Adbox

Saturday, 12 July 2025

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWATAKA WAGANGA WAKUU NCHINI KUONGEZA JUHUDI KANUNI ZA AFYA

7/12/2025 06:18:00 pm

DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuongeza juhudi katika kutoa hamasa kwa wananchi ili kuzingatia kanuni za afya bora na kuchukua hatua madhubuti za kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza.






Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Amesema ni vema elimu itakayotolewa izingatie ujenzi na matumizi ya vyoo bora, unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni nyakati zote muhimu ili kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza, uondoshaji salama wa majitaka katika ngazi ya kaya na maeneo ya umma pamoja na kutibu maji ya kunywa kwa njia ya kuchemsha au kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam.


 

Vilevile Makamu wa Rais ametoa rai kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuvitunza vifaa tiba ikiwemo mashine za kisasa za uchunguzi na matibabu pamoja na magari ya kubeba wagonjwa yaliyonunuliwa na Serikali ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.

 

Pia amewasihi kuimarisha eneo la utunzaji wa kumbukumbu za matumizi ya dawa na vifaa tiba ili kuleta ufanisi katika utunzaji wa dawa na vifaa tiba na kuepuka upotevu. Amesema kutokuwepo na kumbukumbu sahihi za matumizi ya dawa na vifaa tiba hutatiza katika usambazaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa, na kutoa mwanya wa wizi na matumizi yasiyo sahihi.

 

Halikadhalika Makamu wa Rais amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kulipa kipaumbele suala la utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya dawa ili kuisaidia jamii kutambua na kuepuka madhara ya matumizi holela ya dawa hususani dawa za maumivu na antibiotics ambazo zikitumiwa kiholela madhara yake ni makubwa. Pia amewataka kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa kiapo cha maadili katika kuwahakikishia wananchi huduma bora.

 

Aidha ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma wakati Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.

 

Amesema katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora za afya, Serikali imeweka kipaumbele suala la rasilimali watu yenye weledi, ambapo imeajiri jumla ya watumishi wapya 25,936 wa kada mbalimbali za afya katika ngazi ya msingi. Hatua hiyo imesaidia kukabili upungufu wa watumishi na kuongeza uwiano kati ya watoa huduma na wagonjwa. Ameongeza kwamba Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika eneo hilo hususani kwenye kada za kimkakati, ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa wananchi.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali imefanikisha ujenzi wa jumla ya vituo kutolea huduma za afya 7414 ikiwemo vituo vilivyokuwepo na vilivyojengwa Awamu ya Sita. Amesema kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan jumla ya hospitali kongwe 48 zimekarabatiwa, ujenzi wa majengo ya huduma za dharura 87, majengo ya huduma za wagonjwa mahututi 30 pamoja na mifumo ya hewa tiba 21.

 

Ameongeza kwamba katika kipindi cha miaka minne jumla ya wakinamama zaidi ya laki tisa waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za uzazi pingamizi waliweza kufanyiwa upasuaji salama katika vituo vya afya vilivyoboreshwa na vilivyojengwa upya.

 

Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya Afya ikiwemo kuongeza bajeti kufikia trilioni 2.6 kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Amesema kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Bajeti ya Wizara ya Afya imefikia trilioni 7.15 hivyo kufanya mageuzi makubwa ya utoaji huduma za afya nchini. Amesema Wizara inatarajia kuanzisha chaneli maalumu ya Afya (Afya Tv) ili iweze kutangaza taarifa zinazohusu afya kwa wananchi.

 

Amesema juhudi mbalimbali katika kuboresha sekta ya afya zimesaidia kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kumaliza ugonjwa wa Marbug ndani ya muda mfupi wa siku 54, kuimarisha diplomasia ya kimataifa katika sekta ya afya, kupungua kwa vifo vya mama na mtoto, kupungua kwa vifo vinavyotokana na dharura, kuongezeka kwa tiba utalii.

 

Ameongeza kwamba kwa sasa Tanzania inatarajia kuwa kuwa kituo cha umahiri wa matibabu ya upandikizaji ini, kituo cha umahiri matibabu ya mfumo wa mkojo, matibabu ya uzazi kwa wanaume, akili mnemba katika upasuaji, matibabu ya damu na upandikizaji uloto, matibabu ya figo, matumizi ya nyuklia katika matibabu ya saratani.

 

Awali akisoma risala, Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa Dkt. Best Magoma ameipongeza serikali kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya kuanzia ngazi ya afya ya msingi. Pia ameiomba Serikali kuhakikisha inapunguza uhaba wa nyumba za watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kukabiliana na dharura zinazowapata wananchi hususani nyakati za usiku.

 

Mkutano huo wa siku tatu una kauli mbiu isemayo “Wajibu wa Waganga Wakuu wa Miko ana Halmashauri katika kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote”


Thursday, 10 July 2025

RAIS SAMIA KINARA , NISHATI SAFI YA KUPIKIA DUNIANI.

7/10/2025 08:08:00 pm

 Aungwa mkono- Eng. Sangweni

Apongeza kasi ya Dkt. Biteko na Uongozi Menejimenti ya Nishati katika kufanikisha Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia.


Asifu juhudi za TANESCO  na REA katika kutekeleza  Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia.


Atoa Rai kwa Watanzania kuhamia kwenye Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mha. Charles Sangweni ametoa Rai kwa Wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suhuhu Hassan katika Kampeni ya Kitaifa  ya kuhamia kwenye Nishati Safi ya Kupikia.

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 09 Julai, 2025  na Mha. Charles Sangweni alipotembelea Banda la TANESCO  katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-Salaam yanayoendelea jijini Dar-es-Salaam.

Amesema Tanzania tuna bahati kuwa, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jemedari Mkuu wa Majeshi ya nchi yetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ndiye Kinara wa Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia Duniani.



Amesema, Wizara ya Nishati na Watanzania wote kiujumla, ni muhimu tuunge mkono juhudi zinazofanywa na Rais wetu katika kuhakikisha Watanzania wanahamia katika Nishati Safi ya Kupikia kwanza kwa  kuhakikisha tunapokea na tunaendana na Kauli Mbiu ya Nishati Safi ya Kupikia na kuunga mkono jitihada alizozianzisha.

Amesema, "kama Watendaji, tumefurahi kuona, wenzetu wa TANESCO wameunga Mkono juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kuja na kampeni ya kuhamasisha  matumizi ya vyombo mbadala vya umeme vinavyotumia umeme kidogo na ambavyo vinahakikisha Nishati inayotumika kwa ngazi ya kawaida kabisa majumbani inakuwa ni  Nishati Safi." Ameeleza kwa hisia za kuvutiwa na hatua hiyo Mha. Sangweni.

Mha. Sangweni ameeleza zaidi kuwa, katika kutembelea Banda la TANESCO, ameona vitu vingi, ikianzia kwa REA  Usambazaji wa Umeme unavyofanyika kwa kasi na hii inaonyesha kuunga mkono Juhudi za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi wengine wa Wizara akiwemo  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko

Pia, Mha. Sangweni amesema vilevile katika Banda la TANESCO amekuta Wadau wanauza majiko ya umeme yanayotumia Nishati ya umeme kidogo sana ikilinganishwa na majiko mengine ya kawaida.


Mkurugenzi Mkuu huyo wa PURA ameeleza  kufurahishwa kwake zaidi na  majiko hayo yanayotumia mfumo wa sumaku kupitisha moto  kuwa na mfumo wa ku-sence  pale ambapo sufuria haiko jikoni na namna yanavyopunguza kabisa upotevu wa umeme ambao hautumiki.

