Adbox

Tuesday, 2 December 2025

matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 yalikuwa ni matukio ya kupangwa yakiwa na lengo la kuiangusha dola ya Tanzania.

12/02/2025 06:34:00 pm
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga wakati wote kukabiliana na wanaoratibu, kupanga na kufadhili matukio ya uvunjifu wa amani yaliyopangwa kufanyika aidha Disemba 09 ama Disemba 25, 2025.

Rais Samia amebainisha hayo leo Jumanne Disemba 02, 2025 wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, akikaririwa awali akisema kwamba matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 yalikuwa ni matukio ya kupangwa yakiwa na lengo la kuiangusha dola ya Tanzania.

"Ndugu zangu nilisema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, lililopita limepita, kwa maneno tunasikia lipo jingine linapangwa lakini inshaallag Mola hatosimama nao, litapeperuka.

Lakini nataka niseme, nilimsikia mmoja kati ya waandaaji wa nje anasema ebu tarehe tisa lihairisheni subirini Krismasi kwasababu sasa hivi wamejipanga, nataka niwaambie wakati wowote wakija tumejipanga." Amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine Rais Samia amesema kama binadamu kukosana kupo, akikiri kuwa si kila wakati serikali inakuwa haina mapungufu, akisisitiza umuhimu wa kukaa, kuzungumza na kuondoa mapungufu 

Monday, 1 December 2025

WATANZANIA WANATAKA UWAZI NA UCHUNGUZI KAMILI- JAJI OTHMAN CHANDE

12/01/2025 05:58:00 pm

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Jaji Mkuu mstaafu Mohammed Chande Othman amesema Watanzania wanataka uchunguzi kamilifu wa Matukio ya Oktoba 29 pamoja na kutaka uwazi kwenye kutekeleza wajibu wao.

Jaji mstaafu Othman amebainisha hayo leo Jumatatu Disemba Mosi, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari, akisisitiza kuwa baadhi ya Mikutano yao wataifanya hadharani na mingine faragha ili kulinda haki za watu wengine.

"Mikutano yetu mingine itafanyika kwenye hadhara na mingine itabidi tuende kwenye faragha kwenye mazingira maalumu ili kulinda haki za mtu na Tanzania sasahivi tuna sheria ya kulinda faragha za watu." Amesema Jaji Othman.

Mwenyekiti huyo wa tume ameeleza kuwa matakwa hayo ya watanzania wameyapokea na ndiyo watakayoyatumia katika kujibu hadidu za rejea katika utekelezaji wa majukumu yao ya uchunguzi wa matukio hayo ya Oktoba 29, 2025.

TUSIKUBALI KUCHONGANISHWA NA WACHACHE WENYE MASLAHI BINAFSI- MWIGULU

12/01/2025 05:12:00 pm

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa kwenye Ziara yake ya Kikazi Mkoani Arusha, amesisitiza umuhimu wa kulinda amani kwa maendeleo na ustawi wa Watanzania, akiwataka wananchi kuamka na kuwakataa wale wote wanaowachonganisha kwa maslahi yao binafsi.

Akieleza kuwafahamu baadhi ya Watanzania wanaolipwa fedha ili kuwagombanisha na kuwataka kuingia barabarani kufanya vurugu, Mhe. Nchemba ameeleza kuwa wanaohamasisha vurugu nchini wamekuwa na visingizio kadhaa vya kuwahadaa wananchi huku lengo lao likiwa ni kuwagombanisha watanzania ili kutaka kuzifaidi rasilimali za nchi.

"Zimetokea vurugu, kwa aina  ya vurugu zilivyotokea, kwanini hatushtuki? Wanatumia visingizio vingine lakini hapa kuna mchezo. Zimetolewa fedha wakapewa vijana na wale Vijana wakaandaa Vijana wenzao na kuwataka kufanya vurugu. Leo tujiulize wale wanaotoa hizo fedha watazirudishaje? Na kama ni maandamano, Kiongozi wake alikuwa nani? Waliandamana kutoka wapi kwenda wapi? Ajenda yao ilikuwa ipi? Tunachonganishwa mno, kuna jambo watu wanatafuta. Amkeni Watanzania." Amesema Waziri Mkuu.

Mhe. Mwigulu akizungumza katika Mkutano wake wa hadhara kwenye Viwanja vya Magufuli, Leganga, Usa River, Wilayani Arumeru, amesisitiza kuwa ikiwa Tanzania itapoteza amani na utulivu wake, jamii na serikali itashindwa kukabiliana na umaskini, gharama kubwa za maisha na kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana, akiwataka Watanzania kutorubuniwa na kuingia kwenye Vitendo vya Uvunjifu wa amani.
Adbox