Adbox

Wednesday, 12 November 2014

Mkutano wa TCRA na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wafanyika jijini Dar

11/12/2014 11:11:00 am

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Prof. John Nkoma akitoa hotuba yake wakati wa ufungumzi wa Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.Picha na Othman Michuzi.
Inginia Andrew Kisaka akitoa Mada katika  Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali katika wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini.
Sehemu ya Maafisa wa TCRA wakiwa kwenye Mkutano huo.
Moja ya Mada zinazoendeleo kutolewa katika Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Assah Mwambene akitoa hotuba yake wakati  akifunga Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania uliokuwa na lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,unaoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wanablog waliohudhulia Mkutano huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Mabel Masasi akizungumza katika Mkutano huo.
Baadhi ya Wanalibeneke wakiendelea kuuliza maswali mbali mbali katika mkutano huo.
Mdau Josephat Lukaza na Dada Shamim Mwasha wakiwa mkutanoni hapo.
Prof. John Nkoma akijibu maswali ya wanablog.

Mdau Fred Njeje akidaka taswira.

Mkutano ukiendelea.
Mdau Henry Mdimu akitoa hoja.
Mdau akitafakari kabla ya kuuliza swali.
Wanablog kazini.


Tuesday, 14 October 2014

TOKOMEZA UJANGILI ,OKOA UTALII WETU WAFANYIKA JIJINI ARUSHA

10/14/2014 05:57:00 pm
 Mhe. Allan Kijazi akipokea mfano wa Tembo katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.




 Waziri Nyalandu akijadili jambo na muandaaji katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.
 Nakaaya Sumari katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.
 Mrisho Mpoto Akijinyoosha .....
 Mrisho Mpoto katikati ya wadau wa TOKOMEZA UJANGILI , OKOA UTALII
 Peter Msechu
 Peter Msechu akitoa Burudani katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.

 Mrisho Mpoto katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.
 Peter Msechu katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.
 Wadau wa Utalii wakipata picha na Peter Msechu katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.
 Mdau wa utalii akipata picha na Mrisho Mpoto katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.

 Walter Emmanuel wa Nothern Shots katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo.
Sirili Akko akiongea jambo katika maadhimisho ya TOKOMEZA UJANGILI WA TEMBO ,OKOA UTALII WETU Uliofanyika kwa matembezi na kuhitimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid , Jijini Arusha Leo. Picha Zote Na Gadiola Emanuel na Walter Emanuel wa Northern Shots 

Wednesday, 10 September 2014

KIVUKO CHA MV. KIGAMBONI KUANZA KAZI KESHO KUTWA

9/10/2014 04:04:00 pm


Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watendaji mbalimbali hawapo pichani kutoka, Wizara ya Ujenzi, TEMESA na Kikosi cha Maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamefanya kazi kubwa ya ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ngazi kwenda kukagua Kivuko cha MV Kigamboni ambacho matengenezo yake makubwa yanakamilika leo.
Luteni Kanali Gwanafi kulia akimuongoza Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwenda kukagua Kivuko cha MV Kigamboni sehemu ya chini mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.
Luteni Kanali Gwanafi wapili kutoka kulia akitoa maelezo kuhusu ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Kigamboni kama inavyoonekana.
Taswira-Kivuko cha MV Kigamboni kinavyoonekana mara baada ya Ukarabati wake.
Luteni Kanali Gwanafi kulia akimuonesha Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli sehemu ya juu ya Kivuko cha MV Kigamboni.
Luteni Kanali Gwanafi kushoto akimuonyesha Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu sehemu ya chini ilivyokarabatiwa.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha MV Kigamboni huku akipatiwa maelezo kuhusu ukarabati wake.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Luteni Kanali Gwanafi kuhusu mambo mbalimbali wanayofanya ndani ya kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni mara baada ya ukaguzi wake. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Kivuko cha MV Kigamboni kinatarajiwa kuanza safari zake za usafirishaji rasmi kesho kutwa mara baada ya ukarabati wake kukamilika.

Waziri wa Magufuli alitoa kauli hio leo wakati akikagua kivuko hicho ambacho kilikuwa kikikarabatiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia kikosi cha Wanamaji.

Mheshimiwa Magufuli aliongeza kuwa hicho ambacho kinategemewa na wananchi wengi waishio Kigamboni na maeneo jirani kinategemewa kuteremshwa majini kesho jioni mara baada ya maji kujaa na kesho kutwa kuanza rasmi shughuli zake za usafirishaji.

“Nimekagua na kujionea kazi inavyoendelea na nimeridhishwa na mlipofikia mpaka sasa, naamini kazi imefanyika ipasavyo, hivyo basi palipobaki ni matengenezo madogo, kutokana na utendaji wenu wa kazi naamini kesho Kivuko hicho kitateremshwa majini na kesho kutwa kuanza safari”, Alisema Waziri Magufuli.

Aidha, Mheshimiwa Magufuli alikipongeza kikosi hicho cha Navy kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa wanamaliza ukarabati huo kwa wakati licha ya changamoto nyingi walizokumbana nazo.

Sambamba na hilo, Waziri Magufuli amesema kuwa ndani ya Wiki tatu au nne Boti ya Kutoka Dar hadi Bagamoyo itawasili kwani imeshateremshwa majini huko inapotengenezwa na kilichobaki ni kuifikisha Dar es Salaam

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, amepongeza Jeshi la Wananchi Tanzania kupitia Kikosi cha majini kwa uzalendo wao waliouonesha kwa kukamilisha ujenzi huo kwa gharama nafuu na kwa wakati ili kurejesha huduma za usafirishaji.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Marceline Magessa amesema kuwa ukarabati wa MV Kigamboni ulikuwa katika hatua za marekebisho mbalimbali ikiwemo utoaji kutu, kupaka rangi, usafi na uzibaji wa matundu pembezoni mwa kivuko hicho.

Naye kamanda wa kikosi cha majini Brigedia Jenerali Rogastian Laswai amezitaja changamoto zilizowakabili wakati wa utengenezaji wa kivuko hicho kuwa ni pamoja na kushindwa kupaka rangi kutokana na uwepo wa mvua pamoja na kupwa na kujaa kwa maji

Ukarabati wa Kivuko cha MV Agosti 14 mwaka huu mpaka kukamilika kwake hivi leo.

Friday, 29 August 2014

MMILIKI WA HOTEL YA SNOCREST ATAKIWA KULIPA ZAIDI YA BILIONI 3

8/29/2014 01:33:00 am

PICHA YA MUONEKANO WA HOTEL YA SNOW CREST

Mahakama kuu nchini kitengo cha biashara kanda ya Arusha imemuamuru mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa ndani ya hoteli hiyo.


Mbali na agizo hilo mahakama hiyo pia imeagiza washtakiwa wanne kati ya watano katika kesi hiyo  walipe  kiasi cha riba cha asilimia 4 ya fedha hizo  tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo na kiasi kingine cha asilimia 7 tangu kufungwa kwa shauri hilo hadi siku ya malipo.


Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Robert Makaramba mbele ya mahakama hiyo mara baada ya kueleza kuridhika na ushahidi uliowailishwa na upande wa mlalamikaji kupitia kwa wakili wake Melkizedek Lutema.


Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa nambari 9 ya mwaka 2012 Ndika alieleza kutapeliwa jumla ya $ 1.7 milioni  sawa na sh,3 bilioni baada ya kupatiwa hati mbili za eneo la hoteli hiyo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba eneo la hoteli hiyo lina hati tatu.


Katika hati ya madai mlalamikaji anadai kuwa hati moja kati ya tatu ilikuwa na mkopo wenye riba wa kiasi cha sh,1.5 bilioni kupitia benki mojawapo hapa nchini na baada ya kugundulika hilo ilikwamisha biashara ya mauziano ya hoteli hiyo.


Kwa mujibu wa nakala ya hukumu iliyosainiwa na Jaji Makaramba washtakiwa watano katika kesi hiyo mshtakiwa wa kwanza ,Wilfred Tarimo,Derick Tarimo,Doreen Tarimo ambaye ni mke wa mshtakiwa wa kwanza Irene Tarimo pamoja na kampuni ya Snowcrest And Wildlife Safaris Ltd  wameamriwa kumlipa Ndika fedha hizo pamoja na kiasi cha riba hadi tarehe ya kukazia hukumu.


Mbali na agizo hilo washtakiwa wote katika kesi hiyo pia waliamriwa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo  tangu ilipoanza kuunguruma huku wakipewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30  tangu hukumu hiyo ilipotolewa.


Akihojiwa jijini Arusha wakili wa upande wa mlalamikaji,Lutema alisema kuwa wao wameridhika na hukumu hiyo na kwa sasa wanajiandaa kuwasilisha gharama za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza kuunguruma mnamo Januari 5 mwaka 2012.

Adbox