Tuesday 8 October 2013

VIONGOZI WA TYCC WAKISOMA RISALA

Mwanafunzi ambaye ni Mmoja wa viongozi wa Tyccc kanda ya Tanga kwa jina la Douglos Gasper aliyevalia miwani(wa kwanza kutoka kushoto)ambaye pia ni mhazini wa kikundi hicho,akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi kwenye mahafali yao ya dini ya kidato cha nne yaliyofanyika katika ukumbi wa Magreth Hall uliopo jijini Tanga.

Kiongozi huyo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi pamoja na kadamnasi iliyokuwepo kwenye mahafali hayo ambapo alielezea changamoto wanazokumbana nazo katika kuendesha kikundi chao wakiwa shuleni.

Gasper alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakizuiliwa na uongozi wa shule katika suala zima la kuendesha vipindi vyao dini ikiwemo kuimba kwaya wawapo mashuleni  huku walimu hao wakitumia vipindi hivyo kufundisha masomo mengine jambo ambalo limepelekea wanafunzi wengi kutokuwa na hofu ya Mungu hata kutofahamu kabisa neno la Mungu.

Pia alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili katika utendaji kazi wao ni ufinyu wa kipato kwani hawana biashara yoyote hivyo kulazimika kutoa ela zao mifukoni pale kunapokuwa kumehitajika utatuzi wa jambo fulani na kwamba hali hiyo imepelekea shughuli zao kutokwenda kwa ufanisi.

Waliiomba serikali na uongozi wa dini ya kikristo kuwapa msaada pale watakapokuwa wanahitji msaada ikiwa ni pamoja na kuwawekea walimu wa dini kwenye shule zao ili kuweza kuepukana na tatizo lililokihtiri la kufeli masomo ya dini ya kikristo tofauti na dini nyingine.

Categories:

0 comments: