Dodoma
Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, amezindua zoezi la ugawaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Katesh, wilaya ya Hanang, ambapo jumla ya mitungi 3,000 iliyokamilika na vifaa vyake imetolewa kwa wananchi kwa bei nafuu ya ruzuku ya shilingi 17,500 (elfu kumi na saba na mia tano) kwa kila mtungi. Aidha, imeelezwa kwa mkoa mzima wa Manyara jumla mitungi 16,275 itasambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu.
Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote mkoani Manyara kusimamia kwa makini zoezi hili, ili kuhakikisha mitungi hiyo inauzwa kwa bei iliyokubaliwa na kuepuka udanganyifu wa baadhi ya Mawakala/wafanyabiashara wasio waaminifu.
“Natoa rai kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha utaratibu unazingatiwa, na mitungi hii inawafikia walengwa kwa bei ya shilingi 17,500 kama ilivyopangwa. Hatutavumilia wafanyabiashara watakaojaribu kulangua na kuuza kwa bei ya juu ili kujipatia faida isiyo halali,” amesema Sendiga kwa msisitizo.
Mheshimiwa Sendiga ameeleza kuwa kampeni hii ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inahoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan za kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa, na pia kulinda afya ya wananchi dhidi ya moshi unaosababisha magonjwa ya njia ya hewa.
Mpango huu wa ruzuku unatarajiwa kupunguza mzigo wa gharama ya awali kwa wananchi ya kununua majiko ya gesi na hivyo kuwa chachu ya mabadiliko kuelekea upishi salama na rafiki kwa mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, leo Julai 11. 2025 amezindua zoezi la ugawaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Katesh, wilaya ya Hanang, ambapo jumla ya mitungi 3,000 iliyokamilika na vifaa vyake imetolewa kwa wananchi kwa bei nafuu ya ruzuku ya shilingi 17,500 (elfu kumi na saba na mia tano) kwa kila mtungi. Aidha, imeelezwa kwa mkoa mzima wa Manyara jumla mitungi 16,275 itasambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu.
Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote mkoani Manyara kusimamia kwa makini zoezi hili, ili kuhakikisha mitungi hiyo inauzwa kwa bei iliyokubaliwa na kuepuka udanganyifu wa baadhi ya Mawakala/wafanyabiashara wasio waaminifu.
“Natoa rai kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha utaratibu unazingatiwa, na mitungi hii inawafikia walengwa kwa bei ya shilingi 17,500 kama ilivyopangwa. Hatutavumilia wafanyabiashara watakaojaribu kulangua na kuuza kwa bei ya juu ili kujipatia faida isiyo halali,” amesema Sendiga kwa msisitizo.
Mheshimiwa Sendiga ameeleza kuwa kampeni hii ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inahoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan za kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa, na pia kulinda afya ya wananchi dhidi ya moshi unaosababisha magonjwa ya njia ya hewa.
Mpango huu wa ruzuku unatarajiwa kupunguza mzigo wa gharama ya awali kwa wananchi ya kununua majiko ya gesi na hivyo kuwa chachu ya mabadiliko kuelekea upishi salama na rafiki kwa mazingira.
DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuongeza juhudi katika kutoa hamasa kwa wananchi ili kuzingatia kanuni za afya bora na kuchukua hatua madhubuti za kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Amesema ni vema elimu itakayotolewa izingatie ujenzi na matumizi ya vyoo bora, unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni nyakati zote muhimu ili kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza, uondoshaji salama wa majitaka katika ngazi ya kaya na maeneo ya umma pamoja na kutibu maji ya kunywa kwa njia ya kuchemsha au kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam.
Vilevile Makamu wa Rais ametoa rai kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuvitunza vifaa tiba ikiwemo mashine za kisasa za uchunguzi na matibabu pamoja na magari ya kubeba wagonjwa yaliyonunuliwa na Serikali ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.
