Adbox

Friday, 14 November 2025

RAIS SAMIA AMTAHADHARISHA DKT. MWIGULU DHIDI YA VISHAWISHI VYA MARAFIKI WA MADARAKA

11/14/2025 02:16:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtakia kheri Waziri Mkuu mpya wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akimtaka kuepuka vishawishi vya ndugu, jamaa na marafiki na badala yake ajielekeze zaidi katika kuwatumikia Watanzania.

Rais Samia amebainisha hayo leo Ijumaa Novemba 14, 2025 katika hotuba yake muda mfupi baada ya kumuapisha Dkt. Nchemba Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, akimtaka kusimamia kikamilifu utekelezaji wa yale yaliyoahidiwa kwa watanzania wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu.

"Kwa umri wako mzigo huu ni mkubwa na vishawishi ni vingi kutoka kwa marafiki, ndugu, jamaa na wengine, nafasi yako hii haina rafiki, haina ndugu, haina jamaa- ni nafasi ya kulitumikia Taifa kwahiyo nikutakie kila la kheri katika utumishi wako." Amesema Rais Samia.

Rais Samia amesisitiza kuwa muda ni mchache katika kutekeleza yale waliyoahidi kwa wananchi, akimtaka kusimamia vyema baraza la Mawaziri kwa kutumia vyema uzoefu wake katika Wizara ya fedha na kumsimamia vyema atakayekuwa Waziri wa fedha ili fedha zipatikane katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Dkt. Samia katika hatua nyingine leo mchana anatarajiwa kuzindua Bunge la 13 la Tanzania, akieleza kuwa katika hotuba yake ataeleza mwelekeo wa Serikali yake na vile vitakavyokuwa vipaumbele katika miaka mitano ijayo.

Thursday, 13 November 2025

WABUNGE WAFUNGUKA UTEUZI WA WAZIRI MKUU NCHI IMEPATA WAZIRI MKUU SAHIHI.

11/13/2025 08:00:00 pm

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu, uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni uamuzi sahihi unaoonyesha dhamira ya kuhakikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kwa weledi na ufanisi.

Wakizungumza nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Dkt. Mwigulu kuthibitishwa rasmi na Bunge kwa kura 369 kati ya kura 371, wabunge hao wamesema wana imani kubwa kuwa Waziri Mkuu huyo ataendelea kusimamia ipasavyo maendeleo ya nchi na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu, na Mbunge wa Simanjiro  (CCM) James Ole Millya wamesema wanaaamini  kuwa Dkt. Mwigulu atatoa kipaumbele katika kutatua changamoto za vijana, hususan tatizo la ukosefu wa ajira, ili kuhakikisha kundi hilo muhimu katika maendeleo ya taifa linanufaika na fursa zilizopo.

Wabunge hao wameongeza kuwa uteuzi huo ni uthibitisho wa uongozi makini wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza misingi ya uwajibikaji, utendaji bora na maendeleo endelevu kwa Watanzania wote.

LUKUVI AMMWAGIA SIFA DKT. MWIGULU "RAIS SAMIA HAJAKOSEA KUMTEUA"

11/13/2025 03:48:00 pm


Mbunge wa Jimbo la Isimani Mkoani Iringa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. William Lukuvi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hajakosea kumteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kutokana na weledi, uwezo wa uzoefu wake katika uongozi nchini.

Lukuvi, Miongoni mwa wanasiasa wa muda mrefu kwenye Bunge la Tanzania ameutaja ubobevu wa kitaaluma wa Dkt. Nchemba kama sababu nyingine muhimu wa yeye kuridhia uteuzi wake, akisema kufanya kwake kazi Benki kuu ya Tanzania kabla ya kuingia kwenye siasa kunathibitisha uwezo mkubwa alionao Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Lukuvi amezungumzia pia uzoefu wa Dkt. Nchemba ndani ya Chama Cha Mapinduzi, akisema amekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa miaka mingi, Mjumbe wa kamati kuu na Mjumbe wa sekretarieti ya Chama hicho pamoja na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kati ya mwaka 2012-2015.

Leo Alhamisi Bunge la 13 la Tanzania limemthibitisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu kwa kura 369 kati ya kura 371 zilizopigwa na sasa kulingana na taarifa ya Ikulu Mteule huyo ataapishwa Ijumaa ya Novemba 14, 2025 Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

TUMEPATA WAZIRI MKUU SAHIHI- ANNA MALECELA

11/13/2025 03:23:00 pm

Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mkoani Kilimanjaro Mhe. Anne Kilango Malecela amesema Rais Samia Suluhu Hassan amegusa mioyo ya Watanzania wengi kutokana na kumteua Mbunge wa Iramba Magharibi Mkoani Singida Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
"Sifa kubwa ya Dkt. Mwigulu ni mtu anayefikika na lazima niseme ukweli kuna watu wakiwa mawaziri wanakuwa vigumu kuwafikia lakini kwa Mwigulu tangu akiwa Naibu Waziri, Waziri mpaka Waziri wa fedha ni mtu anayefikika na kila mtu na nyumbani kwake ni nyumbani kwa watu wengi." Amesema Mhe. Anna Malecela.

Amemuelezea pia kama mtu mwenye upendo kwa kila mmoja, akisema Wabunge wa Bunge la 13 pamoja na Wananchi wa Tanzania wamempata Kiongozi sahihi anayeweza kusimama kuwasemea na kuwatetea.

Malecela ametoa kauli hiyo mapema leo Novemba 13, 2025 Bungeni Mjini Dodoma wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipowasilisha Jina la Dkt. Mwigulu Bungeni hapo ili kuweza kuidhinishwa kuwa Waziri Mkuu, akitarajiwa kuapishwa kesho Ijumaa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tayari kuanza majukumu yake mapya kwa miaka mitano ijayo katika serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

WAZIRI MKUU MTEULE AAHIDI KUREJESHA HESHIMA YA UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

11/13/2025 01:46:00 pm

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Alhamisi Novemba 13, 2025 limemthibitisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiahidi kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha kuwa maono na ahadi za Rais Samia Suluhu Hassan zinateketekelezwa ili kuwaletea wananchi ustawi na maendeleo kwa miaka mitano ijayo.

Uteuzi wa Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa miaka mitano ya awali ya serikali ya awamu ya sita, umetangazwa rasmi bungeni mjini Dodoma, akithibitishwa kwa kura 369 za ndio kati ya 371 zilizopigwa na wabunge huku kura mbili zikiharibika.

Mwigulu anajulikana kama mfano wa mafanikio yanayotokana na bidii na kujituma. Alikulia katika mazingira ya kijijini na alitoka katika familia yenye hali ya kawaida, ambapo aliwahi kuchunga ng'ombe nyikani akiwa kijana mdogo. Maisha hayo yalimfundisha nidhamu, uvumilivu na kuthamini kazi halali. Mara kadhaa amekuwa akisimulia hadithi ya maisha yake kama njia ya kuwahamasisha vijana kupambana kupitia elimu na kujituma.

Akieleza kutambua namna ambavyo Dkt. Samia amejitambulisha kama Kiongozi wa matokeo, katika hotuba yake ya shukrani bungeni Dkt. Mwigulu ametoa rai kwa Watanzania kumtanguliza Mungu na kuhakikisha amani inaendelea kuwepo nchini, akitoa onyo kwa watumishi wazembe, wala rushwa na wenye lugha chafu kwa Watanzania.

"Kwa kuzingatia kazi kubwa iliyopo mbele yetu naomba niseme kuwa watumishi wa umma na Watanzania lazima tuwe tayari, lazima tuende na gia ya kupandia mlima, watumishi wa umma wavivu, wazembe, wala rushwa na wenye lugha mbaya kwa Watanzania tuwe tayari na nitakuja na fekeo na rato, lazima maono ya Rais na ahadi zake zitekelezwe." Amesisitiza Mhe. Mwigulu.

Aidha Mwigulu amemshukuru Rais Samia kwa imani yake kwake pamoja na Wabunge wenzake kwa kumuamini na kumkopesha imani, akisema Watanzania wote watasikilizwa kwa nidhamu kila ofisi ya umma na pamoja na kutoa nafasi sawa kwa wabunge wote wa Bunge la 13 hasa kwa wale walio wachache, wanaotokana na vyama vya upinzani.

Dkt. Mwigulu amewahi kushika nafasi mbalimbali serikalini. Alianza kama Naibu Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete. Baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mwaka 2015, kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2016. Mwaka 2021 aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, nafasi aliyoishikilia hadi uteuzi wake kuwa Waziri Mkuu.

Wednesday, 12 November 2025

WANANCHI WAHIMIZA UVUMILIVU, MCHAKATO WA MARIDHIANO YA KITAIFA

11/12/2025 11:30:00 am


Kama ilivyoahidiwa na Rais wa Tanzania kwamba moja ya ahadi zake ni pamoja na kutafuta maridhiano ya Kitaifa na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya ili kulileta Taifa pamoja na kushughulikia changamoto za wadau mbalimbali, wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamewashauri makundi mbalimbali ya kijamii kuacha mihemko na kuisikiliza serikali, huku serikali pia ikitakiwa kuusikiliza upande wa wananchi kujua kile wanachokitaka.

Kauli za wananchi zinakuja siku chache pia mara baada ya Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kusisitiza dhamira hiyo ya Rais Samia kuhusu maridhiano ya Kitaifa ili kusikiliza wananchi na kuendelea kuifanya Tanzania kuwa yenye amani na utulivu.

"Ni dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaanzisha mazungumzo ya maridhiano ili kuhakikisha hata hao wachache wanapata nafasi ya kusikilizwa ili kuwa na taifa lenye amani na umoja na kuendelea kuwa mfano wa utulivu katika Afrika na dunia.”Alisema Dkt. Nchimbi kwenye Mkutano wa Kimataifa uliofanyika siku mbili zilizopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wanaoishi Chanika, Jijini Dar Es salaam wamesisitiza umuhimu wa maridhiano hayo ili kujenga jamii yenye amani na ustawi, wakirejea athari kubwa zilizotokea wakati wa ghasia na vurugu za Oktova 29, 2025.

Wamelaani pia utafutaji wa haki kwa kuhamasisha na kutenda vitendo vyenye kuhatarisha amani ya Tanzania, wito zaidi ukitolewa kwa vijana kuachana na mihemko na ushawishi wa kufanya vurugu na badala yake kupendelea zaidi njia ya mazungumzo na masikilizano katika kushughulikia changamoto zinazowakabili katika maeneo mbalimbali.

Tuesday, 11 November 2025

RC MAKALLA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI ARUSHA, WAFANYA DUA MAALUM KUOMBEA AMANI

11/11/2025 05:43:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla  amekutana na Viongozi wa dini na wa kimila kutoka Mkoa wa Arusha, akitoa Rai kwa Viongozi hao kuendelea kuhubiri amani kwa waumini na wafuasi wao pamoja na kuiombea nchi ya Tanzania.

CPA Makalla kando ya kujadiliana masuala mbalimbali na Viongozi hao wa dini katika ujenzi wa jamii yenye amani, upendo na mshikamano, alishiriki sala na dua  maalumu iliyoongozwa na Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali akiwemo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya maridhiano ya amani Tanzania Dkt. Israel Ole Maasa.

Rc Makalla amesisitiza umuhimu wa Viongozi hao pia kuendelea kuhubiri kuhusu amani na kushirikiana na waumini wao kuliombea Taifa la Tanzania, Viongozi hao wa dini wakiahidi pia kushirikiana na serikali katika kuhakikisha jamii inakuwa na amani na mazingira tulivu.

"Muhimu kuhubiri kuwa hakuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania na ili tusonge mbele katika maendeleo ni muhimu kuendelea kuwa na amani na utulivu kwahiyo kila mmoja wetu arejeshe matumaini na maombi hayo kwamba Watanzania tunahitaji amani hivyo sala na maombi yetu kwa Mwenyenzi Mungu ni amani na sisi serikali tutaendelea kupokea ushauri wenu na kuufanyia kazi." Amesisitiza Mhe. Makalla.

Viongozi hao wa dini katika maombi yao, wameombea amani ya Tanzania na kuwaombea Viongozi wakuu wa Tanzania wakiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wao wa ngazi mbalimbali akiwemo Mhe. Makalla wakimuomba Mwenyenzi Mungu awape baraka, nguvu na utashi zaidi katika kuwatumikia watanzania na kuhakikisha Tanzania inabaki salama.

TUWAKATAE WACHOCHEZI, GHASIA, VURUGU VINATURUDISHA NYUMA KIMAENDELEO

11/11/2025 05:42:00 pm

Mjasiriamali Kijana Bw. Peter Shaaban Gerald, Mkazi wa Kimara Dar Es Salaam amewasihi Vijana wenzake kujiepusha na uratibu na ufanyaji wa matukio ya ghasia na vurugu, yenye kuhatarisha amani ya Tanzania kwani athari za Kijamii na kiuchumi ni nyingi kutokana na mtindo wa maisha na namna ya kujipatia Kipato kwa Watanzania wengi hususan Vijana.

Ameyaeleza hayo wakati akizungumzia uzoefu alioupata kwa takribani siku saba zilizopita, zikitokana na uharibifu na ghasia za Oktoba 29, 2025 kwenye Majiji na Miji ya Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Songwe, akisema uchumi wake umetetereka pakubwa kutokana na kukosa kipato kulingana na kazi yake ya kumtaka kuwa barabarani kila wakati ili kuwafuata na kuwatafuta wateja.

"Sisi tumezoea kutembea barabarani kujitafutia chochote, na unajua maisha ya Vijana ni gheto (Vyumba vya kuishi) sasa si sahihi kuandamana kwasababu sisi Vijana wengi tuliumia, wengine walizipoteza pia familia zao na tumezoea Tanzania ni nchi ya amani hivyo ni muhimu kuilinda amani yetu sisi kama Vijana." Amesisitiza Bw. Peter.

Peter amekumbusha pia wajibu wa Vijana katika kulinda amani ya Tanzania kwa msingi wa kuliandaa Taifa la kesho kutokana na nguvu kazi yao, akiishukuru serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama kwa kurejesha amani katika maeneo yote nchini na hivyo kuruhusu shughuli za kiuchumi na kijamii kuweza kuendelea kama kawaida.
                 https://www.instagram.com/reel/DQ50-bXjEhQ/?igsh=cDg0djlpdXZtZGNn

Monday, 10 November 2025

MOSHI MWEUPE NJIA YA MARIDHIANO, VIONGOZI WA CHADEMA AKIWEMO AMANI GOLUGWA WAACHIWA KWA DHAMANA

11/10/2025 09:18:00 pm


Siku moja baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza  kuondoa mifarakano na kulileta pamoja Taifa, tayari Viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  wameachiwa kwa dhamana.
Viongozi hao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara John Heche, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa, Mwenyekiti Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama Boniface Jacob (Boni Yai) na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema,  dhamana yao umetolewa leo 10 Novemba 2025

Hii inaweza kuwa hatua nzuri kwenye safari ya Maridhiano kama alivyotangaza  Dkt. Nchimbi, kuondoa mifarakano na kuleta pamoja taifa, kulinda amani na kurudisha umoja baada ya migawanyiko ya Uchaguzi!?

Heche yeye alikuwa anashikiliwa na Polisi tangu Oktoba 22, 2025, alipokamatwa nje ya geti la Mahakama Kuu Dar es Salaam, alipokuwa akienda mahakamani, kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini.

BODABODA WENYE PIKIPIKI ZA MKATABA WALIA NA VURUGU NA GHASIA ZA OKTOBA 29.

11/10/2025 03:15:00 pm

Bwana Issa Salala, Afisa usafirishaji abiria kwa kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda anayefanya shughuli zake Jijini Dar Es Salaam ameeleza namna ambavyo ghasia, vurugu na maandamano ya Oktoba 29, 2025 yalivyomuingiza kwenye madeni makubwa yasiyolipika, kutokana na ghasia zile kuzuka wakati ambao hakuwa na akiba yoyote ndani kwake.

Salala amebainisha hayo wakati akizungumzia athari za ghasia na uharibifu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025 kwenye maeneo mbalimbali ys Mkoa huo, akisema suala hilo lilimfanya yeye kutotoka ndani zaidi ya siku tano, akiendesha pikipiki isiyokuwa yake, suala ambalo lilifanya aliyemkodishia pikipiki kudai malipo yake wakati alipokuwa amesimama kufanya kazi kutokana na vurugu hizo.

Aidha Salala amezungumzia pia mfumuko mkubwa wa bei uliojitokeza kutokana na uhaba wa bidhaa na huduma mbalimbali kwenye eneo lake, akisema Unga uliokuwa ukiuzwa Kilogramu moja shilingi 1,500 waliuziwa shilingi 4,000 huku Mchele wa Shilingi 2,000 kwa Kilo moja wakiuziwa zaidi ya shilingi 5,000.

"Ni muhimu kwasisi Vijana kufikiria mbele kabla hujafanya kitu, vijana walioandamana hawakufikiria matokeo ya baadae. Leo unga wa 1, 500 unaununua 4, 000, Mchele wa 2,000 unaunua 5,000 na kipindi hicho kuna zuio la kutotoka nje kutokana na usalama, sasa hela unatoa wapi? Tumeingia ndani nilikuwa mnene, tumetoka nimepungua kwani mwili umeisha huu sasa hivi." Amesema.

Ni huzuni kila kona vurugu za oktoba 29,2025 zakosesha huduma za kijamii Mwanza

11/10/2025 11:02:00 am
Ghasia, vurugu na uharibifu mkubwa uliofanywa na magenge ya Vijana hapo Oktoba 29, 2025, umewaacha wananchi wa Mkoa wa Mwanza kukosa huduma muhimu za kijamii, huku pia mamia ya wananchi wakikosa ajira na kipato kutokana na matukio ya moto na wizi ulioangamiza maeneo yao ya kazi katika Eneo la Buhongwa Mkoani humo.

Kwa nyakati tofauti, magenge ya Vijana  katika siku ya uchaguzi Mkuu wa Jumatano Oktoba 29, 2025, wakati wengine wakipiga kura kuwachagua Viongozi wao watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo, wao  walivamia, kuiba na kuchoma moto Chuo cha Ufundi stadi VETA cha Buhongwa Mkoani Mwanza pamoja na kuiba na kuteketeza kwa moto Vituo vya uuzaji mafuta vya Olypic Petrol na Lake Oil Energies pamoja na kituo cha uuzaji wa bidhaa mbalimbali cha Empire store Kilichopo Igoma sambamba na magari yaliyokuwa yamepaki kwenye maeneo hayo.

