Adbox

Friday, 10 October 2025

JESHI LA POLISI NCHINI KUWASHUGHULIKIA, WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUHAMASISHA CHUKI.

10/10/2025 01:01:00 pm
Na Mwandishi wetu.

Jeshi la Polisi nchini Tanzania kupitia msemaji wake DCP David Misime limesisitiza kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya Kijamii pamoja na ulinzi wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akibainisha kuwa Jeshi hilo limejipanga kikamilifu kushughulika kikamilifu na wote watakaohatarisha amani ya nchi.

Msemaji huyo pia ameonya kuhusu wanaotumia mitandao vibaya kuhamasisha chuki, uhasama na kusambaza taarifa za kuzusha, akisema sheria inatoa adhabu pia kwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii atakayesambaza (kushare) taarifa ambazo hazina ukweli ama ambazo zine lengo la kuzua taharuki na uhasama.

"Mitandao ya kijamii tukiitumia vibaya inaweza kutufikisha pabaya ikiwemo kutumika kama silaha kuleta uhasama, uzushi na kusambaza uongo kama ambao tunauona kwenye mitandao na nitoe wito kwa jamii unaposambaza taarifa ambazo sio sahihi ni kosa pia kwako unayesambaza taarifa potofu." Amesema Kamanda Misime.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari leo Oktoba 10, 2025, Misime pia ameeleza kuwa wamejipanga vyema kulinda raia na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi Mkuu, akiwapongeza watanzania kwa kuendelea kuelimika na kukuza ustaarabu wao wakati wote wa kampeni, akiomba ushirikiano zaidi wa kufichua uhalifu na wahalifu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Amewatoa hofu pia Watanzania kuhusu yanayoendelea mitandaoni, akisema nchi ni salama na hakuna tatizo lenye kutishia usalama na utulivu siku ya upigaji wa kura, akisema Jeshi la polisi linaendelea kuchukua hatua kwa wanaotumia mitandao hiyo vibaya na kuishukuru serikali kwa uwezeshaji wake mkubwa wa vifaa na vitendea kazi katika udhibiti wa uhalifu na wahalifu.

Amesema Jeshi hilo pia limesambaza Askari polisi zaidi ya 3,900 kwenye Kata zote za Tanzania bara pamoja na Askari 388 kwenye Shehia za Zanzibar wakitoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya mitandao na kuwataka wazazi kuelimisha pia Vijana wao dhidi ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na kuheshimu sheria za Tanzania.

KATIBU MKUU MKOMI,AWAHIMIZA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KUJITOKEZA KUPIGA KURA OKTOBA 29

10/10/2025 12:55:00 pm
Na mwandishi wetu

Katibu Mkuu Ofsi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi, amewahamasisha watumishi wa umma kote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza katika kikao cha tatu cha Baraza la Nane la Wafanyakazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili, Mkomi alisema licha ya kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, ana mapenzi na ustawi wa taifa, hivyo ni muhimu kwa kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura, hasa watumishi wa umma, kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kidemokrasia.

"Nawaomba wenzangu watumishi wa umma tujitokeze kwa wingi siku ya Oktoba 29 kwenda kupiga kura huu ni wajibu wetu wa kikatiba na njia ya kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya nchi yetu," alisema Mkomi.

Aidha, alibainisha kuwa hata viongozi wa kisiasa wamekuwa wakihamasisha familia zao kujitokeza kupiga kura, hivyo ni vyema pia kwa wafanyakazi wa umma kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwa amani na utulivu.

 "Niwaombe wajumbe wa baraza hili na watumishi wote, tusiwe nyuma. Tuwe mfano wa kuigwa katika kujenga demokrasia kwa kushiriki uchaguzi," alisisitiza.

Kauli hiyo imekuja wakati nchi ikijiandaa kwa uchaguzi ambao unatarajiwa kushirikisha wananchi katika kuchagua viongozi watakaowakilisha maeneo yao, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya maendeleo.

Mwisho.

WAZEE MKOANI DODOMA WAAHIDI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA, WAOMBA KUPEWA KIPAUMBELE KWENYE FOLENI.

10/10/2025 12:55:00 pm
Na Mwandishi wetu Dodoma

Wazee wa Mkoa wa Dodoma waaswa kuhamasisha jamii kujitokeza Oktoba 29,2025 kupiga kura pamoja na kuhakikisha wanasimamia vijana na kuwasihi kulinda amani ya nchi yetu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati akizungumza na Wazee hao leo  juu ya umuhimu wao wa kuhamasisha jamii kujitokeza kupiga kura.

Aidha amesema kuwa ni jukumu la Kila mwananchi kuchagua viongozi wenye tija na maendeleo hivyo amewasihi wazee kuwa mstari wa mbele kwenye suala la uchaguzi kwani maendeleo yaliyofanywa na Serikali yanaonekana dhahiri.
Aidha amesema Dodoma ya miaka 10 iliyopita si sawa na Dodoma ya sasa kwani hata hadhi ya viwanja imeongezeka na kila mtu amekuwa akivutiwa na Dodoma hivyo anaipongeza Serikali kwa kufanya Dodoma kuwa ya kuvutia.

"Dodoma ya sasa si kama ya zamani Dodoma sasa inavutia na ni kimbilio la watanzania na wageni wa kimataifa kuwekeza Dodoma na hii ni kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Serikali"Amesema Senyamule 

Sanjari na hayo amesema kuwa Serikali imeamua kutoa Elimu juu ya magomjwa yasiyoambukizwa ili waweze kuhakikisha wazee wanakuwa imara kwenye Afya Kwa kufanya mazoezi na Kuzingatia mlo mzuri kulingana na umri wao.

"Kupitia nyie tutaweza kujua changamoto mlizonazo na kuweza kuhakikisha tunazitatua kwani wazee ni tunu ya taifa hili"Ameongeza Senyamule

Wazee hao nao walipata nafasi ya kuelezea changamoto zao Kwa Mkuu wa Mkoa wanazokumbana nazo kwenye huduma za Kijamii ikiwemo hospitali ambapo Mzee Bakari Chaurembo ameiomba Serikali kuwaangalia Kwa jicho la 3 Kwa kuhakikisha wanapatiwa Bima ya Afya ili waweze kupata huduma kwa urahisi na wakati kipindi wanapokwenda kwenye vituo vya Afya.

Akijibu hoja za wazee hao Mkuu wa Mkoa amesema atahakikisha anashughulikia changamoto zote ikiwemo huduma mbovu Kwa wazee kwenye vituo vya Afya,pamoja na kuboresha miundombinu  kama barabara ili kuweza kukidhi matakwa ya Wazee hao.

"Kwenye ishu ya Wazee kutopanga foleni siku ya kupiga kura tutaliwasilisha Kwa TUME ya uchaguzi ili muweze kutengenezewa utaratibu mzuri"Amesisitiza Senyamule

VIONGOZI WA DINI NA WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA MABALOZI WA AMANI

10/10/2025 10:01:00 am
Na mwandishi wetu

Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali nchini pamoja na waandishi wa habari, wametakiwa kutumia nafasi zao kwenye jamii kuhimiza amani na umoja wa kitaifa, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu, ili kuepusha mifarakano na migawanyiko miongoni mwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa Mkoani Iringa leo Alhamisi Oktoba 09, 2025 wakati wa warsha ya siku moja iliyoratibiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikisha waandishi wa habari na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali Mkoani humo.
Mwezeshaji wa semina hiyo, Uzima Justine, amesema huu ni wakati sahihi kwa viongozi wa dini kutoa ujumbe unaowaunganisha Watanzania, badala ya maneno yanayoweza kuchochea chuki au migawanyiko.

“Chochote kisichounganisha watu na kuleta amani si cha kweli,” alisema Uzima, akisisitiza kwamba wajibu wa viongozi wa dini ni kujenga maridhiano na upendo wakati wote, hasa katika kipindi cha uchaguzi.

Kwa upande wake, Mratibu wa warsha hiyo, Omary Ibrahim, ambaye ni Afisa Miradi wa BAKWATA Makao Makuu, alisema warsha hiyo imelenga kuwaongezea uelewa washiriki kuhusu nafasi yao muhimu katika kulinda amani kupitia maneno na matendo yao.

“Tupo Iringa na tumewakutanisha waandishi wa habari pamoja na viongozi wa dini — watu ambao wanaweza kujenga au kubomoa. Lengo letu ni kuwajengea uwezo ili wakatoe elimu sahihi kwa wananchi, wasitoke nje ya misingi ya ukweli,” alisema Omary.

Aliongeza kuwa wakati mwingine haki ya kukusanya, kuchakata na kusambaza habari haitumiki ipasavyo, jambo linaloweza kuleta mkanganyiko kwa jamii na kuhatarisha amani ya nchi.

Katika warsha hiyo wito umetolewa kwa taasisi za dini na vyombo vya habari kushirikiana kwa karibu zaidi katika kutoa elimu ya uraia, kueleza kwa uwazi umuhimu wa amani, na kupinga taarifa au mafundisho yanayoweza kugawa jamii.