Pia amewasihi kuimarisha eneo la utunzaji wa kumbukumbu za matumizi ya dawa na vifaa tiba ili kuleta ufanisi katika utunzaji wa dawa na vifaa tiba na kuepuka upotevu. Amesema kutokuwepo na kumbukumbu sahihi za matumizi ya dawa na vifaa tiba hutatiza katika usambazaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa, na kutoa mwanya wa wizi na matumizi yasiyo sahihi.
Halikadhalika Makamu wa Rais amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kulipa kipaumbele suala la utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya dawa ili kuisaidia jamii kutambua na kuepuka madhara ya matumizi holela ya dawa hususani dawa za maumivu na antibiotics ambazo zikitumiwa kiholela madhara yake ni makubwa. Pia amewataka kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa kiapo cha maadili katika kuwahakikishia wananchi huduma bora.
Aidha ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma wakati Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
Amesema katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora za afya, Serikali imeweka kipaumbele suala la rasilimali watu yenye weledi, ambapo imeajiri jumla ya watumishi wapya 25,936 wa kada mbalimbali za afya katika ngazi ya msingi. Hatua hiyo imesaidia kukabili upungufu wa watumishi na kuongeza uwiano kati ya watoa huduma na wagonjwa. Ameongeza kwamba Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika eneo hilo hususani kwenye kada za kimkakati, ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali imefanikisha ujenzi wa jumla ya vituo kutolea huduma za afya 7414 ikiwemo vituo vilivyokuwepo na vilivyojengwa Awamu ya Sita. Amesema kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan jumla ya hospitali kongwe 48 zimekarabatiwa, ujenzi wa majengo ya huduma za dharura 87, majengo ya huduma za wagonjwa mahututi 30 pamoja na mifumo ya hewa tiba 21.
Ameongeza kwamba katika kipindi cha miaka minne jumla ya wakinamama zaidi ya laki tisa waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za uzazi pingamizi waliweza kufanyiwa upasuaji salama katika vituo vya afya vilivyoboreshwa na vilivyojengwa upya.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya Afya ikiwemo kuongeza bajeti kufikia trilioni 2.6 kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Amesema kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Bajeti ya Wizara ya Afya imefikia trilioni 7.15 hivyo kufanya mageuzi makubwa ya utoaji huduma za afya nchini. Amesema Wizara inatarajia kuanzisha chaneli maalumu ya Afya (Afya Tv) ili iweze kutangaza taarifa zinazohusu afya kwa wananchi.
Amesema juhudi mbalimbali katika kuboresha sekta ya afya zimesaidia kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kumaliza ugonjwa wa Marbug ndani ya muda mfupi wa siku 54, kuimarisha diplomasia ya kimataifa katika sekta ya afya, kupungua kwa vifo vya mama na mtoto, kupungua kwa vifo vinavyotokana na dharura, kuongezeka kwa tiba utalii.
Ameongeza kwamba kwa sasa Tanzania inatarajia kuwa kuwa kituo cha umahiri wa matibabu ya upandikizaji ini, kituo cha umahiri matibabu ya mfumo wa mkojo, matibabu ya uzazi kwa wanaume, akili mnemba katika upasuaji, matibabu ya damu na upandikizaji uloto, matibabu ya figo, matumizi ya nyuklia katika matibabu ya saratani.
Awali akisoma risala, Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa Dkt. Best Magoma ameipongeza serikali kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya kuanzia ngazi ya afya ya msingi. Pia ameiomba Serikali kuhakikisha inapunguza uhaba wa nyumba za watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kukabiliana na dharura zinazowapata wananchi hususani nyakati za usiku.
Mkutano huo wa siku tatu una kauli mbiu isemayo “Wajibu wa Waganga Wakuu wa Miko ana Halmashauri katika kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote”
Aungwa mkono- Eng. Sangweni
Apongeza kasi ya Dkt. Biteko na Uongozi Menejimenti ya Nishati katika kufanikisha Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia.
Asifu juhudi za TANESCO na REA katika kutekeleza Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia.
