga Mkono kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025, wakilaani uwepo wa hamasa ya kufanyika kwa maandamano siku hiyo wakiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua Viongozi wanaowataka.

Viongozi hao wametoa tamko hilo katika eneo la Donyomorwak Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro kwenye Mkutano wao wa kawaida wa Orkiama ambapo akisoma tamko hilo kwaniaba ya Viongozi hao, Bw. Jeremia Laizer, Katibu wa Malaigwanani Tanzania, ameeleza pia kwamba Jamii hiyo itamuunga Mkono Kiongozi mwenye kutanguliza mbele maslahi ya wananchi pamoja na kulinda amani na utulivu wa Tanzania.

"Tunawahimiza wananchi wote kudumisha amani, mshikamano na utulivu, kuanzia ngazi ya shina, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda hadi Taifa zima, tukiepuka maneno ya uchochezi, migawanyiko, na fitina. Tuchague maendeleo, umoja, na mustakabali mwema wa vizazi vya sasa na vijavyo. Tuwe nguzo ya amani, nuru ya matumaini, na urithi wa thamani kwa Taifa letu. Tanzania kwanza, amani kwanza." Amesema Bwana Laizer.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa Mkutano huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine amewapongeza malaigwanani hao kwa msimamo wao huo pamoja na kuonesha kuridhika na utendaji wa serikali ya awamu ya sita, akiwataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

Aidha baadhi ya Viongozi wengine wa jamii hiyo pia wameahidi kuwa mabalozi wa kueneza amani katika maeneo yao katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu, wakisisitiza athari za maandamano yasiyofuata taratibu kuwa ni pamoja na uharibifu na uvunjifu wa amani ambapo waathirika wakubwa mara zote wamekuwa wanawake, watoto pamoja na wazee.

Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith

10/21/2025 04:26:00 pm


Wakati Tanzania ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya Kijani, Dkt. Judith Mhina Spendi, ametoa wito kwa Watanzania wote kusimama pamoja kulinda amani ya taifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dkt. Judith alitangaza kongamano la amani litakalofanyika kuanzia Oktoba 25 hadi 27 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama, likiwakutanisha viongozi wa dini, vijana, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali.
Dkt. Judith alisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo, ikieleza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi kutokana na utulivu uliopo. “Hakuna maendeleo bila amani, hakuna uchaguzi huru bila utulivu, na hakuna taifa imara bila mshikamano,” alisema. Akihitimisha hotuba yake, alitoa wito kwa Watanzania wote kuwa sauti ya amani, umoja na ukweli.

“Mimi naahidi amani, wewe je?” — Dkt. Judith Mhina Spendi

Viongozi wa Dini Mkoa wa Katavi waahidi Mshikamano uchaguzi mkuu 29 Oktoba

10/21/2025 04:26:00 pm

Viongozi wa dini Mkoa wa Katavi wamefanya Kikao maalumu kujadili kuhusu amani na Mshikamano wa Watanzania, wakihamasisha wananchi kuendelea kutunza na kudumisha amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025.
Viongozi hao Kwa pamoja wamesema kila Mtanzania anayo nafasi ya kuilinda tunu ya amani tukiyoachiwa na baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na uchaguzi usiwe sehemu ya kuleta mgawanyiko na kuvuruga amani kwani kukosekana kwa amani kwenye Jamii kunachangia Kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na kamati ya amani ambaye pia ni Shekhe wa Mkoa waka Katavi Sheikh Mashaka Nassor Kakulukulu amesema katika kipindi hiki watanzania wanatakiwa kuungana na kuzika tofauti za udini ukabila na nyinginezo ili kuvuka salama katika kipindi cha uchaguzi na amani ndio nguzo ya maendeleo kwani hakuna maendeleo pasipo amani.

Saturday, 18 October 2025

WOTE WENYE HOMA ZA UCHAGUZI MSIKUBALI ZIKAPANDA KICHWANI, TUTAWADHIBITI- KANALI MTAMBI

10/18/2025 01:35:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewaonya wale wote watakaojaribu kuhamasisha ama kuleta uvunjifu wa amani wakati wa mchakato wa uchaguzi Mkuu hapo Oktoba 29, 2025 akitahadharisha wale wote wanaotaka kupandisha homa ya uchaguzi kutojaribu kufanya hivyo kwani watashughulikiwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kanali Mtambi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 17, 2025 katika ukumbi wa Mwembeni Complex katika ufunguzi wa Mafunzo ya walimu kutoka mikoa minane ya Kanda ya ziwa na Kanda ya Magharibi, mafunzo yanayofanyika Mkoani humo, akiwahakikishia waalimu hao na wananchi wa Mkoa huo kuwa wamejipanga kikamilifu ,kuhakikisha kila mmoja anatumia haki yake ya kuchagua Kiongozi amtakaye katika mazingira tulivu na yenye amani na usalama wa kutosha.

"Huu ni mwaka wa uchaguzi na mwezi huu ndiyo hasa tumefika kunako sasa shughuli za kisiasa zimekuwa zikiendelea vizuri katika Mkoa wetu, Vyama vyote vimepata fursa sawa, Wagombea wamepata muda mzuri wa kunadi sera zao, Wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kusikiliza Wagombea kupitia Vyama mbalimbali, demokrasia Mkoa wa Mara imekua na inaendelea kupevuka."

"Naomba pia nitumie fursa hii kama Mwenyekiti wa Kamati ya usalama Mkoa, niwatanabaishe wale ambao wakati wa uchaguzi homa ya uchaguzi inapopanda inakimbilia kichwani na kuleta mfetuko wa vichwa, sasa vichwa vikifetuka wengine hufanya mambo yasiyokubalika, nitumie fursa hii kutoa onyo kwao, homa ya uchaguzi ikikupanda tafakari vizuri sera na itkadi ya Chama chako, usiniletee fujo katika Mkoa wa Mara na kama utajaribu utakutana na moto mkali kweli kweli na hapa sipepesi macho, hatutamvumilia yeyote atakayechafua hali ya hewa kwasababu tu amepata homa ya uchaguzi akaamua kujifanya kuwa kichaa, naomba asiwepo yeyote mwenye wazo la namna hiyo." Amesema Mhe. Mtambi.

Mtambi Alisema Mkoa wa mara Vyama vyote katika Mkoa huo vinaendelea kufanya kampeni zake za Amani na Utulivu suala linalotoa fursa ya ushiriki wa wananchi kwenye mikutano ya Kampeni kwa Vyama mbalimbali vya siasa katika Mkoa huo.

VIONGOZI WA KIMASAI WAAHIRISHA TOHARA KWA VIJANA 2, 000 KUPISHA UCHAGUZI MKUU*

10/18/2025 01:35:00 pm


Laigwanani Mkuu wa Jamii ya Kimasai nchini TanzBania Bwana Isack Ole Kisongo Meijo ametangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la tohara kwa Vijana wa kimasai lililokuwa lifanyike kuanzia Oktoba 21-30 mwaka huu ili kutoa fursa kwa Vijana zaidi ya 2, 000 waliokuwa washiriki kwenye zoezi hilo kwenda kushiriki kupiga kura Oktoba 29, 2025.