Thursday, 9 October 2025

VIONGOZI WA DINI WASISITIZA UMUHIMU WA AMANI KWA MAENDELEO YA TANZANIA

10/09/2025 01:38:00 pm
Dodoma

Kuelekea kwenye Zoezi la uchaguzi Mkuu wa Tanzania Jumatano ya Oktoba 29, 2025, Viongozi wa dini, kijamii pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dodoma wameungana pamoja kuhimiza amani, wakiitaja kama rasilimali muhimu kwa maendeleo ya Kijamii, kiuchumi, Viongozi wa dini wakisema amani ndiyo Neema muhimu zaidi kwenye nchi yoyote duniani.

Mchungaji Pendo Yohana kutoka Kijiji cha Michese, Askofu Antony Saimon, Mwenyekiti wa Umoja wa madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma pamoja na Sheikh Ahmed Said Ahmed, Msemaji wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, ni miongoni mwa Viongozi wa dini wanaohamasisha kuhusu amani, wakisisitiza kila Mtanzania kuwa Mlinzi wa amani na kujiepusha na matendo yote yenye kuhatarisha amani iliyopo.

Kulingana na tafiti mbalimbali zinaonesha uwepo wa uhusiano kati ya amani na maendeleo katika ujenzi wa Taifa bora na lenye uchumi imara pamoja na kuruhusu kupatikana kwa mahitaji muhimu ya binadamu na huduma stahiki ikiwemo elimu bora, afua bora na ulinzi na usalama kwa wote.

Aidha kwa Upande wake Emmanuel Kamome, dereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma pamoja na Shukuru Chimwaga, Msemaji wa Chama cha waigizaji Mkoa wa Dodoma wametoa wito pia wa kulinda amani iliyopo nchini, wakiahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha ulinzi wa amani hasa wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Wananchi hao wa Dodoma wameungana na Viongozi na wagombea mbalimbali wa nafasi za Urais wa Tanzania akiwemo Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pamoja na wengine wamekuwa wakitahadharisha Vijana na Jamii kutokubali kutumika na wasioitakia mema Tanzania na kuweza kuvuruga na kuhatarisha amani ya Tanzania kwa kisingizio cha uchaguzi Mkuu, wakisisitiza kuwa uchaguzi ni tendo la kidemokrasia na sio sababu ya machafuko na vurugu kwenye Jamii.

Maandamano yana athari kubwa ikiwemo vifo kwa watoto, wazee na wanawake tusikubali maandamano.

10/09/2025 01:37:00 pm
Na mwandishi wetu

Wananchi na wapigakura wa Tanzania wamesisitizwa kupuuza na kutokubali kuhadaika na watu na baadhi ya wanasiasa wanaohamasisha vurugu na maandamano Jumatano ya Oktoba 29, 2025 siku ya upigaji wa kura kwenye uchaguzi Mkuu wa Tanzania.


Wananchi tuliozungumza nao akiwemo Shaban Maulid na Adrian Malikale wamewasihi wananchi kujifunza na kutathmini athari za vurugu na machafuko kwa jamii hasa kwa watoto, wanawake na wazee, wakiahidi kutoandamana na kusisitiza kufuatwa kwa taratibu na sheria zinazotambulika kisheria wakati wa zoezi la upigaji kura.

"Ni muhimu sana kutokubali kushawishiwa au kudanganyika kwenda kuandamana kwa namna yoyote ile ifikapo Oktoba 29, 2025. Tujitokeze tupige kura, turudi nyumbani kuendelea na shughuli zetu kama mimi mama lishe nitakavyofanya. " amesema Bi. Zuhura Mohamed.

Tayari serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewahakikishia watanzania wote utulivu, amani na usalama siku hiyo ya upigaji wa kura, wakihimiza kila mmoja kujitoke kwa wingi kumchagua Kiongozi wamtakaye bila ya hofu yoyote na kubainisha kuwa wamejipanga kuhakikisha kila mmoja anaitumia haki yake ya kikatiba bila bugudha, usumbufu na hofu ya vurugu.

Wednesday, 8 October 2025

Watanzania waeleza umuhimu wa kutii sheria na Miongozo ya uchaguzi," ifikapo Oktoba 29, 2025 tupige kura na kurejea majumbani"

10/08/2025 11:03:00 am
Na mwandishi wetu. 

Wananchi wenye haki ya kupigakura katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ili kuchagua Viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo na kutimiza wajibu wao wa Kikatiba na kidemokrasia.

