Adbox

Friday, 30 January 2026

WAZIRI MAKONDA AWAPOKEA UMIKIDO KWA MIKONO MIWILI AHAIDI KUWAPA USHIRIKIANO

1/30/2026 01:14:00 pm
Na Mwandishi wetu,Dodoma

Katika kuendelea kuimarisha umoja na kujitambulisha kwa Mamlaka mbalimbali, Mwenyekiti wa Umoja wa Vyombo vya Habari Mitandaoni Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), Benny Majata, amefanya mazungumzo mafupi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Januari 29, 2026

Katika mazungumzo hayo, sambamba na kujitambulisha kwa Waziri Makonda, Majata amemweleza kuhusu malengo ya kuanzishwa kwa UMIKIDO, ikiwemo kusimamia maudhui yenye weledi, kuhamasisha maadili ya habari mtandaoni, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na Serikali.

Kwa upande wake, Waziri Makonda amesema milango ya Wizara ipo wazi kwa UMIKIDO kufika ofisini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kina juu ya namna Wizara itakavyoweza kusaidia umoja huo kutimiza malengo yake.

WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUTOANA JASHO JAN.31,2026 DODOMA

1/30/2026 12:49:00 pm
Na Doreen Aloyce,Dodoma


WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Bunge Azania Bonanza linalotarajiwa kuwakutanisha mashabiki wa Simba na Yanga Jumamosi Januari 31, 2026 Jijini Dodoma mbapo Bank ya Azania ndio Mdhamini mkuu katika Bonanza hilo.

Akizungumza na vyombo vya hanari Bungeni Dodoma Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Mhe. Festo Sanga,wakati akizungumzia maandalizi ya bonanza hilo  ambapo amesema Bonanza hilo ni maono ya Bunge, menejimenti na Spika kuhakikisha linakuwa kiungo cha kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali.

Amesema Bank ya Azania imekuwa ikionesha ushirikiano mkubwa Kwa Serikali Kwa miaka miaka mitatu mfululizo ambapo pia amepokea vifaa vya michezo huku akiipongeza Bank hiyo Kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha.

Mhe.Sanga amesema mashabiki wa Simba na Yanga wanatarajiwa kupimana nguvu katika bonanza hilo litakalowakutanisha wabunge, wafanyakazi wa Bunge, wizara pamoja na taasisi mbalimbali.


“Bonanza hili ni maono ya Bunge, menejimenti na Spika kuhakikisha linakuwa kiungo cha kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali, kwa kuwa Bunge ni chombo cha wananchi,” amesema Sanga.

Mhe.Sanga amesema bonanza hilo pia linalenga kudumisha umoja na mshikamano kati ya Bunge na taasisi mbalimbali, sambamba na kuunga mkono sekta ya michezo.

"Kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu tunaishukuru sana Azania Bank Kwa kuendelea Kutoa ushirikiano wao katika sekta ya Michezo". Amesema.

Amesema washiriki wote, wakiwemo wabunge na watumishi wa Bunge, wataanza matembezi ya pamoja kuanzia saa 12:00 asubuhi jirani na Chuo cha Mipango Dodoma kabla ya kuanza kwa michezo rasmi katika viwanja vya John Melini.

Hata hivyo amesema Bonanza hilo wanatarajiwa kujitolea kuchangia damu salama kwa hiari katika tukio hilo litakalofanyika Jumamosi, Januari 31, 2026, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin Miyuji jijini Dodoma.

Thursday, 29 January 2026

POLISI NJOMBE WAKANUSHA TAARIFA ZA ASKARI KUCHOMWA MOTO NA KUPORWA SILAHA

1/29/2026 09:29:00 am

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari limekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa katika Mitandao ya Kijamii nchini zikiambatana na picha mjongeo (Video), zikieleza uwepo wa Askari Polisi wa Mkoa huo aliyechomwa moto na kisha kuporwa silaha Mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Banga, Januari 28, 2026 amesema kuwa katika Mkoa wa Njombe hakuna tukio kama hilo, akionya dhidi ya wanaoandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji.

"Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali kuacha kwani ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na hakuna faida yoyote kwa wanaofanya hivyo pamoja na familia zao na kwa jamii kwa ujumla." Amesema Kamanda Banga.