Ole Kisongo ametoa maelezo hayo leo oktoba 17, 2025 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla wakati wa Baraza la Maigwanani Mkoa wa Arusha, akimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wapo tayari kwa uchaguzi na kulinda kulinda amani wakati wote wa uchaguzi Mkuu kwenye jamii yao.

"Hiyo siku ni takatifu katika Taifa la Tanzania, Hiyo siku ni njema na tumeambiana jamii ya kimasai kuwa hatujawahi kushika mkia, tunataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Vijiji vyetu sasa Ukitahiri Vijana 1,000 leo utapunguza kura kwani Mgonjwa atashindwa kwenda kupiga kura. Tunataka kushiriki vyema kupiga kura sote." Amesisitiza Ole Kisongo.
Kwa upande wake Mhe. Makalla katika salamu zake amewapongeza na kuwashukuru Viongozi na Jamii nzima ya Kimasai kwa kutambua umuhimu wa amani na kuridhika na kazi nzuri ya kimaendeleo inayoendelea kutendwa na serikali ya awamu ya sita, akiwahamasisha kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wengine kujitokeza kupiga kura na kulinda amani ya nchi.

CPA Makalla pia amewataka wananchi mara baada ya kupiga kura kurejea majumbani mwao na kuachia mamlaka husika kuendelea na zoezi la usimamizi na ulinzi wa kura, akiwahakikishia kuwa Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kuhakikisha Mkoa unakuwa salama na tulivu kuanzia sasa, wakati wa kura na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Friday, 17 October 2025

TUME YA UCHAGUZI YAWATAHADHARISHA WANAOSHAWISHI KUTOPIGA KURA “NI KOSA KISHERIA’

10/17/2025 10:55:00 pm

Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhan Kailima, amewatahadharisha wananchi na wadau wa siasa nchini kuwa kuhamasisha watu kutoshiriki kupiga kura ni kosa la kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024.

Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha UTV, Kailima amesema kifungu cha 129 cha sheria hiyo kinaeleza wazi kuwa mtu yeyote anayetumia nguvu, vitisho, au udanganyifu kumshawishi mpiga kura kuacha kupiga kura anatenda kosa la ushawishi mbaya, na anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Amefafanua kuwa kifungu hicho kinakataza mtu yeyote kutumia au kutishia kutumia nguvu, vurugu, au hila ya aina yoyote kwa lengo la kumshawishi mpiga kura kupiga au kuacha kupiga kura, akisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuvunja masharti hayo.

KAMANDA MULIRO "TUMEJIPANGA OKTOBA 29" | AWATOA HOFU WANANCHI "TIMIZENI WAJIBU WENU KIKATIBA"*

10/17/2025 10:55:00 pm
Na mwandishi wetu

Jeshi la Polisi nchini limesema litaendelea kufuatilia kwa kina, kuzuia, kubaini na kutanzua matishio ya Usalama siku ya Oktoba 29, .

Pia limetoa rai kwa Wananchi kujitokeza kushiriki ili kutimiza haki na wajibu wao wa Kikatiba bila ya kuwa na hofu yoyote.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 15, 2025 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro.

Wakazi wa Pwani wadai kusubiri uchaguzi mkuu 29 Oktoba kwa shauku kubwa"tutatoka na watoto wetu kupiga kura

10/17/2025 10:55:00 pm
TUNAAMINI UCHAGUZI UTAKUWA WA AMANI NA USALAMA UTAKUWEPO- WANANCHI WA KIBAHA

Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani wamesema wana uhakika kuwa uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa wa amani na haki kwa kila mmoja anayeshiriki uchaguzi huo, wakiamini kuwa siku ya Oktoba 29, 2025 kutakuwa na amani na utulivu pia kutokana na uthibitisho na uhakika walioupata kwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyesema kuwa serikali na Vyombo vya Dola vimejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kupiga kura katika mazingira salama na tulivu kote nchini.

Wananchi hao akiwemo Bi. Mwinyimvua Kasosoma na Mwanaidi Stephano, wakazi wa Kwa Mathias, Kibaha Mkoani Pwani wamesema hayo leo Oktoba 15, 2025 wakati wakizungumza na mwandishi wetu na kusisitiza kuwa wao na familia zao watajitokeza wote wenye sifa kwenda kupiga kura na kumchagua Kiongozi wanayeamini atawaletea maendeleo.

Aidha wamekumbusha umuhimu wa kuheshimu sheria na Miongozo yote ya Uchaguzi Mkuu, wakisema mara baada ya Kupiga kura ni muhimu kila mmoja kuondoka kwenye Vituo vya kupigia kura na kwenda kuendelea na shughuli nyingine za kiuchumi, wakijitenga na baadhi ya maneno ya wanasiasa wanaowataka wafuasi wao kusalia vituoni ili kuhakikisha ulinzi wa kura ama kuachana na upigaji wa kura na kuandamana ili kuitika hamasa ya baadhi ya wanaharakati na wanasiasa.

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unafanyika Oktoba 29, 2025 ambapo Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari amewahakikishia wananchi wote usalama na utulivu wa kutosha siku hiyo, akionya wale wote wanaopanga kufanya vitendo vya uhalifu ama uvunjifu wa amani nchini.

RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29.

10/17/2025 10:55:00 pm
Na mwandishi wetu , Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amewahakikishia wazee na wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa wamejipanga Vyema kuhakikisha siku ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kutakuwa na amani na mazingira tulivu ya upigaji kura, akitoa wito kwa kila Mwananchi mwenye sifa kujitokeza kwa wingi kuchagua Viongozi wanaowataka ili kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo.
CPA Makalla ametoa wito huo wakati wa matembezi ya amani ya Wazee wa Mkoa wa Arusha, waliofanya matembezi hayo Jijini Arusha kwaajili ya kuliombea Taifa amani kama sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Wakianzia matembezi hayo kwenye Viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kwenda Mnara wa saa, Metropole, Idara ya maji, kituo cha Mabasi Arusha na baadaye kumalizia tukio lao kwenye Viwanja vya Makumbusho Jijini Arusha.

"Kupiga kura ni haki ya Kikatiba ya kila Mtanzania. Wazee wangu mtukumbushe na kuwakumbusha Vijana kuitunza amani, kutumia vyema mitandao ya kijamii lakini Vijana wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi. Niwahakikishie mtapiga kura kwa amani na atakayeshinda atangazwe kushinda." Amesema.

Makalla amewahakikishia wananchi wote amani na usalama katika kipindi hiki cha lala salama za Kampeni, wakati wa upigaji kura na hata baada ya kura, akisema amani ni muhimu kwa maendeleo pamoja na ukuaji wa sekta ya utalii katika Mkoa huo ulio kitovu cha utalii kwa upande wa Tanzania bara.

Kwa upande wao baadhi ya wazee walioshiriki matembezi hayo kwaniaba ya wenzao wamewasihi wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuhimiza kila mmoja kulinda amani ya Mkoa wa Arusha, wakisema amani imekuwa tunu muhimu ya maendeleo na ustawi wa watu wa Mkoa wa Arusha.