Wananchi hao pia akiwemo Mwanahuba Jumbe Ramadhani wamesisitiza umuhimu wa kutii sheria na Miongozo ya uchaguzi, akisema ifikapo Oktoba 29, 2025 mara baada ya zoezi la kupiga kura ni muhimu kila mmoja akarejea nyumbani na kuendelea na shughuli zake badala ya kutii wito unaotolewa na baadhi ya wanasiasa wa kulinda kura kwenye Vituo, kazi ambayo ni ya mawakala wa vyama vya siasa na tume huru ya Taifa ya uchaguzi.

Richard Alphonce na Bw. Abdallah Ismail Haruna, wakazi wa Dar Es Salaam wakisisitiza kuwa kura ni haki ya kimsingi, wamebainisha kuwa mabalozi wazuri wa uchaguzi kwa kuhamasisha Vijana wenzao kupiga kura na kujitokeza kwa wingi kwani kura ndio njia pekee ya kidemokrasia ya kuweza kumchagua Kiongozi sahihi pamoja na kuwawajibisha wale walioko madarakani na walioshindwa kutimiza ahadi na matarajio ya wananchi.

POLEPOLE ATAKIWA KUJISALIMISHA OFSI YA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI.

10/08/2025 11:03:00 am
Na mwandishi wetu

Jeshi la Polisi nchini Tanzania kupitia kwa Msemaji wake DCP David Misime limesisitiza kuwa bado linaendelea kumsubiri Ndugu Humphrey Polepole ili aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai ili atoe maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia Mitandao yake ya Kijamii.

Ikumbukwe kuwa Jumatatu Septemba 15, 2025 Jeshi la Polisi lilisema kuwa limefungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi CCM.
 "Tuhuma ambazo ametoa na anaendelea kuzitoa kulingana na jinsi alivyozielezea zinaashiria uwepo wa makosa ya kijinai na kwa mujibu wa sheria zinahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapo wasilishwa mahakamani. 

Tuhuma hizo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii, baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo au ushahidi na vielelezo vitakavyo thibitisha tuhuma hizo ili kuwezesha hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na ndivyo utaratibu wa kisheria ulivyo" Taarifa hiyo ya Polisi ilieleza.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limeeleza kuona taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya kijamii na ndugu zake kuwa Mtu huyo ametekwa usiku wa kuamkia Oktoba 06, 2025 na kueleza kuwa tayari wameanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wa madai ya kutekwa kwake.

Mwisho.

Monday, 6 October 2025

Wananchi "Hatukubali kurubuniwa, kujiingiza kwenye maandamano Oktoba tunatiki"

10/06/2025 10:04:00 am
Na mwandishi wetu

Jamii imesisitizwa kujitokeza kwa Wingi Oktoba 29, 2025 na kupiga kura kuwachagua Viongozi wanaofaa na wanaoweza kuwaletea maendeleo ya kweli kama sehemu ya kutimiza Haki ya kila Mwananchi Kikatiba lakini pia katika kuamua hatma ya maisha ya Kila mmoja katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Wito huo umetolewa na Wananchi wa Tabata Jijini Dar Es Salaam leo Jumatatu Oktoba 06, 2025 wakati wakizungumza na Mwandishi wetu wa habari, wakisisitiza pia kila mmoja kufanya tafakuri na kutokubali kurubuniwa na kujiingiza kwenye maandamano yanayoratibiwa na kuhamasishwa na watu wasiokuwa nchini na wasioitakia mema Tanzania.

Ally Kazimoto ni mmoja wa waliozungumza nasi ambapo ametanabainisha kujiandaa vyema kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao na kuhamasisha Vijana wenzake kutorubuniwa kuandamana, akisema ni muhimu kabla ya kuandamana kujiuliza athari za maandamano hayo,akisisitiza kuwa haki haidaiwi kwa kuvunja sheria na miongozo iliyopo nchini.

Kwa upande wake Raskazia Mwita na Hamis Maneno, wamewasihi Vijana na Wanawake kutafakati hatma ya Watoto na familia zao kabla ya kuandamana hiyo Oktoba 29, wakieleza kuwa ni ubinafsi kuandamana bila kujali haki na usalama wa wengine kwani maandamano ya Oktoba ni batili na hayakubaliki kutokana na Serikali kuitenga siku hiyo kuwa maalumu kwaajili ya uchaguzi mkuu peke yake.

POLISI KUWASAKA WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUHAMASISHA NIA OVU NA UPOTOSHAJI

10/06/2025 10:03:00 am
Na Mwandishi wetu.

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewahakikishia watanzania wote kuwa litaendelea kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika Mamlaka nyingine za haki Jinai wale wote ambao kupitia Mitandao mbalimbali ya Kijamii wamekuwa na tabia ya kutengeneza, kuandika na kusambaza maandishi na picha mjongeo za kuhamasisha watu kufanya  vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa ni kinyume  na maadili na utamaduni wa Mtanzania ikiwa pia ni kinyume na sheria za nchi.


Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania DCP David Misiime imeeleza kuwa vitendo hivyo vinasukumwa na dhamira ovu ambapo pamoja na kwamba ni kinyume cha sheria za nchi, vimekuwa vikisababisha hofu na taharuki kwa wananchi wema walio wengi kuliko wao wenye nia Ovu bila ya kuwa na sababu zozote za msingi.

"Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia Watanzania kuwa linaendelea kuwasaka na kuwakamata na kuwafikisha katika Mamlaka nyingine za haki jinai kwa hatua za kisheria kama ambavyo limeshafanya kwa waliokwisha kamatwa." Imesema taarifa ya Jeshi la Polisi.

Polisi kupitia taarifa yake ya leo Jumapili Oktoba 05, 2025 kwa waandishi wa habari imetaarifu pia kwamba bado inaendelea na kushughulika na uhalifu huo na bado wengine hawajafikiwa na mkono wa sheria, wakiwataka kutojidanganya bali wakumbuke kuwa kinachosubiriwa sasa  ni muda sahihi na ukamilishaji wa taratibu za kuwafikia wakati wowote kuanzia sasa kulingana na ushahidi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Sunday, 5 October 2025

Kupiga kura ni heshima, wajibu na silaha ya Demokrasia

10/05/2025 03:19:00 pm
KUPIGA KURA NI HESHIMA, WAJIBU NA SILAHA YA KIDEMOKRASIA

Upo ushahidi madhubuti unaoonesha uwepo wa tija ya k upiga kura Katika uchaguzi Mkuu wa Tanzania licha ya uwepo wa mitazamo na kauli mbalimbali kuwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ni kupoteza muda tofauti na uhalisia ulivyo, uchaguzi ukitajwa kama heshima, wajibu na silaha ya Kidemokrasia kote duniani.

"Kupiga kura ni haki ya Kikatiba, inayomuwezesha kila Mtanzania kushiriki katika maamuzi ya nchi kwa njia ya amani, kupitia kura wananchi huamua ni nani awaongoze katika nafasi za kisiasa kama Rais, Wabunge na Madiwani na hii ni njia halali ya kushiriki katika ujenzi wa Taifa na kuhakikisha kuwa sauti ya mwananchi inasikika." Amesema Mchambuzi wa siasa Ally Said alipozungumza nasi.

Kulingana na Mchambuzi huyo, wananchi wanapojitokeza kwa wingi kupiga kura wana nafasi ya kuchagua Viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo, kupitia kura matatizo ya huduma duni za jamii yanaweza kushughulikiwa, Kura ikiimarisha pia misingi ya demokrasia na utawala bora kwa kuwafanya walioko madarakani kuwajibika kwa wananchi kwa kujua kuwa wanaweza kuondolewa kwa kura ikiwa hawatatimiza wajibu na ahadi zao.

John James, Mwananchi wa Goba Jijini Dar Es salaam anasema anafahamu kuhusu haki yake ya kupiga kura, akihimiza umuhimu wa kuwachagua wale wanaojua shida za wananchi na wenye kujali mahitaji ya wananchi. Akieleza kuwa mabadiliko ha kweli yanapatikana kupitia kura na si vurugu, matusi, jazba ama maandamano ya kutaka kushinikiza mambo isivyo halali.

Ushiriki wa uchaguzi unatoa nafasi kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika maamuzi yanayogusa maisha yao ya kila siku ambapo Viongozi wanaochaguljwa kwa ushirikishwaji wa wananchi wanakuwa na uwezo wa kutengeneza mipango ya maendeleo inayokidhi mahitaji halisi ya eneo husika, wito ukitolewa kwa kila mwananchi mwenye sifa kujitokeza kupiga kura kwa amani, kuheshimu sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuepuka kuvunja sheria kwa kuhamasisha wananchi kutokupiga kura ama kulinda kura kwenye Vituo vya upigaji kura.

DAR ES SALAAM WAELEZA UTAYARI WAO WA KUSHIRIKI KUPIGA KURA, WAYAKATAA MAANDAMANO

10/05/2025 03:01:00 pm
Na Mwandishi wetu. 

Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamesema wapo tayari kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakijitenga na ushawishi unaofanywa mtandaoni wa kuwataka kuandamana na kutojitokeza kupiga kura, wakieleza kufahamu vyema umuhimu wa amani na athari za vurugu na maandamano ikiwemo vifo, majeraha na kuporomoka kwa uchumi kutokana na kukosekana utulivu wa wao kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.


