MWENGE wa Uhuru umezindua miradi 6 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 4.3 katika Halmashauri ya mbili ya wilaya ya nzega ambazo ni nzega vijijini na nzega mjini zote zipo mkoani i Tabora.
Akizungumza kwa nyakati tofauti akiwa katika eneo la miradi hiyo jana Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Ismail Al Usi alionesha kuridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika ikiwemo ubora wa miradi hiyo.
Alibainisha kuwa miradi hiyo iliyopo katika sekta ya elimu, afya, huduma za utawala, uwezeshaji wananchi kiuchumi na miundombinu ya barabara imeakisi dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuboresha maisha ya wananchi.
Awali akipikea mwenge huo mkuu wa wilaya ya nzega , ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega, Naitapwaki Tukai alisema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutumia Mwenge wa Uhuru kama chombo muhimu cha kuhamasisha maendeleo, mshikamano wa kitaifa na ushiriki wa wananchi katika miradi ya kijamii na kiuchumi.
Katika halmashauri ya wilaya ya Nzega Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri mbili za Nzega Mji na Nzega kwa umbali wa kilomita 117.2 ukianza na Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa kupitia jumla ya miradi sita ya maendeleo inayogharimu shilingi bilioni 2.3, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Miradi hiyo ilijumuisha ujenzi wa kituo cha mafuta cha Nyarubanda Oil kilichogharimu shilingi bilioni 1.092, ujenzi wa zahanati ya Ipilili uliogharimu shilingi milioni 103, pamoja na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya walimu na matundu sita ya vyoo kwa gharama ya shilingi milioni 92.
Aidha alisema kwamba miradi mingine ni wa kikundi cha vijana wajasiriamali cha Constrafrica waliopatiwa fedha asilimia 10 kiasi cha shilingi milioni 19.
Pia mwenge huo uliweka jiwe la msingi mradi wa upanuzi wa mfuko wa kusafisha na kutibu maji Nzega unaotekelezwa kwa shilingi milioni 620 na mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Lumambo–Kitongo hadi FDC unaogharimu shilingi milioni 462.1.
Aidha, Mwenge wa Uhuru mwaka huu unabeba kaulimbiu isemayo: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”, ikiwa ni wito kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi huku wakidumisha amani, mshikamano na utulivu wa kitaifa.
Mkuu wa mkoa wa Tabora ,Paulo Chacha amewataka wananchi Kuyatumia maonyesho ya nane nane kujifunza mbinu Bora za uzalishaji wa mazao ya Kilimo,Mifugo na uvuvi kupata maarifa sahihi zitakazowasaidia kufanya uzalishaji wenye tija ili waweze kujikwamua kiuchumi .
Kauli hiyo ilitolewa jana wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya nane nane kwa Kanda ya Magharibi yaliyofanyika katika viwanja vya Ipuli mkoani Tabora.
Chacha alisema kwamba maonyesho hayo yalitumika vizuri yanaweza keta Tija kwa wakulima na kuweza kuongeza uzalishaji mkubwa.
"Wengi wetu tupo kwa lengo la kuona kujifunnza mbinu Bora , uzalishaji mazao ya Kilimo ,mifumgo na uvuvi ili kupata maarifa yatakayotusaidia kupiga hatua kwenye Mapinduzi ya kijani na hivyo kuinua Pato na uchumi kwa Kaya zetu na taifa kwa ujumla " alisema Chacha.
Kwa upande wake , Msajili wa Mamlaka ya Wanunuzi wa Mbegu kutoka Wizara ya Kilimo Twalib Njohole alibainisha lengo la maonyesho ya nane nane ni kutoa elimu na teknolojia bora ya kilimo ili kuongeza uhakika wa uzalishaji wa mazao.
Afisa Masoko wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Okia John, aliwataka Wakulima kutumia Mbegu ambazo zimethibitishwa na mdhibiti ubora ili waweze kupata mavuno bora .