Wednesday, 15 October 2025

AFANDE SELE AWATAKA VIJANA KUACHA MIHEMKO NA KUTISHIA KUSUSIA UCHAGUZI MKUU OKTOBA MWAKA HUU

10/15/2025 08:22:00 pm
Mwanamuziki na mfalme wa mashairi Tanzania, Selemani Msindi maarufu kama Afande Sele,amewataka Watanzania hususan vijana kuacha kuwa na mihemko ya kususia kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

 Aidha Afande Sele amesisitiza kuwa kutoshiriki ni kujinyima haki ya kikatiba jambo ambalo sio sahihi katika kulijenga Taifa la baadae.

 Akizungumza akiwa mkoani Morogoro, Afande Sele amesema vijana wanapaswa kutumia nguvu yao kwa kushiriki katika kupiga kura badala ya kujiingiza kwenye maandamano yanayoandaliwa na watu wasiolitakia mema taifa.

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

10/15/2025 08:08:00 pm
Na mwandishi wetu. 

Mufti na Sheikh Mkuu wa Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Bin Zubeir Ally amewataka Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani na ustawi wa jamii hasa wakati huu ambapo Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Mbele ya waumini wa kiislamu Katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Mufti Sheikh Abubakar amesema amani ndiyo msingi wa uislamu na chachu ya maendeleo ya jamii yoyote ile, akisisitiza kuwa waislamu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha utulivu na mshikamano vinaendelea kuwepo.

"Maandishi yanasema wala msieneze katika nchi uharibu wowote wa kuweza kuleta matatizo. Je uislamu umezungumza amani? Niwaambie kuwa Msaafu mzima tukiufasiri ni amani, amani tupu, Mtume kipindi chote anazungumzia amani. Kipindi hiki tufundishe na tutangaze juu ya amani na mmomonyoko wa maadili." Amesisitiza kusema Mufti huyo.

Mufti pia ameeleza kuhusu umuhimu wa malezi ya watoto katika misingi ya dini, akieleza kuwa hilo ndilo jambo la msingi katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili unaozidi kushika kasi katika jamii, akitoa rai kwa wazazi na walezi kuwalea watoto wao kwa maadili ya dini na kulinda maadili ya Taifa kwa vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Denis Masanja amewataka wananchi wote wa Wilaya hiyo wenye sifa na waliojiandikisha kwenye daftari na Mpigakura kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 ili kutimiza haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura.

TAASISI ZA KIDINI NA ELIMU WAFANYA MDAHALO KUSISITIZA AMANI NCHINI

10/15/2025 08:08:00 pm
Na mwandishi wetu. Dar es Salaam

Taasisi za kidini na kielimu kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran zimefanya mdahalo maalumu Jijini Dar Es Salaam wenye lengo la kusisitiza na kudumisha amani, mshikamano, utulivu na haki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu. 

Mdahalo huo umewakutanisha viongozi wa dini, wanazuoni, na wadau wa amani ambapo Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelical Fellowship Church Tanzania, Baba Askofu Charles Asher, amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kutumia haki yao ya kikatiba kwa amani katika kuchagua viongozi wanaowataka, huku akisisitiza kuwa Tanzania imeendelea kuwa mfano wa utulivu barani Afrika tangu ilipopata uhuru.

Amesema uchaguzi siyo uwanja wa uhasama, bali ni fursa ya kuimarisha demokrasia na kujenga mustakabali wa taifa. “Kila mmoja wetu ana jukumu la kulinda amani. Tofauti za kisiasa haziwezi kuwa sababu ya kuvuruga umoja tuliojenga kwa miaka mingi,” amenukuliwa akisema Askofu Asher.

Kwa kadri teknolojia inavyozidi kukua na kadri uhuru unavyoongezeka wakati mwingine kumekuwa na hali za taharuki kwasababu ya kutokuwa na mwelekeo mmoja wa watu na sisi kama Viongozi wa dini ni kuileta jamii pamoja na kuwafundisha namna ya kuyapokea yaliyo mema. Tunawajibika pia kuwaweka pamoja na kutunza tunu ya umoja wa Watanzania." Amesema Askofu Asher.

Kwa upande wake Sheikh Mulasar Lulat, miongoni mwa waliohudhuria kongamano hilo ameeleza kuwa kuelekea uchaguzi mkuu ni muhimu kuendelea kudumisha na kuitunza amani na kulinda misingi ya amani nchini, akiwataka Watanzania kujiepusha na vurugu na uchochezi unaofanywa mitandaoni, akiwataka kutokubali kuyumbishwa na watu wasioheshimu na kuilinda misingi ya tunu za amani na mshikamano wa nchi.

Tuesday, 14 October 2025

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania , Gerson Msigwa atoa kauli kali kwa Watanzania awatoa hofu uchaguzi mkuu.

10/14/2025 10:09:00 am
Na Mwandishi wetu

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa amewahakikishia Watanzania wote wenye sifa na waliojiandikisha kwenye daftari na mpiga kura kuwa serikali ya awamu ya sita inatambua kikamilifu wajibu wake wa kulinda haki ya kila Mtanzania ikiwemo haki ya Kikatiba ya Kuchagua na kuchaguliwa, akiwahimiza kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025.

Msemaji huyo wa serikali amewatoa hofu pia Watanzania dhidi ya yale yanayosemwa mtandaoni kuelekea siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akisema serikali na Vyombo vya Dola vimejipanga na kujiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa amani na katika mazingira tulivu na salama ili kutoa fursa ya kila mmoja kuitumia haki yake ya Kikatiba.

"Naomba niwahakikishie Watanzania wote kuwa amani ipo tena ya kutosha kwahiyo msiwe na wasiwasi wowote serikali hii ni makini, Vyombo vyetu vyote vya Dola vimejiandaa kikamilifu kuhakikisha utulivu na amani ya kutosha. Nenda kachague Kiongozi unayemtaka na hakuna mtu yoyote atakayefanya chochote. Achaneni na maneno yanayotengenezwa mtandaoni kuwatishia watu na kuwaaminisha vitu ambavyo havitatokea." Amesema Msigwa.

Aidha Msigwa pia amehimiza watanzania kuendelea kujiandaa na upigaji huo wa kura kwa kusikiliza mikutano ya Kampeni ya Wagombea Udiwani, Ubunge na Urais wa Tanzania ili kuwa na maamuzi sahihi ya kuchagua Kiongozi anayefaa badala ya kusubiri kuchaguliwa Kiongozi wa eneo lako na watu wengine.

Tazama Wakazi wa Mapinga waonesha hisia zao uchaguzi mkuu

10/14/2025 10:09:00 am
Na mwandishi wetu, Pwani

Wananchi wa Mapinga Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamehamasika kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, wakihamasisha watanzania wote waliojiandikisha kwenye daftari la Mpigakura, kutumia haki yao ya Kikatiba kuweza kuchagua Viongozi sahihi watakaowaletea maendeleo.