Aidha wahalifu hao pia kando ya kuiba na kuteketeza kwa moto Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Buhongwa Mkoani humo, waliiba mali na samani mbalimbali za Ofisi pamoja na kuteketeza kituo cha Polisi Buhongwa, Kiwanda cha magodoro cha Super Banco na Kiwanda cha Vita Foam mkoani humo, suala ambalo limetajwa kuwaacha mamia ya Vijana na wananchi wa Mkoa huo na Mikoa ya jirani kukosa huduma mbalimbali na zaidi ajira kutokana na uharibifu huo mkubwa.

TUIJENGE NCHI YETU KWA PAMOJA NA KUOMBEA AMANI IDUMU- KIROBA

11/10/2025 11:02:00 am

Adam Kiroba, Mkazi wa Mkera, Chanika, Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam,  amewataka watanzania hususani Vijana kote nchini kudumisha amani, mshikamano na upendo kwenye jamii na kujiepusha na vurugu na uvunjifu wa amani kwani mara zote waathirika wakubwa wa vurugu mara zote wamekuwa akinamama, Watoto, Wazee pamoja na wale wasiokuwa na hatia kutoka kundi la wananchi wenye kipato cha chini.

"Mimi ninachowaomba watanzania ni kuwa nchi yetu inasifika kuwa kisiwa cha amani, tuendelee na sifa hiyo kwasababu machafuko ya juzi athari zake tumeziona na wengine mpaka leo biashara na sehemu za kuishi hawana. Niwasihi watanzania wenzangu tudumishe amani iliyopo na tusiwe sehemu ya kuhamasisha hicho kinachoendelea na tuwe wavumilivu na kuangalia namna ya kuijenga nchi yetu." Amesisitiza Bw. Kiroba.

Bw. Kiroba akizungumza na mwandishi wetu wa habari leo Jumapili Novemba 09, 2025 amewataka pia Vijana kutofuata mikumbo kutoka kwa baadhi ya watu, akiwahamasisha pia wale wote wenye kuamini katika Mungu kupitia dini zao na madhehebu mbalimbali kuendelea kuiombea nchi ya Tanzania ili amani, umoja na mshikamano viendelee kudumu kwa maslahi ya kila Mtanzania.

Amesisitiza pia umuhimu wa kutambua faida za amani kwenye jamii, akisema ghasia na vurugu za Oktoba 29, 2025 kumewagharimu pia watu wasiokuwa na hatia, kusababisha ugumu wa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii pamoja na kupanda kwa gharama za maisha na kuyumba kwa uchumi kwa watu wengi wa kipato cha chini.

Saturday, 8 November 2025

Amani imerejea aeleza namna mfumuko wa bei uliwaathiri asema mafuta ya petroli yaliuzwa kwa shilingi 15,000 kwa Lita moja

11/08/2025 06:11:00 pm
AMANI IMEREJEA, TUNAISHUKURU SERIKALI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

Shaban Moshi Shaban, Afisa usafirishaji kwa kutumia Pikipiki maarufu kama Bodaboda kwenye eneo la Kimara mwisho Mkoani Dar Es Salaam, ameishukuru serikali pamoja Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania, kwa jitihada kubwa zilizochukuliwa ili kuirejesha amani ya Tanzania, akieleza kuwa vurugu za Oktoba 29, 2025 ziliwaweka kwenye wakati mgumu kiuchumi na kijamii.

Bw. Moshi wakati akizungumza na chombo hiki cha habari, amesema ghasia hizo pamoja na zuio la kutoonekana nje kuanzia saa kumi na mbili Jioni lililotolewa na Jeshi la Polisi liliwaletea athari nyingi za kiuchumi kutokana na kukosa abiria na kipato, kwani shughuli za usafirishaji walikuwa wamezoea kuzifanya kwa muda wa saa 24.

"Kitu walichokifanya waliokuwa wakijiita waandamanaji ni kitu ambacho hakifai kwani maandamano haya hayakuwa na ujumbe wowote kwa serikali lakini pia maandamano yale yalikuwa kosa kisheria kwasababu walifanya uhalifu pia katika baadhi ya sehemu kwahiyo niwashauri waache hicho walichokifanya." Amesema Bw. Moshi.

Aidha ameeleza pia namna ambavyo mfumuko wa bei uliwaathiri kwa kiasi kikubwa, akisema mafuta ya petroli yaliuzwa kwa shilingi 15,000 kwa Lita moja hivyo kusababisha adha kubwa kwao ikiwa ni pamoja na kuwapoteza wateja waliolalamikia kupanda kwa bei za usafiri huo wa Pikipiki.

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUFUATA TARATIBU SAHIHI KUDAI HAKI ZAO

11/08/2025 11:12:00 am

Wito umetolewa kwa watanzania wa kutii sheria, kuisikiliza serikali na kutafuta haki kwa namna na taratibu zinazoruhusiwa kisheria badala ya kuratibu na kufanya ghasia, uharibifu na vurugu kama sehemu ya kushinikiza serikali kutekeleza matakwa mbalimbali.

Asraji Likwati, Mwenyekiti wa wasafirishaji abiria kwa njia ya Pikipiki Kimara Mkoani Dar Es Salaam ametoa wito huo leo Novemba 08, 2025 wakati akizungumzia athari za ghasia zilizotokea Jumatano ya Oktoba 28, 2025 siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akiwakosoa baadhi ya vijana ambao walifanya ghasia hizo na kuiba na kuharibu mali na vitega uchumi vya wananchi wa hali ya chini wasiokuwa na nafasi yoyote kisiasa na wasiohusika na kile kilichokuwa kikilalamikiwa na makundi hayo.

"Nitoa wito tu kwamba tuisikilize serikali, haki tuitafute kwa taratibu sahihi kwani ni wengi waliovunjiwa na kuibiwa mfano unaenda kumuibia mangi ambaye hana hata ushawishi na masuala ya kisiasa. Juzi hapa tumelalamika kuhusu mwendokasi serikali ikatusikia na kuleta mabasi mapya, leo wanayachoma moto, kiukweli hii haikubaliki." Amesisitiza Bwana Likwati.

Ameeleza athari nyingine kuwa ni pamoja na kudorora kwa mzunguko wa fedha, kuathirika kwa biashara kati ya Tanzania na nchi jirani zenye kuitegemea bandari ya Dar Es Salaam pamoja na kutikisika kwa sifa ya Tanzania kimataifa ya kuwa Taifa lenye amani, uhuru na mshikamano kwa watu wake.

MALI ZA UMMA NA WATU BINAFSI ZIMECHOMWA, HAYAKUWA MAANDAMANO, ZILIKUWA VURUGU

11/08/2025 09:07:00 am

Samwel Salum Mkazi wa kimara Jijini Dar es Salaam amelaani maandamano ya Oktoba 29 akieleza kuwa lengo lake lilikuwa kuharibu mali, kujeruhi na kusababisha hasara kubwa kwa uchumi wa Tanzania.


Bwana Samwel ameyasema haya alipozungumza na waandishi wa Habari kuhusu manufaa na athari za maandamano hayo ambayo kwake ameyaita vurugu na Wala sio maandamano kwani yalikuwa hayana ujumbe wowote kwa Serikali

Friday, 7 November 2025

WANANCHI WALIA NA UGUMU WA MAISHA ULIOSABABISHWA NA GHASIA ZA OKTOBA 29

11/07/2025 10:15:00 am


Kutatizika kwa shughuli za kiuchumi kwa takribani siku tano mara baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kumeelezwa kusababisha adha kubwa ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam hasa kwa wale ambao wamekuwa tegemeo kwa familia na wazazi wao.

Kauli hiyo imeelezwa na wananchi wa Mkoa huo wakati wakizungumza na waandishi wa habari, siku chache mara baada ya Tangazo la Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutaka shughuli za Kijamii na kiuchumi kuendelea kama kawaida mara baada ya ghasia na vurugu za Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

"Kutokana na vurugu na ghasia za Oktoba 29, sisi wananchi tunaotegemewa na familia na wazazi tumeathirika sana, siku tano kwenye maisha yetu ni nyingi sana na bahati mbaya hali hii ambayo mimi ni mara ya kwanza kuishuhudia haijaangalia kipato cha mtu kwasababu kukosekana kwa amani kulikotokea kumesababisha hata wenye kipato kukosa huduma na bidhaa muhimu." Amesema Bw. Habibu Sadick, Dereva wa Bajaji Jijini Dar Es Salaam.

Kwa upande wake Iddi Mzese, Mkazi wa Changarawe Jijini Dar Es Salaam kando ya kusisitiza namna ambavyo ghasia na vurugu hizo zilivyosababisha ugumu wa maisha, amewataka Vijana kujiepusha na mikumbo yenye kupelekea kujiingiza kwenye ghasia na uvunjifu wa amani, akihimiza ulinzi wa amani na mshikamano uliopo nchini.

Thursday, 6 November 2025

MPAKA WA TANZANIA NA KENYA NI SALAMA- RC MAKALLA*

11/06/2025 08:24:00 pm

 *_Aridhishwa na usalama na ufanyaji biashara eneo la Namanga_* 

 *_Aeleza umuhimu wa Mpaka huo kibiashara na ustawi wa Jamii_* 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ameeleza kuridhishwa na hali ya ulinzi na usalama katika Mpaka wa Namanga unaounganisha Mataifa ya Tanzania na Kenya kupitia Mkoa wa Arusha, akiwashukuru watendaji wa Pande zote mbili wanaofanya kazi kwenye Kituo cha pamoja cha forodha Namanga kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa pande zote.

Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Alhamisi Novemba 06, 2025 Mjini Namanga wakati alipoambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kwaajili ya kukagua hali ya Ulinzi na usalama katika eneo hilo pamoja na kuangazia ufanyaji wa biashara katika eneo hilo mara baada ya maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka shughuli zote za Kijamii na kiuchumi kuendelea katika maeneo mbalimbali nchini mara baada ya uchaguzi Mkuu.

"Nithibitishe kuwa Mpaka wa Tanzania na Kenya ni salama na kituo cha pamoja cha forodha Namanga kipo salama. Kituo hiki ni muhimu kwa nchi zetu zote mbili na kwa wananchi hususani hawa wa Mpakani kwani wao pia ni wanufaika wa moja kwa moja na fursa za kiuchumi na biashara kwahiyo ni muhimu kuendelea kueneza amani, umoja na mshikamano kwenye mpaka huu kwani sote ni wanufaika." Amesema Mhe. Makalla.

CPA Makalla kadhalika amewapongeza  Viongozi na watendaji wa kituo hicho cha forodha ka kuendelea kuimarisha mahusiano na kukuza biashara katika eneo hilo suala ambalo limekifanya Kituo hicho pia kuwa eneo muhimu la mabadilishano ya bidhaa kati ya Tanzania na Kenya, akisema kutetereka kwa Mpaka huo kuna athari kubwa kwa uchumi wa nchi hizo na ustawi wa jamii.

Kwa Upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) kwenye Kituo hicho cha Namanga Bw. Nicholous Mugambi amemuhakikishia CPA Makalla kuwa wataendelea kushirikiana na Mamlaka za Tanzania katika kukuza mahusiano na biashara miongoni mwa nchi hizo mbili, akisisitiza umuhimu wa amani kama msingi wa kufikia mafanikio katika biashara na ustawi wa wananchi wa Tanzania na Kenya.

HAKUNA VITA NZURI, TUILINDE AMANI YA NCHI YETU- MOSHI

11/06/2025 03:40:00 pm

Mfanyabiashara ndogondogo wa Mitaa ya Kongo na Pemba, Kariakoo Jijini Dar Es salaam Bw. Elia Moshi amesisitiza kuwa mara zote haki huwa haidaiwi kwenye machafuko na ghasia, akitoa wito wa Vijana kufikiri juu ya athari za machafuko kabla ya kujiingiza kwenye Hamasa zinazotolewa kwenye Mitandao ya Kijamii na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania.

Bw. Moshi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar Es Salaam, siku tatu mara baada ya hali ya ulinzi na utulivu kurejea katika maeneo mengi nchini mara baada ya ghasia na fujo zilizojiri kwenye Miji mbalimbali nchini wakati wa uchaguzi Mkuu wa Tanzania Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

"Vijana niwaaambie kuwa hakuna Vita nzuri, Vita vina athari kubwa hasa kwetu sisi wa kipato cha chini. Wanaohamasisha Vijana kuingia barabarani wana maisha yao mazuri na hutowaona barabarani ni muhimu kutathmini wale wanaohamasisha ghasia hizo na athari zake kabla ya kuchukua maamuzi." Amesema.

Akizungumzia athari za ghasia hizo, Moshi amesema uchumi ulidorora na kusababisha mfumuko wa bidhaa muhimu za kila siku, akisema kukosa utamaduni wa kuweka akiba kwa Watanzania wengi kumekuwa sababu pia ya wengi kuathirika kutokana na kukosa akiba ya chakula kwenye nyumba zao.

TUTUMIE MITANDAO YA KIJAMII VIZURI NA TULINDE MIUNDOMBINU YETU

11/06/2025 03:40:00 pm

Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wametoa wito wa matumizi sahihi ya Mitandao ya Kijamii na kujiepusha na utoaji wa maoni na uhamasishaji wa uvunjifu wa amani kupitia Mitandao hiyo, wakiiomba serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwasamehe Vijana waliojiingiza katika uvunjifu wa amani kwa kufanya vurugu za Oktoba 29, 2025 katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa nyakati tofauti wakizungumza na Chombo hiki cha habari, Wananchi hao akiwemo Mombeki Gervas na Baraka Nyange, wameeleza pia athari za machafuko na ghasia hizo zilizotokea kwenye Mkoa huo, wakisema mbali ya uharibifu wa miundombinu na mali za umma na za binafsi, wenye familia wamekuwa waathirika zaidi wa ghasia hizo zilizodumu kwa zaidi ya siku mbili.

"Sisi tuna majukumu na zaidi familia zetu. Tofauti na mazoea tuliyokuwa nayo tunapomaliza uchaguzi, Uchaguzi wa mwaka huu umekuja na maandamano na tulikuwa hatuna akiba na maisha ya dar tunayajua huwezi kula bila ya kutoka." Amesisitiza kusema Bw. Mombeki.

Kwa upande wake Bw. Nyange amesema "Hii nchi ni ya kwetu, miundombinu iliyoharibika ni ya Watanzania kwahiyo tunapoharibu miundombinu tunayotumia sisi wenyewe maana yake tunajiumiza wenyewe na tunaumiza uchumi wetu wenyewe." Amesisitiza.

Nyange kando ya kuwataka watanzania hususani Vijana kutumia vyema mitandao ya kijamii nchini kwa maslahi ya Tanzania, amesisitiza pia kulinda na kuitunza miundombinu inayojengwa na serikali nchini, akisema miundombinu hiyo imejengwa kwa faida ya watanzania wenyewe katika kurahisisha shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Wednesday, 5 November 2025

HUDUMA YA MWENDOKASI YASITISHWA KUPISHA TATHMINI YA UHARIBIFU ULIOFANYIKA OKTOBA 29.

11/05/2025 07:46:00 am

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Albert John Chalamila ametangaza kusitisha huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu kama mwendokasi kati ya Gerezani - Kimara na Gerezani - Mbagala Jijini Dar Es Salaam.

Kusitishwa kwa huduma hiyo kulingana na Mhe. Chalamila katika Taarifa yake kwa Vyombo vya habari, kunalenga kutoa nafasi ya kufanyika kwa tathmini ili kujua uharibifu uliofanyika wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025 jijini Dar es Salaam.

Katika maandamano hayo, waandamaji waliharibu miundombinu hususan vituo vya mwendokasi, zaidi katika vituo vilivyopo barabara ya Morogoro kwa kuvunja vituo, mifumo ya ukataji wa tiketi na kuvichoma moto baadhi ya vituo vya kushusha na kupakia abiria.

Chalamila katika taarifa yake amewataka wananchi wote waliokuwa watumiaji wa usafiri huo kutafuta njia mbadala za usafiri katika kipindi hiki wakati ambao unafanyika utaratibu wa kurudisha hali kama ilivyokuwa awali.

“Tunasitisha mara moja usafiri huu ili kufanya tathmini ya kina ya uharibifu uliotokea kwani mifumo ya ukataji tiketi imeharibiwa jambo ambalo linahitaji muda ili kurudisha hali kama ilivyokuwa awali,” amesema Chalamila.

Mkuu huyo wa Mkoa katika hatua nyingine amewaagiza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA kutoa vibali vya muda mfupi kwa mabasi ya kawaida ili yaweze kutoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwenye njia hizo ambazo zilikuwa zikitegemea mabasi ya mwendokasi yaliyosimama kutoa huduma katika barabara tajwa.

WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAHIMIZA AMANI, WAKITAKA WANASIASA KUACHA MALUMBANO

11/05/2025 07:45:00 am

Wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam wameeleza athari kubwa za kiuchumi na Kijamii zilizotokana na ghasia na vurugu za baada ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025, wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake ya kutaka ulinzi na usalama kuimarishwa na shughuli za kijamii na kiuchumi kurejea katika hali yake ya kawaida.

Bw. Eliezer Wilson, Mjumbe wa Taasisi ya Machinga wa Kariakoo (KAWASO) kwa niaba ya wafanyabiashara wadogo wa soko hilo, ametoa kauli hiyo siku moja mara baada ya kuapishwa kwa Rais Samia, ambapo katika hotuba yake ya awali alikemea vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani vilivyotokea Oktoba 29- 31, 2025 kwa baadhi ya watu kuvunja, kuharibu na kutekeleza mali za umma na za binafsi katika mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Mkoani Songwe.

Naye Mfanyabiashara na Kiongozi wa Wafanyabiashara wa soko hilo Bw. Jabir Makunga 
ameeleza athari za ghasia hizo zilizodumu tangu siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 29, 2025 kuwa ni pamoja na Vifo na tabu zilizotokana na kukosekana kwa huduma za matibabu kwenye Vituo vya afya kwenye Mikoa iliyokumbwa na ghasia hizo, huduma za usafiri kudorora, mfadhaiko, hofu na wasiwasi, ukosefu wa mahitaji muhimu ya kila siku pamoja na mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu.

Akieleza kuhusu athari kubwa za Kijamii na kiuchumi zilizojitokeza kutokana na vurugu, ghasia na maandamano ya Oktoba 29, 2025 Mkoani Dar Es Salaam, Mfanyabiashara Fadhil Mwango amewataka Vijana kujiepusha na kufuata mikumbo isiyofaa na yenye kuhamasisha kuhusu Uvunjifu wa amani nchini badala yake wafuate taratibu rasmi zilizopo katika kuwasilisha kero walizonazo.

Tuesday, 4 November 2025

HALI YA USALAMA MKOA WA ARUSHA NI SHWARI- RC MAKALLA

11/04/2025 05:27:00 pm

 *_Atoa rai kwa wananchi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi_* 

 *_Awahakikishia wananchi Ulinzi na usalama wa kutosha_* 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Arusha, wageni na Watalii wanaofika Mkoani Arusha kuwa hali ya ulinzi na usalama Mkoani Arusha ni shwari na shughuli za kijamii na kiuchumi zimerejea katika hali yake ya kawaida.

Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Jumanne Novemba 04, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, mara baada ya Kikao cha Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa, akisema kwamba Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga pia kuhakikisha huduma za ulinzi na usalama zinakuwepo muda wote ili kuruhusu shughuli za kijamii na kiuchumi za kila siku kuendelea kama ilivyo kawaida.

Aidha katika kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa hapo jana, CPA Makalla amewataka wamiliki wa Vituo vya mafuta kufungua vituo vyao pamoja na maeneo mengine ya biashara, akiwataka Viongozi wa serikali za Mitaa na Vijiji kuendelea kutimiza jukumu lao la kuhakikisha usalama unakuwepo wa kutosha katika maeneo yao na kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria kwa Mamlaka husika.

Katika hatua nyingine CPA Makalla amewaagiza Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zote Mkoani Arusha chini ya usimamizi wa Katibu Tawala wa Mkoa, kuhakikisha huduma za usafi wa mazingira zinasimamiwa kikamilifu kwa kuondoa taka zote kwenye maeneo ya  masoko na makazi ya wananchi ili kuepukana na magonjwa ya milipuko kutokana na mrundikano wa takataka.

YALIYOTOKEA HAYAKUWA MAANDAMANO, ZILIKUWA FUJO NA GHASIA DHIDI YA USTAWI WA TANZANIA

11/04/2025 05:18:00 pm

Oktoba 29, 2025 nchi yetu ya Tanzania ilishiriki uchaguzi Mkuu wa kuwachagua Diwani, Mbunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndani ya saa 72 Tanzania ikampata Rais, Madiwani na Wabunge ambapo Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameapishwa Jana Jumatatu Novemba 03, 2025 kuwa Rais wa awamu ya sita akiwashinda wenzake kutoka Vyama 17 vilivyosimamisha wagombea wa nafasi ya Urais.

Wakati wa kula Kiapo, Dkt. Samia kama ilivyokuwa wakati akikabidhiwa hati ya ushindi kutoka kwa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, amerejea tena msisitizo wake wa kuwataka Watanzania kutofanya mzaha dhidi ya amani ya Tanzania, akionya kuhusu vurugu zilizotokea katika baadhi ya maeneo nchini hususani katika Miji ya Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha na Songwe - Wengi wakimuunga mkono na kuziita ghasia na fujo na si maandamano kama ambavyo baadhi ya wengi wamekuwa wakieleza mitandaoni.

Uhalali wa fujo na ghasia unakuja pia kufuatia kauli ya Jeshi la Polisi na marejeo yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyeeleza kuwa taarifa za kiitelejensia zimebainisha kuwa wengi wa waliokuwa wanaongoza ghasia na fujo hizo zilizoambatana na mashambulizi ya kuchoma na kuharibu mali si raia wa Tanzania sambamba na kile ambacho tumekiona Mitandaoni, waliokuwa wakihamasisha ghasia hizo wakiwa pia si wakazi wa Tanzania na wengine ni wale walioukana Utanzania wao na wakiwa na historia za kufaidika pale panapotokea sintofahamu na migawanyiko miongoni mwa Watanzania.

Miongoni mwa wageni wahudhuriaji waliopata fursa ya kutoa salamu zao, amekuwa ni Rais wa Zambia Mhe. Hikainde Hichilema. Katika salamu zake kando ya kuonya Watanzania kutoujaribu upande wa pili wa amani na vile ilivyo ngumu kurejea katika Amani ikiwa itapotezwa, ameshauri wanaohisi kuonewa kutokuwa na chaguo la kuingia barabarani kufanya vurugu na ghasia na badala yake wawe na chaguo sahihi na la kufaa la mazungumzo katika kuondoa na kutatua changamoto zilizopo, akirejea historia ya Taifa lake, kutotendewa haki kwa Chama chake katika chaguzi mbalimbali na namna ambavyo chama chake kiliheshimu, kusimamia na kutetea amani ya Zambia, katikati ya changamoto na vikwazo vilivyokuwepo.

"Sishauri na sitakuwa mshauri wa wananchi na wanasiasa wenzangu kutaka watu waingie barabarani kufanya fujo kama ilivyotokea juzi, hakuna faida ya kufanya hivyo na hakuna namna ambavyo mtafanikiwa kupata haki kwa njia ya fujo na ghasia." Amesisitiza Rais Hichilema wa Zambia.

Ili kudhihirisha kuwa hayakuwa maandamano bali fujo na Ghasia, Mchambuzi Michael Msubya anasema maandamano ni lazima yawe na malengo, yafanyike kwa kuzingatia sheria na yadhamirie kuleta ama kutoa ujumbe fulani ikiwa tu yatakuwa halali kisheria na yenye kuungwa mkono na umma, akionesha kushangazwa na kile kilichofanyika Oktoba 29, 2025.

" Haiwezekani mtake mabadiliko kupitia vurugu na machafuko, haiwezekani mseme mnataka mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi au kutuma ujumbe wa kuonewa halafu mnaenda kuchoma vituo vya mafuta vya watu, mnaiba mali za watu madukani na kule Mwanza tumeona wanaenda kuiba mpaka bia kwenye bar za watu, zile zilikuwa vurugu na zinapaswa kupingwa na kila mtu mpenda amani na maendeleo." Ameongeza kusema Bw. Msubya.

Tayari Dkt. Samia kamati za ulinzi na usalama kwenye Mikoa yote ya Tanzania bara zimetekeleza maagizo ya Rais Samia aliyoyatoa hapo jana ya kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na shughuli za kijamii na kiuchumi zinarejea katika hali yake ambapo kwa Mikoa mbalimbali nchini Ikiwemo Arusha na Dar Es Salaam, kumeshuhudiwa biashara na masoko ya bidhaa mbalimbali yakifunguliwa pamoja na huduma ya usafiri na usafirishaji ikirejea kama ilivyokuwa awali.

RC MAKALLA AONGOZA WANANCHI WA ARUSHA KUPIGA KURA*

11/04/2025 05:16:00 pm

 *_Asema hali ya usalama mkoa Arusha ni Shwari na Salama_* 
 
 *_Awahimiza wananchi wenye sifa kujitokeza kutumia haki yao ya Kikatiba_* 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla mapema asubuhi ya leo Oktoba 29,2025 amewaongoza wananchi wa mkoa wa Arusha kupiga kura kwa kutimiza wajibu wake na kutumia haki yake ya Kikatiba ya kuchagua viongozikatiba ya kkuchagua viongozi.

CPA Makalla mara baada ya kukamilisha zoezi la upigaji kura kwenye Kituo chake cha AICC Hospitali Jijini Arusha, ameendelea kuwahakikishia wananchi wote kuwa hali ya usalama iko shwari na kuwataka wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kutimiza haki yako ya kikatiba  ya kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Aidha, CPA Makalla ametumia muda huo kuwahamasisha wananchi wa Arusha wenye sifa kujitokeza kupiga kura huku akiwathibitishia wananchi wote kuwa, Tume imeweka utaratibu mzuri kwa kuwa na vituo vingi, ambavyo vinawezesha mpiga kura kutotumia muda mrefu kusimama kituoni.

"Mimi mwenyewe nimeshatimiza wajibu wangu, vituo tayari viko wazii, kuanzia saa 01:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni, nimefurahi utaratibu ni mzuri hakuna foleni kubwa vituo ni vingi hivyo mtu akifika kituoni hatatumia muda mrefu, kila mtu atumie muda huo kwenda  kwenye kituo alichojuandikisha" Amebainisha CPA  Makalla.

Dkt. Tulia Atoa Wito wa Amani na Ushiriki Kwenye Uchaguzi

11/04/2025 05:16:00 pm

Spika wa Bunge ambaye pia ni mgombea wa Jimbo la Uyole, Dkt.Dkt. Tulia Atoa Wito wa Amani na Ushiriki Kwenye Uchaguzi Tulia Ackson, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu, akisisitiza umuhimu wa kutumia haki yao ya kidomokrasia kuchagua viongozi wanaowataka.

Dkt. Tulia alitoa wito huo mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Tambukareli, ambako aliwasihi wananchi wasikae majumbani bali washiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa taifa.

Amesema uchaguzi ni fursa ya wananchi kuamua mustakabali wa nchi yao kupitia kura, hivyo ni wajibu wa kila mwenye sifa kuhakikisha anatumia haki hiyo kwa utulivu na uwajibikaji.

Aidha, amewapongeza watendaji wa tume ya uchaguzi kwa maandalizi mazuri na kuhimiza kuendelea kudumisha amani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi.

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens

11/04/2025 05:15:00 pm
Na Mwandishi wetu, Dodoma

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens inayokwenda kuliwakilisha Taifa na ukanda wa CECAFA katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa upande wa soka la wanawake.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo mara baada kumalizika kwa zoezi la upangaji wa makundi liliofanyika Cairo nchini Misri Octoba 27, 2025 ambapo JKT Queens imepangwa Kundi B likijumuisha Bigwa mtetezi TP Mazembe kutoka DR Congo, Asec Mimosas kutoka Ivory Coast na Gaborone United kutoka Botswana.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 8, 2025 hadi Novemba 21, 2025.

Aidha Meja Jenerali Mabele ametoa wito kwa watanzania kushabikia timu hiyo ya kizalendo yenye wachezaji wazawa kama inavyofanyika mara zote kwa kwa timu za Simba na Yanga zinapowakilisha nchi.

JKT Queens inawakilisha Tanzania na Ukanda wa CECAFA kwa ujumla kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake ambapo jumla ya timu 8 zitashiriki.

Monday, 27 October 2025

CWT YAWAHAKIKISHIA WATANZANIA USHIRIKI WA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025

10/27/2025 11:17:00 am

Chama cha waalimu nchini Tanzania CWT kimewataka waalimu kote nchini kuendelea na msimamo wao wa kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba, 2025 kwenda kupiga kura kwani ndiyo msimamo wa Chama ambao ulikwisha tolewa na Msemaji wa Chama hicho ambaye ni Rais wa Chama Cha waalimu nchini Tanzania Bw. Suleiman Ikomba.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CWT Mwalimu Joseph Misalaba kwenda kwa Makatibu wa CWT, Mikoa na Wilaya imesisitiza waalimu pia na umma kwa ujumla kuwa Mabalozi wazuri wa Upendo, amani, umoja na mshikamano kwaajili ya maendeleo thabiti ya Tanzania kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye, wakiishukuru pia serikali kwa kuendelea kutatua kero za waalimu kwa kushirikiana na CWT.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa CWT imekuja baada ya kuzuka kwa uvumi mitandaoni zikieleza kuwa Chama Cha Waalimu kimesusia uchaguzi Mkuu wa Keshokutwa Jumatano, ambapo Mwalimu Misalaba amekanusha taarifa hizo na akitaka Watanzania wazipuuzie.

"Chama Cha Waalimu Tanzania kinapenda kukanusha kwa nguvu zote taarifa zinazosambaa kupitia Mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya Vyombo vya habari ikihamasisha walimu kutoshiriki kwenye shughuli za uchaguzi Mkuu ambazo baadhi ya waalimu hutumika kama wasaidizi wa shughuli za uchaguzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za serikali ya Tanzania." Amesema Katibu Mkuu huyo.

Mwalimu Misalaba pia ametoa rai kwa waalimu, wamachama wa CWT na watanzania wote kwa ujumla kupuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli wala msingi wowote, akisema zinalenga kuleta taharuki, uzushi na uchonganishi ambao unapaswa kupingwa kwa nguvu zote ili kuendelea kulinda amani, umoja na utulivu ambao ni tunu ya Taifa.

CWT imewahakikishia waalimu, serikali na wananchi wote kuwa kitaendelea kushirikiana na mamlaka husika katika kuhakikisha kuwa tabia ya utoaji wa taarifa potofu inakomeshwa ili kulinda misingi na madhumuni ya uwepo wa vyama vya Wafanyakazi kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

VIONGOZI WA DINI SINGIDA NA DODOMA WAHIMIZA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

10/27/2025 11:15:00 am

Zikiwa zimesalia siku nne pekee kabla ya Watanzania kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, baadhi ya viongozi wa dini kutoka Mikoa ya Singida na Dodoma wamewataka vijana kuepuka vishawishi vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani, wakisisitiza kwamba utulivu wa Taifa ni msingi wa maendeleo na umoja wa kitaifa.
Wakizungumza leo jijini Dodoma katika kongamano la viongozi wa dini mbalimbali kutoka Kanda ya Kati, viongozi hao wamehimiza vijana na wananchi kwa ujumla kuendelea kutimiza majukumu yao ya kijamii na kidini, huku wakielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda amani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

Akitoa wito huo, Askofu Evance Chande wa Kanisa la Carmel Assemblies of God alisema vijana ndio nguvu kazi ya Taifa, hivyo wanapaswa kutumia nafasi yao kujenga badala ya kubomoa.

“Tunapaswa kuikumbatia amani kama tunavyokumbatia imani zetu. Uchaguzi ukipita, Tanzania inabaki kuwa moja, hivyo tusikubali kugawanywa kwa misingi ya kisiasa,” alisema Askofu Chande.

Kwa upande wake, Sheikh Mustapha Rajab, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Kanda ya Kati na mgeni rasmi wa kongamano hilo, aliwahimiza wananchi kutii mamlaka na kufuata taratibu zinazotolewa na Serikali pamoja na viongozi wa dini.

 “Amani si jambo la bahati mbaya, ni matokeo ya utii na hekima. Tukitii viongozi wetu na kuheshimu sheria, Taifa litaendelea kubaki salama,” alisema Sheikh Rajab.

Kongamano hilo lililolenga kuliombea Taifa amani na utulivu kuelekea uchaguzi, lilibebwa na kaulimbiu isemayo “Kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania, amani na utulivu ni jukumu letu.
Viongozi hao walikubaliana kuwa jukumu la kulinda amani si la Serikali pekee, bali ni la kila mwananchi, na wakasisitiza umuhimu wa maombi, maelewano, na uvumilivu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.

Saturday, 25 October 2025

HAKI HAIPATIKANI KUPITIA VURUGU NA MAANDAMANO- TWARIQA TANZANIA

10/25/2025 05:22:00 pm

Kiongozi Mkuu wa Taasisi ya Twariqa Tanzania, Sheikh Said Hamis Migire, amesisitiza umuhimu wa Kila Mtanzania kuwajibika katika kudumisha amani na utulivu kabla, wakati wa upigaji wa kura na hata baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 akifananisha amani na yai ambalo likivunjika ni vigumu kulirejesha katika hali yake ya awali.

Akizungumza na waandishi wa habari pembezoni mwa dua maalumu ya kuombea amani iliyofanyika katika Zawia Kuu, Makao makuu ya taasisi hiyo jijini Arusha, na kuhudhuriwa na mamia ya waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini, Sheikh Migire amesema ni muhimu kila Mtanzania kujiepusha na vurugu na viashiria vingine vyovyote vyenye kutishia tunu za Taifa, akihimiza kutafakati kabla ya kuchukua hatua yoyote inayoenda kinyume na tamaduni na ustaarabu.

“Amani ni kama yai likivunjika ni ngumu sana kulirudisha. Tumeona mataifa mengi ya Afrika yaliyopoteza amani, na sasa wanajuta." Amesema.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Twariqa Taifa, Sheikh Haruna Hussen ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini kuungana kwa pamoja katika maombi ya kuombea amani, akisisitiza kuwa jukumu la kulinda amani ni la kila Mtanzania.

“Na sisi kama viongozi wa dini tunao wajibu wa kuhubiri amani usiku na mchana. Amani ni msingi wa taifa.
Tunawaomba Watanzania wasidanganyike bali tushike amani yetu kwa mikono miwili." Amesema Sheikh Haruna.

TUKAE PAMOJA KUOMBEA AMANI- KARDINALI RUGAMBWA

10/25/2025 05:20:00 pm

Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora nchini Tanzania amesisitiza umuhimu wa Jamii kuombwa amani ya Tanzania na mshikamano Miongoni mwa watanzania kama ambavyo Vitabu vitakatifu vilivyoagiza kukaa pamoja kwa umoja.

Kardinali Rugambwa amebainisha hayo leo Oktoba 24, 2025 wakati wa Kongamano la maombi lililofanyika Tabora na kukusisha waumini wa dini na madhehebu mbalimbali Mkoani humo wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

"Sisi ni watoto wa baba mmoja, tukae pamoja na kuwa tayari kufanya mambo pamoja ikiwemo amani, haki, upendo, ushirikiano, kwamba umoja ambao ni tunu ya Taifa letu idumu lakini pia uwepo wa mashirikiano na kukaa kwa pamoja kama ndugu kusikilizana pale kwenye matatizo na pale palipo na shida ama matatizo tuone namna gani ya kuyashughulikia." Amesema Kardinali Rugambwa.

Kiongozi huyo wa dini nchini Tanzania ameongeza pia kwamba kuombea amani ni maelekezo ya Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo, ambaye amekuwa akionesha kwa vitendo namna ambavyo amekuwa akishirikiana na Viongozi wa dini nyingine kukaa na kusali pamoja kwa kukuza imani zao kwa Mungu mmoja ambaye kila muumini wa dini amekuwa akimuamini pamoja na kuimarisha na kukuza maridhiano miongoni mwa jamii sambamba na kuombea amani.