Polisi pia imesema inaendelea kumfuatilia mtu ama watu waliochukua na kutumia picha mjongeo ya tukio la zamani ambalo askari walikwenda kutoa msaada kwa wananchi na kutengenezea taarifa hiyo ya uongo na kisha kuisambaza katika mitandao ya kijami

Aidha Kamanda Banga amesema Polisi wanaendelea kutekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na wananchi kupitia programu za Polisi Jamii ili kubaini na kuzuia uhalifu sambamba na kufanya doria, misako na operesheni katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha maisha na mali za wananchi zinakuwa salama wakati wote.

MWANACHAMA WA CHADEMA ARUSHA MATATANI KWA KUIBA 'FEDHA ZA LISSU'

1/29/2026 08:49:00 am

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetangaza kumkamata Bw. Fredrick Mbwambo, Mwanachama wa Chadema na Mkazi wa Arusha kwa tuhuma za wizi wa fedha ambazo alikuwa amezikusanya kutoka kwa wananchi waliokuwa wamechanga kwaajili ya Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Tundu Lissu kupitia Kampeni yao ya "Funga mwaka na Tundu Lissu".

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo leo Jumatano Januari 28, 2026 Jijini Arusha mbele ya wanahabari, amesema ukamataji wa mtuhumiwa huyo umefanyika baada ya Polisi kupokea malalamiko kutoka kwa Bw. Alute Mughwai, aliyeeleza kubaini wizi wa fedha zilizokuwa zimechangwa.

"Ufuatiliaji wa awali umeonesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za makampuni tofauti ya simu na inadaiwa zilihamishwa kwenye namba mbili za simu, moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ikiwa ni ya kampuni ya simu ya nchi jirani." Amesema Kamanda Masejo.

Aidha Polisi ya Arusha imesema kutokana na malalamiko hayo jalada lilifunguliwa kwa mujibu wa taratibu na uchunguzi kuanza sambamba na ukamataji huo na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wengine waliotuhumiwa kuhusika katika wizi huo pamoja na vielelezo unaendelea ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata.

Wednesday, 28 January 2026

UMIKIDO WAZIDI KUPAA ,WAJITAMBULISHA KWA WAZIRI KATAMBI

1/28/2026 07:43:00 pm

Mwenyekiti wa Umoja wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), Benny Majata, amefanya mazungumzo mafupi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, leo Januari 28, 2026 Majata alimweleza Waziri Katambi juu ya malengo ya UMIKIDO katika kusimamia maudhui yenye weledi, kuhamasisha maadili ya habari mtandaoni na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali.

Waziri Katambi amepongeza hatua ya umoja huo kujitambulisha, na ameuhimiza UMIKIDO kufika ofisini kwake ili kufanya mazungumzo ya kina kuhusu masuala ya kimaadili, matumizi salama ya mitandao, pamoja na namna vyombo vya habari mtandaoni vinavyoweza kushirikiana na serikali katika kulinda usalama na maslahi ya Taifa.

RAIS SAMIA ANAAHIDI NA KUTEKELEZA "NI MFANO SAHIHI KWETU WASICHANA"

1/28/2026 07:10:00 pm

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa na Wanawake na Mabinti wa Kitanzania kama Kiongozi wa mfano na mwanamke mwenye athari chanya kiasi cha kutoweza kupimika kwa wanawake na mabinti wa Tanzania, Wakimsifu na kumpongeza kwa ujasiri na umahiri wake mkubwa katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kauli hiyo imebainishwa na Bi. Asina Sancho, Kijana na Mjasiriamali wa Kitanzania, akisema Rais Samia amewapa sababu mabinti wengi ya kuamini kuwa wanaweza kufikia malengo yao na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kupambania ndoto zao.

"Mama Samia ametutia nguvu sisi mabinti kuamini kuwa tunaweza kusimama na kutimiza ndoto zetu, hata katika nyakati za majaribio, Mama Samia ametupa nguvu ya kuamini hakuna linaloshindikana. Katika imani pia Mhe. Rais amesemwa katika namna nyingi mbaya na bado amekuwa na imani na kuwasamehe waliomkosea licha ya wao waliomkosea kutotaka msamaha." Amesema Bi. Sancho.

Aidha katika maelezo yake wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo Januari 28, 2026, Sancho amemsifu Rais Samia kwa utekelezaji wake wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na maboresho makubwa katika sekta za huduma za kijamii nchini, mambo ambayo ameyatekeleza katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Akizungumzia siku 100 za awali za kipindi cha pili cha Rais Samia, Sancho ameeleza kuhusu utekelezaji wa ahadi yake ya kuanza mchakato wa Bima ya afya kwa wote pamoja na utoaji wa ajira zaidi ya 12, 000 kwenye sekta ya afya na elimu kama alivyokuwa ameahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025.

Tuesday, 27 January 2026

DKT. MWIGULU ASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITI, DODOMA

1/27/2026 11:48:00 am

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 27, 2026 ameshiriki zoezi la upandaji miti, mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa Jijini Dodoma.

Zoezi hilo ni sehemu ya hatua ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira. 

Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu akiwa ameambatana na mwenza wake Mama Neema Mwigulu, amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha namna alivyo kiongozi mwenye maono, mbunifu na anayejali maslahi mapana ya Taifa.

“Shughuli hii imekuwa na utofauti kwa kusababisha miti ipandwe kila kona ya nchi, kwenye vitabu vyetu vitukufu, kupanda mti ni moja ya ibada kwasababu wanufaika wa miti ni wengi”

Kadhalika, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa Watanzania kuadhimisha siku zao za kuzaliwa kwa kupanda miti. “Tunapokuwa na jambo la kukumbuka la aina hii, tufanye kitu ambacho kinaweka alama na manufaa kwa watu wengine”.

Mheshimiwa Waziri Mkuu amepanda mtu aina ya MDODOMA/MTIMAJI (Trichilia Emetica).

Sunday, 25 January 2026

KANISA LA ACK WAIRIMA LASHAMBULIWA KWA MABOMU, GACHAGUA ANUSURIKA

1/25/2026 09:54:00 pm


Makabiliano makubwa yameshuhudiwa katika Kanisa la ACK Wairima, Kaunti ya Nyeri alikokuwa anahudhuria ibada ya leo Jumapili Januari 25, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. Rigathi Gachagua.

Kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, Polisi waliokuwa wamefunika nyuso zao wametupa mabomu ya kutoa machozi na kurusha risasi za moto katika kanisa hilo, watu kadhaa wakijeruhiwa huku Gagachua na ujumbe wake wakofanikiwa kutoroka.

Hii si mara ya kwanza kwa Naibu huyo wa Rais wa zamani kushambuliwa kanisani ambapo Wiki mbili zilizopita shambulio kama hilo lilitokea nje ya kanisa la Independent Pentecostal Church of Africa (AIPCA) huko Kiamworia, Gatundu Kusini ambapo mafuriko yalitokea baada ya makundi hasimu ya vijana waliokuwa na virungu kuhusika katika vurugu nje ya Kanisa hilo.

Kwenye chapisho lake kwenye Mtandao wa X Gachagua amedai kuwa yeye na washirika wake walinaswa ndani ya Kanisa hilo baada ya shambulio hilo kutokana na kile alichokiita Jaribio la mauaji, akitoa wito wa wananchi kudumisha maombi dhidi ya amani ya nchi hiyo, akidai pia kuchomwa moto kwa magari yake.

Friday, 23 January 2026

WATENDAJI KITUO CHA UOKOZI MWANZA WATAKIWA KUTOA HUDUMA ZA DHARURA KWA SAA 24

1/23/2026 11:46:00 am

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda – Mwanza, chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 19.8, kuhakikisha kituo hicho kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu.

Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza 

Amesisitiza kuwa huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika.

“Hii ni kazi ya kuokoa maisha. Uzembe, kusinzia au kuchelewesha kutoa msaada ni kuhatarisha maisha ya Watanzania. Kituo hiki lazima kifanye kazi saa 24.”

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema ujenzi wa kituo hicho ni uthubitisho wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia watanzania na kujali changamoto mbalimbali nchini. 

“Kituo hiki kilikuwa kijengwe mwaka 2018 kwenda Mwaka 2020, kilisimama baada ya wenzetu kujitoa, lakini Rais Dkt. Samia akasema tutakijenga kituo hiki kwa fedha zetu ili wavuvi waweze kupata huduma ya usalama katika kazi zao”

MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA VIJIJINI MATATANI KWA UCHOCHEZI

1/23/2026 11:33:00 am

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetangaza kumkamata na kumshikilia Bi. Getruda Japhet Lengesela, Mkazi wa Nsalala- Mbalizi na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Ijumaa Januari 23, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Benjamin Kuzaga imesema Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana Januari 22, 2026 saa tatu usiku eneo la Nsalala, Mji mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwa ni pamoja na uchochezi.

Kulingana na Polisi, upelelezi unakamilishwa na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yake mara baada ya upelelezi kukamilika.

Thursday, 22 January 2026

TUTACHUKUA HATUA KALI KWA WATAKAOTUMIA TAARIFA BINAFSI ZA WATU KINYEMELA- PDPC

1/22/2026 09:59:00 pm

Tume ya taarifa ya ulinzi wa Taarifa binafsi Tanzania PDPC imetangaza kuanza mara moja kwa ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria kwa Taasisi za umma na za binafsi, zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 22, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt. Emmanuel Mkilia amesema zoezi hilo linafanyika mara baada ya muda wa hiari kuisha kulingana na tangazo la Tume hiyo lililoweka ukomo wa Aprili 8, 2026 kwa Taasisi husika kukamilisha usajili wao.

"Ukaguzi huu utahusisha kubaini Taasisi za umma na za binafsi zinazokusanya, kuhifadhi kuchakata na kusafirisha taarifa binafsi nje ya nchi bila kuzingatia matakwa ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi sura ya 44 na kanuni zake na PDPC tutachukua hatua kali za kisheria dhidi ya yeyote, taasisi ama kampuni itakayokiuka sheria hii ikiwa ni pamoja na faini, kifungo, fidia kwa waathirika ama vyote kwa pamoja." Amesema Dkt. Mkilia.

Aidha PDPC imesema mtu ama Taasisi itakayobainika kutumia taarifa ya mtu binafsi bila ridhaa yake au kinyume na taratibu zilizowekwa kisheria, Taasisi hiyo itawajibishwa Ipasavyo bila ya kujali hadhi ama ukubwa wa Taasisi itakayokiuka misingi ya sheria katika ulinzi wa taarifa binafsi.

Pamoja na mafanikio yanayotokana na ukuaji wa TEHAMA duniani, kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo ulinzi wa taarifa binafsi ambazo zimekuwa zikikusanywa, zikichakatwa na wakati mwingine kusafirishwa kutoka nchi moja kwenda nyingine bila kuzingatia utaratibu na misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi iliyokubalika kisheria.

WANANCHI WA UKONGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUDUMISHA AMANI NA USALAMA

1/22/2026 09:32:00 am

Wananchi wa Ukonga Mkoani Dar Es Salaam wametoa pongezi na Shukrani kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha amani, utulivu na usalama katika Jimbo lao la Ukonga, suala ambalo limewezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea.

Kwaniaba ya wananchi wengine wa Jimbo hilo wakati akizungumza na Chombo chetu cha habari, Bw. Salum Issa Salum, Mkazi wa Kata ya Buyuni ameeleza kuwa licha ya kupitia baadhi ya changamoto mwishoni mwa mwaka jana, hali kwasasa ni shwari na hatua za maendeleo zimeendelea kushuhudiwa katika Kata hiyo na maeneo mengine kote Tanzania.

"Nisemee zaidi katika miundombinu, Mama amesikia kilio chetu na sasa barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa DMDP kutoka hapa kwetu kwenda Kivule." Amesema Bw. Salum.

Katika maelezo yake, Mwananchi huyo amemuombea uhai zaidi na afya njema Rais Samia, akisisitiza pia umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuilinda amani ya Tanzania ili kutoa fursa ya Taifa na kila mwananchi kupiga hatua za kimaendeleo.

