Doreen Aloyce,Dodoma
CHAMA cha MapinduI CCM kimetangaza uteuzi wa awali wa Majina ya Wanachama watakaoshiriki katia zoezi la kura za maoni kwa nafasi za Ubunge na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi nchini kwenye jumla ya Majimbo 272 ya Tanzania Bara huku Zanzibar majimbo ya uwakilishi ni 50.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Katibu wa Itikadi,uenezi na Mafunzo wa Chama hicho,CPA Amos Makalla wakati akitangaza Majina hayo ambapo amesema idadi ya Wagombea kwa Mwaka huu imevunja rekodi kwani nafasi ya wagombea Ubunge katika majimbo ni zaidi ya 5000 na Madiwamani ni zaidi ya elfu30.
CPA Makalla amebainisha kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,katika kikao chake kilichofanyika Jula28 Mwaka 2025 Jijini Dodoma pamoja na mambo mengine imepitia na kujadili majina ya wanachama wake walio omba na kupendekezwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama hicho.
Katika hatua nyingine,CPA Makalla amewataka wale ambao majina yao hayajateuliwa kuwa watulivu kwani Chama bado kina nafasi nyingi.
Wagombea walikuwa wengi sana, kazi ya kuandaa orodha haikuwa nyepesi. Tulihakikisha tunamaliza kwa usahihi mkubwa, kwa kuzingatia maoni na mapendekezo ya vikao halali vya chama,” alisema Makalla.
shukrani kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaongoza na kuwawezesha wajumbe kushiriki vikao mbalimbali, ikiwemo vile vya kimtandao vilivyolenga kufanya marekebisho ya katiba ya chama na kutoa mwongozo wa mchakato wa uteuzi.
“Tunamshukuru sana Mwenyekiti wetu kwa kutuongoza kwa hekima na uthabiti. Pia tunaishukuru Kamati Kuu kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa uadilifu na mshikamano,” aliongeza
Katibu huyo wa NEC pia alisema kuwa idadi kubwa ya wagombea ni ishara kwamba CCM kinaendelea kukubalika miongoni mwa wananchi na kina wanachama wengi barani Afrika, hali inayodhihirisha uimara wake kisiasa.
Hata hivyo amewataka watanzania kuendelea kufatilia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuangalia majina ya wabunge ambayo yametangazwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment