Adbox

Friday, 30 January 2026

WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUTOANA JASHO JAN.31,2026 DODOMA

Na Doreen Aloyce,Dodoma


WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Bunge Azania Bonanza linalotarajiwa kuwakutanisha mashabiki wa Simba na Yanga Jumamosi Januari 31, 2026 Jijini Dodoma mbapo Bank ya Azania ndio Mdhamini mkuu katika Bonanza hilo.

Akizungumza na vyombo vya hanari Bungeni Dodoma Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Mhe. Festo Sanga,wakati akizungumzia maandalizi ya bonanza hilo  ambapo amesema Bonanza hilo ni maono ya Bunge, menejimenti na Spika kuhakikisha linakuwa kiungo cha kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali.

Amesema Bank ya Azania imekuwa ikionesha ushirikiano mkubwa Kwa Serikali Kwa miaka miaka mitatu mfululizo ambapo pia amepokea vifaa vya michezo huku akiipongeza Bank hiyo Kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha.

Mhe.Sanga amesema mashabiki wa Simba na Yanga wanatarajiwa kupimana nguvu katika bonanza hilo litakalowakutanisha wabunge, wafanyakazi wa Bunge, wizara pamoja na taasisi mbalimbali.


“Bonanza hili ni maono ya Bunge, menejimenti na Spika kuhakikisha linakuwa kiungo cha kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali, kwa kuwa Bunge ni chombo cha wananchi,” amesema Sanga.

Mhe.Sanga amesema bonanza hilo pia linalenga kudumisha umoja na mshikamano kati ya Bunge na taasisi mbalimbali, sambamba na kuunga mkono sekta ya michezo.

"Kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu tunaishukuru sana Azania Bank Kwa kuendelea Kutoa ushirikiano wao katika sekta ya Michezo". Amesema.

Amesema washiriki wote, wakiwemo wabunge na watumishi wa Bunge, wataanza matembezi ya pamoja kuanzia saa 12:00 asubuhi jirani na Chuo cha Mipango Dodoma kabla ya kuanza kwa michezo rasmi katika viwanja vya John Melini.

Hata hivyo amesema Bonanza hilo wanatarajiwa kujitolea kuchangia damu salama kwa hiari katika tukio hilo litakalofanyika Jumamosi, Januari 31, 2026, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin Miyuji jijini Dodoma.

No comments:

Adbox