VIONGOZI WA CHADEMA MBEYA WASHIKILIWA WAKIHAMASISHA MIKUSANYIKO BATILI

1/22/2026 09:14:00 am

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Mbeya Bw. Masaga Pius Kaloli na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Mbeya Elisha Chonya kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya mikusanyiko isiyokuwa halali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa Januari 21, 2026 saa tisa alasiri katika Kijiji na Kata ya Inyala baada ya Polisi kupata taarifa za uwepo wa Viongozi hao katika eneo hilo wakifanya maandalizi na wakiwahamasisha watu kukusanyika ili kufanya Mkutano bila bila kufuata taratibu za kisheria zilizopo.

"Pamoja na kukiuka kwa makusudi taratibu hizo za kisheria, ikimbukwe kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimezuiliwa na Mahakama kufanya shughuli zozote za kisiasa." Amesema Kamanda Kuzaga.

Taarifa hiyo ya Polisi Mkoa wa Mbeya imeendelea kueleza kuwa upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.

Friday, 9 January 2026

TABORA WAUPOKEA MWAKA MPYA KWA AMANI NA UTULIVU MKUBWA

1/09/2026 11:19:00 am
TABORA WAUPOKEA MWAKA MPYA KWA AMANI NA UTULIVU MKUBWA

Wananchi wa maeneo mbalimbali Mkoani Tabora wameshiriki kwa namna mbalimbali kusherehekea sikukuu ya Mwaka mpya 2026 na kuuaga mwaka 2025, Burudani za muziki katika sehemu mbalimbali za starehe zikionekana kujaa zaidi, amani na utulivu ukitawala pia katika maeneo hayo.


Wengine pia kama ilivyo utamaduni wa wananchi wa Tabora, wameonekana jana usiku Januari Mosi, 2026 wakiwa kwenye mitaa mbalimbali wakiimba na kusherehekea kuumaliza mwaka 2025 na kuuanza mwaka mpya 2026.

Polisi pia wameonekana katika maeneo yote yenye mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwepo ili kutoa fursa ya kila mmoja kufurahi na wengine kuendelea na biashara zao bila ya vitisho vyovyote vya uvunjifu wa amani kwenye jamii.

Jana Disemba 31, 2025 wakati wa hotuba yake ya kuukaribisha mwaka Mpya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, aliwatakia kheri na mafanikio tele watanzania wote, akiahidi kwamba serikali yake itaendelea kuwatumikia watanzania wote kikamilifu ikiwa ni pamoja na kujenga umoja wa Kitaifa nchini, akitoa rai ya kutokubali kugawanyika kiitikadi na kimtazamo wanapoendelea na ujenzi wa Taifa lao.

AMANI YATAWALA, WATANZANIA WAKISHEREHEKEA MWAKA MPY

1/09/2026 11:19:00 am

Tanzania kama ilivyo kwenye Mataifa mengine kote duniani inasherehekea mwaka mpya wa 2026, Mamilioni wakishuhudia fataki, sherehe za kitamaduni na kidini na mikusanyiko ya kifamilia na kindugu, kuashirikia mwanzo wa mwaka mpya wa 2026 wakiwa na wingi wa matumaini ya ustawi na maendeleo yao binafsi.

Mkoani Dar Es Salaam, leo mchana katika maeneo mbalimbali kumeendelea kushuhudiwa mikusanyiko ya watu, ikiwemo eneo maarufu la Coco Beach, Wilayani Kinondoni ambapo watu wazima kwa watoto wameshuhudiwa wakibarizi katika fukwe hizo usalama ukiimarishwa na Polisi waliokuwa doria, kuhakikisha kila mmoja anaifurahia siku hii.

"Tunafurahi kuingia mwaka mpya, mwaka jana umekuwa na mchanganyiko wa mambo lakini tunamshukuru Mungu kwa hatua za maendeleo tulizopiga na zaidi kwa kuendelea kuitunza amani yetu. Niwaombe watanzania tusirudi tena kule kwenye vurugu, tuione thamani ya amani, tuilinde na tuwakatae wote wanaotaka kuipoteza." Amesema Bi. Amina Seleman, mmoja wa wananchi waliozungumza nasi Coco Beach.

Tofauti na wachache kwenye Mitandao ya kijamii walivyokuwa wakihamasisha kufanyika kwa maandamano hii leo, amani imeendelea kushuhudiwa, Watanzania wakipuuza miito hiyo ya maandamano na kuendelea na sherehe za mwaka mpya 2026.
Adbox