"Tumeona kwamba, usipoweka sufuria basi hakuna moto ambao un


atoka na wakati mwingine ukiwa umejisahau, kunakuwa na timer ambayo inaweza ikazima jiko kulingana na jinsi ulivyo- set." Amesema Mha. Sangweni.

Amefafanua kuwa, hiyo yote ni katika kuhakikisha kwamba bili iliyokuwa inakuja kwa kiasi kikubwa ambayo ilikuwa inakuja kutokana na majiko ambayo hayana control kama hizo, inaenda kupungua kwa kiasi kikubwa sana.


"Hatua hiyo itatufanya sisi ambao vipato vyetu sio vikubwa kuona kuwa kutumia umeme sio anasa tena bali ni Matumizi Bora Kabisa ya Nishati ambayo iko safi na inayofaa kwa matumizi na ulinzi wa mazingira kama ambavyo Viongozi wetu wa nchi wamekuwa wakituhimiza na kusisitiza ili kama nchi tuingie kwenye Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia." Amesema Mha. Sangweni.



Sunday, 24 July 2016

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ALIPOTEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI

7/24/2016 01:19:00 am


 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya kuanza kutumika hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)

Tuesday, 16 February 2016

OFA YA UPENDO KUTOKA HUAWEI MSIMU HUU WA VALENTINE

2/16/2016 06:12:00 pm
Mabalozi wa Huawei wakipozi siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakipata picha ya ukumbusho na balozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa wateja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wateja walioshiriki katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Kushoto) akimkabidhi Mteja mfuko wa zawadi pamoja na kadi katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3   inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki hii, Mlimani City Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa mabalozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam. 

Na Mwandishi wetu, 
Kampuni ya simu ya Huawei, inayoshika nafasi ya tatu kwa utengenezaji na uuzaji wa simu za mkononi ulimwenguni imezindua promosheni ya Valentine ya muda wa wiki 3 inayohusisha vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji zawadi kwa wanunuzi wa simu za Huawei kutoka kwenye maduka yao mbalimbali ya rejareja yaliyosajiliwa.
Promotion hiyo itahusisha simu kuu mbili ambazo ni Huawei P8 na Huawei G8. Zawadi zinazotolewa kwa wateja ni pamoja na “selfie sticks, spika za Bluetooth na T-shirts. Pamoja na zawadi zote hizo ,wateja hao pia wanapewa fursa ya kupata picha nzuri za kumbukumbu ili waweze kuzitumia kwenye mitandao ya kijamii kama instagram na mingine.
Kampeni hii Iliyozinduliwa wikiendi hii mjini Dar es Salaam eneo la  Mlimani City, inawaahidi wateja wa Huawei kuona thamani ya pesa yao kutokana na zawadi watakazopatiwa .
Kwa mujibu wa report ya simu za mkononi ya hivi karibuni nchini Tanzania ilivyochapishwa mwaka jana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya watanzania wanaotumia simu za mkononi, waliojisajili imeongezeka kwa asilimia 16 kwa mwaka 2014 kufikia milioni 31.86 hiyo ni sawa na asilimia 67 kwa watanzania wote wanaotumia simu.
Huawei Tanzania wanaahidi kuendelea kutatua uhitaji wa wateja wao kwa kuwapatia   simu zenye ubora wa hali ya juu na orijino.
Tunatarajia kutoa huduma bora ya mawasiliano na intanet kwa bei nafuu kwa wananchi na pia kuwazawadia wateja wetu wale wazamani na wapya,  vifaa bora na vya kisasa vitakavyoweza kuongeza wigo katika matumizi ya simu zao za smatiphone  na intaneti pia” alisema Bw. Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania katika uzinduzi wa Promotion hiyo.
Akielezea promosheni hiyo, Bw. Peter Zhangjunliang alisema; promosheni hii ya wiki 3 ni ya nchi nzima na ipo wazi kwa watanzania wote watakao nunua simu za G8 na P8 kutoka Huawei.”

Huawei, rafiki yako kwa simu origino.

