Adbox

Tuesday, 29 July 2025

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WATAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

7/29/2025 12:30:00 pm

NA.MWANDISHI WETU - DODOMA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewaasa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.


Ameyasema hayo Tarehe 29 Julai, 2025 wakati akifungua Mkutano na Watumishi wa Ofisi hiyo ambapo alisema kuwa ni  muhimu kuwa na nidhamu ya kazi, kushirikiana na kuendelea kuwa wabunifu katika majukumu ya kila siku, na kuwakumbusha watumishi kuwa kazi wanazofanya zinagusa maisha ya mamilioni ya wananchi, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha anatoa huduma bora na kwa viwango vya juu. 


“Pia, nawasihi kuendelea kujenga mshikamano miongoni mwenu. Tunaposhirikiana, tunajenga nguvu ya pamoja ambayo hakuna changamoto inayoweza kutuzuia. Nawaomba tuendelee kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo mmoja. Kumbukeni kuwa, kila mchango wenu una thamani kubwa katika kufanikisha malengo ya Ofisi yetu na Taifa kwa ujumla.” Alifafanua Dkt. Yonazi.


Katibu Mkuu Yonazi aliendelea kusema kuwa, katika kuboresha Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Ofisi imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa kushughulikia changamoto zinazohusu mazingira ya kazi na maslahi ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na  kukuza ubunifu katika utendaji kazi wa kila siku na kuimarisha mifumo bora zaidi ya kufuatilia maendeleo ya kazi na kuhakikisha kila mfanyakazi anawajibika ipasavyo kwa nafasi yake.

Katika Mkutano huo watumishi wataweza kupata Elimu kutoka kwa wataalam wa  Mfuko wa Uwekezaji wa UTT kuhusu umuhimu wa kuwekeza, pamoja na mambo mengine pia watapewa elimu  itakayowakumbusha masuala mbalimbali yanayohusu uzingatiaji wa maadili ya utumishi wa umma, masuala ya Afya hususan homa ya ini na magonjwa yasiyoambukizwa.

Monday, 28 July 2025

CCM INATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE MUDA HUU,MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA LEO

7/28/2025 06:09:00 pm
Dodoma

Katibu wa Siasa, mafunzo na uenezi CPA Amos Makala anatarijia kutangaza majina ya wagombea Ubunge, udiwani pamoja na nafasi za uwakilishi wa viti maalum kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2025.

Tembelea DOREEN BLOG NA DOREEN TV mara kwa mara upate habari motomoto na uhakika.



DKT. TULIA AITAKA DUNIA KUKABILIANA NA VIKWAZO VINAVYOWAKWAMISHA WANAWAKE

7/28/2025 05:54:00 pm


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza majadiliano muhimu yaliyoandaliwa na UN Women kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, yaliyolenga kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana duniani.



Majadiliano haya yamefanyika  katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Mjadala umejikita katika kuainisha mikakati bora ya kutekeleza ahadi zilizowekwa katika Ajenda ya 2030, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama, pamoja na Azimio la Beijing.

Aidha, washiriki wamebainisha kuwa changamoto kama ukosefu wa elimu na mifumo dhaifu ya afya zinaweza kutatuliwa iwapo jamii zitajitahidi kulinda mafanikio yaliyopatikana, kwa kuimarisha mifumo ya kisheria, kisiasa na kifedha kwa ajili ya kuendeleza usawa wa kijinsia.



Katika mchango wake, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesisitiza umuhimu wa kuweka usawa wa kijinsia na utekelezaji wa Ajenda ya 2030 kuwa vipaumbele vya kimataifa, huku akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana katika kukabiliana na vikwazo vinavyokwamisha juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuwawezesha wanawake na wasichana. 

Amesisitiza kuwa “wakati wa kuchukua hatua ni sasa”, hasa wakati ambapo dunia inakabiliwa na changamoto nyingi zinazotishia maendeleo ya kijinsia.

