Rais Samia amebainisha hayo leo Jumanne Disemba 02, 2025 wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, akikaririwa awali akisema kwamba matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 yalikuwa ni matukio ya kupangwa yakiwa na lengo la kuiangusha dola ya Tanzania.
"Ndugu zangu nilisema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, lililopita limepita, kwa maneno tunasikia lipo jingine linapangwa lakini inshaallag Mola hatosimama nao, litapeperuka.
Lakini nataka niseme, nilimsikia mmoja kati ya waandaaji wa nje anasema ebu tarehe tisa lihairisheni subirini Krismasi kwasababu sasa hivi wamejipanga, nataka niwaambie wakati wowote wakija tumejipanga." Amesema Rais Samia.
Katika hatua nyingine Rais Samia amesema kama binadamu kukosana kupo, akikiri kuwa si kila wakati serikali inakuwa haina mapungufu, akisisitiza umuhimu wa kukaa, kuzungumza na kuondoa mapungufu


No comments:
Post a Comment