MULIRO AONYA WANAOPANGA KUANDAMANA NA KUFANYA VURUGU DSM

10/25/2025 05:20:00 pm

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewaonya wale wote wanaopanga, kuratibu ama kutaka kushiriki kwenye uvunjifu wa amani ikiwemo kufanya vurugu na maandamano Oktoba 29, 2025, akisema Jeshi hilo limekula kiapo kulinda nchi pamoja na raia na mali zao.

Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 24, 2025 wakati wa kongamano la Vyuo na Vyuo Vikuu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Kongamano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza na kuwashirikisha wanafunzi wa shule za Sekondari, Vyuo na Vyuo Vikuu, akiwataka Vijana pia kuwa waangalifu na kutafakari kuhusu misukumo na mihemko yao kulingana na aina na makundi ama watu wanaoambatana nao.

"Tukiwa kama watu tuliokula kiapo tunawaleza kuwa tutatimiza jukumu letu la kuhakikisha kuwa watu wanakuwa salama, watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura, wafuate sheria na sisi tutakuwepo barabara kuwalinda wote wanaoenda kutimiza jukumu lao la Kikatiba la kwenda kupigakura. Siku hiyo kutakuwa hakuna maandamano wala hakuna vurugu, siku hiyo ni ya upigaji wa kura bila hofu."Amesema.

Kama Muliro pia amesisitiza kuwa Vijana kuwa na fikra chanya ama hasi katika kujadili jambo fulani sio kitu kibaya ila kuipeleka mitazamo hasi kwenye vitendo vya vurugu ndiyo kosa kisheria, akiwataka pia Vijana kulinda hatma zao kwa kuhakikisha nchi inakuwa na amani ili kuwawezesha kutimiza malengo na ndoto zao kiuchumi, kisiasa na Kijamii.

Friday, 24 October 2025

DC KARANGA AWAHAKIKISHIA WANANCHI USALAMA, WALIOPOTEZA KADI ZA MPIGAKURA WAITWA VITUONI

10/24/2025 11:27:00 am

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha Mhe. Dkt. Lameck Ng'ang'a Karanga, amewahakikishia usalama na mazingira tulivu wananchi wote wa Wilaya hiyi katika Kipindi cha lala salama cha Kampeni za Uchaguzi Mkuu, wakati wa Upigaji kura na hata baada ya Mchakato huo kukamilika, akiwataka wananchi kupuuza Taarifa za Mitandaoni za kutokuwa na uchaguzi Jumatano Ijayo Oktoba 29, 2025.

Dkt. Karanga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake akisisitiza pia wapigakura wote kurejea Majumbani mara baada ya kukamilisha zoezi la Upigaji wa kura na kuachana na baadhi ya hamasa zinazofanywa kwenye Mitandao ya Kijamii kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wanaohamasisha wafuasi wao kusalia vituoni kulinda kura suala ambalo ni jukumu la Polisi na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini Tanzania.

Kwa upande wake Bi. Farida Kimambo, Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Karatu, ameeleza kuwa maandalizi ya uchaguzi Mkuu 2025 yamekamilika, akisema vituo vya kupigia kura ni vile vilivyotumika kujiandikishia, akiwataka wananchi kufika sasa kwenye Vituo hivyo kuhakiki Taarifa na Majina yao.

"Mpigakura ambaye kitambulisho chake kimepotea ama kuharibika anaweza kupiga kura kwa kutumia leseni ya udereva, pasi ya kusafiria au kitambulisho cha NIDA ili aweze kupiga kura lazima awe amejiandikisha kwenye daftari la mpigakura na lazima jina alilojiandikishia liwe limefanana na Jina la kwenye Kitambulisho, leseni au pasi yake ya kusafiria." Amesema Msimamizi huyo wa uchaguzi.

Bi. Kimambo pia ameeleza kuwa Oktoba 25, 2025 watakuwa na semina ya mafunzo kwa makarani waongoza wapigakura kura kwenye Vituo vya Kupigia kura na Oktoba 26 na 27 watafanya mafunzo mengine kwa wasimamizi wa Vituo na wasaidizi wasimamizi wa Vituo ili kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa pamoja na kuyafahamu majukumu yao wakati wa zoezi la upigaji kura hapo Oktoba 29, 2025. 

Thursday, 23 October 2025

USAFIRI WA SGR DAR ES SALAAM- DODOMA WAREJEA, TRC YAOMBA RADHI KWA USUMBUFU

10/23/2025 04:35:00 pm

Shirika la reli Tanzania limeufahamisha umma wa Watanzania kuwa huduma za usafiri wa treni za SGR zimerejea na kuendelea kama kawaida, likiomba radhi kwa wateja wake kwa usumbufu uliojitokeza, shirika likiwashukuru pia Wananchi kwa uvumilivu wao katika kipindi ambacho huduma za usafiri huo zilipotatizika kutokana na hitilafu iliyotokea mapema leo Alhamisi Oktoba 23, 2025.

Mapema leo Shirika la Reli Tanzania lilitoa taarifa kwa Vyombo vya habari likieleza kuhusu ajali ya Treni ya EMU iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar Es Salaam kwenda Dodoma majira ya saa mbili asubuhi kutokana na hitilafu za uendeshaji, tukio ambalo lilitokea Kituo cha Ruvu na kwa taarifa za shirika hilo hakukuwa na athari kubwa za ajali hiyo.

Timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa uchukuzi, Mkurugenzi wa shirika la TRC, Vyombo vya ulinzi na usalama na menejimenti ya TRC ilianza haraka kushughulikia changamoto hiyo na kufanya na uchunguzi wa kina wa kuhakikisha kuwa huduma hizo zimerejea haraka.

RC Malima atoa Onyo kali kwa wanaoratibu vietendo vya uvunjifu wa Amani uchaguzi mkuu

10/23/2025 12:43:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima, ametoa onyo kali kwa makundi au watu wenye nia ya kuanzisha fujo ama vurugu wakati wa kipindi cha uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara na makini kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa nchini.

Malima ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 22, 2025, wakati wa Kongamano la Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu, lililoandaliwa na Taasisi ya Ukumbusho wa Zakkat Tanzania na kufanyika mkoani Morogoro, akisema kuwa baadhi ya watu wanaojaribu kuvuruga amani nchini ni watu wanaoshawishiwa na kuiga matendo kutoka nje, na hawana nia njema na Taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa , amesema watanzania wanapaswa kukataa kwa nguvu zote watu wanaoeneza chuki na kuhatarisha maisha ya wengine, hasa katika kipindi hiki nyeti cha uchaguzi.

Naye Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, Dkt. George Pindua, ameahidi kuwa viongozi wa dini wataendelea kuhubiri amani, mshikamano na upendo ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya utulivu.

NDANI YA MIAKA MINNE YA DKT. SAMIA MADARAKANI UCHUMI UMEPAA- PROF. ASSAD

10/23/2025 12:21:00 pm

 _Agusia tatizo la ukosefu wa Ujuzi kwa wahitimu_ 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) na Mkaguzi Mkuu mstaafu wa hesabu za serikali (CAG)  Profesa Mussa Juma Assad, amesema hali ya uchumi wa Tanzania kwa sasa kwa miaka hii minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni nzuri ukilinganisha na miaka ya nyuma, huku ukuaji wa uchumi ukiendelea kwa kasi na mfumuko wa bei ukiwa katika viwango vinavyoridhisha.

Akizungumza na waandishi wa habari kando ya Kongamano la Kitaaluma la kujadili Utekelezaji wa Uchumi Jumuishi kuelekea Dira 2050, lililoandaliwa na MUM kwa ushirikiano na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), Profesa Assad amesema uchumi wa nchi umekua kwa wastani wa asilimia 6 katika kipindi cha miaka minne iliyopita suala ambalo limesaidia watanzania kuendelea kupata mahitaji yao muhimu kama Vyakula, elimu ma mahitaji mengine.

“Kwa jumla uchumi wa Tanzania umekuwa kwa wastani wa asilimia sita. GDP, kupanda na kushuka kwa pato la taifa kumekaa vizuri ukilinganisha na nchi jirani. Hali ya kiuchumi ni nzuri zaidi kuliko Kenya na Rwanda,” amesema Profesa Assad.

Profesa Assad amesema kuwa vigezo vya kiuchumi vya sasa vinaonyesha uwezo bora zaidi wa wananchi kuendesha maisha yao ukilinganisha na miaka ya nyuma, jambo linalodhihirisha uimara wa uchumi wa nchi.

Aidha Profesa Assad ameeleza kuhusu changamoto ya vijana wanaohitimu vyuo vikuu kukosa ujuzi wa vitendo, akibainisha kuwa tatizo siyo kutokuwa sehemu ya uchumi, bali kukosa stadi za kazi, akisema Vijana wanaotoka Vyuoni wanapaswa kupewa mafunzo ya ujuzi kwa vitendo baada ya kumaliza masomo akisema jambo hili linapaswa kubebwa na serikali na sekta binafsi kwa kutoa kozi na fursa fupi za Vijana hao kujifunza zaidi kwa vitendo masuala mbalimbali ili kupata ujuzi.

Wednesday, 22 October 2025

WAHADZABE WA KARATU WAISUBIRI KWA HAMU OKTOBA 29

10/22/2025 12:32:00 pm

Jamii ya Wahadzabe wanaopatikana kwenye eneo la Mang'ola Wilayani Karatu Mkoani Arusha wameahidi kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya Kikatiba ya kuchagua Viongozi katika uchaguzi Mkuu wa Jumatano ijayo Oktoba 29, 2025.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 22, 2025, wakiishukuru serikali pia kwa kuwakumbuka na kuwajumuisha katika zoezi hilo la Kikatiba licha ya kuishi kwao maeneo ya pembezoni na Jamii nyingine, wakisema wanatarajia kushiriki kwenye uchaguzi huo kikamilifu ili kuwachagua Viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo.