Pantaleo Mushi Mkazi wa Mbezi Beach amesema anafahamu jukumu lake la Kikatiba la kupiga kura, akihamasisha Vijana wengine kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya Kikatiba kupiga kura na kuchagua Kiongozi wamtakaye, akieleza kuwa athari za kutopiga kura ni kuruhusu kuchaguliwa kwa Kiongozi asiyemtaka na kumnyima fursa Kiongozi sahihi kuweza kushika Madaraka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika Ngazi ya Kata, Jimbo na kwenye Nafasi ya Urais.

Kwa upande wao Said Nassor na Yusuph Ibengwe, wakazi wa Kawe, wameeleza kutofahamu lolote kuhusu maandamano na kusisitiza wananchi kutokubali kurubuniwa katika kuharibu amani ya Tanzania kwa maslahi binafsi ya baadhi ya wanasiasa, wakihimiza wananchi kutumia haki yao vyema ya Kikatiba kuchagua Viongozi wanaowataka kwa njia ya amani hapo Oktoba 29. 2025 siku ya Upigaji kura na kutojihusisha na vurugu ama kusalia vituoni kulinda kura.

Kulingana na baadhi ya wachambuzi wa siasa, mabadiliko yanaanzia kwenye sanduku la kura na ikiwa hutopiga kura, mtu mwingine ataamua hatma yako. Kupiga kura sio haki tu bali ni jukumu lako kama raia kwani unapokaa kimya bila kupiga kura unapoteza haki yako na kuwapa wengine fursa ya kuamua kuhusu maisha yako, serikali yako na mustakabali wa nchi yako. Wanahimiza kutokubali kupoteza sauti yako wakiamini kuwa kura yako ina thamani katika kuitengeneza jamii unayoitaka kwasasa na kizazi kijacho.

JESHI LA JWTZ LATOA UFAFANUZI KUWA LITAENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKATIBA ,UANINIFU,UTII NA UHODARI KWA KUZINGATIA KIAPO CHAO"

10/05/2025 10:03:00 am
Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limesema kuwa limebaini uwepo wa baadhi ya watu wanaotumia mitandao mbalimbali ya Kijamii kuweka maudhui na ujumbe mbalimbali wenye kuchochea kuliingiza Jeshi hilo katika masuala ya siasa.
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na uhusiano kutoka kwenye Jeshi hilo Makao makuu Kanali Bernad Masala Mlunga amewaambia waandishi wa habari leo Jumamosi Oktiba 04, 2025 kuwa baadhi ya hoja hizo zinazochapishwa mitandaoni zinatolewa na watu walio katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi pamoja na watu walioachishwa Jeshi kwa kuwa na tabia na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na siasa na harakati mbalimbali.

Taarifa ya Kanali Mlunga imesisitiza kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ linaendelea kutekeleza majukumu yake Kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chao.

JWTZ wametoa taarifa hiyo siku moja mara baada ya mtu mmoja aliyejitambulisha kama Kapteni wa JWTZ John Charles Tesha, akisema yeye ni Mkufunzi wa zana za anga za kivita katika shule ya Anga (SAK) na akieleza kupitia mtandao wa Youtube kuhusu masuala mbalimbali ya siasa za Tanzania na uchaguzi Mkuu ujao, akitoa shutuma mbalimbali pia kwa baadhi ya Viongozi walioko madarakani na wastaafu, familia zao na watu wao wa karibu, tuhuma ambazo hazina uthibitisho.

Mwisho

NI SHANGWE WAKAZI WA DAR ES SALAAM,UJIO WA MAGARI MAPYA YA MWENDO KASI ,WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI.

10/05/2025 10:03:00 am
Na Mwandishi wetu ,Dar es Salaam

Siku Chache mara baada ya serikali Kuiongeza Kampuni ya Mofat Limited ili kutoa huduma ya usafiri kwenye mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT,  wananchi wa Jiji la Dar Es salaam wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa hatua za haraka zilizochukuliwa, wakisema kwasasa adha ya usafiri imeisha na hawalazimiki kukaa muda mrefu kwenye Vituo vya daladala pamoja na kupunguza muda wa kukaa Vituoni kwa muda mrefu.


Oktoba 02, 2025 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alitembelea mradi huo wa mabasi yaendayo haraka kwenye Vituo vya Kimara na Kivukoni, akiagiza mabasi 60 yaende kuongeza huduma ya usafiri katika eneo hilo na leo tumefika kwenye baadhi ya Vituo kujionea hali ilivyo baada ya ongezeko la mabasi hayo na kubaini uchache wa abiria kwenye Vituo hivyo tofauti na awali.