Kuhusu Huawei
Kampuni ya Huawei imejizatiti katika kutengeneza bidhaa bora kwa matoleo tofauti ulimwenguni, kutoa huduma rafiki za simu, kwenye intaneti kwa wateja wake. Kampuni ya Huawei inajulikana duniani katika utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti na vifaa vya majumbani.
Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2015, bidhaa vya Kampuni ya Huawei zinapatikana  zaidi ya nchi 150 ulimwenguni kote. Huawei ni kampuni ya 3 katika usambazaji wa simu (2015) ikiwa imesambaza zaidi ya milioni 100 ulimwenguni. Kampuni ya Huawei imeanzisha ushirikiano  na makampuni makubwa duniani kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom. 
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea www.huaweidevice.com

Monday, 25 May 2015

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CHADEMA ,JAFARY MICHAEL AFUNGUA MATAWI MAPYA MOSHI

5/25/2015 03:48:00 pm

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema na meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi katika kata ya Longuo mjini Moshi.
Ofisi mpya ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Longuo B .
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema taifa na meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael akikata utepe kufungua ofisi mpya ya kata ya Longuo B.
Meya Michael akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kufungua ofisi ya kata ya Chadema.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema akitia saini katika kitabu cha wageni wakati wa ufunguzi wa ofisi ya kata ya Longuo B.
Diwani wa kata ya Longuo B,Ray Mboya akitia saini katika kitabu hicho.
Baadhi ya makada wa Chadema manispaa ya Moshi wakishuhudia zoezi hilo.
Ofisi mpya ya Chadema kata ya, Longuo  manispaa ya Moshi ikafunguliwa rasmi.

Na Dixon Busagaga .

Sunday, 28 December 2014

FREDRICK SUMAYE: KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA

12/28/2014 02:08:00 pm


1Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine tayari kwa tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa huo jijini Mbeya , Mh. Fredrick Sumaye amewaasa watanzania kumcha mungu na kuchagua viongozi waadilifu wenye uzalendo wa nchi, wenye kupenda na kuhurumia wananchi masikini na wenye hofu ya mungu ili kulinda amani ya nchi yetu jambo litakalofanya hata maombi yanayofanyika kuombea taifa la Tanzania yapokelewa na Mungu , Tamasha hilo kesho linaendelea mkoani Iringa ambapo wakazi wa mjini Iringa wanapata nafasi nyingine ya kumcha mungu kwa njia ya uimbaji 2Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama 3Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizindua albam ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya yenye inayoitwa Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane kulia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama. 4Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu David Mwasota akiiombea albam ya Mubhopege Pa Finganilo ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya huku Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakishiriki katika maombi hayo. 5Mwimbaji wa muziki wa injili Upendo Nkone akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati wa tamasha la Krismas leo. 6Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa jukwaani. 7Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa akitunzwa na mashabiki wake wakati akiimba jukwaani. 10Tumaini Njole na wacheza shoo wake wakiwa angani wakati wakifanya vitu vyao jukwaani. 11Mashabiki walishindwa kukaa chini wakati wote wa tamasha. 14Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake jukwaani. 15Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake jukwaani. 17Mashabiki wakipata taswira kwa simu zao huku burudani ikiendelea. 18Mwimbaji Emmanuel Mgogo naye amefanya mambo makubwa sana katika tamasha hilo. 20Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili. 21Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake na wacheza shoo wake huyu amekuwa pia akifanya maonesho kama haya Ulaya na Marekani .. 22
Edson Mwasabwite kulia ni Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo wakionyesha vitu vikubwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 23Mwimbaji kutoka Kenya Ritha Kisava ambaye ameshiriki Tamasha la Krismas kwa mara ya kwanza akiimba hii ilikuwa kama utabulisho wake kwa mashabiki wa muziki wa Injili nchini Tanzania. 25Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakati wa tamasha hilo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA)
Adbox