"Kwaniaba ya wenzangu Jamii ya Wahadzabe niwahakikishie kuwa tutaenda kupiga kura tarehe 29 na tutachagua Viongozi watakaoenda kutuangalia sisi kwa ujumla Wahadzabe wote ili tufanikiwe kimaendeleo kwasababu sisi tunaishi porini na hatujui mengi yanayoendelea kwahiyo tutawachagua wanaoweza kutuletea maendeleo huku." Amesema mmoja wa wananchi wa Jamii hiyo.

Kwa upande wao Ruben Mathayo, Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Tanzania na Mariam Anyanyire, Mhamasishaji ndani ya jamii hiyo, wameeleza kuwa muamko ni mkubwa kwa jamii hiyo kuelekea uchaguzi Mkuu wakiahidi kuwa kila mwenye haki na sifa ya kupiga kura atajitokeza siku hiyo kuwachagua Viongozi wanaowataka.

HATUTOWAACHA SALAMA WANAOPANGA KUVURUGA UCHAGUZI MKUU- RC SENDIGA

10/22/2025 10:58:00 am

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbeth Sendiga ameonya Vikali wale wote ama Vikundi vinavyopanga au kuratibu kufanya vurugu na fujo wakati wa Oktoba 29, 2025, siku ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania,  akiwahakikishia wananchi wa Mkoa huo usalama na mazingira tulivu kuanzia sasa, siku ya upigaji kura na hata baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi Mkuu.

Mhe. Sendiga ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 21, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Babati kuhusu maandalizi mbalimbali ya kiserikali kuelekea uchaguzi Mkuu, akihimiza ushirikiano zaidi kati ya serikali, Wananchi, Vyama vya siasa na wadau wengine kuelekea kwenye uchaguzi huo Mkuu wa wiki ijayo Oktoba 29, 2025.

"Kama serikali tunawajibu wa kukemea mapema, yeyote ama kundi linalopanga kufanya vurugu kwa kujishawishi mwenyewe ama kushawishiwa kwa makusudi ama kwa bahati mbaya kwenda kutufanyia vurugu katika siku hii, sisi kama serikali tunatoa onyo kubwa na kali kabisa hatutokuacha salama na hatutakuvumilia. Amua mapema unakuja Mtaani tukutane ama tupige kura kwa amani turudi nyumbani.

"Hatutamvumilia atakayevuruga siku hii maalumu kwa upigaji wa kura. Mkoa wa Manyara ni "Wrong number",kamwe usijaribu kuvuruga siku hii ya neema na baraka kwa wananchi kuamua hatma ya miaka yao mitano ijayo." Amesema Mhe. Sendiga.

Mhe. Sendiga pia ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kusisitiza umuhimu wa kurejea nyumbani na kuendelea na shughuli nyingine badala ya kuendelea kujihusisha na uvunjifu wa sheria ikiwemo kusalia vituoni kama ambavyo baadhi ya Vyama vya siasa vinavyoshawishi wanachama wao kusalia vituoni ili kulinda kura suala ambalo ni kinyume na miongozo ya uchaguzi Mkuu.

Tuesday, 21 October 2025

WANNE JELA MIAKA SABA KWA JARIBIO LA KUMTEKA MFANYABIASHARA

10/21/2025 06:38:00 pm

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Kinondoni, Dar Es Salaam imewahukumu Vijana wanne wakiwemo Mabondud 3ia wawili kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kumteka Mfanyabiashara Deogratus Tarimo, tukio lililoteka hisia za wengi Mitandaoni, wengi wakiwahusisha watu hao na Maafisa wa Vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Vijana hao waliohukumiwa ni Fredrick Nsato (21) Mkazi wa Kibamba, Isaack Mwaifuani (29) Mkazi wa Kimara, Benki Mwakalebela (40) na Bato Twelve (32) Mkazi wa Kimara Bonyokwa Mkoani Dar Es Salaam.

Kabla ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhani Rugemalira kusoma hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Daisy Makakala amesema pamoja na kuwa hana kumbukumbu za makosa ya nyuma ya watuhumiwa wote wanne lakini anaiomba mahakama itoe adhabu sawa na kifungu cha sheria walichoshtakiwa nacho ili jamii ya Tanzania na dunia nzima ifahamu kuwa wanaotenda vitendo vya utekaji wa Raia wa makundi mbalimbali siyo Maafisa waJeshi la Polisi, bali ni watu wa kawaida ambao wamekuwa wakifanya vitendovya kiuhalifu kwa sababu mbalimbali.
"Naomba mahakama iwape adhabu kali washtakiwa kwa sababu vitendo vya utekaji vimeshamiri sana nyakati hizi, hali inayopelekea Jeshi la Polisi kulaumiwa kwa utekaji huo. Hawa watuhumiwa wangefanikiwa kumkamata Deogratius Tarimo akapotea asionekane Jamii ingeamini kuwa ni Polisi ndiyo wamempoteza hasa na vile wakati wanamkamata walikuwa wakijitambulisha kama Askari Polisi toka Kituo cha Gogoni wakati wakijua ni uongo. Hivyo ili kutoa fundisho kwa hawa watuhumiwa waliokutwa na hatia na jamii yote kwa ujumla mahakama iwape adhabu kali."amesema Wakili Makakala.

Kwa upande wao washtakiwa wao waliomba wapunguziwe adhabu na kudai kuwa wao walikuwa wanasaidia kumteka tu baada ya rafiki yao Frederick kuwaomba wamsaidie kumteka, kwa madai kuwa wanahisi Deo alitembea na mke wa rafiki yake Fredrick.

Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka, Fredrick na wenzake walitenda kosa hilo Novemba 11, 2024 eneo la Kiluvya Madukani Lingwenye, lllilopo Wilaya ya Ubungo ambapo Ilielezwa kuwa siku hiyo ya tukio katika eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja walijaribu kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo kwa nia ya kumuweka kizuizini isivyo halali ambapo Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani mahakamani hapo, Desemba 6, 2024 na kusomewa shtaka hilo.

TUNALAANI WOTE WANAOHAMASISHA MAANDAMANO- MALAIGWANAN K'NJARO

10/21/2025 04:27:00 pm

 _Waahidi kuwachagua walinda amani na mshikamano wa Taifa_ 

Viongozi wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania maarufu kama (Malaigwanan) wametoa tamko lao rasmi kwa nchi nzima, la kuunga Mkono kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025, wakilaani uwepo wa hamasa ya kufanyika kwa maandamano siku hiyo wakiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua Viongozi wanaowataka.

Viongozi hao wametoa tamko hilo katika eneo la Donyomorwak Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro kwenye Mkutano wao wa kawaida wa Orkiama ambapo akisoma tamko hilo kwaniaba ya Viongozi hao, Bw. Jeremia Laizer, Katibu wa Malaigwanani Tanzania, ameeleza pia kwamba Jamii hiyo itamuunga Mkono Kiongozi mwenye kutanguliza mbele maslahi ya wananchi pamoja na kulinda amani na utulivu wa Tanzania.

"Tunawahimiza wananchi wote kudumisha amani, mshikamano na utulivu, kuanzia ngazi ya shina, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda hadi Taifa zima, tukiepuka maneno ya uchochezi, migawanyiko, na fitina. Tuchague maendeleo, umoja, na mustakabali mwema wa vizazi vya sasa na vijavyo. Tuwe nguzo ya amani, nuru ya matumaini, na urithi wa thamani kwa Taifa letu. Tanzania kwanza, amani kwanza." Amesema Bwana Laizer.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa Mkutano huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine amewapongeza malaigwanani hao kwa msimamo wao huo pamoja na kuonesha kuridhika na utendaji wa serikali ya awamu ya sita, akiwataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

Aidha baadhi ya Viongozi wengine wa jamii hiyo pia wameahidi kuwa mabalozi wa kueneza amani katika maeneo yao katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu, wakisisitiza athari za maandamano yasiyofuata taratibu kuwa ni pamoja na uharibifu na uvunjifu wa amani ambapo waathirika wakubwa mara zote wamekuwa wanawake, watoto pamoja na wazee.

Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith

10/21/2025 04:26:00 pm


Wakati Tanzania ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya Kijani, Dkt. Judith Mhina Spendi, ametoa wito kwa Watanzania wote kusimama pamoja kulinda amani ya taifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dkt. Judith alitangaza kongamano la amani litakalofanyika kuanzia Oktoba 25 hadi 27 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama, likiwakutanisha viongozi wa dini, vijana, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali.
Dkt. Judith alisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo, ikieleza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi kutokana na utulivu uliopo. “Hakuna maendeleo bila amani, hakuna uchaguzi huru bila utulivu, na hakuna taifa imara bila mshikamano,” alisema. Akihitimisha hotuba yake, alitoa wito kwa Watanzania wote kuwa sauti ya amani, umoja na ukweli.

“Mimi naahidi amani, wewe je?” — Dkt. Judith Mhina Spendi
Adbox