Adbox

Sunday, 7 December 2025

RC MTAKA ALIA NA VIJANA WA GEN_Z NCHINI, AWATAKA KULINDA AMANI YA NCHI YAO.


Na Mwandishi wetu,Njombe

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amekisihi  kikundi cha vijana wanaojiita Gen_Z kutambua kuwa wao ni kizazi  kinachobeba matumaini na sura ya taifa,hivyo wanapaswa kulinda Amani badala ya kujiingiza kwenye makundi ya kutaka kuangamiza Taifa.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo kwenye Ibada katika Kanisa la wa Adventist Wasabato lililopo Mkoa wa Njombe ambapo ametumia Fursa hiyo kuisihi jamii hususani Vijana kutambua kuwa Amani ni Tunda la Haki ambapo ni wajibu wa kuilinda Amani ya nchi yetu kwa Wivu Mkubwa,

 “Mkoa wetu bado upo salama,hauna matishio ya kihalifu,tunaendelea kujenga mazingira thabiti ya ulinzi wa watu na mali,ili kutoa fursa kwa wananchi wetu kuendelea kufanya shughuli zao za uzalishaji mali na mahangaiko yao ya kujipatia kipato cha siku, 

"Na kuongeza " Usalama wa mkoa wetu, utatuongezea imani kwa wawekezaji wetu mbalimbali kuendelea kuamini kwamba Njombe ni mahala sahihi pa wao kuweka mitaji yao,wana Njombe tushikamane kuhakikisha tunaziepuka aina yoyote ya chokochoko zitakazoashiria uhalibifu wa mali, uwekezaji,miradi ya umma na binafsi,au uharibifu wa uhai wa wananchi wenzetu." Amesema  Rc  Mtaka.

Hata hivyo amewataka Wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo husika pale watakapoona na  kuhisi dalili yoyote inayoashiria uvunjifu wa amani , kuhatarisha usalama wa eneo lao ,kwani ulinzi shirikishi huanza na wanajamii mmoja mmoja kwa kutoa taarifa kwa wakati.

Ikumbukwe kuwa kupitia mitandao ya kijamii kumekuwepo na baadhi ya wanaharakati walioanzisha kikundi kinacho jiita wana Gen _Z cha kuhamasisha maandamano na uvunjifu wa Amani Nchini jambo ambalo halikubaliki kwa Taifa na jamii kwa ujumla.

Mwisho.

No comments:

Adbox