"Tarehe 29 nitaamka asubuhi na familia yangu yote tutaenda kupiga kura na ninawasihi Watanzania wenzangu tutumie haki yetu ya Kikatiba na tujitokeze kwa wingi tukapige kura kuwachagua Viongozi tunaowataka na usipopiga kura utachaguliwa Viongozi usiowataka na matokeo yake ni malalamiko." Amekaririwa akisema Fatuma Mkumba, Mkazi wa Mapinga.

Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakizungumza na Chombo hiki cha habari leo Jumatatu Oktoba 13, 2025 wamesisitiza pia umuhimu wa kila mmoja kupiga kura, wakisema Viongozi sahihi wanaochaguliwa na watu ndiyo wenye kuweza kuwaletea maendeleo katika ngazi mbalimbali na zaidi wakihamasisha kuchagua Viongozi kutokana na sera, ahadi na yale yote wanayoendelea kuyaeleza katika Mikutano yao ya Kampeni nchi nzima.

Kwa upande wake Bi. Tukae Rashid, Mkazi wa Mkoa wa Pwani amesisitiza pia umuhimu wa kuheshimu sheria na taratibu za uchaguzi, akiwashauri Wapigakura wengine kurejea majumbani na kwenye sehemu zao za kazi mara baada ya kumaliza kupiga kura badala ya kujiingiza kwenye Uvunjifu wa sheria ikiwemo kusalia Vituoni kulinda kura kama ambavyo baadhi ya wanasiasa na Vyama vya siasa vimekuwa vikishawishi wanachama wake kubakia Vituoni ili kulinda kura walizozipiga.

Tayari Rais wa Awamu ya sita ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama amewahakikishia watanzania wotw utulivu, amani na usalama siku ya upigaji wa kura, akiwahimiza kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo la kidemokrasia na kutotishwa na yeyote wakiwemo wale wanaohamasisha kufanya vurugu na maandamano wakati wa Uchaguzi huo.

Monday, 13 October 2025

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO

10/13/2025 01:13:00 pm
Na mwandishi wetu

Katibu Mkuu kutoka  Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na watu Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga, amewataka vijana kote nchini Tanzania kutumia haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaoakisi matumaini, malengo na ndoto za taifa la Tanzania katika kipindi cha mitano ijayo.

Walakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vijana Tanzania linalofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa City Park Garden, Jijini Mbeya na kuhudhuriwa na Vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini, Maganga amesema vijana wana nafasi kubwa katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, hivyo ni muhimu wakatumia fursa hiyo kuchagua viongozi wanaolenga ustawi wa taifa.

“Vijana ni nguvu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii zetu, Hivyo ni lazima tutumie vyema nguvu hii kubadilisha dunia kuwa mahali bora kwaajili ya watu wote. Hivyo, ninawasihi mjitokeze kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, na kuchagua viongozi wenye dira sahihi kwa taifa letu,” amesema Bi. Maganga.

Katibu Mkuu huyo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea pia ya kuweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha vijana, ikiwamo mifumo ya kisera, kisheria, Kitaasisi pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia utoaji wa Mikopo na usaidizi mwingine unayolenga kuongeza ushiriki wao katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Ameongeza kuwa kongamano hilo ni jukwaa muhimu kwa vijana wa Kitanzania kubadilishana mawazo, kujifunza na kujadili changamoto zinazowakabili, ili serikali iweze kuyatumia maoni yao katika kuboresha sera na miongozo ya vijana nchini.

Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Rodrick Mpogolo, amewataka vijana kuendelea kuwa wazalendo na kujivunia taifa lao, akisema mchango wao ni muhimu katika kulijenga taifa lenye misingi imara ya maendeleo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, Seleman Mvunye, amesema kongamano hilo limewakutanisha zaidi ya vijana 1,500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Sunday, 12 October 2025

Watu wenye ulemavu wapaza sauti zao tusishawishike na kurubuniwa kuchagua viongozi wa shinikizo la kupewa chochote.

10/12/2025 07:07:00 pm
Na mwandishi wetu ,Morogoro.

Kuelekea uchaguzi Mkuu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025 wa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wa Tanzania, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imetoa rai kwa watu wenye ulemavu  kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo na kutetea maslahi ya kundi hilo.

Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Morogoro Bw. Christopher Mwakajinga ametoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya utoaji elimu ya kuwajengea uelewa juu ya masuala ya rushwa yenye kauli mbiu: ‘Kataa Rushwa katika Uchaguzi“ kwa viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu na mahitaji maalum mkoani Morogoro.

Mwakajinga amesema ushiriki wa makundi ya watu wenye mahitaji maalum katika uchaguzi si hisani bali ni haki yao ya msingi inayotokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo wanapaswa kushiriki uchaguzi mkuu kikamilifu bila kuwa na vikwazo vyovyote.

Amesema katiba yetu inatoa fursa kwa watanzania wote ambao wametimiza miaka 18 kuwa na haki ya kushiriki kwenye uongozi wa nchi na imetolewa bila kujali ulemavu wa mtu ,vipato vyao, ,hivyo wanapaswa kuitumia sawa na watanzania wengine wasio na ulemavu.

“ Ni lazima tuwekeane mazingira huru na sawa ili muweze kulitumia zoezi hili la msingi la haki ya kupinga kura,“amesema Mwakajinga .

Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu kwa nyakati tofauti wamewasihi wenzao wasishawishike na kurubuniwa kuchagua viongozi wa shinikizo la kupewa chochote, bali watumie haki yao kuchagua viongozi wanaowataka ili wawaletee maendeleo yao na Taifa na watakaodumisha amani ya Tanzania.

MAELFU YA WANANCHI WA MKURANGA "TUPO TAYARI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA AMANI"

10/12/2025 04:24:00 pm
PWANI

Wananchi wa Mkuranga Mkoani Pwani wamesema wapo tayari kwa ushiriki wa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 wakiwahimiza pia Vijana kutumia fursa hiyo na haki ya kikatiba ili kuchagua Viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo kwa miaka mitano ijayo.
Wananchi hao akiwemo Mzee Maulid Mwigange na Mariam Ngayonga wakati wakizungumza na Vyombo vya habari, wamewatoa wasiwasi pia wananchi na kwa kuwaeleza kuwa Oktoba 29, 2025 kutakuwa na usalama na amani ya kutosha kutokana na namna ambavyo serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata nafasi kamili na usalama wa kushiriki kupiga kura.

"Tutachagua Kiongozi anayetufaa na tumehamasika kushiriki kwasababu ya maendeleo mengi tu tunayoyashuhudia Mkuranga ikiwemo stendi nzuri na hatubugudhiwi." Ameongeza kusema Mohamed Makame, mwananchi na mfanyabiashara mdogo wa Mkuranga.

Kwa upande wake Habiba Jasmin, Kijana na mjasiriamali mdogo wa Mkuranga ametoa wito wa Vijana kutumia vyema fursa ya upigaji kura kuamua kuhusu hatma yao ya miaka mitano ijayo, akiombea kheri uchaguzi huo ili ufanyike na umalizike kwa amani ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku za uchumi.