Friday, 25 July 2025

RAIS DKT.SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA DODOMA

7/25/2025 04:13:00 pm
Na Doreen Aloyce, Dodoma


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameshiriki maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa waliopigania Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika Mji wa Serikali Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Dk.Samia ameongoza maadhimisho hayo kwakuweka Mkuki na ngao huku  Jenerali Jacob Mkunda akiweka Sime na shada la maua ambapo kiongozi wa Mabalozi ameweka Shada la maua kama ishara yakuwakumbuka mashujaa hao.


Awali kulitanguliwa na mizinga miwili ambayo ilipigwa na kufuatiwa na Wimbo wa Taifa.

Akizungumza kwaniaba ya mashujaa hao,Mwakilishi wa mashujaa waliopigana vita vya kagera Balozi  Brigedia Jenerali Francis Benard Mndolwa amesema anajivunia kuwa mmoja wa wapigania uhuru na kuwa mzalendo Kwa nchi yake na amewasihi wafanyakazi wote kuwa wazalendo.


Nao baadhi ya wananchi wameelezea kuhusiana na siku hiyo ya mashujaa.



Ikumbukwe kuwa siku ya Mashujaa huadhimishwa kila Mwaka mnamo Julai 25 kwa kuwakumbuka Mashujaa wote ambao walitoa maisha yao kwaajili ya kupigania uhuru kwa kulinda amani na heshima ya nchi.


MWISHO

Thursday, 24 July 2025

JAB Yakabidhi Press Card kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Michuzi Media Group

7/24/2025 05:57:00 pm
IMG-20250723-WA0078
IMG-20250723-WA0081
●Waandishi Wengine Watakiwa Kuhakiki Viambatisho Katika Mfumo


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amemkabidhi rasmi Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) Mkurugenzi Mtendaji wa Michuzi Media Group, Muhidin Issa Michuzi, kwa niaba ya waandishi wengine wanaoendelea kukamilisha taratibu za kupata vitambulisho hivyo.


Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu la Bodi hiyo katika kuhakikisha kuwa waandishi wote nchini wanakuwa na vitambulisho halali kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016.


IMG-20250723-WA0072
IMG-20250723-WA0079
Akizungumza baada ya kukabidhi kitambulisho hicho, Wakili Kipangula amempongeza Michuzi pamoja na waandishi wengine waliokwishapatiwa vitambulisho vyao kwa kufuata taratibu na kukidhi vigezo vinavyotakiwa kisheria.


Amesisitiza kuwa mchakato wa utoaji wa vitambulisho bado unaendelea na ametoa wito kwa waandishi ambao maombi yao hayajakamilika kuingia katika mfumo rasmi wa Bodi ili kuhakiki viambatisho walivyowasilisha.
IMG-20250723-WA0077
IMG-20250723-WA0073


“Kuna baadhi ya waombaji ambao viambatisho vyao havifunguki, havisomeki, vimerudiwa au havikidhi matakwa ya kisheria kama vile vyeti visivyotambulika au kukosekana kwa barua za utambulisho kutoka kwa waajiri,” amesema Wakili Kipangula.


Ametoa rai kwa waandishi kuhakikisha wanafuata maelekezo yanayotolewa kupitia mfumo kabla ya kuwasiliana moja kwa moja na Bodi kuhusu hali ya maombi yao.
IMG-20250723-WA0074
IMG-20250723-WA0075
JAB imekuwa ikitekeleza jukumu la kuthibitisha na kusimamia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanahabari wanatambulika rasmi na kuwa na vitambulisho halali vinavyotolewa kwa mujibu wa sheria.


Michuzi ameishukuru Bodi kwa mchakato huo na kuwataka waandishi wengine kuhakikisha wanazingatia taratibu ili kuimarisha tasnia ya habari kwa weledi na uwajibikaji.

RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA MASHUJAA KESHO JULAI 25 MWAKA HUU

7/24/2025 04:14:00 pm

Na Doreen Aloyce, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mashujaa yatakayofanyika 25 Julai, 2025 katika Viwanja vya Mnara wa Mashujaa vilivyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Akizungumza leo Julai 24 ,2025 Jijini Dodoma na waandishi wa habari jijini Dodoma kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (Mb), amesema maadhimisho hayo ni alama muhimu ya kuenzi mchango wa Watanzania waliojitolea kwa ajili ya uhuru, amani na maendeleo ya Taifa.



 “Siku ya Mashujaa ni siku ya kitaifa inayotukumbusha uzalendo wa mashujaa wetu  waliolinda mipaka ya Taifa, waliopambana kwa ajili ya uhuru na waliotoa sadaka kubwa kwa ajili ya amani tunayoifurahia leo,” amesema Dkt. Biteko.

Ameeleza Maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika, huku akisisitiza kuwa Julai 24, 2025 saa 6:00 usiku, Mwenge wa Kumbukumbu ya Mashujaa utawashwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule kwa niaba ya Rais, kuashiria kuanza kwa siku ya maombolezo ya mashujaa wa Taifa.



Amesema Maadhimisho ya Julai 25 yataanza saa 3:00 asubuhi kwa gwaride rasmi la heshima linaloongozwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Usiku wa siku hiyo, saa 6:00, Mwenge wa Kumbukumbu utazimwa rasmi kuashiria hitimisho la shughuli za maadhimisho kwa mwaka huu.

Mbali na hayo Dkt. Biteko ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika tukio hilo muhimu kwa historia ya Taifa, akieleza kuwa kila Mtanzania anao wajibu wa kutambua na kuenzi mchango wa mashujaa kwa vitendo vya uzalendo, mshikamano na kuchapa kazi kwa maendeleo ya nchi.



“Tunapoadhimisha siku hii, tunapaswa kujiuliza: Je, sisi kama kizazi cha sasa tunaendeleza misingi waliyoiacha mashujaa wetu? Ushujaa hauishii vitani pekee, bali uko katika kila tendo jema kwa Taifa letu,” amesisitiza.

Amevitaka vyombo vya habari, wanahabari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kushirikiana na Serikali katika kuelimisha umma kuhusu maana, historia na umuhimu wa Siku ya Mashujaa.

“Hii ni siku ya kumkumbuka Mtanzania mwenzetu aliyesimama kwa ajili ya wengine,tuwaambie watoto wetu maana ya ushujaa, thamani ya kujitolea, na umuhimu wa kupenda Taifa lao,” amesema Dkt. Biteko.

Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa hufanyika kila mwaka nchini kote kama njia ya kuenzi maisha, mchango na maono ya waliolinda uhuru wa Taifa, na mwaka huu 2025, Serikali imepanga kuyafanya kwa heshima, uzito na mshikamano wa hali ya juu.

=MWISHO=

Tuesday, 22 July 2025

NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha, Yajadili Fursa, Ufanisi wa Huduma Zake Kwa wateja.

7/22/2025 01:10:00 am


Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka kampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadili na wateja hao namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.

Katika kufanikisha hilo, jana benki hiyo kupitia timu yake ya Biashara na Uwekezaji (CIB) iliandaa hafla maalum ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini humo ikiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa benki hiyo Bw, Elvis Ndunguru sambamba na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo kutoka makao makuu na matawi yake ya jijini Arusha.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Bw Ndunguru alisema tukio hilo ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuendelea kuwa karibu zaidi na wateja wake kwa nia ya kutambulisha huduma zake mpya ikiwemo huduma ya NBC Connect mahususi kwa kundi hilo la wateja, kupata mrejesho wa huduma hizo kutoka kwa wateja hao sambamba na kutoa fursa kwa wateja kubadilishana fursa za biashara.