"Tuna mhakikishia Mkulima Mbegu ambayo tunampa hapa kwenye hili banda atakapofika ni Mbegu bora kwa sababu imethibitisha na mdhibiti ubora wa Mbegu" Okia alisisitiza
Maonyesho ya nane nane kwa Kanda ya magharibi yanafanyika kwenye viwanja vya Ipuli ambapo tamati yake itakuwa Agosti 8,2025 ambapo yatafungwa na Mkuu wa mkoa wa Kigoma Saimon Silo.
"maonyesho haya yamebebwa na kauli mbiu ya " _Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi"._
Mradi wa upanuzi wa majisafi ya Ziwa Victoria toka Makomero hadi Mgongoro utawanufaisha Zaidi ya wakazi 8000 wa vitongoji viwili na kijiji kimoja Wilayani Igunga mkoani Tabora.
Akizungumza kabla ya kuzinduliwa mradi huo uliogharimu Shilingi 840 milioni ambao uliwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Igunga,Iguwasa,Alex Ntonge alisema unawanufaisha wakazi ambao walikuwa wakihangaika kutafuta maji.
Alieleza kuwa wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya maji na kuwafanya watumie muda mqingi kuhangaikia maji.
Kwa sasa alisema adha waliyokuqa nayo wakazi hao imeisha kwani wanapata huduma ya majisafi na salama kupitia mradi huo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025,Ismail Ali Ussi,aliipongeza Iguwasa kwa kuhakikisha wakazi wake wanapata maji na kusema kuwa sekta ya maji inafanya kazi nzuri.
Alisema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi nzuri ya kuhakikisha fedha nyingi zaidi zinaenda sekta ya maji ambayo nayo haijamuangusha kwa kuwa na miradi yenye ubora.
Alieleza kuwa watumishi wa sekta hiyo wanafanyankazi nzuri sana na hawana budi kupongezwa kutokana na utendaji aao mzuri wa kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Sauda Mtondoo alisema kukamilika kwa mradi huo kunafanya wakazi wanaopata majisafi na salama mjini Igunga kufikia asilimia mia moja.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa wa Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kusimamia kikamilifu na kwa ufanisi utekelezaji wa Itifaki ya Jumuiya hiyo dhidi ya Rushwa ili kujenga ukanda usio na Rushwa.
Amesema kuwa Itifaki ya SADC Dhidi ya Rushwa bado ni nyenzo muhimu katika kufanikisha utawala bora, amani na muungano endelevu wa kikanda hivyo viongozi hao wanapaswa kuhakikisha kuwa juhudi za kupambana na rushwa zinaendelezwa.
Ametoa wito huo leo (Agosti 04, 2025) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Utekelezaji wa Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Dhidi ya Rushwa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.
“Lazima tukiri kwamba rushwa ni tishio kwa usalama. Inachochea uhalifu uliopangwa, usafirishaji haramu wa binadamu, ugaidi, na kudhoofika kwa utawala wa sheria.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni, nchi Wanachama wa SADC ikiwemo Tanzania zimeendelea kuimarisha sheria za mapambano dhidi ya rushwa, kuziwezesha Taasisi zinazosimamia udhibiti na mapambano dhidi ya rushwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za rushwa kwa ustawi wa Taifa.
“Hata ushirikiano wa kikanda katika mapambano dhidi ya rushwa umeimarika kwa kubadilishana taarifa, mashirikiano katika masuala ya sheria pamoja na uchunguzi wa pamoja katika kushughulikia masuala ya rushwa ya kikanda”
Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania kwa upande wake, inachukulia mapambano dhidi ya rushwa kama kipaumbele cha kitaifa na jambo la msingi kwa maendeleo Taifa na usalama wa Taifa.
“Njia iliyo mbele huenda ikawa ndefu, lakini tusiwaze kushindwa. Kwa ushirikiano endelevu, maono ya kimkakati, na utashi wa kisiasa, tunaweza na tunapaswa kujenga ukanda wa SADC usio na rushwa”
Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza viongozi hao kwa kuendelea kusimamia mikakati mbalimbali ya kupiga vita rushwa ikiwemo kuanzishwa kwa mfumo imara ya ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa SADC. Pamoja na Kielelezo cha Jitihada za Kikanda za Kupambana na Rushwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stegomena Tax amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kusimama imara katika kuendeleza utawala bora na kuheshimu utawala wa sheria, ambayo ni nguzo kuu katika mapambano yao ya pamoja dhidi ya rushwa.