BAKWATA MWANZA WAELEKEZA WAUMINI WAKE KUANZA MFUNGO KUOMBEA AMANI YA TANZANIA

10/12/2025 04:11:00 pm
Mwanza

Baraza la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limewaelekeza waumini wake wa kufunga kwa maombi kuanzia Alhamisi ya Oktoba 23, 2025 hadi siku yatakapotangazwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025 na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.


Akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza hilo Mkoa wa Mwanza Sheikh wa Mkoa huo wa Mwanza Hassan Kabeke amesema hatua hiyo inalenga kuiombea nchi amani na mshikamano, akisisitiza kuwa ni wajibu wa Kila Mtanzania kushiriki katika kuilinda amani hiyo ambayo imekuwa msingi wa maendeleo binafsi na ya Tanzania.

"Tarehe 23 Vituo vyetu vyote na misikiti yetu watafunga mpaka siku yatakapotangazwa matokeo. Ni maelekezo tumeyatoa. Hakuna kitu kigumu kama kukubali njaa lakini tutafunga kwaajili ya nchi hii kwani tunao wajibu wa kupigania amani ya nchi hii hasa kwa kurejea historia ya baadhi ya wazee wetu na wazee wa imani nyingine wameshiriki kuutafuta uhuru wa nchi hii." Amesema Sheikh Hassan Kabeke.

Kiongozi huyo pia wa imani amehimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi Mkuu ujao, akitaka Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya Vikao vya familia ili kukumbushana umuhimu wa kupiga kura sambamba na masuala mengine ya kijamii na kuachana na baadhi ya hamasa za maandamano na ulinzi wa kura vituoni unaotolewa na baadhi ya wanasiasa kwenye Mitandao ya kijamii.

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa dini amemtaja Dkt. Samia kama kiongozi hodari na aliyepokea nchi katika wakati ambao nchi iliandamwa na msiba na matatizo kadhaa ya kiuchumi, akiachiwa pia miradi mingi michanga iliyohitaji kuendelezwa, miradi ambayo sasa imekamilika na Taifa limeendelea kusalia tulivu, lenye amani pamoja na mshikamano.

Friday, 10 October 2025

MUFTI ABUBAKAR ATOA KAULI NZITO KWA WATANZANIA "TULINDE AMANI"

10/10/2025 06:22:00 pm
Na Mwandishi wetu, Njombe

Waumini wa dini ya Kiislamu na Watanzania kwa ujumla wamehamasisha kujitokeza kwa wingi hapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ili kupiga kura na kuwachagua Viongozi sahihi wanaoweza kuwaletea maendeleo sambamba na wote kuwajibika kuitunza amani ya Tanzania.

Wito huo umetolewa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Ali Mbwawa wakati wa Mkutano maalumu wa viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu Mkoani Njombe, Mkutano uliofanyika Masjid Taqwa, Mwembetongwa Mjini Makambako, akisema amani ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo na ustawi wa Taifa, akiwataka waumini wa dini hiyo kuwa mfano wa kuigwa katika kudumisha utulivu na mshikamano.

"Niwakumbushe kuwa Mtume wetu ni mtume wa amani, ni Mtume wa Kheri, Mtume wa baraka na ameitangaza amani amani hiyo kama alivyoitangaza Mungu. Niwakumbushe Vijana amani ndiyo jambo kubwa kuliko yote asije mtu hapa akawadanganya kwaajili ya kuondosha amani halafu wewe ukakubali. Muislamu kila jambo ukiambiwa fikiria ujue linafaa au halifai. Lindeni amani. Chungeni amani na kila mkipata hadhara simamemi semeni na hubirini kuhusu amani." Amesisitiza Mufti Abubakar.

JESHI LA POLISI NCHINI KUWASHUGHULIKIA, WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUHAMASISHA CHUKI.

10/10/2025 01:01:00 pm
Na Mwandishi wetu.

Jeshi la Polisi nchini Tanzania kupitia msemaji wake DCP David Misime limesisitiza kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya Kijamii pamoja na ulinzi wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akibainisha kuwa Jeshi hilo limejipanga kikamilifu kushughulika kikamilifu na wote watakaohatarisha amani ya nchi.

Msemaji huyo pia ameonya kuhusu wanaotumia mitandao vibaya kuhamasisha chuki, uhasama na kusambaza taarifa za kuzusha, akisema sheria inatoa adhabu pia kwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii atakayesambaza (kushare) taarifa ambazo hazina ukweli ama ambazo zine lengo la kuzua taharuki na uhasama.

"Mitandao ya kijamii tukiitumia vibaya inaweza kutufikisha pabaya ikiwemo kutumika kama silaha kuleta uhasama, uzushi na kusambaza uongo kama ambao tunauona kwenye mitandao na nitoe wito kwa jamii unaposambaza taarifa ambazo sio sahihi ni kosa pia kwako unayesambaza taarifa potofu." Amesema Kamanda Misime.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari leo Oktoba 10, 2025, Misime pia ameeleza kuwa wamejipanga vyema kulinda raia na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi Mkuu, akiwapongeza watanzania kwa kuendelea kuelimika na kukuza ustaarabu wao wakati wote wa kampeni, akiomba ushirikiano zaidi wa kufichua uhalifu na wahalifu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Amewatoa hofu pia Watanzania kuhusu yanayoendelea mitandaoni, akisema nchi ni salama na hakuna tatizo lenye kutishia usalama na utulivu siku ya upigaji wa kura, akisema Jeshi la polisi linaendelea kuchukua hatua kwa wanaotumia mitandao hiyo vibaya na kuishukuru serikali kwa uwezeshaji wake mkubwa wa vifaa na vitendea kazi katika udhibiti wa uhalifu na wahalifu.

Amesema Jeshi hilo pia limesambaza Askari polisi zaidi ya 3,900 kwenye Kata zote za Tanzania bara pamoja na Askari 388 kwenye Shehia za Zanzibar wakitoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya mitandao na kuwataka wazazi kuelimisha pia Vijana wao dhidi ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na kuheshimu sheria za Tanzania.

KATIBU MKUU MKOMI,AWAHIMIZA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KUJITOKEZA KUPIGA KURA OKTOBA 29

10/10/2025 12:55:00 pm
Na mwandishi wetu

Katibu Mkuu Ofsi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi, amewahamasisha watumishi wa umma kote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza katika kikao cha tatu cha Baraza la Nane la Wafanyakazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili, Mkomi alisema licha ya kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, ana mapenzi na ustawi wa taifa, hivyo ni muhimu kwa kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura, hasa watumishi wa umma, kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kidemokrasia.

"Nawaomba wenzangu watumishi wa umma tujitokeze kwa wingi siku ya Oktoba 29 kwenda kupiga kura huu ni wajibu wetu wa kikatiba na njia ya kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya nchi yetu," alisema Mkomi.

Aidha, alibainisha kuwa hata viongozi wa kisiasa wamekuwa wakihamasisha familia zao kujitokeza kupiga kura, hivyo ni vyema pia kwa wafanyakazi wa umma kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwa amani na utulivu.