“Tukiwa kama muhimili muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na kukuza ushirikiano kati yetu na wateja wetu. Hii inasababishwa na mabadiliko yanayotokana na ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia tunayoyafanya kila siku’’

“Hivyo hatua hii ya kukutana na wateja wetu wakubwa inatoa fursa kwetu kuelezea maboresho makubwa tuliyofanya kwenye huduma zetu hivi karibuni sambamba na kutambulisha huduma mpya zilizorahisishwa zaidi kidigitali na zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu.’’ Alisema

Aidha, kupitia mpango huo benki hiyo imekuwa ikielezea mikakati yake mipana inayolenga kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wateja hao, kuwajengea mitandao ya kibiashara miongoni mwao sambamba na kuwasogezea huduma za kibenki karibu zaidi huku huduma ya NBC Connect ikitajwa kama suluhisho muhimu katika kuwasogezea huduma za kibenki wateja hao wakubwa yakiwemo mashirika na kampuni binafsi, pamoja na taasisi za serikali.

“Tunaamini kuwa msingi wa huduma za kipekee ni kuelewa mahitaji na matakwa ya wateja wetu, matukio kama haya yanatupatia mitazamo au maono yanayotusaidia kuwa wabunifu zaidi na kuboresha uzoefu wa kibenki kwa ujumla.” Aliongeza Bw Ndunguru.

Aidha, Bw Ndunguru alitaja baadhi ya mambo muhimu ambayo benki hiyo imekuwa ikiyazingatia katika kukuza ushirikiano na taasisi za kibiashara hapa nchini kuwa ni pamoja na utoaji wa suluhisho zenye ubunifu katika huduma za kifedha, Ubunifu wa kiteknolojia, Ubia wa kimkakati, Kukuza Ukuaji wa Uchumi pamoja na Uwajibikaji kwa jamii huku kipaumbeke kikiwekwa zaidi kwenye masula ya Elimu, Afya na uhifadhi wa mazingira.

“Hivyo basi NBC tunazialika jumuiya za wafanyabiashara kuangalia fursa na faida za kushirikiana na taasisi hii ya fedha ambayo ina dhamira ya dhati na mafanikio yao, kwa kukuza ushirikiano na kutoa zana zinazohitajika katika ukuaji. NBC inalenga kuwa mshirika mwaminifu anaayetegemewa katika biashara hapa nchini,’’ alibainisha.

Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoani Arusha walisema imekuja wakati muafaka hasa katika kipindi hiki ambacho mkoa huo upo kwenye mapinduzi makubwa ya kiuchumi kutokana ustawi mkubwa wa sekta ya utalii ikiwa ni matunda ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mkakati wake wa Royal Tour.

“Kwa sasa mkoa wa Arusha tupo kwenye kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi yanayochagizwa na ukuaji wa sekta ya utalii, biashara, kilimo na viwanda. Ni habari njema kwetu kuona kwamba benki ya NBC ambayo inatuhudumia wadau wengi kwenye sekta hizi inatuunga mkono kupitia huduma zao za kisasa ikiwemo zile za kidigitali ambazo kiukweli zimekuwa msaada mkubwa hususani kwenye huduma za miamala ya kifedha na makusanyo ya serikali,’’ alisema Bw Abdallah Kiwango kutoka Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).


Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.


Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (kulia) akibadilishana Mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.





Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (katikati aliesimama) akisalimiana na baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.






Baadhi ya wateja wa benki ya NBC jijini Arusha wakifuatilia hafla hiyo







Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (kulia) sambamba na maofisa wengie wa benki hiyo wakizungumza na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.

Sunday, 20 July 2025

CPA AMOS MAKALA AWATAKA WATIA NIA KUWA WAPOLE TAREHE YASOGEZWA MBELE.

7/20/2025 10:41:00 am



Doreen Aloyce, Dodoma

WALIOTANGAZA nia ya kugombea nafasi ya ubunge na udiwani wametakiwa kuwa wapole kwani mchakato rasmi wa kuwateua wagombea watakao ingia kwenye kura za maoni  tarehe 28 mwezi wa saba tofauti na ilivyokuwa tarehe 19 mwezi huu.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi bh Makala alipokuwa akizungumza na waandishih wa habari juu ya kuhairiahwa tarehe iliyokuwa imepangwa.