Atoa Rai kwa Watanzania kuhamia kwenye Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mha. Charles Sangweni ametoa Rai kwa Wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suhuhu Hassan katika Kampeni ya Kitaifa ya kuhamia kwenye Nishati Safi ya Kupikia.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 09 Julai, 2025 na Mha. Charles Sangweni alipotembelea Banda la TANESCO katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-Salaam yanayoendelea jijini Dar-es-Salaam.
Amesema Tanzania tuna bahati kuwa, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jemedari Mkuu wa Majeshi ya nchi yetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ndiye Kinara wa Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia Duniani.
Amesema, Wizara ya Nishati na Watanzania wote kiujumla, ni muhimu tuunge mkono juhudi zinazofanywa na Rais wetu katika kuhakikisha Watanzania wanahamia katika Nishati Safi ya Kupikia kwanza kwa kuhakikisha tunapokea na tunaendana na Kauli Mbiu ya Nishati Safi ya Kupikia na kuunga mkono jitihada alizozianzisha.
Amesema, "kama Watendaji, tumefurahi kuona, wenzetu wa TANESCO wameunga Mkono juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kuja na kampeni ya kuhamasisha matumizi ya vyombo mbadala vya umeme vinavyotumia umeme kidogo na ambavyo vinahakikisha Nishati inayotumika kwa ngazi ya kawaida kabisa majumbani inakuwa ni Nishati Safi." Ameeleza kwa hisia za kuvutiwa na hatua hiyo Mha. Sangweni.
Mha. Sangweni ameeleza zaidi kuwa, katika kutembelea Banda la TANESCO, ameona vitu vingi, ikianzia kwa REA Usambazaji wa Umeme unavyofanyika kwa kasi na hii inaonyesha kuunga mkono Juhudi za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi wengine wa Wizara akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko
Pia, Mha. Sangweni amesema vilevile katika Banda la TANESCO amekuta Wadau wanauza majiko ya umeme yanayotumia Nishati ya umeme kidogo sana ikilinganishwa na majiko mengine ya kawaida.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa PURA ameeleza kufurahishwa kwake zaidi na majiko hayo yanayotumia mfumo wa sumaku kupitisha moto kuwa na mfumo wa ku-sence pale ambapo sufuria haiko jikoni na namna yanavyopunguza kabisa upotevu wa umeme ambao hautumiki.
"Tumeona kwamba, usipoweka sufuria basi hakuna moto ambao un
Amefafanua kuwa, hiyo yote ni katika kuhakikisha kwamba bili iliyokuwa inakuja kwa kiasi kikubwa ambayo ilikuwa inakuja kutokana na majiko ambayo hayana control kama hizo, inaenda kupungua kwa kiasi kikubwa sana.
"Hatua hiyo itatufanya sisi ambao vipato vyetu sio vikubwa kuona kuwa kutumia umeme sio anasa tena bali ni Matumizi Bora Kabisa ya Nishati ambayo iko safi na inayofaa kwa matumizi na ulinzi wa mazingira kama ambavyo Viongozi wetu wa nchi wamekuwa wakituhimiza na kusisitiza ili kama nchi tuingie kwenye Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia." Amesema Mha. Sangweni.
![]() |
| Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema na meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi katika kata ya Longuo mjini Moshi. |
![]() |
| Ofisi mpya ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Longuo B . |
![]() |
| Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema taifa na meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael akikata utepe kufungua ofisi mpya ya kata ya Longuo B. |
![]() |
| Meya Michael akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kufungua ofisi ya kata ya Chadema. |
![]() |
| Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema akitia saini katika kitabu cha wageni wakati wa ufunguzi wa ofisi ya kata ya Longuo B. |
![]() |
| Diwani wa kata ya Longuo B,Ray Mboya akitia saini katika kitabu hicho. |
![]() |
| Baadhi ya makada wa Chadema manispaa ya Moshi wakishuhudia zoezi hilo. |
![]() |
| Ofisi mpya ya Chadema kata ya, Longuo
manispaa ya Moshi ikafunguliwa rasmi. Na Dixon Busagaga . |