“Warsha hii, imekuja wakati muafaka, ikiwa ni jukwaa la kubadilishana uzoefu bora, kuimarisha ushirikiano, na kuoanisha juhudi zetu katika kupambana na rushwa kwa ufanisi zaidi katika ukanda huu.”
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kupambana na Rushwa ya SADC, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila amesema kuwa kupitia mikakati Miwili ya Kupambana na Rushwa ya (2018-2022) na (2023-2027), wamefanikiwa kuandaa mtaala wa Kikanda uliowekwa viwango vya uchunguzi na kinga dhidi ya rushwa, kuandaa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Kikanda wa Kupambana na Rushwa pamoja na Kuandaliwa kwa Tathmini ya Kikanda ya Mapambano Dhidi ya Rushwa.
Watumishi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(Takukuru) , taasisi simamizi za maadili pamoja na mamlaka simamizi za maadili ya kitaaluma wametakiwa kuendelea kushirikiana na kuwekeza kwenye mikakati ambayo itaakisi na kuimarisha utendaji kazi wa wataalamu wanaotoa huduma kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Crispin Chalamila,
wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simazi za maadili ya kitaaluma.
Chalamila amesema kuwa uwepo wa mawasiliano baina yao utasaidia kuimarisha hali ya uadilifu katika maeneo yao na kuchukua hatua kwa wale wachache watakaoonekana kwenda kinyume na utaratibu uliowekwa.
“Ninatoa rai kwetu wote kwamba, mawasilisho na majadiliano yetu yatuongoze kwenye ubunifu wa mikakati ya kuboresha misingi ya maadili ya utendaji na maadili ya kitaaluma kama njia mojawapo ya kuimarisha utoaji wa huduma katika utumishi wa umma, kudhibiti vitendo vya rushwa kwa lengo la kuleta ustawi kwa wananchi,”
alisema Chalamila
Hata hivyo, aliwasihi washiriki wa kikao hicho kuendeleza mawasiliano na ushirikiano kati yao taasisi simamizi za maadili pamoja na mamlaka simamizi za maadili ya kitaaluma ili kuimarisha hali ya uadilifu katika maeneo yao na kuchukua hatua kwa wale wachache watakaoonekana kwenda kinyume na utaratibu uliowekwa.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Felister Shuli, alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanya mwaka 2021 na ofisi hiyo ulibaini kuwa suala la maadili nchini linaendelea kuimarika.
“Utafiti ule ulionyesha kuwa suala la maadili nchini linaendelea kuimarika kwani wananchi wengi hivi sasa wanaripoti matukio ya ufunjifu wa maadili lakini pia watumishi wa umma hivi sasa wanazingatia suala la maadili ya utumishi wa umma kazini,”alisema
Alisema licha ya mafanikio hayo bado zipo changamoto chache ikiwamo kwenye ngazi ya familia hivyo ipo haja ya kuendelea kukumbushana ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Baadhi ya taasisi zilizoshiriki kwenye kikao hicho ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Ofisi ya Mkaguzi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Mamlaka ya Udhibiti Manunuzi ya Umma (PPRA), Bodi ya Mkandarasi (CRB),Bodi ya Baraza la Wakunga na Wauguzi (TNMC).
Nondo Oscar Awasha MOTO wa Ubunifu kwa Vijana"
-
*Mfugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Nondo akionyesha moja ya mbwa anaowauza*
Na Woinde Shizza, Arusha
Mfugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Nondo Oscar, ...
-
[image: SPORT AND THE SUSTAINABLE DEVELOPMENT]
*The United Nations* have long recognized, advocated for and supported the
important contributions of spor...
Munere veritus fierent cu sed, congue altera mea te, ex clita eripuit evertitur duo. Legendos tractatos honestatis ad mel. Legendos tractatos honestatis ad mel.
, click here →