Na Lucas Raphael,Tabora
MWENGE wa Uhuru umezindua miradi 6 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 4.3 katika Halmashauri ya mbili ya wilaya ya nzega ambazo ni nzega vijijini na nzega mjini zote zipo mkoani i Tabora.
Akizungumza kwa nyakati tofauti akiwa katika eneo la miradi hiyo jana Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Ismail Al Usi alionesha kuridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika ikiwemo ubora wa miradi hiyo.
Alibainisha kuwa miradi hiyo iliyopo katika sekta ya elimu, afya, huduma za utawala, uwezeshaji wananchi kiuchumi na miundombinu ya barabara imeakisi dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuboresha maisha ya wananchi.
Awali akipikea mwenge huo mkuu wa wilaya ya nzega , ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega, Naitapwaki Tukai alisema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutumia Mwenge wa Uhuru kama chombo muhimu cha kuhamasisha maendeleo, mshikamano wa kitaifa na ushiriki wa wananchi katika miradi ya kijamii na kiuchumi.
Katika halmashauri ya wilaya ya Nzega Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri mbili za Nzega Mji na Nzega kwa umbali wa kilomita 117.2 ukianza na Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa kupitia jumla ya miradi sita ya maendeleo inayogharimu shilingi bilioni 2.3, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Miradi hiyo ilijumuisha ujenzi wa kituo cha mafuta cha Nyarubanda Oil kilichogharimu shilingi bilioni 1.092, ujenzi wa zahanati ya Ipilili uliogharimu shilingi milioni 103, pamoja na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya walimu na matundu sita ya vyoo kwa gharama ya shilingi milioni 92.
Aidha alisema kwamba miradi mingine ni wa kikundi cha vijana wajasiriamali cha Constrafrica waliopatiwa fedha asilimia 10 kiasi cha shilingi milioni 19.
Pia mwenge huo uliweka jiwe la msingi mradi wa upanuzi wa mfuko wa kusafisha na kutibu maji Nzega unaotekelezwa kwa shilingi milioni 620 na mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Lumambo–Kitongo hadi FDC unaogharimu shilingi milioni 462.1.
Aidha, Mwenge wa Uhuru mwaka huu unabeba kaulimbiu isemayo: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”, ikiwa ni wito kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi huku wakidumisha amani, mshikamano na utulivu wa kitaifa.
mwisho
No comments:
Post a Comment