 "Niwaombe wajumbe wa baraza hili na watumishi wote, tusiwe nyuma. Tuwe mfano wa kuigwa katika kujenga demokrasia kwa kushiriki uchaguzi," alisisitiza.

Kauli hiyo imekuja wakati nchi ikijiandaa kwa uchaguzi ambao unatarajiwa kushirikisha wananchi katika kuchagua viongozi watakaowakilisha maeneo yao, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya maendeleo.

Mwisho.

WAZEE MKOANI DODOMA WAAHIDI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA, WAOMBA KUPEWA KIPAUMBELE KWENYE FOLENI.

10/10/2025 12:55:00 pm
Na Mwandishi wetu Dodoma

Wazee wa Mkoa wa Dodoma waaswa kuhamasisha jamii kujitokeza Oktoba 29,2025 kupiga kura pamoja na kuhakikisha wanasimamia vijana na kuwasihi kulinda amani ya nchi yetu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati akizungumza na Wazee hao leo  juu ya umuhimu wao wa kuhamasisha jamii kujitokeza kupiga kura.

Aidha amesema kuwa ni jukumu la Kila mwananchi kuchagua viongozi wenye tija na maendeleo hivyo amewasihi wazee kuwa mstari wa mbele kwenye suala la uchaguzi kwani maendeleo yaliyofanywa na Serikali yanaonekana dhahiri.
Aidha amesema Dodoma ya miaka 10 iliyopita si sawa na Dodoma ya sasa kwani hata hadhi ya viwanja imeongezeka na kila mtu amekuwa akivutiwa na Dodoma hivyo anaipongeza Serikali kwa kufanya Dodoma kuwa ya kuvutia.

"Dodoma ya sasa si kama ya zamani Dodoma sasa inavutia na ni kimbilio la watanzania na wageni wa kimataifa kuwekeza Dodoma na hii ni kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Serikali"Amesema Senyamule 

Sanjari na hayo amesema kuwa Serikali imeamua kutoa Elimu juu ya magomjwa yasiyoambukizwa ili waweze kuhakikisha wazee wanakuwa imara kwenye Afya Kwa kufanya mazoezi na Kuzingatia mlo mzuri kulingana na umri wao.

"Kupitia nyie tutaweza kujua changamoto mlizonazo na kuweza kuhakikisha tunazitatua kwani wazee ni tunu ya taifa hili"Ameongeza Senyamule

Wazee hao nao walipata nafasi ya kuelezea changamoto zao Kwa Mkuu wa Mkoa wanazokumbana nazo kwenye huduma za Kijamii ikiwemo hospitali ambapo Mzee Bakari Chaurembo ameiomba Serikali kuwaangalia Kwa jicho la 3 Kwa kuhakikisha wanapatiwa Bima ya Afya ili waweze kupata huduma kwa urahisi na wakati kipindi wanapokwenda kwenye vituo vya Afya.

Akijibu hoja za wazee hao Mkuu wa Mkoa amesema atahakikisha anashughulikia changamoto zote ikiwemo huduma mbovu Kwa wazee kwenye vituo vya Afya,pamoja na kuboresha miundombinu  kama barabara ili kuweza kukidhi matakwa ya Wazee hao.

"Kwenye ishu ya Wazee kutopanga foleni siku ya kupiga kura tutaliwasilisha Kwa TUME ya uchaguzi ili muweze kutengenezewa utaratibu mzuri"Amesisitiza Senyamule

VIONGOZI WA DINI NA WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA MABALOZI WA AMANI

10/10/2025 10:01:00 am
Na mwandishi wetu

Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali nchini pamoja na waandishi wa habari, wametakiwa kutumia nafasi zao kwenye jamii kuhimiza amani na umoja wa kitaifa, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu, ili kuepusha mifarakano na migawanyiko miongoni mwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa Mkoani Iringa leo Alhamisi Oktoba 09, 2025 wakati wa warsha ya siku moja iliyoratibiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikisha waandishi wa habari na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali Mkoani humo.
Mwezeshaji wa semina hiyo, Uzima Justine, amesema huu ni wakati sahihi kwa viongozi wa dini kutoa ujumbe unaowaunganisha Watanzania, badala ya maneno yanayoweza kuchochea chuki au migawanyiko.

“Chochote kisichounganisha watu na kuleta amani si cha kweli,” alisema Uzima, akisisitiza kwamba wajibu wa viongozi wa dini ni kujenga maridhiano na upendo wakati wote, hasa katika kipindi cha uchaguzi.

Kwa upande wake, Mratibu wa warsha hiyo, Omary Ibrahim, ambaye ni Afisa Miradi wa BAKWATA Makao Makuu, alisema warsha hiyo imelenga kuwaongezea uelewa washiriki kuhusu nafasi yao muhimu katika kulinda amani kupitia maneno na matendo yao.

“Tupo Iringa na tumewakutanisha waandishi wa habari pamoja na viongozi wa dini — watu ambao wanaweza kujenga au kubomoa. Lengo letu ni kuwajengea uwezo ili wakatoe elimu sahihi kwa wananchi, wasitoke nje ya misingi ya ukweli,” alisema Omary.

Aliongeza kuwa wakati mwingine haki ya kukusanya, kuchakata na kusambaza habari haitumiki ipasavyo, jambo linaloweza kuleta mkanganyiko kwa jamii na kuhatarisha amani ya nchi.

Katika warsha hiyo wito umetolewa kwa taasisi za dini na vyombo vya habari kushirikiana kwa karibu zaidi katika kutoa elimu ya uraia, kueleza kwa uwazi umuhimu wa amani, na kupinga taarifa au mafundisho yanayoweza kugawa jamii.

Thursday, 9 October 2025

VIONGOZI WA DINI WASISITIZA UMUHIMU WA AMANI KWA MAENDELEO YA TANZANIA

10/09/2025 01:38:00 pm
Dodoma

Kuelekea kwenye Zoezi la uchaguzi Mkuu wa Tanzania Jumatano ya Oktoba 29, 2025, Viongozi wa dini, kijamii pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dodoma wameungana pamoja kuhimiza amani, wakiitaja kama rasilimali muhimu kwa maendeleo ya Kijamii, kiuchumi, Viongozi wa dini wakisema amani ndiyo Neema muhimu zaidi kwenye nchi yoyote duniani.

Mchungaji Pendo Yohana kutoka Kijiji cha Michese, Askofu Antony Saimon, Mwenyekiti wa Umoja wa madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma pamoja na Sheikh Ahmed Said Ahmed, Msemaji wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, ni miongoni mwa Viongozi wa dini wanaohamasisha kuhusu amani, wakisisitiza kila Mtanzania kuwa Mlinzi wa amani na kujiepusha na matendo yote yenye kuhatarisha amani iliyopo.

Kulingana na tafiti mbalimbali zinaonesha uwepo wa uhusiano kati ya amani na maendeleo katika ujenzi wa Taifa bora na lenye uchumi imara pamoja na kuruhusu kupatikana kwa mahitaji muhimu ya binadamu na huduma stahiki ikiwemo elimu bora, afua bora na ulinzi na usalama kwa wote.

Aidha kwa Upande wake Emmanuel Kamome, dereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma pamoja na Shukuru Chimwaga, Msemaji wa Chama cha waigizaji Mkoa wa Dodoma wametoa wito pia wa kulinda amani iliyopo nchini, wakiahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha ulinzi wa amani hasa wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Wananchi hao wa Dodoma wameungana na Viongozi na wagombea mbalimbali wa nafasi za Urais wa Tanzania akiwemo Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pamoja na wengine wamekuwa wakitahadharisha Vijana na Jamii kutokubali kutumika na wasioitakia mema Tanzania na kuweza kuvuruga na kuhatarisha amani ya Tanzania kwa kisingizio cha uchaguzi Mkuu, wakisisitiza kuwa uchaguzi ni tendo la kidemokrasia na sio sababu ya machafuko na vurugu kwenye Jamii.

Maandamano yana athari kubwa ikiwemo vifo kwa watoto, wazee na wanawake tusikubali maandamano.

10/09/2025 01:37:00 pm
Na mwandishi wetu

Wananchi na wapigakura wa Tanzania wamesisitizwa kupuuza na kutokubali kuhadaika na watu na baadhi ya wanasiasa wanaohamasisha vurugu na maandamano Jumatano ya Oktoba 29, 2025 siku ya upigaji wa kura kwenye uchaguzi Mkuu wa Tanzania.


Wananchi tuliozungumza nao akiwemo Shaban Maulid na Adrian Malikale wamewasihi wananchi kujifunza na kutathmini athari za vurugu na machafuko kwa jamii hasa kwa watoto, wanawake na wazee, wakiahidi kutoandamana na kusisitiza kufuatwa kwa taratibu na sheria zinazotambulika kisheria wakati wa zoezi la upigaji kura.

"Ni muhimu sana kutokubali kushawishiwa au kudanganyika kwenda kuandamana kwa namna yoyote ile ifikapo Oktoba 29, 2025. Tujitokeze tupige kura, turudi nyumbani kuendelea na shughuli zetu kama mimi mama lishe nitakavyofanya. " amesema Bi. Zuhura Mohamed.

Tayari serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewahakikishia watanzania wote utulivu, amani na usalama siku hiyo ya upigaji wa kura, wakihimiza kila mmoja kujitoke kwa wingi kumchagua Kiongozi wamtakaye bila ya hofu yoyote na kubainisha kuwa wamejipanga kuhakikisha kila mmoja anaitumia haki yake ya kikatiba bila bugudha, usumbufu na hofu ya vurugu.

Wednesday, 8 October 2025

Watanzania waeleza umuhimu wa kutii sheria na Miongozo ya uchaguzi," ifikapo Oktoba 29, 2025 tupige kura na kurejea majumbani"

10/08/2025 11:03:00 am
Na mwandishi wetu. 

Wananchi wenye haki ya kupigakura katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ili kuchagua Viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo na kutimiza wajibu wao wa Kikatiba na kidemokrasia.

Wananchi hao pia akiwemo Mwanahuba Jumbe Ramadhani wamesisitiza umuhimu wa kutii sheria na Miongozo ya uchaguzi, akisema ifikapo Oktoba 29, 2025 mara baada ya zoezi la kupiga kura ni muhimu kila mmoja akarejea nyumbani na kuendelea na shughuli zake badala ya kutii wito unaotolewa na baadhi ya wanasiasa wa kulinda kura kwenye Vituo, kazi ambayo ni ya mawakala wa vyama vya siasa na tume huru ya Taifa ya uchaguzi.

Richard Alphonce na Bw. Abdallah Ismail Haruna, wakazi wa Dar Es Salaam wakisisitiza kuwa kura ni haki ya kimsingi, wamebainisha kuwa mabalozi wazuri wa uchaguzi kwa kuhamasisha Vijana wenzao kupiga kura na kujitokeza kwa wingi kwani kura ndio njia pekee ya kidemokrasia ya kuweza kumchagua Kiongozi sahihi pamoja na kuwawajibisha wale walioko madarakani na walioshindwa kutimiza ahadi na matarajio ya wananchi.

POLEPOLE ATAKIWA KUJISALIMISHA OFSI YA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI.

10/08/2025 11:03:00 am
Na mwandishi wetu

Jeshi la Polisi nchini Tanzania kupitia kwa Msemaji wake DCP David Misime limesisitiza kuwa bado linaendelea kumsubiri Ndugu Humphrey Polepole ili aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai ili atoe maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia Mitandao yake ya Kijamii.

Ikumbukwe kuwa Jumatatu Septemba 15, 2025 Jeshi la Polisi lilisema kuwa limefungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi CCM.
 "Tuhuma ambazo ametoa na anaendelea kuzitoa kulingana na jinsi alivyozielezea zinaashiria uwepo wa makosa ya kijinai na kwa mujibu wa sheria zinahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapo wasilishwa mahakamani. 

Tuhuma hizo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii, baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo au ushahidi na vielelezo vitakavyo thibitisha tuhuma hizo ili kuwezesha hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na ndivyo utaratibu wa kisheria ulivyo" Taarifa hiyo ya Polisi ilieleza.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limeeleza kuona taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya kijamii na ndugu zake kuwa Mtu huyo ametekwa usiku wa kuamkia Oktoba 06, 2025 na kueleza kuwa tayari wameanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wa madai ya kutekwa kwake.

Mwisho.

Monday, 6 October 2025

Wananchi "Hatukubali kurubuniwa, kujiingiza kwenye maandamano Oktoba tunatiki"

10/06/2025 10:04:00 am
Na mwandishi wetu

Jamii imesisitizwa kujitokeza kwa Wingi Oktoba 29, 2025 na kupiga kura kuwachagua Viongozi wanaofaa na wanaoweza kuwaletea maendeleo ya kweli kama sehemu ya kutimiza Haki ya kila Mwananchi Kikatiba lakini pia katika kuamua hatma ya maisha ya Kila mmoja katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Wito huo umetolewa na Wananchi wa Tabata Jijini Dar Es Salaam leo Jumatatu Oktoba 06, 2025 wakati wakizungumza na Mwandishi wetu wa habari, wakisisitiza pia kila mmoja kufanya tafakuri na kutokubali kurubuniwa na kujiingiza kwenye maandamano yanayoratibiwa na kuhamasishwa na watu wasiokuwa nchini na wasioitakia mema Tanzania.

Ally Kazimoto ni mmoja wa waliozungumza nasi ambapo ametanabainisha kujiandaa vyema kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao na kuhamasisha Vijana wenzake kutorubuniwa kuandamana, akisema ni muhimu kabla ya kuandamana kujiuliza athari za maandamano hayo,akisisitiza kuwa haki haidaiwi kwa kuvunja sheria na miongozo iliyopo nchini.

Kwa upande wake Raskazia Mwita na Hamis Maneno, wamewasihi Vijana na Wanawake kutafakati hatma ya Watoto na familia zao kabla ya kuandamana hiyo Oktoba 29, wakieleza kuwa ni ubinafsi kuandamana bila kujali haki na usalama wa wengine kwani maandamano ya Oktoba ni batili na hayakubaliki kutokana na Serikali kuitenga siku hiyo kuwa maalumu kwaajili ya uchaguzi mkuu peke yake.

POLISI KUWASAKA WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUHAMASISHA NIA OVU NA UPOTOSHAJI

10/06/2025 10:03:00 am
Na Mwandishi wetu.

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewahakikishia watanzania wote kuwa litaendelea kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika Mamlaka nyingine za haki Jinai wale wote ambao kupitia Mitandao mbalimbali ya Kijamii wamekuwa na tabia ya kutengeneza, kuandika na kusambaza maandishi na picha mjongeo za kuhamasisha watu kufanya  vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa ni kinyume  na maadili na utamaduni wa Mtanzania ikiwa pia ni kinyume na sheria za nchi.


Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania DCP David Misiime imeeleza kuwa vitendo hivyo vinasukumwa na dhamira ovu ambapo pamoja na kwamba ni kinyume cha sheria za nchi, vimekuwa vikisababisha hofu na taharuki kwa wananchi wema walio wengi kuliko wao wenye nia Ovu bila ya kuwa na sababu zozote za msingi.

"Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia Watanzania kuwa linaendelea kuwasaka na kuwakamata na kuwafikisha katika Mamlaka nyingine za haki jinai kwa hatua za kisheria kama ambavyo limeshafanya kwa waliokwisha kamatwa." Imesema taarifa ya Jeshi la Polisi.

Polisi kupitia taarifa yake ya leo Jumapili Oktoba 05, 2025 kwa waandishi wa habari imetaarifu pia kwamba bado inaendelea na kushughulika na uhalifu huo na bado wengine hawajafikiwa na mkono wa sheria, wakiwataka kutojidanganya bali wakumbuke kuwa kinachosubiriwa sasa  ni muda sahihi na ukamilishaji wa taratibu za kuwafikia wakati wowote kuanzia sasa kulingana na ushahidi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Sunday, 5 October 2025

Kupiga kura ni heshima, wajibu na silaha ya Demokrasia

10/05/2025 03:19:00 pm
KUPIGA KURA NI HESHIMA, WAJIBU NA SILAHA YA KIDEMOKRASIA

Upo ushahidi madhubuti unaoonesha uwepo wa tija ya k upiga kura Katika uchaguzi Mkuu wa Tanzania licha ya uwepo wa mitazamo na kauli mbalimbali kuwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ni kupoteza muda tofauti na uhalisia ulivyo, uchaguzi ukitajwa kama heshima, wajibu na silaha ya Kidemokrasia kote duniani.

"Kupiga kura ni haki ya Kikatiba, inayomuwezesha kila Mtanzania kushiriki katika maamuzi ya nchi kwa njia ya amani, kupitia kura wananchi huamua ni nani awaongoze katika nafasi za kisiasa kama Rais, Wabunge na Madiwani na hii ni njia halali ya kushiriki katika ujenzi wa Taifa na kuhakikisha kuwa sauti ya mwananchi inasikika." Amesema Mchambuzi wa siasa Ally Said alipozungumza nasi.

Kulingana na Mchambuzi huyo, wananchi wanapojitokeza kwa wingi kupiga kura wana nafasi ya kuchagua Viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo, kupitia kura matatizo ya huduma duni za jamii yanaweza kushughulikiwa, Kura ikiimarisha pia misingi ya demokrasia na utawala bora kwa kuwafanya walioko madarakani kuwajibika kwa wananchi kwa kujua kuwa wanaweza kuondolewa kwa kura ikiwa hawatatimiza wajibu na ahadi zao.

John James, Mwananchi wa Goba Jijini Dar Es salaam anasema anafahamu kuhusu haki yake ya kupiga kura, akihimiza umuhimu wa kuwachagua wale wanaojua shida za wananchi na wenye kujali mahitaji ya wananchi. Akieleza kuwa mabadiliko ha kweli yanapatikana kupitia kura na si vurugu, matusi, jazba ama maandamano ya kutaka kushinikiza mambo isivyo halali.

Ushiriki wa uchaguzi unatoa nafasi kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika maamuzi yanayogusa maisha yao ya kila siku ambapo Viongozi wanaochaguljwa kwa ushirikishwaji wa wananchi wanakuwa na uwezo wa kutengeneza mipango ya maendeleo inayokidhi mahitaji halisi ya eneo husika, wito ukitolewa kwa kila mwananchi mwenye sifa kujitokeza kupiga kura kwa amani, kuheshimu sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuepuka kuvunja sheria kwa kuhamasisha wananchi kutokupiga kura ama kulinda kura kwenye Vituo vya upigaji kura.

DAR ES SALAAM WAELEZA UTAYARI WAO WA KUSHIRIKI KUPIGA KURA, WAYAKATAA MAANDAMANO

10/05/2025 03:01:00 pm
Na Mwandishi wetu. 

Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamesema wapo tayari kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakijitenga na ushawishi unaofanywa mtandaoni wa kuwataka kuandamana na kutojitokeza kupiga kura, wakieleza kufahamu vyema umuhimu wa amani na athari za vurugu na maandamano ikiwemo vifo, majeraha na kuporomoka kwa uchumi kutokana na kukosekana utulivu wa wao kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.


Pantaleo Mushi Mkazi wa Mbezi Beach amesema anafahamu jukumu lake la Kikatiba la kupiga kura, akihamasisha Vijana wengine kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya Kikatiba kupiga kura na kuchagua Kiongozi wamtakaye, akieleza kuwa athari za kutopiga kura ni kuruhusu kuchaguliwa kwa Kiongozi asiyemtaka na kumnyima fursa Kiongozi sahihi kuweza kushika Madaraka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika Ngazi ya Kata, Jimbo na kwenye Nafasi ya Urais.

Kwa upande wao Said Nassor na Yusuph Ibengwe, wakazi wa Kawe, wameeleza kutofahamu lolote kuhusu maandamano na kusisitiza wananchi kutokubali kurubuniwa katika kuharibu amani ya Tanzania kwa maslahi binafsi ya baadhi ya wanasiasa, wakihimiza wananchi kutumia haki yao vyema ya Kikatiba kuchagua Viongozi wanaowataka kwa njia ya amani hapo Oktoba 29. 2025 siku ya Upigaji kura na kutojihusisha na vurugu ama kusalia vituoni kulinda kura.

Kulingana na baadhi ya wachambuzi wa siasa, mabadiliko yanaanzia kwenye sanduku la kura na ikiwa hutopiga kura, mtu mwingine ataamua hatma yako. Kupiga kura sio haki tu bali ni jukumu lako kama raia kwani unapokaa kimya bila kupiga kura unapoteza haki yako na kuwapa wengine fursa ya kuamua kuhusu maisha yako, serikali yako na mustakabali wa nchi yako. Wanahimiza kutokubali kupoteza sauti yako wakiamini kuwa kura yako ina thamani katika kuitengeneza jamii unayoitaka kwasasa na kizazi kijacho.
Adbox