Miongoni mwa wananchi hao akiwemo Sikuzani Mohamed Muuzi na Mzee Festo Mbilinyi wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa ongezeko la mabasi hayo, wakisema kwasasa usafiri umekuwa rahisi kwao na hawatumii muda mrefu vituoni kama ilivyokuwa awali, wakilazimika kusubiri basi kwa zaidi ya saa moja.
Wengi wa abiria pia wamesisitiza kuanza kufikiria kuacha magari yao binafsi nyumbani na kuanza kutumia usafiri huo wa umma ambapo katika hatua nyingine abiria wengi pia wameonekana wakipanda mabasi mapya na kuacha yale ya zamani kwa madai tofauti ikiwemo kutaka magari hayo mapya kutokana na kuwa na kiyoyozi, madereva wakionekana kila wakati kuwataka abiria kufunga vioo ili kuruhusu viyoyozi hivyo kufanya kazi vyema.

Wednesday, 3 September 2025

KATIBU MKUU CHAMA CHA MADEREVA WA SERIKALI (CMST)NYABANGE ATUMA PONGEZI KWA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

9/03/2025 11:35:00 am
Doreen Aloyce ,Dodoma
 
 Katibu Mkuu wa Chama Cha. madereva wa Serikali (CMST,) Castro Nyabange amesema kuwa chama chicho kinampongeza kwa dhati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua mbalimbali za kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo madereva.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa  Mkutano wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST), uliofunguliwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa .

Nyambage amesema kuwa chama kinatambua mchango wa Serikali 
 Amesema chama hicho kimekuwa nguzo muhimu katika kuboresha huduma za udereva Serikalini na kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

“Upandishaji wa mishahara kwa watumishi umetugusa pia sisi madereva, awali sisi madereva wa Serikali tulikuwa na mishahara ya viwango vya chini sana, tunaahidi kufanya kazi bega kwa bega na Serikali kwa kuzingatia weledi katika utendaji.”
 


Aidha amesema chama kinajivunia kuanzishwa ofsi mbili Dodoma na Zanzibar licha ya changamoto zinazo wakabili ikiwemo ukosefu wa fedha za kuendesha shughuli zao pamoja na waajiri kutowa ruhusu madereva kuhudhuria vikao mbalimbali.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema madereva ni mhimili muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali na nidhamu na uadilifu ndio msingi wa heshima wa kada hiyo.



“Sisi Serikali tutahakikisha ustawi wa madereva unakuwa kipaumbele chetu, wao wakiishi vizuri maana yake ni kwamba watafanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.”
 
Waziri Ulega amesema lengo la mkutano huo ni kujadili changamoto na kubadilisha uzoefu na kuimarisha mshikamano.

Awali akifungua mkutano huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa madereva wa Serikali wanawajibu wa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu ikiwemo ukaguzi wa gari kabla na baada ya safari, kujaza na kutunza kikamilifu taarifa za safari na matengenezo.

Amewataka madereva na wasimamizi wahakikishe usalama wa vyombo vya usafiri, abiria, mizigo na nyaraka za Serikali pamoja na kutumia vifaa vya kisasa vya usalama, na kujiepusha na tabia zinazoweza kuhatarisha maisha, mali na siri za Serikali.

Pia, Waziri Mkuu amewahakikishia madereva hao kuwa Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili madereva ili kuendelea kuimarisha mazingira ya kazi na ustawi wa madereva wa Serikali kote nchini.
 


“Changamoto mlizowasilisha ni mwendelezo wa kazi kubwa iliyopo mbele yetu, na kwa ushirikiano kati ya Serikali, Waajiri na Chama cha Madereva, tutaendelea kusonga mbele kwa hatua madhubuti ili kuboresha kada hii muhimu kwa manufaa ya Taifa letu.”
 
Pia, Waziri Mkuu amewataka waajiri wahakikishe stahiki za madereva zinalipwa kwa wakati, mafunzo ya mara kwa mara yanafanyika, miundo ya ajira inatekelezwa ipasavyo na wanapewa kipaumbele katika motisha mbalimbali.



Mkutanao huo wenye kaulimbiu isemayo “Dereva wa Serikali, Epuka Ajali, Linda Gari Lako na Watumiaji Wengine wa Barabara na Oktoba Shiriki Uchaguzi Mkuu”.
 umehudhuriwa na madereva wa Serikali zaidi ya 2,500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Mwisho.

Thursday, 28 August 2025

MKURUGENZI WA ( INEC ) AONDOA FOMU ZA UTEUZI ZA WAGOMBEA KITI CHA RAIS KWENYE UBAO WA MATANGAZO AGOST 28, 2025

8/28/2025 07:23:00 pm
MWANDISHI WETU, DODOMA

 Tume Huru ya Taifa ya chaguzi(INEC)Imeondoa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika ubao wa matangazo wa Tume ikiwa zimepita saa 24 za kubandikwa fomu hizo ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria.

MKURUGENZI wa (INEC) 
Ramadhani Kailima ameondoa fomu hizo jijini Dodoma  Agosti 28 mwaka huu 2025 .

Kailima akiongozana na watumishi wa Tume ,ambapo Fomu hizo za wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilibandikwa ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Fomu hizo zilibandikwa na Tume Saa 10:00 jioni ya Agosti 27, 2025 ambayo ilikuwa ni siku ya uteuzi na kuondolewa leo Agosti 28, 2025 Saa 10: 00 jioni.



Wednesday, 27 August 2025

BALOZI DKT, ASHA ROSE MIGIRO APOKELEWA RASMI MAKAO MAKUU CCM,AAHIDI USHINDI KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA

8/27/2025 01:25:00 pm

Na Sebastian Mavyeo, Dodoma

 ‎Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Dkt.Asha Rose Migiro ameishukuru kamati kuu ya CCM Taifa kwa kumteua kuwa mrithi wa Dkt.Emanuel Nchimbi katika nafasi hiyo huku akiahidi  kutekeleza ilani ya chama hicho.

Dkt.Migiro ameyasema hayo leo Agosti 26,2025 wakati alipopokelewa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini hapa Dodoma na aliyekuwa katibu mkuu CCM Taifa Dkt.Emanuel Nchimbi ambaye kwa sasa atakuwa mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.2025.‎‎

Amesema kuteuliwa kwake kumetokana na ushirikiano mkubwa aliyopewa na wanachama wa CCM kipindi alipokuwa  kiongozi wa chama hicho katika   nyadhifa mbalimbali.


‎‎"Nishukuru kamati ya Halmashauri kuu ya CCM kwa kukubali mimi niwe mrithi wa Dkt.Nchimbi,Dkt.Nchimbi ana uzoefu mkubwa ndani ya CCM ameingia akiwa mdogo hadi sasa, hivyo naamini uwezo wake ni mkubwa ndani ya chama.‎‎

"Wanachama wa CCM ndio mtaji na raslimali zetu,kwa upande wangu kuwa katibu mkuu wa CCM ni kutokana na nyie kunipa ushirikiano katika kazi mbalimbali nilizozifanya ndani ya chama hiki hivyo tutahakikisha wagombea wetu wote wanapata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu,"amesema Dkt.Migiro.

‎‎Awali aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Taifa Dkt.Emanuel Nchimbi amemshukuru mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa katibu mkuu wa chama hicho kwa kipindi chote alichoongoza . 

huku akiwashukuru wanachama wa CCM kwa ushirikiano waliyompatia kipindi cha uongozi wake.‎‎"kwanza wana CCM  wa Dodoma ni wakarimu sana na watakuonesha ushirikiano,tunaipongeza halmashauri kuu ya CCM kwa kukuteua wewe ,tunavishukuru vikao vya CCM kwa kuona uzito wa nafasi hii na kumteua mtu anayesitahili pia nimshukuru mwenyekiti wa CCM  kwa nafasi aliyonipa kipindi chote pamoja na wana ccm kwa ushirikiano mlionionesha,"amesema Dkt.Nchimbi.‎

Mwish

Saturday, 23 August 2025

RC. MKOA WA ARUSHA KENAN KIHONGOS ACHUKUA KITI CHA AMOS MAKALLA .

8/23/2025 10:20:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Kenan Kihongos ametangazwa rasmi kuwa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo chama cha mapinduzi (CCM).

Akizungumza na vyombo vya Habari makao makuu ya chama cha mapinduzi CCM mara baada ya kutangaza majina ya wagombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM, Aliyekuwa katibu wa Itikadi,uenezi na mafunzo Ccm Amos Makala amesema kuwa kuanzia sasa Mh.Kenan Kihongos anachukua nafasi hiyo.



MH.AESHI HILALY ATANGAZWA RASMI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SUMBAWANGA MJINI

8/23/2025 09:32:00 pm




Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly ametangwa rasmi kugombea Ubunge akitetea nafasi yake . 

Mh.Aeshi amekuwa kiongozi bora katika kutetea maslah ya wananchi na Taifa kwa ujumla. 

Aeshi amekiwa hodari kuchangia  hoja mbalimbali Bungeni za kuleta maendeleo ndani ya Jimbo lake. 


Adbox