Makala amesema kuwa kuhahiriahwa kwa ratiba ya awali inatokana na wagombea wa ubunge na udiwani kuwa wengi hivyo chama kinatakiwa kuhakikiaha kinafanya uchambuzi makini ili kuwapata wagombea makini kwa kutuenda haki kwa kila mtu.

Ameeleza kuwa kabla ya  wa wagombea ubunge na udiwani tarehe 28 mwezi wa saba kitafanyika kikao cha kamati kuu tarehe 26 mwezi wa saba na kufuatiwa na kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya CCM ambacho nacho kitafanyika tarehe 26 mwezi wa saba mwaka huu.

Friday, 18 July 2025

WACHIMBAJI WA MADINI SINGIDA WATAKIWA KUWA MFANO WA UADILIFU NA UZALENDO KATIKA UCHIMBAJI

7/18/2025 01:10:00 pm


Na Mwandishi Wetu ,Singida


Serikali kupitia Tume ya Madini imewataka wachimbaji wa madini ya ujenzi, hususan mchanga, mkoani Singida kuhakikisha wanafanya shughuli zao kwa uadilifu, uaminifu na kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida, Eng. Sabai Nyansiri, amewakumbusha wachimbaji kuwa uchimbaji holela, kutorosha madini au kufanya kazi bila leseni ni kosa la jinai linalozorotesha mapato ya Serikali na maendeleo ya sekta.

“Lazima kila mchimbaji awe na leseni halali  ya madini na apate risiti stahiki wakati wa kufanya malipo. Hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kuwa michango yao inakwenda serikalini kwa maendeleo ya Taifa,” amesema Eng. Nyansiri.

Amefafanua kuwa leseni za uchimbaji wa mchanga hutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja, na wachimbaji wanapaswa kuzihuisha kwa wakati ili kuepuka kufutiwa au kumpisha muombaji mwingine.

Aidha, Eng. Nyansiri ameeleza kuwa Mkoa wa Singida una fursa nyingi za madini ya ujenzi na unaendelea kushuhudia ongezeko la shughuli za uchimbaji. 

Amesisitiza kuwa Serikali, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji kuhusu uchimbaji salama, endelevu na wenye tija.

_“Tunaendelea kuboresha miundombinu na mazingira rafiki kwa wachimbaji. Vilevile tunakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya Singida kuja kuwekeza katika madini ya kokoto, mawe na mchanga,”_ ameongeza.

Kwa upande wake, Mjiolojia Geofrey Mutagwa kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, amehimiza wachimbaji hao kujiunga kwenye vikundi au vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na fursa za mikopo na huduma mbalimbali za Serikali.

Katika maoni yao, baadhi ya wachimbaji  wa madini waliopatiwa elimu wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ya Serikali. Yusuph Irunde, mchimbaji kutoka mtaa wa Mungumaji, kata ya Kisasida, amesema elimu hiyo imewapa mwanga mkubwa na kuwajengea uwezo wa kuendesha shughuli zao kwa weledi.

_“Tunamshukuru sana Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Eng. Nyansiri na Serikali kwa kutufikia moja kwa moja. Elimu hii inatuwezesha kuwa wachimbaji bora na wa kisasa’’,_ amesema Irunde kwa furaha.


Saturday, 12 July 2025

RC TABORA CHACHA ABAINISHA MAFANIKIO YA MKOA IPO BIl. 34.9 HUDUMA ZA AFYA

7/12/2025 06:57:00 pm

 Dodoma


Mkoa wa Tabora   umepokea jumla ya Shilingi Bilioni 34.9 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za Afya za Afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete ikiwemonujenzi wa wodi ya wazazi ya ghorofa mbili itakayo kuwa  mkombozi kwa olkm waishio mijini na Vijini na kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.h bg


Akizungumza na Vyombo vya Habari Jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Paul Chacha juu ya mafanikio ya miaka minne ya  Serikali ya awamu ya sita amesema  Mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo afya  ambapo fedha imetumika  kuimarika kwa miundombinu ya kutolea huduma za Afya, kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za Afya karibu na wananchi. 









Aidha ameongeza kuwa Mkoa wa Tabora katika Sekta ya maji inabaki historia kwani vijiji vyenye huduma za maji safi vimeongezeka hadi kufikia  505 mwaka 2025.

....CUE IN Paul Chacha Rc Tabora.

 Mkoa  wa Tabora umeendelea kuhimiza umuhimu wa kutekeleza miradi ya kimkakati kwa lengo la kuongeza mapato na kuwezesha utoaji wa 

RC WA MANYARA SENDIGA AZINDUA ZOEZI LA USAMBAZAJI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA BEI YA RUZUKU

7/12/2025 06:37:00 pm

Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, amezindua zoezi la ugawaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.


Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Katesh, wilaya ya Hanang, ambapo jumla ya mitungi 3,000 iliyokamilika na vifaa vyake imetolewa kwa wananchi kwa bei nafuu ya ruzuku ya shilingi 17,500 (elfu kumi na saba na mia tano) kwa kila mtungi. Aidha, imeelezwa  kwa mkoa mzima wa Manyara jumla mitungi 16,275 itasambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.


Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu.


Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote mkoani Manyara kusimamia kwa makini zoezi hili, ili kuhakikisha mitungi hiyo inauzwa kwa bei iliyokubaliwa na kuepuka udanganyifu wa baadhi ya Mawakala/wafanyabiashara wasio waaminifu.


“Natoa rai kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha utaratibu unazingatiwa, na mitungi hii inawafikia walengwa kwa bei ya shilingi 17,500 kama ilivyopangwa. Hatutavumilia wafanyabiashara watakaojaribu kulangua na kuuza kwa bei ya juu ili kujipatia faida isiyo halali,” amesema Sendiga kwa msisitizo.


Mheshimiwa Sendiga ameeleza kuwa kampeni hii ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inahoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan za kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa, na pia kulinda afya ya wananchi dhidi ya moshi unaosababisha magonjwa ya njia ya hewa.


Mpango huu wa ruzuku unatarajiwa kupunguza mzigo wa gharama ya awali kwa wananchi ya kununua majiko ya gesi na hivyo kuwa chachu ya mabadiliko kuelekea upishi salama na rafiki kwa mazingira.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, leo Julai 11. 2025 amezindua zoezi la ugawaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.


Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Katesh, wilaya ya Hanang, ambapo jumla ya mitungi 3,000 iliyokamilika na vifaa vyake imetolewa kwa wananchi kwa bei nafuu ya ruzuku ya shilingi 17,500 (elfu kumi na saba na mia tano) kwa kila mtungi. Aidha, imeelezwa  kwa mkoa mzima wa Manyara jumla mitungi 16,275 itasambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.





Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu.


Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote mkoani Manyara kusimamia kwa makini zoezi hili, ili kuhakikisha mitungi hiyo inauzwa kwa bei iliyokubaliwa na kuepuka udanganyifu wa baadhi ya Mawakala/wafanyabiashara wasio waaminifu.


“Natoa rai kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha utaratibu unazingatiwa, na mitungi hii inawafikia walengwa kwa bei ya shilingi 17,500 kama ilivyopangwa. Hatutavumilia wafanyabiashara watakaojaribu kulangua na kuuza kwa bei ya juu ili kujipatia faida isiyo halali,” amesema Sendiga kwa msisitizo.


Mheshimiwa Sendiga ameeleza kuwa kampeni hii ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inahoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan za kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa, na pia kulinda afya ya wananchi dhidi ya moshi unaosababisha magonjwa ya njia ya hewa.


Mpango huu wa ruzuku unatarajiwa kupunguza mzigo wa gharama ya awali kwa wananchi ya kununua majiko ya gesi na hivyo kuwa chachu ya mabadiliko kuelekea upishi salama na rafiki kwa mazingira.

Adbox